Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 404

Wakati Mungu anapoongea, unafaa kupokea mara moja maneno Yake na kuyala. Haijalishi ni kiwango kipi unachokielewa, shikilia mtazamo kwamba uzingatie tu kulila, kulijua, na kulitia katika matendo neno Lake. Hili ni jambo unalofaa kufanya. Usiwe na wasiwasi kuhusu ni kiwango kipi cha ukubwa ambacho kimo chako kinaweza kuwa; zingatia tu katika kula neno Lake. Hivi ndivyo binadamu anavyofaa kushirikiana. Maisha yako ya kiroho kimsingi ni kuingia katika uhalisia pale ambapo unakula na kunywa neno la Mungu na kulitia katika matendo. Hufai kuzingatia jambo lolote jingine. Viongozi wa kanisa wanafaa kuwaongoza ndugu wote katika namna ya kula na kunywa neno la Mungu. Huu ndio wajibu wa viongozi wote wa kanisa. Wawe wachanga au wazee, wote wanafaa kuchukulia kula na kunywa maneno ya Mungu kwa umuhimu na kuyatia maneno Yake katika mioyo yao. Ukiingia katika uhalisia huu, utakuwa umeingia katika Enzi ya Ufalme. Siku hizi, wengi huhisi kwamba hawawezi kuishi bila kula na kunywa neno la Mungu, na haijalishi ni wakati gani, wanahisi kwamba neno Lake ni geni Kisha ndipo binadamu anapoanza kuwa katika njia sahihi. Mungu hutumia neno Lake katika kufanya kazi na kumruzuku binadamu. Wakati wote wanapotamani na kuwa na kiu ya neno la Mungu, wataingia katika ulimwengu wa neno Lake.

Mungu ameongea pakubwa. Unayo maarifa kiasi kipi kuyahusu? Umeingia hadi kiwango kipi? Kama kiongozi wa kanisa bado hajawaongoza ndugu katika uhalisia wa neno la Mungu, basi wamekuwa wazembe katika wajibu wao na kushindwa kukamilisha majukumu yao! Haijalishi ni kina kipi cha kula na kunywa kwako kwa neno, au ni kiasi kipi unachoweza kupokea, lazima ujue namna ya kula na kunywa neno Lake; lazima uchukulie neno Lake kwa umuhimu na uelewe umuhimu na haja ya kushiriki kama huko. Mungu ameongea sana. Kama hutakula na kunywa neno Lake, wala hulitafuti ama kulitia neno Lake katika matendo, huwezi kuchukuliwa kama unayemsadiki Mungu. Kwa sababu unamsadiki Mungu, lazima ule na kunywa neno Lake, upitie neno Lake, na uishi kwa kudhihirisha neno Lake. Hivi tu ndivyo unavyomsadiki Mungu! Kama unasema umemsadiki Mungu ilhali huwezi kuongea maneno Yake yoyote au kuyatia katika matendo, huchukuliwi kuwa unamsadiki Mungu. Hivi ni “kuutafuta mkate ili kuikabili njaa.” Tukizungumzia tu ushuhuda mdogo mdogo, masuala ya kipuzi na masuala ya juujuu, na kutokuwa na hata kiwango kidogo cha uhalisia hakumaanishi kusadiki Mungu. Hivyo basi, bado hujang’amua njia sahihi ya kumsadiki Mungu. Kwa nini ule na kunywa zaidi ya maneno ya Mungu? Je, inadhaniwa kuwa imani usipokula na kunywa maneno Yake na kutafuta tu kupaa mbinguni? Ni nini hatua ya kwanza kwake yule anayesadiki neno Lake Mungu? Ni katika njia gani Mungu humfanya binadamu kuwa mtimilifu? Unaweza kufanywa kuwa mtimilifu bila ya kula na kunywa neno la Mungu? Unaweza kuchukuliwa kuwa mtu wa ufalme bila ya neno la Mungu kuwa uhalisia wako? Ni nini hasa kusadiki Mungu? Wanaomwamini Mungu wanafaa kumiliki tabia nzuri kwa nje, angalau, na kilicho na umuhimu mkubwa zaidi ni kuwa na neno la Mungu. Haijalishi ni nini, huwezi kuligeukia neno la Mungu. Maarifa yako katika Mungu na kukamilishwa kwa mapenzi Yake vyote vinatimizwa kupitia kwa neno Lake. Kila taifa, dhehebu, dini, na sekta zitaweza kushindwa kupitia kwa neno kwenye siku za usoni. Mungu ataongea moja kwa moja, na watu wote watashikilia neno la Mungu katika mikono yao; kupitia haya watu watafanywa kuwa watimilifu. Neno la Mungu limeenea kotekote: Watu huongelea neno la Mungu na kutenda kulingana na neno la Mungu, huku likiwa limehifadhiwa ndani bado huwa ni neno la Mungu. Kwa ndani na hata kwa nje, wanarowekwa katika neno la Mungu, na hivyo basi wanafanywa kuwa watimilifu. Wale wanaokamilisha mapenzi ya Mungu na wanaweza kumshuhudia Yeye ndio wale walio na neno la Mungu kama uhalisi.

Kuingia katika Enzi ya Neno, yaani, Enzi ya Ufalme wa Milenia, ndiyo kazi ambayo inakamilishwa sasa. Kuanzia sasa, fanya mazoezi ya kushiriki kuhusu neno la Mungu. Ni kupitia tu kula na kunywa neno Lake na kulipitia ndipo unapoweza kuonyesha neno la Mungu. Ni kupitia tu maneno yako ya uzoefu ndipo wengine wanapoweza kushawishika na wewe. Kama huna neno la Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuongea neno la Mungu. Kama huwezi, hii yaonyesha kwamba Roho Mtakatifu bado hajakufanyia kazi na ungali bado hujafanywa kuwa mtimilifu. Huu ndio umuhimu wa neno la Mungu. Je, unao moyo ulio na kiu ya neno la Mungu? Wale walio na kiu ya neno la Mungu huwa na kiu ya ukweli, na binadamu kama hao tu ndio wanaobarikiwa na Mungu. Katika siku za usoni, kunayo maneno mengi zaidi ambayo Mungu atatamka kwenye madhehebu na dini zote. Kwanza anaongea na kutoa sauti Yake miongoni mwenu na kuwafanya kuwa kamili kabla ya kusonga mbele na kuongea na kutoa sauti Yake kwa Mataifa na kuwashinda. Kupitia kwa neno, wote wataweza kushawishika kwa uaminifu na kwa kikamilifu. Kupitia neno la Mungu na ufunuo Wake, tabia iliyopotoka ya binadamu imepungua. Wote wanao wajihi wa binadamu, na tabia asi ya binadamu imelegea vilevile. Neno linafanya kazi kwa binadamu kupitia kwa mamlaka na linamshinda binadamu ndani ya nuru ya Mungu. Kazi ambayo Mungu atafanya katika enzi ya sasa, pamoja na jambo kuu katika kazi Yake vyote vinaweza kupatikana ndani ya neno Lake. Kama hulisomi neno Lake, hutaelewa chochote. Kupitia kula na kunywa kwako mwenyewe kwa neno Lake, kuwa na ushirika na ndugu, na kile utakachopitia kwa uhalisi, maarifa yako ya neno la Mungu yatakuwa pana. Na hapo tu ndipo unapoweza kuishi kwa kulidhihirisha kwa kweli katika uhalisia.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp