Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili)

Mwanzoni, wakati Yesu alikuwa bado hajafanya rasmi huduma Yake, kama wanafunzi waliomfuata, wakati mwingine pia Yeye alihudhuria mikutano, na kuimba tenzi, Akasifu, na kusoma Agano la Kale kwa hekalu. Baada Yeye kubatizwa na kupanda, Roho alishuka rasmi juu yake na kuanza kufanya kazi, Akifichua utambulisho Wake na huduma Aliyokuwa afanye. Kabla ya haya, hakuna aliyejua utambulisho Wake, na mbali na Maria, hata Yohana hakujua. Yesu alikuwa 29 Alipobatizwa. Baada ya ubatizo wake kukamilika, mbingu zilifunguliwa, na sauti ikasema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Baada ya Yesu kubatizwa, Roho Mtakatifu alianza kumshuhudia kwa njia hii. Kabla ya kubatizwa Akiwa na umri wa 29, Alikuwa ameishi maisha ya mtu wa kawaida, kula wakati Alipotakiwa kula, kulala na kuvaa kawaida, na hakuna chochote kumhusu kilikuwa tofauti. Bila shaka hii ilikuwa tu kwa nyama ya macho ya mwanadamu. Wakati mwingine Alikuwa mnyonge sana, na wakati mwingine Hakuweza kupambanua mambo, kama tu ilivyoandikwa kwa Biblia “Akili Yake ilikua pamoja na umri Wake.” Haya maneno yanaonyesha tu kwamba Alikuwa na ubinadamu sawa na kawaida, na Hakuwa hasa na tofauti na watu wengine wa kawaida. Alikuwa pia amelelewa kama mtu wa kawaida, na hakuwa na chochote maalum kumhusu. Hata hivyo Alikuwa chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu. Baada ya kubatizwa, Alianza kujaribiwa, baada yake Akaanza kufanya Huduma Yake na kufanya kazi, na Alimiliki nguvu, na hekima, na mamlaka. Hii si kusema kwamba Roho Mtakatifu hakufanya kazi ndani Yake, ama hakuwa ndani Yake kabla ya ubatizo Wake. Kabla ya ubatizo Wake Roho Mtakatifu pia aliishi ndani Yake lakini Hakuwa ameanza rasmi kazi Yake, kwani kuna mipaka ya wakati Mungu afanyapo kazi Yake, na zaidi ya hayo, watu wa kawaida wana mwendo kawaida wa kukua. Roho Mtakatifu alikuwa daima anaishi ndani Yake, Yesu alipozaliwa, Alikuwa tofauti na wengine, na nyota ya asubuhi ilionekana; kabla Yeye kuzaliwa, malaika alimtokea Yusufu kwa ndoto na kumweleza kuwa Maria angejifungua mtoto wa kiume, na kwamba mtoto huyo alipatwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Haikuwa tu baada ya kubatizwa kwa Yesu, iliyokuwa wakati Roho Mtakatifu pia alianza rasmi kazi Yake, ndipo Roho Mtakatifu alishuka kama njiwa juu yake. Huo msemo kwamba Roho Mtakatifu alishuka kama njiwa juu yake inamaanisha kuanza rasmi kwa huduma Yake. Roho wa Mungu alikuwa ndani yake mbeleni, lakini Hakuwa ameanza kufanya kazi, kwani wakati hukuwa umefika, na Roho hakuanza kazi upesi. Roho alimshuhudia kupitia ubatizo. Alipotoka nje ya maji, Roho alianza rasmi kufanya kazi ndani Yake, iliyoashiria kuwa Mungu wa mwili alikuwa ameanza kutimiza huduma Yake, na alikuwa ameanza kazi ya ukombozi, hiyo ni, Enzi ya Neema ilikuwa imeanza rasmi. Na hivyo, kuna wakati wa kazi Ya Mungu, bila kujali kazi Anayoifanya. Baada ya ubatizo Wake, hakukuwa na mabadiliko fulani kwa Yesu; Alikuwa bado ndani ya mwili wake kawaida. Ni kwamba tu alianza kazi Yake na kufichua utambulisho wake, na Alijawa na mamlaka na nguvu. Kwa swala hili, Alikuwa tofauti kuliko awali. Utambulisho wake ulikuwa tofauti, kusema kwamba kulikuwa na mabadiliko muhimu kwa hadhi Yake; huu ulikuwa ushahidi wa Roho Mtakatifu, na haikuwa kazi iliyofanywa na mwanadamu. Mwanzoni, watu hawakujua, na walikuja kujua kidogo wakati Roho Mtakatifu alimshuhudia Yesu kwa njia hiyo. Kama Yesu angekuwa amefanya kazi kubwa kabla ya Roho Mtakatifu kumshuhudia, lakini bila shuhuda ya Mungu Mwenyewe, basi bila kujali jinsi kazi Yake ilivyokuwa kubwa, watu hawangejua kuhusu utambulisho Wake, kwani jicho la mwanadamu halingekuwa na uwezo wa kuiona. Bila hatua ya ushuhuda wa Roho Mtakatifu, hakuna ambaye angemtambua kama Mungu wa mwili. Kama, baada ya Roho Mtakatifu kumshuhudia, Yesu angeendelea kufanya kazi kwa njia hiyo hiyo, bila tofauti yoyote, basi haingekuwa na athari hiyo. Na hii hasa imeonyeshwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu pia. Baada ya Roho Mtakatifu kuwa na ushuhuda, Roho Mtakatifu alipaswa kujionyesha Mwenyewe, ili uweze kuona wazi kuwa Alikuwa Mungu, kwamba kulikuwa na Roho wa Mungu ndani Yake; ushuhuda wa Mungu hukukosea, na hii ingethibitisha kwamba ushuhuda Wake ulikuwa sahihi. Iwapo kazi ya awali na baadaye ingekuwa sawa, basi huduma Yake ya mwili, na kazi ya Roho Mtakatifu, haingekuwa maarufu, na hivyo mwanadamu hangekuwa na uwezo wa kutambua kazi ya Roho Mtakatifu, kwani hakuwa na tofauti wazi. Baada ya kuwa na ushuhuda, Roho Mtakatifu alilazimika kutetea huu ushuhuda, na hivyo ilimlazimu kuonyesha hekima na mamlaka Yake ndani ya Yesu, ambayo ilikuwa tofauti na wakati wa kale. Bila shaka, hii haikuwa athari ya ubatizo; ubatizo ni sherehe tu, ni kwamba tu ubatizo ulikuwa njia ya kuonyesha kwamba ulikuwa wakati wa kufanya huduma Yake. Kazi hiyo ilikuwa ya kufanya wazi nguvu kubwa za Mungu, kufanya wazi ushuhuda wa Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu angechukua jukumu la ushuhuda huu mpaka mwisho. Kabla ya kufanya huduma Yake, Yesu pia alisikiliza mahubiri, Alihubiri na kueneza injili katika maeneo mbalimbali. Hakufanya kazi yoyote kubwa kwa sababu muda bado hukuwa umewadia ili Afanye huduma Yake, na pia kwa sababu Mungu Mwenyewe alijificha kwa unyenyekevu ndani ya mwili, na Hakufanya kazi yoyote hadi wakati ulipofika. Hakufanya kazi kabla ya ubatizo kwa sababu mbili: Kwanza, kwa sababu Roho Mtakatifu hakuwa ameshuka rasmi juu Yake kufanya kazi (ndiyo kusema, Roho Mtakatifu hakuwa amempea Yesu nguvu na mamlaka ya kufanya kazi kama hii), na hata kama Angekuwa anajua utambulisho Wake Mwenyewe, Yesu hangeweza kufanya kazi Aliyonuia kufanya baadaye, na ingembidi kusubiri hadi siku Yake ya ubatizo. Huu ulikuwa wakati wa Mungu, na hakuna ambaye angeweza kuikiuka, hata Yesu Mwenyewe; Yesu Mwenyewe hangeweza kuipinga kazi Yake Mwenyewe. Bila shaka, huu ulikuwa unyenyekevu wa Mungu, na pia sheria ya kazi ya Mungu; Kama Roho wa Mungu hangefanya kazi, hakuna ambaye angeweza kufanya kazi Yake. Pili, kabla Yeye kubatizwa, Alikuwa tu mwanadamu wa kawaida sana, bila tofauti na watu wa kawaida; hiki ni kipengele kimoja cha jinsi Mungu wa mwili alikuwa kawaida. Mungu wa mwili hakuenda kinyume na mipango ya Roho wa Mungu; Alifanya kazi kwa njia taratibu na kawaida. Ilikuwa tu baada ya kubatizwa ndipo kazi Yake ilikuwa na nguvu na mamlaka. Ambayo ni kusema, hata kama alikuwa Mungu wa mwili, Hakufanya matendo yasiyo ya kawaida, na Alikua kwa njia sawa na watu wa kawaida. Kama Yesu alikuwa ashaujua utambulisho wake, Alikuwa amefanya kazi kubwa eneo yote kabla ya ubatizo Wake, na Alikuwa tofauti na watu wa kawaida, kujionyesha Mwenyewe kuwa ajabu, basi haingewezekana tu kwa Yohana kufanya kazi yake, lakini pia hakungekuwa na njia ya Mungu kuanza hatua ifuatayo ya kazi Yake. Na hivyo hii ingethibitisha kwamba alichofanya Mungu kilienda mrama, na kwa mwanadamu, ingeonekana kuwa Roho wa Mungu na Mungu wa mwili hawakutoka mahali moja. Hivyo, kazi ya Yesu iliyorekodiwa kwa Biblia ni kazi iliyofanywa baada ya Yeye kubatizwa, kazi iliyofanywa katika kipindi cha miaka mitatu. Biblia haijarekodi Alichofanya kabla ya kubatizwa kwa sababu Hakufanya kazi hii kabla ya kubatizwa. Alikuwa tu mtu wa kawaida, na Aliwakilisha mtu wa kawaida; kabla ya Yesu kuanza kufanya huduma Yake, Hakuwa na tofauti na watu wa kawaida, na wengine hawangeona tofauti yoyote na yeye. Ilikuwa tu baada ya Yeye kufikia 29 ndipo Yesu alijua kwamba Alikuwa amekuja kukamilisha hatua ya kazi ya Mungu; kabla; Yeye Mwenyewe hakujua, kwani kazi Aliyoifanya Mungu ilikuwa kawaida. Alipohudhuria mkutano kwa sinagogi Akiwa na umri wa miaka kumi na miwili, Maria alikuwa akimtafuta, na alisema tu sentensi moja kwa namna sawa na mtoto mwingine yeyote: “Mama! Hujui kwamba ni lazima Niyaweke mapenzi ya Baba Yangu juu ya mengine yote?” Bila shaka, kwa vile alitwawa mwili na tendo la Roho Mtakatifu, Yesu hangeweza kuwa maalum kwa namna fulani? Lakini umaalum Wake hukumaanisha hakuwa kawaida, ila tu kuwa Alimpenda Mungu zaidi ya mtoto mwingine mdogo. Ingawa Alionekana kama mwanadamu, kiini Chake bado kilikuwa maalum na tofauti na cha wengine. Lakini, ilikuwa tu baada ya ubatizo ndipo Alipohisi Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani Yake, ndipo Alipohisi kuwa Mungu Mwenyewe. Ni baada tu na Yeye kuhitimu miaka 33 ndipo Alitambua kweli kuwa Roho Mtakatifu alinuia kufanya kazi ya usulubisho kupitia kwake. Akiwa na umri wa miaka 32, Alikuja kujua baadhi ya ukweli wa ndani, kama tu ilivyoandikwa kwa Injili ya Mathayo: “Naye Simoni Petro akajibu na kusema, Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aishiye. … Kutoka wakati huo kuendelea Yesu alianza kuwaonyesha wanafunzi wake, jinsi ilivyompasa kwenda Yerusalemu, na kupitia mateso mengi ya wazee na makuhani wakuu na waandishi, na kufishwa, na afufuke tena siku ya tatu.” Hakujua awali kazi Aliyotakiwa kufanya, lakini kwa wakati maalum. Hakujua kwa kina punde tu Alipozaliwa; Roho Mtakatifu alifanya kazi polepole ndani Yake, na kulikuwa na mchakato wa kazi. Kama, hapo mwanzoni, Angejua kuwa yeye ni Mungu, na Kristo, na Mwana wa Adamu wa mwili, kwamba Alikuwa akamilishe kazi ya usulubisho, basi mbona Hakufanya kazi awali? Mbona tu baada ya kuwaeleza wanafunzi Wake kuhusu huduma Yake ndipo Yesu alipohisi huzuni, na kusali kwa bidii kwa ajili ya hii? Mbona Yohana alimfungulia njia na kumbatiza kabla ya Yeye kuelewa mambo mengi ambayo Hakuyaelewa? Kinachothibitishwa na hii ni kwamba ilikuwa kazi ya Mungu wa mwili, na hivyo ili aelewe, na kutimiza, kulikuwa na mwendo, kwani alikuwa Mungu wa mwili, na kazi Yake ilikuwa tofauti na ile iliyofanywa moja kwa moja na Roho.

Kila hatua ya kazi ya Mungu hufuata mkondo mmoja na sawa, na hivyo katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, kila hatua imefuatwa kwa karibu na ifuatayo, kutoka msingi wa dunia hadi leo. Kama hakungekuwa na mtu wa kupisha njia, hakungekuwa na mtu wa kuja baadaye; Kwani kuna wale wanaokuja baadaye, kuna wale wanaopisha njia. Kwa njia hii kazi imepitishwa chini, hatua kwa hatua. Hatua moja inafuata ingine, na bila mtu wa kufungua njia, haitawezekana kuanza kazi, na Mungu angekosa namna ya kupeleka kazi Yake mbele. Hakuna hatua inayopingana na nyingine, na kila hatua inafuata nyingine katika mlolongo kuunda mkondo; hii yote inafanywa na Roho Yule Yule. Lakini bila kujali iwapo mtu atafungua njia, ama kuendeleza kazi ya mwingine, hii haiamui utambulisho wake. Hii si sawa? Yohana aliifungua njia, na Yesu akaendeleza kazi yake, hivyo hii inathibitisha kwamba utambulisho wa Yesu ni chini kuliko wa Yohana? Yehova alifanya kazi Yake kabla Yesu, hivyo unaweza kusema kuwa Yehova ni mkubwa kumliko Yesu? Iwapo waliopasha njia ama kuendeleza kazi za wengine sio muhimu; kilicho muhimu ni kiini cha kazi zao, na utambulisho unaowakilishwa. Hii si sawa? Kwa vile Yesu alinuia kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, ilimbidi Awainue wale ambao wangefanya kazi ya kupasha njia. Yohana alipoanza tu kuhubiri, alisema, “Itayarisheni ninyi njia ya Bwana, yafanyeni mapito yake kuwa nyoofu. Ninyi tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni uko karibu.” Aliongea hivi tangu mwanzoni, na mbona aliweza kuyasema maneno haya? Kwa suala la utaratibu ambao maneno haya yalisemwa, ni Yohana aliyezungumzia kwanza injili ya ufalme wa mbinguni, na Yesu aliyezungumza baadaye. Kulingana na dhana za mwanadamu, ni Yohana aliyeifungua njia mpya, na bila shaka Yohana alikuwa mkubwa kumliko Yesu. Lakini Yohana hakusema yeye ni Kristo, na Mungu hakumshuhudia kama Mwana mpendwa wa Mungu, lakini Alimtumia tu kufungua na kuandaa njia ya Bwana. Alimpisha Yesu njia, lakini hangefanya kazi kwa niaba ya Yesu. Kazi zote za mwanadamu pia zilidumishwa na Roho Mtakatifu.

Katika enzi ya Agano la Kale, ni Yehova aliyeongoza njia, na kazi ya Yehova iliwakilisha enzi nzima ya Agano la Kale, na kazi zote zilizofanywa Israeli. Musa tu alizingatia hizi kazi duniani, na kazi zake zinahesabika kama ushirikiano uliotolewa na mwanadamu. Wakati huo, Yehova ndiye aliyezungumza, na Akamwita Musa, na kumlelea miongoni mwa watu wa Israeli, na kumfanya Musa kuwaongoza nyikani hadi Kanaani. Hii haikuwa kazi ya Musa mwenyewe, lakini hiyo iliyoagizwa kibinafsi na Yehova, na hivyo Musa hawezi kuitwa Mungu. Musa pia aliiweka chini sheria, lakini sheria hii iliamrishwa kibinafsi na Mungu aliyeifanya izungumzwe na Musa. Yesu pia alitengeneza amri, na kuondoa sheria ya Agano la Kale na kuweka amri ya enzi jipya. Mbona Yesu ni Mungu Mwenyewe? Kwa sababu haya si mambo sawa. Wakati huo, kazi aliyoifanya Musa haikuwakilisha enzi, wala haikufungua njia mpya; alielekezwa mbele na Yehova, na alikuwa tu anatumiwa na Mungu, Yesu alipokuja, Yohana alikuwa amefanya hatua ya kazi ya kupisha njia, na alikuwa ashaanza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni (Roho Mtakatifu alikuwa ameanza hii). Yesu alipojitokeza, Alifanya moja kwa moja kazi Yake Mwenyewe, lakini kulikuwa na tofauti kubwa kati ya kazi Yake na kazi na matamshi ya Musa. Isaya pia alizungumzia unabii mwingi, lakini mbona yeye hakuwa Mungu Mwenyewe? Yesu hakuzungumzia unabii mwingi lakini mbona Alikuwa Mungu Mwenyewe? Hakuna anayethubutu kusema kwamba kazi zote za Yesu wakati huo zilitoka kwa Roho Mtakatifu, wala hathubutu kusema zote zilitoka kwa matakwa ya mwanadamu, ama zilikuwa kabisa kazi za Mungu Mwenyewe. Mwanadamu hana njia yoyote ya kuchambua mambo haya. Inaweza kusemwa kwamba Isaya alifanya kazi kama hiyo, na kuzungumzia unabii huo, na yote yalitoka kwa Roho Mtakatifu; hayakutoka moja kwa moja kwa Isaya mwenyewe, lakini yalikuwa ufunuo kutoka kwa Yehova. Yesu hakufanya kazi nyingi sana, na Hakusema maneno mengi sana, wala Hakuzungumzia unabii mwingi. Kwa mwanadamu, mahubiri Yake hayakuonekana hasa ya kupandishwa cheo, lakini alikuwa Mungu Mwenyewe, na mwanadamu hawezi kueleza haya. Hakuna aliyewahi kumwamini Yohana, ama Isaya, ama Daudi, wala hakuna aliyewahi kuwaita Mungu, ama Daudi Mungu ama Yohana Mungu, hakuna aliyewahi kuzungumza hivi, na ni Yesu tu aliyewahi kuitwa Kristo. Uainishaji huu umefanywa kulingana na ushahidi wa Mungu, kazi Aliyoifanya, na huduma Aliyoifanya. Kuhusu watu wakuu wa Biblia—Ibrahimu, Daudi, Yoshua, Danieli, Isaya, Yohana na Yesu—kupitia kazi waliyoifanya, unaweza kusema ni nani aliye Mungu Mwenyewe, na ni watu wapi walio manabii, na ni wapi walio mitume. Ni nani aliyetumiwa na Mungu, na nani aliyekuwa Mungu Mwenyewe, inatofautishwa na kuamuliwa na asili na aina za kazi walizozifanya. Iwapo huwezi kusema tofauti, basi hii inadhihirisha kwamba hujui maana ya kumwamini Mungu. Yesu ni Mungu kwa sababu Alizungumza maneno mengi, na kufanya kazi nyingi hasa maonyesho Yake ya miujiza nyingi. Vivyo hivyo, Yohana, pia alifanya kazi nyingi, na kuzungumza maneno mengi, Musa pia; mbona hawakuitwa Mungu? Adamu aliumbwa moja kwa moja na Mungu; mbona hakuitwa Mungu, badala tu ya kuitwa kiumbe? Mtu akikwambia, “Leo, Mungu amefanya kazi nyingi sana, na kuzungumza maneno mengi; Yeye ni Mungu Mwenyewe. Basi, vile Musa alivyozungumza maneno mengi, lazima yeye pia ni Mungu Mwenyewe!” inapaswa uwarudishie swali, “Wakati huo, mbona Mungu alimshuhudia Yesu, na sio Yohana, kama Mungu Mwenyewe? Je, Yohana hakumtangulia Yesu? Ni ipi iliyokuwa kubwa, kazi ya Yohana ama Yesu? Kwa mwanadamu, Yohana anakaa mkubwa kumliko Yesu, lakini mbona Roho Mtakatifu alimshuhudia Yesu, na sio Yohana?” Hiki kitu kimoja kinafanyika leo! Mwanzoni, Musa alipowaongoza watu wa Israeli, Yehova alimwongelesha kutoka miongoni mwa mawingu. Musa hakuzungumza moja kwa moja lakini badala yake aliongozwa moja kwa moja na Yehova. Hii ilikuwa kazi ya Israeli ya Agano la Kale. Ndani ya Musa hamkuwa na Roho, ama nafsi ya Mungu. Hangeweza kufanya kazi hiyo, na hivyo kuna tofauti kubwa kati ya aliyoifanya na Yesu. Na hiyo ni kwa sababu kazi walizozifanya zilikuwa tofauti! Iwapo mtu anatumiwa na Mungu, ama ni nabii, mtume, ama Mungu Mwenyewe, unaweza kubainishwa na asili ya kazi yake, na hii itakomesha mashaka yenu, Kwa Biblia, imeandikwa kwamba Kondoo peke yake ndiye anayeweza kuivunja mihuri saba. Kupitia zama zote kumekuwa na wachambuzi wengi wa maandiko miongoni mwa watu wakuu, na hivyo unaweza kusema kwamba wote ni Kondoo? Unaweza kusema kwamba maelezo yao yote yalitoka kwa Mungu? Walikuwa tu wachambuzi; hawana utambulisho wa Kondoo. Wanastahilije kuivunja mihuri saba? Ni ukweli kwamba “Kondoo peke yake anaweza kuivunja mihuri saba,” Lakini Hakuji tu kuivunja mihuri saba; hakuna umuhimu wa kazi hii, inafanywa kwa bahati. Yeye yu wazi kabisa kuhusu kazi Yake Mwenyewe; ni muhimu Kwake kutumia muda mwingi kutafsiri maandiko? Ni lazima “enzi ya Kondoo ya kuitafsiri maandiko” iongezwe kwa kazi ya miaka elfu sita? Anakuja kufanya kazi mpya, lakini pia Anatoa ufunuo kadhaa kuhusu kazi za nyakati za zamani, kufanya watu waelewe ukweli wa kazi ya miaka elfu sita. Hakuna haja ya kueleza vifungo vingi kutoka Biblia; kazi ya leo ndiyo iliyo kuu, hiyo ni muhimu. Unapaswa kujua kwamba Mungu haji hasa kuivunja muhiri saba, ila kufanya kazi ya wokovu.

Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja.

Bila mwanzo wa hatua hii mpya ya kazi, ni nani ajuaye umbali upi ninyi wainjilisti, wahubiri, wachambuzi na wanaoitwa wanadamu wa kiroho wangeenda! Bila mwanzo wa hatua hii mpya ya kazi, mnachozungumzia ni cha zamani! Ama inapaa kwa kiti cha enzi, au kutayarisha kimo cha kuwa mfalme; ama kukanusha binafsi au kuhini mwili wa mtu; ama kuwa mtulivu au kujifunza masomo kutoka mambo yote; ama unyenyekevu au upendo. Hii ni kuimba wimbo sawa na zamani? Ni jambo tu ya kuita kitu kimoja na jina lingine! Ama kufunika kichwa cha mtu na kuvunja mkate, au kuweka mikono na kuomba, na kuponya wagonjwa na kutoa mapepo. Kunaweza kuwa na kazi ingine mpya? Kunaweza kuwa na matarajio ya maendeleo? Ukiendelea kwa njia hii, utayafuata mafundisho kwa upofu, ama ufuate mkataba. Mnaamini kazi yenu kuwa ya juu mno, lakini hamjui kwamba yote yalipitiwa na kufundishwa na hao “watu wazee” wa nyakati za zamani? Yote mnayoyasema na kufanya si maneno ya mwisho ya hao watu wazee? Siyo malipo ya hawa watu wazee kabla wafariki? Unafikiri kuwa vitendo vyenu vinashinda vile vya mitume na manabii wa vizazi vilivyopita, na pia kushinda mambo yote? Mwanzo wa hatua hii ya kazi umetamatisha kuabudu kwenu kwa kazi ya Mshahidi Lee ya kutaka kuwa mfalme, na kupaa kwa kiti cha enzi, na kukamata kiburi na fujo yenu, kwa hivyo hamna uwezo wa kuingilia hatua hii ya kazi. Bila hatua hii ya kazi, mngezama hata zaidi katika kutokombolewa. Kuna mengi yaliyo mzee miongoni mwenu! Kwa bahati nzuri, kazi ya leo imewarudisha; kama si hivyo, nani anajua mwelekeo ambao mngechukua! Kwa kuwa Mungu ni Mungu ambaye daima ni mpya na kamwe si mzee, mbona hutafuti mambo mapya? Mbona daima unakwamilia mambo ya kale? Na hivyo, kuijua kazi ya Roho Mtakatifu leo una umuhimu mkubwa!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp