Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 518

Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu. Ingawa ni uamuzi wa watu kama hawa kumfuata Mungu, hawafaidi chochote. Wale wasiopata chochote kwenye mkondo huu ndio watakaotupiliwa mbali, na ni wale watu wanaofanya juhudi za chini zaidi. Haijalishi ni hatua gani ya kazi ya Mungu unayopitia, lazima uandamane na maono makuu. Bila maono kama haya, itakuwa vigumu kwako kukubali kila hatua ya kazi mpya, kwa maana mwanadamu hana uwezo wa kuwaza kuhusu kazi mpya ya Mungu, ni kuu kushinda mawazo ya mwanadamu. Kwa hivyo bila mchungaji kumlinda mwanadamu, bila mchungaji kushirikiana na mwanadamu kuhusu maono hayo, mwanadamu hana uwezo kukubali kazi hii mpya. Iwapo mwanadamu hawezi kupokea maono haya, basi hawezi kupata kazi mpya ya Mungu, na iwapo mwanadamu hawezi kutii kazi mpya ya Mungu, basi mwanadamu hana uwezo wa kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na hivyo ufahamu wake wa Mungu ni bure. Kabla mwanadamu atimilize maneno ya Mungu, lazima ayajue maneno ya Mungu, hivyo ni kusema, aelewe mapenzi ya Mungu; ni kwa njia hii tu ndiyo maneno ya Mungu yanaweza kutekelezwa kwa usahihi na kulingana na moyo wa Mungu. Hili lazima liwe na kila mmoja anayetafuta ukweli, na ndiyo njia ambayo lazima kila mmoja anayejaribu kumjua Mungu aipitie. Njia ya kuyajua maneno ya Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na pia njia ya kuijua kazi ya Mungu. Na hivyo, kujua maono hakuashirii tu kuujua ubinadamu wa Mungu mwenye mwili, lakini pia kunajumuisha kujua maneno na kazi ya Mungu. Kutokana na maneno ya Mungu wanadamu wanapata kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutokana na maneno ya Mungu wanapata kuelewa tabia ya Mungu na pia kujua kile Mungu alicho. Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. Iwapo unaamini kwa Mungu kwa ajili tu ya kuamini kwa Mungu, na huamini kwa Mungu kwa ajili ya kumjua Mungu, basi hakuna ukweli katika imani yako, na haiwezi kuwa safi—kuhusu hili hakuna tashwishi. Iwapo, wakati wa harakati anapopata kumuonja Mungu, mwanadamu anapata kumjua Mungu polepole, basi hatua kwa hatua tabia yake itabadilika pia, na imani yake itaongezeka kuwa ya kweli zaidi. Kwa njia hii, wakati mwanadamu anafaulu katika imani yake kwa Mungu, ataweza kumpata Mungu kwa ukamilifu. Mungu alijitoa pakubwa kuingia katika mwili mara ya pili na kufanya kazi Yake binafsi ili mwanadamu apate kumjua Yeye, na ili mwanadamu aweze kumwona. Kumjua Mungu ndiyo matokeo ya mwisho yanayofikiwa katika mwisho wa kazi ya Mungu; ndilo hitaji la mwisho la Mungu kwa mwanadamu. Anafanya hili kwa ajili ya ushuhuda Wake wa mwisho, na ili kwamba mwanadamu mwishowe na kwa kikamilifu aweze kumgeukia Yeye. Mwanadamu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kumjua Mungu, na ili ampende Mungu lazima amjue Mungu. Haijalishi vile anavyotafuta, au kile anachotafuta kupata, lazima aweze kupata ufahamu wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumridhisha Mungu. Ni kwa kumjua Mungu tu ndio mwanadamu anaweza kumwamini Mungu kwa ukweli, na ni kwa kumjua Mungu tu ndio anaweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Wale wasiomjua Mungu hawataweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Kumjua Mungu kunahusisha kujua tabia ya Mungu, kuelewa mapenzi ya Mungu, na kujua kile Mungu alicho. Na haijalishi ni kipengee gani cha kumjua Mungu, kila mojawapo kinamhitaji mwanadamu alipe gharama, na kinahitaji nia ya kutii, ambapo bila hivi hakuna atakayeweza kufuata mpaka mwisho. Kazi ya Mungu hailingani na mawazo ya mwanadamu hata kidogo, tabia ya Mungu na kile Mungu alicho ni vitu vigumu sana kwa mwanadamu kufahamu, na yote Anayosema na kufanya Mungu ni makuu sana yasiyoeleweka na mwanadamu; iwapo mwanadamu anatamani kumfuata Mungu, na hana nia ya kumtii Mungu, basi mwanadamu hatafaidi chochote. Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, Mungu Amefanya kazi nyingi ambayo haieleweki na mwanadamu na ambayo mwanadamu amepata ugumu kuikubali, na Mungu amesema mengi yanayofanya mawazo ya mwanadamu magumu kupona. Ilhali Hajawahi kukomesha kazi Yake kwa sababu mwanadamu ana ugumu mwingi; Ameendelea kufanya kazi na kuzungumza, na hata ingawa idadi kubwa ya “wanajeshi” wameangamia njiani, Yeye bado Anaendelea na kazi Yake, na bado anateua kundi baada ya kundi la watu walio tayari kukubali kazi Yake mpya. Yeye hawahurumii wale “mashujaa” walioangamia, na badala yake anawathamini wale wanaoikubali kazi Yake mpya na maneno. Lakini ni kwa sababu gani ndiyo Anafanya kazi kwa njia hii, hatua kwa hatua? Ni kwa nini Yeye kila mara huwaondoa na kuchagua watu wengine? Ni kwa nini Yeye hutumia mbinu za aina hii kila mara? Kusudi la kazi Yake ni ile wanadamu wapate kumjua, na ili waweze kutwaliwa na Yeye. Kanuni ya kazi Yake ni kufanya kazi kwa wale wanaoweza kutii kazi Anayofanya leo, na sio kufanya kazi kwa wale wanaotii kazi Yake ya zamani, na wanaipinga kazi Yake ya leo. Hii ndiyo sababu hasa Amewafuta na kuwaangamiza watu wengi.

Matokeo ya funzo la kumjua Mungu haliwezi kufikiwa kwa siku moja au mbili: Mwanadamu lazima apate uzoefu wa matukio mengi, apitie mateso, na awe na utiifu wa kweli. Kwanza kabisa, anza na kazi na maneno ya Mungu. Lazima uelewe kumjua Mungu kunajumuisha nini, jinsi ya kupata maarifa kuhusu Mungu, na jinsi ya kumwona Mungu katika matukio yako. Hili ndilo kila mtu lazima afanye wakiwa bado hawajamjua Mungu. Hakuna anayeweza kushika kazi na maneno ya Mungu kwa mara moja, na hakuna anayeweza kupata maarifa ya ukamilifu wa Mungu kwa muda mfupi. Kinachohitajika ni harakati mahususi ya matukio, na bila haya hakuna mwanadamu atakayeweza kumjua au kumfuata Mungu kwa kweli. Mungu Anapofanya kazi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kumjua. Zaidi kazi ya Mungu inavyokinzana na mawazo ya mwanadamu, ndivyo ufahamu wa mwanadamu Kwake unavyofanywa upia na wenye kina kirefu. Iwapo kazi ya Mungu ingebaki milele bila kubadilika, basi mwanadamu angekuwa tu na ufahamu mdogo wa Mungu. Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa, lazima mjue kwa ukamilifu maono ya vitu ambavyo Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria, Alichofanya wakati wa Enzi ya Neema, na kile Afanyacho wakati wa Enzi ya Ufalme. Lazima mjue kazi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp