Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 528

Kwa wale ambao wanatakiwa kufanywa wakamilifu, hatua hii ya kazi ya kushinda ni ya lazima; Ni baada ya kushindwa tu ndipo mwanadamu anaweza kuiona kazi ya kufanywa mkamilifu. Hakuna maana kubwa ya kufanya kazi ya kushindwa, ambayo itakufanya usiwe mwenye kufaa kufanya kazi yoyote ya Mungu. Hutakuwa na uwezo wowote wa kufanya kazi yako ya kueneza injili, kwa sababu hufuati maisha, na hujibadilishi na kujifanya mpya, na hivyo basi huna uzoefu kamili wa maisha. Katika kazi hii ya hatua kwa hatua, uliwahi kuwa na nafasi ya mtendaji-huduma, na foili, lakini kwa hakika usipofuata kuwa kama Petro, na ufuasi wako sio kama wenye njia ambayo Petro alifanywa mkamilifu, basi, kiasili hutapata mabadiliko katika tabia yako. Kama wewe ni mtu anayefuata kuwa mkamilifu, basi utakuwa na ushuhuda, na utasema: “Katika hii kazi ya hatua kwa hatua ya Mungu, nimekubali kazi ya Mungu ya adabu na hukumu, na hata kama nimepitia mateso mengi, nimepata kujua jinsi Mungu hufanya mwanadamu kuwa mkamilifu, nimepata kazi iliyofanywa na Mungu, nimekuwa na maarifa ya haki ya Mungu, na adabu Yake imeniokoa. Tabia Yake ya haki imekuja juu yangu, na ikaniletea baraka na neema, na hukumu Yake na adabu imenilinda na kunitakasa. Kama singeadibiwa na kuhukumiwa na Mungu, na kama maneno makali ya Mungu hayangekuja juu yangu, singalimjua Mungu, ama kuokolewa. Leo, naona, kama kiumbe, kwamba mtu hafurahii tu vitu vilivyoumbwa na Muumba, lakini pia, la maana sana ni kwamba viumbe vyote watafurahia haki ya tabia ya Mungu, na kufurahia hukumu Yake ya haki, kwa sababu tabia ya Mungu ina umuhimu katika furaha ya Mwanadamu. Kama kiumbe ambaye amepotoshwa na Shetani, kila mmoja anafaa kufurahia tabia ya haki ya Mungu. Katika tabia Yake ya haki, kuna adabu na hukumu, na pia, kuna upendo mkuu. Ingawa sina uwezo wa kupata kwa kikamilifu upendo wote wa Mungu leo, nimekuwa na bahati nzuri ya kuuona, na katika haya, nimebarikiwa.” Hii ndio njia ambayo wale waliofanywa wakamilifu hutembea na maarifa wanayoongelea. Watu hao wanafanana na Petro; wanao uzoefu sawa na wa Petro. Watu kama hao pia ndio wale ambao wamepokea maisha, na walio na ukweli. Mwanadamu akipitia haya mpaka mwisho, wakati wa hukumu ya Mungu kwa hakika ataweza kikamilifu kujitoa katika ushawishi wa Shetani, na atakuwa wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp