Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 448

Mwanadamu kufanya wajibu wake ni, kwa uhakika, kutimiza yote yaliyo ya asili yake, yaani, yale yawezekanayo kwa mwanadamu. Hapo ndipo wajibu wake hutimizika. Dosari za mwanadamu wakati wa kumhudumia Mungu, hupunguzwa taratibu jinsi uzoefu wake uongezekapo na namna ya uzoefu wake wa hukumu; hayazuii au kuathiri wajibu wa mwanadamu. Wanaoacha kutoa huduma au kuzalisha na kurudi nyuma kwa kuogopa makosa yanayoweza kuwepo katika huduma ndio waoga zaidi miongoni mwa wanadamu wote. Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake asili, na badala yake huzembea na kupitia katika mizunguko, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani? Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake. Mwanadamu akipoteza kile ambacho chaweza kutimizwa kiasili, hawezi kamwe kuitwa mwanadamu, na hafai kusimama kama kiumbe au kuja mbele za Mungu na kumtolea huduma. Aidha, hafai kupokea neema ya Mungu au kutunzwa, kulindwa na kukamilishwa na Mungu. Wengi waliopoteza imani ya Mungu hatimaye hupoteza neema Yake. Si kwamba wanachukia makosa yao tu bali pia hueneza wazo kuwa njia ya Mungu si sahihi. Na wale waasi hupinga hata uwepo wa Mungu; itakuwaje watu wenye uasi kama huo waendelee kupata neema ya Mungu? Wanadamu walioshindwa kutekeleza wajibu wao wameasi sana dhidi ya Mungu na wana mengi ya kumshukuria, lakini wanageuka na kumkong’ota Mungu kwamba ni mkosaji. Je, mwanadamu kama huyo anastahili vipi kufanywa mkamilifu? Je, si huyu ni mmoja wa wale watakaoondolewa na kuadhibiwa? Mwanadamu asiyefanya wajibu wake mbele za Mungu tayari ana hatia ya makosa mazito sana ambayo hata kifo si adhabu stahili, ila bado mwanadamu ana ufidhuli wa kubishana na Mungu na kujilinganisha Naye. Pana faida gani kumkamilisha mwanadamu sampuli hiyo? Ikiwa mwanadamu ameshindwa kutekeleza wajibu wake, anafaa kujihisi mwenye hatia na mdeni; anapaswa kuudharau udhaifu wake na kukosa umuhimu, uasi na uharibifu wake, na zaidi ya hayo, anafaa kujitolea maisha na damu sadaka kwa ajili ya Mungu. Hapo ndipo tu atakapokuwa kiumbe ampendaye Mungu kwa dhati, na ni mwanadamu kama huyu anayestahili baraka na ahadi za Mungu, na kufanywa mkamilifu na Mungu. Na wengi wenu je? Mnamchukuliaje Mungu aishiye miongoni mwenu? Mmefanyaje majukumu yenu mbele Zake? Je, mmefanya yote mliyoitwa kufanya, hata kwa gharama ya maisha yenu? Mmetoa sadaka gani? Je, si mmepokea mengi kutoka Kwangu? Mnaweza kuonyesha tofauti? Mna uaminifu kiasi gani Kwangu? Mmenitolea huduma vipi? Na kuhusu yote Niliyowapa na kuwafanyia je? Je, mmeyazingatia yote? Je, mmeyatathimini haya yote kwa dhamiri yoyote ndogo mliyo nayo? Maneno na matendo yenu yanawezaje kuwa ya kustahili? Je, yawezekana hizo sadaka zenu kidogo zinalingana na yote Niliyowapa? Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna hisia mbovu kunihusu na mko shingo upande. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee. Au sivyo? Hamjui kwamba hamjatimiza wajibu wa kiumbe kamwe? Mnawezaje kuitwa kiumbe? Je, hamtambui wazi mnachopaswa kuonyesha katika maisha yenu? Mmeshindwa kutimiza wajibu wenu, ila mnataka mpate huruma na neema tele za Mungu. Neema hiyo haijaandaliwa kwa wasio na thamani na wa hali duni kama nyinyi, bali kwa wale ambao hawaombi kitu ila wanatoa kwa moyo wa dhati. Wanadamu kama nyinyi, watu duni, hawastahili kufurahikia neema ya mbinguni. Ni ugumu tu wa maisha na adhabu isiyokoma vitayaandama maisha yenu! Ikiwa hamwezi kuwa waaminifu Kwangu, majaaliwa yenu yatakuwa matatizo. Ikiwa hamwezi kuyawajibikia maneno na kazi Yangu, malipo yenu yatakuwa adhabu. Kamwe hamtapata neema, baraka na maisha ya kupendeza katika ufalme. Hii ndiyo hatima na matokeo mnayostahili kupata kwa kujitakia!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp