Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 585

Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, wala si hatua ya kuanza kumshughulikia mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo yote ya kila mtu katika kitabu Changu, na vilevile njia walizozifuata wakiwa wafuasi Wangu, sifa zao asilia, na utendakazi wao wa mwisho. Kwa njia hii, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu na kila mmoja atakuwa wa aina yake kama Nilivyowaweka. Ninaamua mwisho wa kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso au kwa kiwango cha chini sana, kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli ndani yake. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawatimizi mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na malipo kwa vitendo vyao viovu. Sijafanya mabadiliko yoyote katika mpango Wangu tangu kuuanzisha. Ni vile tu, kwa binadamu, wale ambao kwao Mimi huelekeza maneno Yangu wamepungua kwa idadi, kadhalika wale Ninaowakubali kwa dhati. Hata hivyo, Ninasisitiza kwamba mpango Wangu haujawahi kubadilika; badala yake, ni imani na upendo wa mwanadamu ambao hubadilika daima, kufifia daima, kiasi kwamba upo uwezekano wa kila mwanadamu kubadilika kutoka kujipendekeza Kwangu hadi kufikia hali ya kunidharau au hata kunitoa maishani mwake kabisa. Mtazamo Wangu kwenu hautakuwa baridi wala moto hadi pale Nitakapochukizwa sana na hatimaye kuwaadhibu. Hata hivyo, katika siku ya adhabu, bado Nitawaona lakini nyinyi hamtaweza kuniona. Tayari Ninahisi kuwa maisha miongoni mwenu ni ya kuchosha na kuchusha, kwa hivyo ni wazi kuwa, Nimechagua mazingira tofauti Yangu kuishi ili Niepuke maneno yenu mabovu na tabia zenu mbaya ili muache kunitweza na kunifanya mjinga. Kabla Sijawaacha, Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na kweli. Badala yake, mnafaa kufanya yale yote ambayo yanawapendeza watu wote na yana manufaa kwa binadamu wote na pia kwa mwisho wa safari yenu wenyewe, la sivyo, yule atakayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

God Decides Man’s End Based on Whether They Possess the Truth

I

It’s time for God to determine the ending for each person, not the stage at which He began to work man. God writes into His book every word and action of each person, He records them one by one. God decides the destination of everyone not based on age, rank or sufferings, nor the degree to which they invite pity, but according only to whether they possess truth.

II

He notes their path in following Him, their inherent attributes and final performance. In this way no man shall escape the hand of God. All shall be with their kind as He assigns. God decides the destination of everyone not based on age, rank or sufferings, nor the degree to which they invite pity, but according only to whether they possess truth.

III

Those who do not follow God’s will will be punished. This is a fact no one can change. So, all who are punished are so for the righteousness of God, as retribution for countless evil acts. God decides the destination of everyone not based on age, rank or sufferings, nor the degree to which they invite pity, but according only to whether they possess truth, whoa, possess truth.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp