Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 128
Wale tu Wanaonyenyekea Ukuu wa Muumba Ndio Wanaweza Kupata Uhuru wa Kweli Kwa sababu watu hawatambui mipango ya Mungu, na ukuu wa Mungu,...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Machoni Pangu, mwanadamu ndiye mtawala wa vitu vyote. Nimempa mamlaka si haba, Nikimwezesha kusimamia vitu vyote duniani—nyasi iliyo juu ya milima, wanyama katika misitu, na samaki majini. Badala ya kuwa na furaha kwa sababu ya haya, mwanadamu anasumbuliwa na wasiwasi. Maisha yake yote ni yale ya maumivu makali, na kukimbia hapa na pale, na raha kuongezwa kwa utupu, na katika maisha yake yote hakuna uvumbuzi na uundaji mpya. Hakuna anayeweza kujinasua kutoka katika utupu huu wa maisha, hakuna ambaye amegundua maisha ya maana, na hakuna ambaye amepitia maisha ya kweli. Ingawa watu wa leo wote wanaishi chini ya mwanga Wangu unaong’aa, hawajui lolote kuhusu maisha ya mbinguni. Nisipokuwa na huruma kwa mwanadamu na Nisipomwokoa binadamu, basi watu wote wamekuja bure, maisha yao duniani hayana maana, na wataondoka bure, bila chochote cha kujigamba nacho. Watu wa kila dini, nyanja ya jamii, taifa, na dhehebu wote wanajua utupu ulio duniani, na wote wananitafuta na kungoja kurejea Kwangu—ilhali nani ana uwezo wa kunifahamu nitakapofika? Nilitengeneza vitu vyote, niliumba binadamu, na leo nimeshuka kati ya mwanadamu. Mwanadamu, lakini, anagonga nyuma Yangu, na kulipisha kisasi Kwangu. Je, kazi Ninayofanya kwa mwanadamu haina faida yoyote kwake? Je, Mimi hakika sina uwezo wa kumtosheleza mwanadamu? Mbona mwanadamu ananikataa? Mbona mwanadamu ni mbaridi na hana hisia Kwangu? Mbona ardhi imejawa na maiti? Je, hii ndiyo hali ya dunia Niliyomtengenezea mwanadamu? Mbona Nimempa mwanadamu mali isiyo ya kufananishwa, ilhali ananipa Mimi mikono miwili mitupu? Mbona mwanadamu hanipendi kwa kweli? Mbona haji kamwe mbele Zangu? Maneno Yangu yote yamekuwa ya bure? Je, maneno yamepotea jinsi joto lipoteavyo kwa maji? Mbona mwanadamu hataki kushirikiana na Mimi? Je, wakati wa kufika kwa siku Yangu ni wakati wa kufa kwa mwanadamu kweli? Je, hakika Ningeweza kumwangamiza mwanadamu wakati ufalme Wangu utatengenezwa? Mbona, wakati wa mpango Wangu wa usimamizi wote, hakuna ambaye ameweza kuelewa nia Zangu? Mbona, badala ya kuyatunza matamshi ya kutoka kwa mdomo Wangu, mwanadamu anayachukia na kuyakataa? Simkashifu yeyote, ila tu Nawafanya watu wote watulie na kutekeleza kazi ya kujiangalia kwa undani.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 25
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wale tu Wanaonyenyekea Ukuu wa Muumba Ndio Wanaweza Kupata Uhuru wa Kweli Kwa sababu watu hawatambui mipango ya Mungu, na ukuu wa Mungu,...
Kazi ya siku za mwisho inavunja kanuni zote, bila kujali kama umelaaniwa au kuadhibiwa, maadamu tu uisaidie kazi Yangu, na una manufaa kwa...
Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika...
Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake Kama tutazungumzia Ayubu, basi...