Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 356

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako na kila kitu ambacho mwenye Uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya uchungu isiyokuwa na mwisho, pasipo uwezo wa kukuokoa, hukuna matumaini ya kuishi, umeachwa ukipambana na kuzunguka zunguka tu.… Tokea wakati huo, huwezi kuepuka kuteswa na yule mwovu, uko mbali na baraka za mwenye Uweza, mbali na kukimu kwa mwenye Uweza, na unaenenda katika njia ambayo huwezi kurejea nyuma tena. Kuitwa mara milioni hakutaweza kuusisimua moyo wako na roho yako. Umelala fofofo mikononi mwa yule mwovu, aliyekushawishi katika ulimwengu usio na kikomo, pasipo mwelekeo, bila alama za kukuongoza katika njia. Tokea hapo, umepoteza utakaso wako wa kwanza, hali yako ya kutokuwa na hatia, na kuanza kuukimbia uso wa mwenye Uweza. Yule mwovu anauendesha moyo wako katika kila jambo na anakuwa maisha yako. Humwogopi tena, humwepuki tena, humshuku tena. Badala yake, unamchukulia kama Mungu aliye moyoni mwako. Unaanza kumtunza, na kumwabudu, kuwa msiotengana kama kivuli chake, na kujipa mmoja kwa mwingine katika uzima na mauti. Hujui lolote kabisa kuhusu asili yako, kwa nini unaishi, au kwa nini unakufa. Unamtazama mwenye Uweza kama mgeni; hujui mwanzo Wake, sembuse yale yote Aliyokutendea. Kila kitu kutoka Kwake kimekuwa cha kukuchukiza. Huyatunzi wala kujua thamani yake. Unatembea na yule mwovu, tokea siku ile ulipoanza kupokea chakula kutoka kwa mwenye Uweza. Wewe na yule mwovu mmepitia maelefu ya miaka ya dhoruba na tufani. Wewe pamoja naye, mnampinga Mungu, ambaye alikuwa chanzo cha maisha yako. Hutubu, sembuse kujua kwamba umefikia hatua ya maangamizi. Unasahau kwamba yule mwovu amekujaribu, amekutesa; unasahau asili yako. Hivyo tu, yule mwovu amekuwa akikuharibu hatua baada ya hatua, hata mpaka sasa. Moyo wako na roho yako vimekufa ganzi na vimeoza. Hulalamiki tena juu ya dhiki ya dunia, huamini tena kwamba dunia si ya haki. Hata hujali tena juu ya uwepo wa mwenye Uweza. Hii ni kwa sababu umemchukulia mwovu kuwa baba yako wa kweli, na huwezi tena kutengana naye. Hii ndiyo siri iliyo moyoni mwako.

Alfajiri inapofika, nyota ya asubuhi inaonekana mashariki. Ni nyota ambayo haijawahi kuwepo hapo awali. Inaliangaza anga lililo bado na nyota na kuwasha nuru iliyozimwa katika mioyo ya watu. Watu si wapweke tena, kwa sababu ya nuru hii, nuru inayokuangazia wewe na watu wengine. Lakini ni wewe tu unayebaki ukiwa umelala fofofo katika usiku wa giza. Huwezi kuisika sauti, wala kuiona nuru, huwezi kutambua ujio wa mbingu mpya na nchi mpya, enzi mpya. Kwa sababu baba yako anakwambia, “Mwanangu, usiamke, bado ni mapema. Nje kuna baridi, kaa ndani, usije ukachomwa macho yako kwa mkuki na upanga.” Unaamini katika ushawishi wa baba yako pekee, maana unaamini kwamba baba yako yuko sahihi kwa sababu baba ana umri mkubwa kuliko wewe, na kwamba baba anakupenda kweli. Ushawishi na upendo wa namna hiyo vinakufanya usiamini tena hekaya kwamba kuna nuru ulimwenguni, kutojali tena kama ulimwengu una ukweli. Huthubutu tena kutumainia ukombozi kutoka kwa mwenye Uweza. Umeridhika kuwa katika hali hiyo, hutumainii tena ujio wa nuru, na hutazamii tena kuja kwa mwenye Uweza anayejulikana. Machoni pako, yote yaliyo mazuri hayawezi kufufuliwa, wala kuendelea kuwepo. Machoni pako, kesho na siku za baadaye za binadamu zinatoweka na kuangamia. Unayashika sana mavazi ya baba yako, uko tayari kuteseka pamoja naye, ukiogopa kumpoteza msafiri mwenzako na mwelekeo wa safari yako ndefu. Ulimwengu huu mkubwa na wenye giza umewafanya wengi wenu, kuwa majasiri na watu wa kujitahidi sana katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ulimwengu huu. Umewafanya “mashujaa” wengi ambao hawaogopi kifo kabisa. Zaidi ya hayo, umesababisha makundi ya watu waliokufa ganzi na wanadamu walioduwaa ambao hawaelewi makusudi ya kuumbwa kwao. Macho ya mwenye Uweza huwaangazia wanadamu walio katika mateso makali, akisikia vilio vya wale wanaoteseka, akiona kutokuwa na aibu kwa wale wanaoteseka, na akihisi hali ya mwanadamu ya kuwa bila msaada na hofu ya wanadamu waliopoteza wokovu. Wanadamu wanakataa utunzaji Wake, wanakwenda katika njia zao wenyewe, na wanakwepa macho Yake yanayowatazama. Wanaona ni afadhali waonje uchungu wa kilindi cha bahari, pamoja na adui. Kutanafusi kwa mwenye Uweza hakuwezi kusikika tena. Mikono ya mwenye Uweza haiko tayari kuwagusa tena wanadamu wenye kuhuzunisha. Anarudia kazi Yake, akirejesha na kupoteza, mara kwa mara. Tokea wakati huo, Yeye anachoka, na kujihisi mchovu, hivyo Anasitisha kazi Anayoifanya, na Hazungukizunguki kati ya watu.… Watu hawajui kabisa kuhusu mabadiliko haya, hawaelewi kuhusu kuja na kuondoka, huzuni na masikitiko ya mwenye Uweza.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Have You Heard the Almighty Sighing?

I

A morning star at dawn rises in the East. It’s a new star, lighting up the silent sky, igniting faded light in people’s hearts. So they’re no longer lonely or in the dark. But only you lie asleep in the night, you can’t hear the sound or see the light, unable to notice something’s beginning— that there’s a new age, heaven and earth coming. For your “father” says it’s early and cold outside, if you go out there, the sword will pierce your eyes. You believe what your father says to you, since he’s older and truly loves you.

II

Such love and advice make you deny there’s light. You don’t care whether there’s truth in the world. You don’t hope for the Almighty to come save you, or hope to see the light, content with status quo. In your eyes, beautiful things can’t exist; man’s tomorrow and future is doomed, disappears. You hold father tight, glad to suffer with him, fearing you’ll lose your journey’s partner and direction. This vast hazy world has made many like you, unflinching, dauntless in their different roles. It formed many “warriors” who don’t fear death, many numb humans who don’t know why they were made.

III

God looks at the very afflicted mankind. He hears the wailing of suffering ones; He sees how shameless they seem, feels their helplessness, feels their terror at having lost salvation. Man rejects His care, His watching, goes their way. They’d rather taste the bitter sea with the foe. God’s sigh can’t be heard, His hands now won’t touch man. He regains and loses time and time again. He then grows weary and stops His work. He no longer wanders among the people. They can’t see these changes, His coming and going, or His deep sorrow; God’s sighing, God’s sighing.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp