Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
(Sehemu ya Tatu)
Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye. Tangu Alipoanza kusimamia, Mungu amekuwa akisubiria binadamu kumpa moyo wake, kumwacha Mungu kuutakasa na kuufaa ipaswavyo, kumfanya yeye kumtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu, kumfanya yeye kumstahi Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu amewahi kutazamia mbele na kusubiria matokeo haya. Kunao watu kama hawa miongoni mwa rekodi za Biblia? Yaani, kunao wowote kwenye Biblia wanaoweza kutoa mioyo yao kwa Mungu? Kunaye yeyote anayetangulia kabla ya enzi hii? Leo, hebu tuendelee kusoma simulizi za Biblia na kuangalia kama kile kilichofanywa na mhusika huyu—Ayubu—kina muunganisho wowote na mada ya “kumpa Mungu moyo wako” ambayo tunazungumzia kuhusu leo. Hebu tuone kama Ayubu alimtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu.
Maoni yenu ni yapi kuhusu Ayubu? Wakitolea mifano ya maandiko asilia, baadhi ya watu husema kwamba Ayubu “alimcha Mungu na kujiepusha na maovu.” “Alimcha Mungu na kujiepusha na maovu”: Huo ndio ukadiriaji mojawapo asilia wa Ayubu uliorekodiwa kwenye Biblia. Kama mliyatumia maneno yenu binafsi, mnawezaje kumzungumzia Ayubu? Baadhi ya watu wanasema kwamba Ayubu alikuwa binadamu mzuri mwenye busara, baadhi wanasema kwamba alikuwa na imani ya kweli kwa Mungu; baadhi wanasema kwamba Ayubu alikuwa binadamu mwenye haki na utu. Mmeiona imani ya Ayubu, hivi ni kusema, katika mioyo yenu mnaambatisha umuhimu mkubwa kwa na mnaionea wivu imani ya Ayubu. Leo, basi, hebu tuzungumzie kile kilichomilikiwa na Ayubu ambacho Mungu anafurahishwa sana naye. Kisha, hebu tusome maandiko yaliyo hapa chini.
C. Ayubu
1. Ukadiriaji wa Ayubu na Mungu na kwenye Biblia
Ayubu 1:1 Kulikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, ambaye aliitwa Ayubu; na huyo mtu alikuwa mtimilifu na mwaminifu, na ambaye alimcha Mungu, na kuepuka maovu.
Ayubu 1:5 Na ilikuwa hivyo, wakati hizo siku zao za karamu ziliisha, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, na akaamka asubuhi mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote; kwa sababu Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wana wangu wametenda dhambi, na kumlaani Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya kila siku.
Ayubu 1:8 Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?
Ni nini hoja kuu unayoiona kwenye vifungu hivi? Vifungu hivi vitatu vifupi vya maandiko vyote vinahusu Ayubu. Ingawaje ni vifupi, vinaelezea waziwazi alikuwa mtu wa aina gani. Kupitia kwa ufafanuzi wake kuhusu tabia ya kila siku ya Ayubu na mwenendo wake, vinaelezea kila mmoja kwamba, badala ya kukosa msingi, ukadiriaji wa Mungu ya Ayubu ulikuwa na msingi wake na ulikuwa umekita mizizi. Vinatuambia kwamba iwapo ni utathmini wa binadamu kuhusu Ayubu (Ayubu 1:1), au utathmini wa Mungu kuhusu yeye (Ayubu 1:8), tathmini zote zinatokana na matendo ya Ayubu mbele ya Mungu na binadamu (Ayubu 1:5).
Kwanza, hebu tukisome kifungu nambari moja: “Kulikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, ambaye aliitwa Ayubu; na huyo mtu alikuwa mtimilifu na mwaminifu, na ambaye alimcha Mungu, na kuepuka maovu.” Ukadiriaji wa kwanza wa Ayubu kwenye Biblia, sentensi hii ndiyo utathmini wa mwandishi kuhusu Ayubu Kiasili, unawakilisha pia ukadiriaji wa binadamu kuhusu Ayubu, ambayo ni “huyo mtu alikuwa mtimilifu na mwaminifu, na ambaye alimcha Mungu, na kuepuka maovu.” Kisha, hebu tuusome utathmini wa Mungu kuhusu Ayubu: “hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu” (Ayubu 1:8). Kati ya tathmini hizi mbili, moja ilitoka kwa binadamu, na nyingine ikatoka kwa Mungu; ni ukadiriaji aina mbili ulio na maudhui moja. Inaweza kuonekana, basi, kwamba tabia na mwenendo wa Ayubu ulijulikana kwa binadamu, na pia ulisifiwa na Mungu. Kwa maneno mengine, mwenendo wa Ayubu mbele ya binadamu na mwenendo wake mbele ya Mungu ulikuwa sawa; aliweka tabia yake na motisha yake mbele ya Mungu siku zote, ili hivi viwili viweze kuangaliwa na Mungu, na yeye alikuwa mmoja aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo, katika macho ya Mungu, kati ya watu duniani, ni Ayubu tu ambaye alikuwa mtimilifu na mnyofu, ndiye aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.
Maonyesho Mahususi ya Kumcha Mungu kwa Ayubu na Kujiepusha na Maovu katika Maisha Yake ya Kila siku
Kisha, hebu tuangalie maonyesho mahususi ya kumcha Mungu kujiepusha na maovu kwa Ayubu. Juu ya vifungu hivi vinavyotangulia na kufuata, hebu pia tusome Ayubu 1:5, ambayo ni mojawapo ya maonyesho mahususi ya kumcha Mungu na kujiepusha kwa maovu kwa Ayubu. Inahusu namna ambavyo alimcha Mungu na kujiepusha na maovu katika maisha yake ya kila siku; muhimu zaidi, hakufanya tu kile alichostahili kufanya kwa minajili ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwake, lakini pia mara kwa mara alitoa sadaka iliyoteketezwa mbele ya Mungu kwa niaba ya wana wake. Alikuwa na hofu kwamba walikuwa mara nyingi “wametenda dhambi, na kumlaani Mungu katika mioyo yao” wakati wakiwa na karamu. Na uoga huu ulijionyesha vipi ndani ya Ayubu? Maandishi asilia yanatupa simulizi ifuatayo: “Na ilikuwa hivyo, wakati hizo siku zao za karamu ziliisha, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, na akaamka asubuhi mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote.” Mwenendo wa Ayubu unatuonyesha kwamba, badala ya kuonyeshwa katika tabia yake ya nje, kumcha Mungu kwake kulitokea ndani ya moyo wake, na kwamba kumcha Mungu kwake kungepatikana katika kila kipengele cha maisha yake ya kila siku, wakati wote, kwani hakujiepusha na maovu tu yeye mwenyewe, lakini pia alitoa sadaka zilizoteketezwa kwa niaba ya watoto wake wa kiume. Kwa maneno mengine, Ayubu hakuwa tu mwenye hofu ya kutenda dhambi dhidi ya Mungu na kumkataa Mungu katika moyo wake, lakini pia alikuwa na wasiwasi kwamba watoto wake wa kiume walitenda dhambi dhidi ya Mungu na kumkataa Yeye katika mioyo yao. Kutokana na haya ukweli unaweza kuonekana kwamba ukweli wa kumcha Mungu kwa Ayubu unapita uchunguzi, na ni zaidi ya shaka ya binadamu yeyote. Je, alifanya hivi mara kwa mara, au mara nyingi? Sentensi ya mwisho ya maandishi ni “Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya kila siku.” Maana ya maneno haya ni kwamba Ayubu hakuenda na kuangalia watoto wake mara kwa mara au wakati alipenda kufanya hivyo, wala hakutubu kwa Mungu kupitia kwa maombi. Badala yake, aliwatuma mara kwa mara na kuwatakasa watoto wake wa kiume kutoa sadaka iliyoteketezwa kwa niaba yao. Hiyo kauli “bila kusita” hapa haimaanishi alifanya hivyo kwa siku moja au mbili, au kwa muda mfupi tu. Inasema kwamba maonyesho ya kumcha Mungu kwa Ayubu hayakuwa ya muda, na hayakusita kwa maarifa aliyokuwa nayo au kwa maneno aliyotamka; badala yake, njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu iliongoza moyo wake, iliamuru tabia yake, na ilikuwa, ndani ya moyo wake mzizi wa uwepo wake. Kwamba alifanya hivyo bila kusita yaonyesha kwamba, katika moyo wake, mara nyingi alikuwa na hofu kwamba yeye mwenyewe angetenda dhambi dhidi ya Mungu na alikuwa na wasiwasi pia kwamba watoto wake wa kiume na binti zake walitenda dhambi dhidi ya Mungu. Inawakilisha namna tu ambavyo uzito wa njia ambayo alimcha Mungu na kujiepusha na maovu ulibebwa ndani ya moyo wake. Alifanya hivyo bila kusita kwa sababu, ndani ya moyo wake, alikuwa na hofu na wasiwasi—wasiwasi kwamba alikuwa ametenda maovu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu, na kwamba alikuwa amepotoka kutoka kwenye njia ya Mungu, na basi alikuwa hawezi kutosheleza Mungu. Wakati huohuo, alikuwa pia na wasiwasi kuhusu watoto wake wa kiume na binti zake, akiogopa kwamba walikuwa wamemkosea Mungu. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa kawaida wa Ayubu katika maisha yake ya kila siku. Kwa hakika ni mwenendo wa kawaida ambao unathibitisha kwamba kumcha Mungu na kujiepusha kwa maovu kwa Ayubu si maneno matupu tu, kwamba Ayubu aliishi kwa kudhihirisha kwa kweli ukweli kama huo. “Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya kila siku”: Maneno haya yanatuambia kuhusu matendo ya kila siku ya Ayubu mbele ya Mungu. Alipofanya hivi bila kusita, tabia yake na moyo wake vilifika mbele ya Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu mara nyingi alipendezwa na moyo wake na tabia yake? Basi, ni katika hali gani na katika muktadha gani Ayubu alifanya hivi bila kusita? Baadhi ya watu wanasema kwamba ilikuwa ni kwa sababu Mungu alijitokeza kwa Ayubu mara kwa mara na ndiyo maana akatenda hivi; baadhi wanasema kwamba alifanya hivi bila kusita kwa sababu angejiepusha na maovu; na baadhi wanasema kwamba alifikiria kwamba utajiri wake ulikuwa haujaja kwa urahisi, na alijua kwamba alikuwa amepewa na Mungu, na hivyo alikuwa na uoga mwingi wa kupoteza mali yake kutokana na kutenda dhambi dhidi ya au kumkosea Mungu. Je, yapo madai yoyote kati ya haya yaliyo kweli? Bila shaka la. Kwani, kwa macho ya Mungu, kile Mungu amekubali na kupenda sana kuhusu Ayubu si tu kwamba alifanya hivi bila kusita; zaidi ya hapo, ilikuwa ni mwenendo wake mbele ya Mungu, binadamu, na Shetani alipokabidhiwa Shetani na kujaribiwa. Sehemu zilizo hapa chini zinatupa ithibati yenye ushawishi mkubwa zaidi, ithibati ambayo inatuonyesha ukweli wa ukadiriaji wa Mungu kwa Ayubu. Kinachofuata, hebu tusome maandiko kwenye vifungu vifuatavyo.
2. Shetani Anamjaribu Ayubu kwa Mara ya Kwanza (Mifugo Yake Yaibiwa na Janga Lawapata Watoto Wake)
a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu
Ayubu 1:8 Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?
Ayubu 1:12 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, vyote ambavyo anavyo vimo uwezoni mwako; lakini juu yake mwenyewe wewe usinyoshe mkono wako. Hivyo basi Shetani akaondoka mbele za uwepo wa Yehova.
b. Jibu la Shetani
Ayubu 1:9-11 Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.
Mungu Amruhusu Shetani Kumjaribu Ayubu ili Imani ya Ayubu iweze Kufanywa Kuwa Timilifu
Ayubu 1:8 ndiyo rekodi ya kwanza tunayoiona kwenye Biblia kuhusu mabadilishano kati ya Yehova Mungu na Shetani. Na ni nini alichosema Mungu? Maandishi asilia yanatupatia simulizi ifuatayo: “Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?” Huu ulikuwa ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu kwa Shetani; Mungu alisema kwamba alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kabla ya maneno haya kati ya Mungu na Shetani, Mungu alikuwa ameamua kwamba Angemtumia Shetani kujaribu Ayubu—kwamba Angemkabidhi Ayubu kwa Shetani. Kwa mkondo mmoja, hali hii ingethibitisha kwamba uangalizi na utathmini wa Mungu kwa Ayubu ulikuwa sahihi na bila kosa, na ungesababisha Shetani kuaibishwa kupitia kwa ushuhuda wa Ayubu, kwa mkondo mwingine, ingefanya imani ya Ayubu kwa Mungu na kumcha Mungu kuwa timilifu. Hivyo, wakati Shetani alipokuja mbele ya Mungu, Mungu hakutatiza maneno. Alienda moja kwa moja kwenye hoja na kumuuliza Shetani: “Je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?” Katika swali la Mungu kunayo maana ifuatayo: Mungu alijua kwamba Shetani alizunguka kila pahali, na mara nyingi alikuwa amemnyemelea Ayubu, aliyekuwa mtumishi wa Mungu. Alikuwa mara nyingi amemjaribu na kumshambulia, akijaribu kupata njia ya kumwangamiza Ayubu ili kuthibitisha kwamba imani ya Ayubu katika Mungu na kumcha Mungu kwake kusingeweza kubadilika. Shetani pia alitafuta kwa haraka sana fursa za kumhangaisha Ayubu, ili Ayubu aweze kumkataa Mungu na kumruhusu Shetani kumpokonya kutoka kwenye mikono ya Mungu. Lakini Mungu aliuangalia moyo wa Ayubu na kuona kwamba alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alitumia swali moja kumwambia Shetani kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, kwamba Ayubu asingeweza kumwacha Mungu na kufuata Shetani. Baada ya kusikia utathmini wa Mungu kuhusu Ayubu, ndani ya Shetani kukatokea hasira kali iliyotokana na udhalilishaji, na akawa mwenye hasira zaidi, na aliyekosa subira ya kumpokonya Ayubu kutoka kwa Mungu, kwani Shetani alikuwa hajawahi kusadiki kwamba mtu angeweza kuwa mtimilifu na mnyofu, au kwamba angeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Wakati huohuo, Shetani pia alichukizwa na utimilifu na unyofu kwa binadamu, na aliwachukia watu ambao wangeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Na hivyo imeandikwa katika Ayubu 1:9-11 kwamba “Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.” Mungu alikuwa amezoea kwa undani asili ya kijicho ya Shetani, na Alijua vizuri kabisa kwamba Shetani alikuwa na mpango wa muda mrefu wa kumwangamiza Ayubu, na hivyo kwa haya Mungu alitaka, kwa kumwambia Shetani kwa mara nyingine kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimwogopa Mungu na kujiepusha na maovu, kumrudisha Shetani pale anapofaa, kumfanya Shetani kufichua uso wake wa kweli na kumshambulia na kumjaribu Ayubu. Kwa maneno mengine, Mungu alitilia mkazo makusudi kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, na kwa njia hii alimfanya Shetani kumshambulia Ayubu kwa sababu ya chuki na hasira za Shetani kutokana na vile ambavyo Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kutokana na haya, Mungu angemletea Shetani aibu kupitia kwa ukweli kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, na Shetani angeachwa akiwa amedhalilishwa kabisa na kushindwa. Baada ya hapo, Shetani asingekuwa tena na shaka au asingetoa mashtaka kuhusu utimilifu, unyofu, ucha Mungu au hali ya kujiepusha na maovu ya Ayubu. Kwa njia hii, majaribio ya Mungu na yale ya Shetani yalikuwa karibu yasiyoepukika. Yule tu aliye na uwezo wa kustahimili majaribio ya Mungu na yale ya Shetani alikuwa ni Ayubu. Kufuatia mabadilishano haya, Shetani alipewa ruhusa kumjaribu Ayubu. Na hivyo raundi ya kwanza ya mashambulizi ya Shetani ikaanza. Kilengwa cha mashambulizi haya kilikuwa mali ya Ayubu, kwani Shetani alikuwa ametoa mashtaka yafuatayo dhidi ya Ayubu: “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? … Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini.” Kutokana na haya, Mungu alimruhusu Shetani kuchukua kila kitu ambacho Ayubu alikuwa nacho—ambalo ndilo lilikuwa kusudio lenyewe la Mungu kuzungumza na Shetani. Hata hivyo, Mungu alitoa sharti moja kwa Shetani: “vyote ambavyo anavyo vimo uwezoni mwako; lakini juu yake mwenyewe wewe usinyoshe mkono wako” (Ayubu 1:12). Hili ndilo sharti ambalo Mungu alitoa baada ya kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu na akamweka Ayubu kwenye mikono ya Shetani, na hiyo ndiyo mipaka aliyomwekea Shetani: Alimwamuru Shetani kutodhuru Ayubu. Kwa sababu Mungu alijua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba Alikuwa na imani kwamba utimilifu na unyofu wa Ayubu kwake Yeye ulikuwa zaidi ya kutiliwa shaka, na kwamba angeweza kustahimili majaribio; hivyo, Mungu alimruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, lakini akaweka hapo kizuizi kwa Shetani: Shetani aliruhusiwa kuchukua mali ya Ayubu yote, lakini asimguse hata kwa kidole. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba Mungu hakumkabidhi Ayubu kabisa kwa Shetani wakati huo. Shetani angeweza kumjaribu Ayubu kwa mbinu zozote zile ambazo alitaka, lakini hakuweza kumdhuru Ayubu mwenyewe, hata unywele mmoja wa kichwa chake, kwa sababu kila kitu cha binadamu kinathibitiwa na Mungu, iwapo binadamu anaishi ama anakufa inaamuliwa na Mungu na Shetani hana leseni yoyote ya kuthibiti haya. Baada ya Mungu kumwambia Shetani maneno haya, Shetani asingeweza kusubiri kuanza. Alitumia kila mbinu kumjaribu Ayubu, na baada ya muda usiyokuwa mrefu Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng’ombe na mali yote aliyokuwa amepewa na Mungu…. Na hivyo majaribio ya Mungu yakamjia yeye.
Ingawa Biblia inatuambia asili ya jaribio la Ayubu, je Ayubu mwenyewe, ambaye alipatwa na majaribio haya, alijua kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea? Ayubu alikuwa tu binadamu wa kawaida; bila shaka hakujua chochote kuhusu hadithi ile iliyokuwa ikiendelea nyuma yake. Hata hivyo, kumcha Mungu kwake na utimilifu pamoja na unyofu wake, ulimfanya kutambua kwamba majaribio ya Mungu yalikuwa yamemjia. Hakujua ni nini kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme wa kiroho, wala nia alizokuwa nazo Mungu katika majaribio hayo. Lakini alijua kwamba haijalishi ni nini ambacho kingemfanyikia yeye, alifaa kuendelea kushikilia ukweli wa utimilifu na unyofu wake, na kwamba alifaa kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mwelekeo na mwitikio wa Ayubu katika masuala haya uliweza kutazamwa waziwazi na Mungu. Naye Mungu aliona nini? Aliuona moyo wa Ayubu uliyomcha Mungu, kwa sababu kutoka mwanzo hadi wakati ambapo Ayubu alijaribiwa, moyo wa Ayubu ulibakia wazi kwa Mungu, uliwekwa mbele ya Mungu, naye Ayubu hakuwacha utimilifu wala unyofu wake, wala hakutupilia mbali au kugeuka katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—na hakuna kingine chochote kilichokuwa cha kumtosheleza na kumfurahisha Mungu kama haya. Kisha, tutaangalia ni majaribio yapi aliyoyapitia Ayubu na ni vipi ambavyo aliyashughulikia majaribio haya. Hebu tuyasome maandiko.
c. Mwitikio wa Ayubu
Ayubu 1:20-21 Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu, Naye akasema, Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi; Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.
Kwamba Ayubu Anajiwajibikia Yeye Mwenyewe Kurudisha Vyote Anavyomiliki Kunatokana na Kumcha Kwake Mungu
Baada ya Mungu kumwambia Shetani, “vyote ambavyo anavyo vimo uwezoni mwako; lakini juu yake mwenyewe wewe usinyoshe mkono wako.” Shetani aliondoka, muda mfupi baadaye Ayubu alipata mashambulizi ya ghafla na makali: Kwanza, ng’ombe na punda wake waliibwa na watumishi wake kuuwawa; kisha, kondoo na watumishi wake waliteketezwa hadi kiwango cha kuangamia; baada ya hapo ngamia wake walichukuliwa na watumishi wake wakauliwa; hatimaye watoto wake wa kiume na wa kike waliaga dunia. Msururu huu wa mashambulizi ulikuwa ni mateso ambayo alipitia Ayubu kwenye jaribio hili la kwanza. Kama alivyoamrishwa na Mungu, kwenye kipindi hiki cha mashambulizi, Shetani alilenga tu mali ya Ayubu na watoto wake, na hakumdhuru Ayubu mwenyewe. Hata hivyo, Ayubu alibadilishwa papo hapo kutoka kuwa mtu tajiri aliyemiliki utajiri mwingi hadi kuwa mtu asiye na chochote wala lolote. Hakuna yeyote ambaye angestahimili mshangao huu mkubwa au ambaye angeitikia vizuri, ilhali Ayubu aliuonyesha upande wake usio wa kawaida. Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.” Huu ndio uliokuwa mwitikio wa kwanza wa Ayubu baada ya kusikia kwamba watoto wake walikuwa wameaga dunia na alikuwa amepoteza mali yake yote. Zaidi ya yote, hakuonekana ni kana kwamba ameshangazwa, au amepigwa na butwaa chakari, isitoshe hakuonyesha hasira au chuki. Unaona, basi, kwamba moyoni mwake alikuwa tayari ametambua kuwa majanga haya hayakuwa ajali, au yalitokana na mkono wa binadamu, na wala hayakuwa kuwasili kwa kuadhibiwa au adhabu. Badala yake, majaribio ya Yehova Mungu yalikuwa yamemjia yeye; alikuwa ni Yehova Mungu ambaye alitaka kuchukua mali na watoto wake. Ayubu alikuwa mtulivu na mwenye kuelewa haraka wakati huo. Ubinadamu wake wa utimilifu na unyofu ulimwezesha yeye kuweza kufanya uamuzi na uamuzi kwa usahihi kwa njia ya kiasili na kirazini hasa, kuhusu majanga yaliyokuwa yamemsibu, na matokeo yake ni kuwa, alijiendeleza kwa utulivu usio wa kawaida. “Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.” “Akalipasua joho lake” inamaanisha kwamba alikuwa hana nguo, na hakumiliki chochote; “akanyoa kichwa chake” inamaanishwa kwamba alikuwa amerudi mbele ya Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa; “akaanguka chini, na kuabudu” inamaanisha alikuwa amekuja ulimwenguni akiwa uchi, na bado hakuwa na chochote leo, alirudishwa kwa Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa. Mwelekeo wa Ayubu kwa yote yaliyompata usingeweza kutimizwa na kiumbe yeyote wa Mungu. Imani yake kwa Yehova Mungu ilizidi ile ufalme wa imani; huku kulikuwa ni kumcha Mungu kwake, kuwa mtiifu kwa Mungu, na hakuweza tu kutoa shukrani kwa Mungu kwa kumpa yeye lakini pia kuchukua kutoka kwake. Na zaidi ya hayo, aliweza kujiwajibikia yeye mwenyewe ili kurudisha yale yote aliyomiliki, pamoja na maisha yake.
Kumcha Mungu na utiifu wa Ayubu kwa Mungu ni mfano kwa wanadamu, na utimilifu na unyofu wake ulikuwa ndio kilele cha ubinadamu unaofaa kumilikiwa na binadamu. Ingawaje hakumwona Mungu, alitambua kwamba Mungu kwa kweli alikuwepo, na kwa sababu ya utambuzi huu alimcha Mungu—na kutokana na kumcha Mungu kwake, aliweza kumtii Mungu. Alimpa Mungu uhuru wa kuchukua chochote alichokuwa nacho, ilhali hakulalamika, na akaanguka chini mbele ya Mungu na kumwambia kwamba kwa wakati huohuo, hata kama Mungu angeuchukua mwili wake, angemruhusu yeye kufanya hivyo kwa furaha, bila malalamiko. Mwenendo wake wote ulitokana na ubinadamu wake timilifu na mnyofu. Hivi ni kusema, kutokana na kutokuwa na hatia kwake, uaminifu, na upole wake, Ayubu hakutikisika katika utambuzi wake na uzoefu wa uwepo wa Mungu na juu ya msingi huu aliweza kujitolea madai yeye mwenyewe na kuwastanisha kufikiria kwake, tabia, mwenendo, na kanuni za vitendo mbele ya Mungu kulingana na mwongozo wa Mungu kwake yeye na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa ameviona miongoni mwa mambo mengine yote. Baada ya muda, uzoefu wake ulimsababisha yeye kuwa na hali halisi na ya kweli ya kumcha Mungu na kumfanya pia kujiepusha na maovu. Hiki ndicho kilikuwa chanzo cha uadilifu ambao Ayubu alishikilia. Ayubu aliumiliki ubinadamu wa uaminifu, usio na hatia, na wa upole, na alikuwa na uzoefu halisi wa kumcha Mungu, kumtii Mungu na kujiepusha na maovu, pamoja na maarifa kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua.” Ni kwa sababu tu ya mambo haya ndiyo aliweza kusimama imara na kushuhudia katikati ya mashambulizi mabaya kama yale yaliyomsibu kutoka kwa Shetani, na ni kwa sababu tu ya hayo ndiyo aliweza kutomkasirisha Mungu na kutoa jibu la kutosheleza kwake Mungu wakati majaribio ya Mungu yalipomjia. Ingawaje mwenendo wa Ayubu kwenye jaribio la kwanza ulikuwa wa moja kwa moja, vizazi vya baadaye havikuwa na uhakika wa kutimiza hali hiyo ya moja kwa moja hata baada ya kutia bidii maisha yao yote, wala hawangemiliki kwa vyovyote vile mwenendo wa Ayubu uliofafanuliwa hapo juu. Leo, wakikabiliwa na mwenendo wa moja kwa moja wa Ayubu, na katika kuulinganisha na kilio na bidii ya “utiifu wenye hakika na uaminifu hadi kifo” ulioonyeshwa kwa Mungu na wale wanaodai kusadiki Mungu na kufuata Mungu, je mnahisi aibu kwa kina au la?
Wakati unasoma maandiko kuhusu yale mateso yote aliyopitia Ayubu na familia yake, mwitikio wako ni upi? Unapotea kwenye fikira zako? Unashangazwa? Je, majaribio haya yaliyomsibu Ayubu yanaweza kufafanuliwa kama ya “kusikitisha”? Kwa maneno mengine, inatisha vya kutosha kuyasoma majaribio ya Ayubu kama yalivyofafanuliwa kwenye maandiko, kutosema chochote kuhusu vile yangekuwa katika uhalisia. Unaona, basi, kwamba kile kilichomsibu Ayubu hakikuwa “mazoezi,” lakini “vita,” halisi vikiwa na “bunduki” na “risasi” za kweli. Lakini nani alisababisha yeye kuweza kupitia majaribio haya? Yaliweza, bila shaka, kutekelezwa na Shetani, yalitekelezwa na Shetani mwenyewe—lakini yaliidhinishwa na Mungu. Je, Mungu alimwambia Shetani kumjaribu Ayubu kwa njia gani? Hakumwambia. Mungu alimpa Shetani sharti moja tu, na baadaye jaribio hilo likamjia Ayubu. Wakati jaribio lilimjia Ayubu, liliwapatia watu hisia ya maovu na ubaya wa Shetani, ya uoneaji kijicho wake, na uchukivu wake kwa binadamu, na uadui wake kwa Mungu. Katika haya tunaona kwamba maneno yasingeweza kufafanua namna tu ambavyo jaribio hili lilikuwa la kikatili. Inaweza kusemekana kwamba asili ya kijicho ambayo Shetani alimnyanyasa binadamu na uso wake mbaya vyote vilichuliwa kabisa kwa wakati huu. Shetani alitumia fursa hii, fursa iliyotolewa kupitia kwa ruhusa ya Mungu, kumnyanyasa Ayubu kwa njia mbaya na ya kusikitisha, mbinu na kiwango cha ukatili ambao haufikiriki na hauvumiliki kabisa na watu wa leo. Badala ya kusema kwamba Ayubu alijaribiwa na Shetani, na kwamba alisimama imara katika ushuhuda wake wakati wa jaribio hili, ni bora zaidi kusema kwamba katika majaribio hayo yaliyokuwa mbele yake kutoka kwa Mungu Ayubu alianza kuwa katika mapambano na Shetani ili kuulinda utimilifu na unyofu wake, kutetea njia yake ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika shindano hili, Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng’ombe, alipoteza mali yake yote na watoto wake wa kike na kiume—lakini hakuacha utimilifu, unyofu, au hali yake ya kumcha Mungu. Kwa maneno mengine, katika pigano hili na Shetani alipendelea kunyang’anywa mali na watoto kuliko kupoteza utimilifu, unyofu na hali yake ya kumcha Mungu. Alipendelea kushikilia mzizi wa maana ya kuwa binadamu. Maandiko yanatoa simulizi halisi kuhusu mchakato wote ambao Ayubu alipoteza rasilimali zake, na pia ukasimulia mwenendo na mwelekeo wa Ayubu. Simulizi hizi za mkato, na wazi zinatoa hisia kwamba Ayubu alikuwa karibu anao utulivu wakati akipitia jaribio hili, lakini kama kile kilichofanyika kwa hakika kingeundwa upya, na kuongeza asili yale ya kijicho ya Shetani—basi mambo yasingekuwa rahisi au mepesi kama yalivyofafanuliwa kwenye sentensi hizi. Uhalisia ulikuwa wenye ukatili zaidi. Hicho ndicho kiwango cha uharibifu na chuki ambacho Shetani hushughulikia wanadamu na wale wote wanaoidhinishwa na Mungu. Kama Mungu asingekuwa amemwomba Shetani kutodhuru Ayubu, Shetani bila shaka angekuwa amemwua bila ya shaka. Shetani hataki mtu yeyote kumwabudu Mungu, wala hataki wale wenye haki mbele ya macho ya Mungu na wale walio timilifu na wanyofu kuweza kuendelea kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa watu kumcha Mungu na kujiepusha maovu kunamaanisha kwamba wanajiepusha na kumwacha Shetani, na hivyo Shetani alitumia ruhusa ya Mungu kumlimbikizia hasira yake na chuki kwake Ayubu bila huruma. Unaona, basi, mateso aliyoyapitia Ayubu yalikuwa mengi sana, haya yalikuwa mengi kiasi gani ambayo Ayubu alipitia, kuanzia kwenye akili hadi kwenye mwili, kutoka nje hadi ndani. Leo, hatuoni namna ambavyo kwa wakati huu na tunaweza tu kupata kutoka kwenye simulizi za Biblia, mtazamo mfupi wa hisia za Ayubu wakati alipokuwa akipitia yale mateso wakati huo.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?