Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

(Sehemu ya Tano)

Kuhusu Ayubu

Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe, hasa kuhusiana na siri iliyomfanya akapata sifa za Mungu. Hivyo basi leo, hebu tuzungumzie kuhusu Ayubu!

Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake

Kama tutazungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: “hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu.”

Hebu kwanza tujifunze kuhusu utimilifu na unyofu wa Ayubu.

Unaelewa vipi maneno haya “utimilifu” na “unyofu”? Unasadiki kwamba Ayubu hakuwa na lawama, na kwamba aliheshimika? Hili, bila shaka, litakuwa ni ufasiri wa moja kwa moja na uelewa wa “mtimilifu” na “mnyofu.” Muhimu katika uelewa wa kweli wa Ayubu ni maisha halisi—maneno, vitabu, na nadharia pekee haviwezi kutupa majibu yoyote. Tutaanza na kuyaangalia maisha ya Ayubu ya nyumbani, kuangalia namna mwenendo wake wa kawaida ulivyokuwa maishani mwake. Kufanya hivi kutatwambia kuhusu kanuni na malengo yake maishani, pamoja na hulka yake na mambo yale aliyoyafuatilia. Sasa, hebu tuyasome maneno ya mwisho katika Ayubu 1:3: “mtu huyo alikuwa mkubwa zaidi kuwaliko watu wengine wote wa mashariki.” Kile ambacho maneno haya yanasema ni kwamba hadhi na heshima ya Ayubu ilikuwa ya juu sana, na ingawaje hatuambiwi kama alikuwa ndiye mkubwa zaidi kati ya wanaume wote wa mashariki kwa sababu ya wingi wa rasilimali zake au kwa sababu alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, kwa ujumla tunajua kwamba hadhi na heshima ya Ayubu vyote vilithaminiwa sana. Kama ilivyorekodiwa kwenye Biblia, picha za kwanza za Ayubu kwa watu zilikuwa kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu na kwamba alimiliki utajiri mkubwa na alikuwa na hadhi ya kuheshimika. Kwa mtu wa kawaida anayeishi katika mazingira kama haya na hali kama hizo, mlo wa Ayubu, ubora wa maisha, na vipengele mbalimbali vya maisha yake ya kibinafsi vyote vingekuwa malengo ya umakinifu wa watu wengi; hivyo lazima tuendelee kuyasoma maandiko: “Nao wana wake walienda na kufurahia karamu katika nyumba zao, kila kwa siku yake; na wao wakatuma na kuwaita ndugu zao wa kike watatu ili wakule na kunywa pamoja na wao. Na ilikuwa hivyo, wakati hizo siku zao za karamu ziliisha, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, na akaamka asubuhi mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote; kwa sababu Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wana wangu wametenda dhambi, na kumlaani Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya kila siku” (Ayubu 1:4-5). Kifungu hiki kinatuambia mambo mawili: Jambo la kwanza ni kwamba watoto wa kiume na wa kike wa Ayubu walishiriki kwenye karamu mara kwa mara, wakila na wakinywa; pili ni kwamba Ayubu mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa kwa sababu alikuwa na wasiwasi na wao, akiogopa kwamba walikuwa wakitenda dhambi, kwamba katika mioyo yao walikuwa wamemlaani Mungu. Katika maandiko haya maisha ya watu wa aina mbili tofauti yanafafanuliwa. Maisha ya kwanza, watoto wa kiume na kike wa Ayubu, mara nyingi walishiriki kwenye karamu kwa sababu ya ukwasi wao, waliishi kwa ubadhirifu, wakinywa na wakila hadi mioyo yao kutosheka, wakifurahia maisha ya kiwango cha juu yaliyoletwa na utajiri wa anasa. Wakiishi maisha kama haya, ilikuwa lazima kwamba mara kwa mara wangetenda dhambi na kumkosea Mungu—ilihali hawakujitakasa wala kutoa sadaka za kuteketezwa kutokana na hayo yote. Waona, basi, kwamba Mungu hakuwa na nafasi katika mioyo yao, kwamba hawakufikiria kuhusu neema za Mungu, wala kuogopa kumkosea Mungu, isitoshe hawakuogopa kumuacha Mungu katika mioyo yao. Bila shaka zingatio letu si watoto wa Ayubu, lakini ni kwa kile ambacho Ayubu alifanya alipokabiliwa na mambo kama haya; hili ndilo suala lile jingine lililofafanuliwa katika kifungu, na ambalo linahusisha maisha ya kila siku ya Ayubu na kiini cha ubinadamu wake. Wakati Biblia inapofafanua kushiriki kwa watoto wa kike na kiume katika karamu mbalimbali hakuna mahali ambapo Ayubu anatajwa; yasemekana tu kuwa ni watoto wake wa kiume na wa kike walio kula na kunywa pamoja. Kwa maneno mengine, hakuandaa karamu, wala hakujiunga na watoto wake wa kiume na kike katika karamu hizo ili kuendeleza ubadhirifu. Ingawaje alikuwa tajiri, na alimiliki raslimali nyingi na watumishi wengi, maisha ya Ayubu hayakuwa ya anasa. Hakudanganywa na mazingira yake ya juu kabisa aliyoyaishi na wala hakujawa na ulafi wa anasa za mwili au kusahau kutoa sadaka za kuteketezwa kwa sababu za utajiri wake, isitoshe pia haya yote hayakumsababisha kuanza kujiepusha na Mungu ndani ya moyo wake kwa utaratibu. Ni dhahiri shairi, hivyo basi, kwamba Ayubu alikuwa na nidhamu katika hali ya maisha yake, na wala hakuwa mlafi au na imani ya kuwa anasa ni kitu muhimu katika maisha, wala hakushikilia na kupumbazwa na ubora wa maisha, kutoka na baraka za Mungu kwake. Badala yake, alinyenyekea na akawa asiye na majivuno, na kuwa mtulivu na makini mbele ya Mungu, mara nyingi alifikiria kuhusu neema na baraka za Mungu, na siku zote alimcha Mungu. Katika maisha yake ya kila siku, Ayubu mara nyingi alirauka mapema ili kutoa sadaka zilizoteketezwa kwa niaba ya watoto wake wa kiume na kike. Kwa maneno mengine, Ayubu mwenyewe alimcha Mungu na pia alitumaini kwamba watoto wake wangeweza vilevile kumcha Mungu na kutotenda dhambi dhidi ya Mungu. Utajiri wa anasa wa Ayubu haukuwa na mahali popote ndani ya moyo wake, wala haukusawazisha ile nafasi iliyoshikiliwa na Mungu; haijalishi kama ilikuwa ni kwa ajili yake mwenyewe au watoto wake, vitendo vyote vya kila siku vya Ayubu viliunganishwa katika kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kumcha Yehova Mungu kwake hakukuishia kwenye kinywa chake lakini kulitiwa katika vitendo, na kukajionyesha katika kila sehemu ya maisha yake. Mwenendo huu halisi wa Ayubu unatuonyesha kwamba alikuwa mwaminifu, na alimiliki kiini kilichopenda haki na mambo yaliyokuwa mazuri. Kwamba Ayubu mara nyingi alituma sadaka ya kuwateketeza na kwa niaba ya watoto wake wa kiume na kike na kuwatakasa kunamaanisha kwamba hakuruhusu wala kuidhinisha tabia ya watoto wake; badala yake katika moyo wake alichoshwa na tabia yao, na akawashutumu vikali. Alikuwa amethibitisha kwamba tabia ya watoto wake wa kike na kiume haikupendeza Yehova Mungu na hivyo basi mara nyingi aliwaita kwenda mbele ya Yehova Mungu na kutubu dhambi zao. Vitendo vya Ayubu vinatuonyesha upande mwingine wa ubinadamu wake: ule ambao unaonyesha kwamba hakuwahi kutembea na wale ambao mara nyingi walitenda dhambi na kumkosea Mungu, lakini badala yake alijiepusha na kutotaka kuwa nao. Hata ingawaje watu hawa walikuwa watoto wake wa kike na kiume, hakuziacha kanuni zake za kibinafsi kwa sababu walikuwa ukoo wake binafsi wala hakujihusisha kwa dhambi zao kwa sababu ya hisia zake binafsi za moyoni. Badala yake aliwasihi kutubu na kupata ustahimilivu wa Yehova Mungu na akawaonya kutomwacha Mungu kwa ajili ya kujifurahisha kwao kwa ulafi. Kanuni za namna ambavyo Ayubu aliwashughulikia wengine haziwezi kutenganishwa na zile kanuni za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Alipenda kile kilichokubalika na Mungu na kuchukia kile Alichokiona Mungu kuwa mbaya, na akawapenda wale waliomcha Mungu katika mioyo yao, na kuchukia wale waliotenda maovu au kutenda dhambi dhidi ya Mungu. Upendo na chuki kama hiyo zilionyeshwa katika maisha yake ya kila siku, na ndio uliokuwa unyofu wenyewe wa Ayubu ulioonekana katika macho ya Mungu. Kiasili, haya pia ndiyo maonyesho na kuishi kulingana na ubinadamu wa kweli wa Ayubu katika mahusiano yake na wengine katika maisha yake ya kila siku ambao lazima tujifunze kuhusu.

Maonyesho ya Ubinadamu wa Ayubu Wakati wa Majaribio Yake (Kuelewa Utimilifu wa Ayubu, Unyofu, Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu Wakati wa Majaribio Yake)

Kile tulichozungumzia hapo juu ni vipengele mbalimbali vya ubinadamu wa Ayubu zilizoonyeshwa katika maisha yake ya kila siku kabla ya majaribio yake. Bila shaka, maonyesho haya mbalimbali yanatupa ufahamu wa mwanzo pamoja na uelewa wa unyofu wa Ayubu, kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwake, na unatupa uthibitisho wa mwanzo. Sababu inayonifanya kusema “mwanzo” ni kwa kuwa watu wengi bado hawana uelewa wa kweli wa hulka ya Ayubu na kiwango ambacho alifuatilia njia ya kutii na kumcha Mungu. Hivi ni kusema, uelewa wa watu wengi kuhusu Ayubu hauendi zaidi ya ile picha ambayo kwa kiasi fulani inamfaa yeye kama ilivyoelezewa kwa maneno yake kwenye Biblia kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe” na “tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Hivyo, kunayo haja kubwa yetu sisi kuelewa namna ambavyo Ayubu aliishi kwa kudhihirisha ubinadamu wake alipokuwa akipokea majaribu ya Mungu; kwa njia hii, ubinadamu wote wa kweli wa Ayubu utaweza kuonyeshwa kwa wote.

Wakati Ayubu aliposikia kwamba mali yake ilikuwa imeibwa, kwamba watoto wake wa kike na kiume walikuwa wameaga dunia, na kwamba watumishi wake walikuwa wameuliwa, aliitikia hivi: “Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu” (Ayubu 1:20). Maneno haya yanatuambia ukweli mmoja: Baada ya kuzisikiza habari hizi, Ayubu hakushikwa na wasiwasi, hakulia, au kuwalaumu wale watumishi ambao walikuwa wamempa habari hizo, isitoshe hakukagua eneo la uhalifu ili kuchunguza na kuthibitisha ni kwa nini na ni vipi hali ilikuwa hivyo na kutaka kujua ni nini haswa kilichofanyika. Hakuonyesha maumivu au majuto yoyote kutokana na kupoteza mali yake wala hakuanza kupukutikwa na machozi kutokana na kuwapoteza watoto wake, wapendwa wake. Kinyume ni kwamba, akalirarua joho lake kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kuabudu. Vitendo vya Ayubu ni tofauti sana na vile vya binadamu wa kawaida. Vinawachanganya watu wengi, na kuwaruhusu kumkosoa Ayubu ndani ya mioyo yao kwa “kukosa huruma na rehema”. Kwa kupotea ghafla kwa mali yao, watu wa kawaida wangeonekana wamevunjwa moyo, au wanasikitika kweli—au kama ilivyo kwa baadhi ya watu, wanaweza hata kujipata wakiwa wamefadhaishwa moyo. Hii ni kwa sababu, katika mioyo yao, mali ya watu inawakilisha jitihada ya maisha yao yote, ndiyo ambayo maisha yao yanategemea, ndilo tumaini linalowafanya kuishi; kupoteza mali yao kunamaanisha jitihada zao zimeambulia patupu na kwamba hawana tumaini tena na kwamba pia hawana siku za usoni. Huu ndio mwelekeo wa mtu yeyote wa kawaida kuhusiana na mali yake na uhusiano wa karibu alio na mali hiyo, na huu ndio pia umuhimu wa mali katika macho ya watu. Hivyo, idadi kubwa ya watu wanahisi wakiwa wamechanganyikiwa na mwelekeo mtulivu wa Ayubu kuhusiana na kupoteza[a] mali yake. Leo, tutauondoa mkanganyiko huo wa watu hawa wote kwa kuelezea kile kilichokuwa kikipitia moyoni mwa Ayubu.

Akili za kawaida zinakariri kwamba, kwa kuwa alikuwa amepewa rasilimali hizo nyingi na Mungu, Ayubu anafaa kuaibika mbele ya Mungu kwa sababu ya kuzipoteza rasilimali hizi, kwani alikuwa hajazitunza, alikuwa hajashikilia zile rasilimali alizopewa na Mungu. Hivyo, aliposikia kwamba mali yake ilikuwa imeibwa, mwitikio wake wa kwanza ulifaa kuwa kuenda kwenye eneo la uhalifu na kuchukua hesabu ya kila kitu kilichokuwa kimeenda[b] na kisha kutubu kwa Mungu ili aweze kwa mara nyingine kupokea baraka za Mungu. Ayubu, hata hivyo hakufanya hivi—na kiasili alikuwa na sababu zake za kutofanya hivyo. Ndani ya Moyo wake, Ayubu alisadiki pakubwa kwamba kila kitu alichomiliki alikuwa amepewa na Mungu na hakikuwa kimetokana na jitihada zake yeye mwenyewe. Hivyo, hakuziona baraka hizo kama jambo la kutilia maanani, lakini alishikilia ile njia alifaa kuchukua kwa udi na uvumba kama kanuni zake za kuishi. Alizitunza baraka za Mungu, na akatoa shukrani kutokana nazo, lakini hakutamanishwa nazo wala hakutafuta baraka zaidi. Huo ndio uliokuwa mwelekeo wake kuhusu mali. Hakufanya chochote kwa minajili ya kupata baraka, wala kuwa na wasiwasi kuhusu au kuhuzunishwa kutokana na ukosefu au kupoteza baraka za Mungu; hakufurahi kwa njia ya kupindukia na isiyo na mipaka kwa sababu ya baraka za Mungu na wala hakupuuza njia ya Mungu wala kusahau neema ya Mungu kwa sababu ya zile baraka ambazo alifurahia mara kwa mara. Mtazamo wa Ayubu kwa mali yake unafichulia watu ubinadamu wake wa kweli: Kwanza, Ayubu hakuwa binadamu mlafi, na hakuwa na madai katika maisha yake yakinifu. Pili, Ayubu hakuwahi kuwa na wasiwasi au kuogopa kwamba Mungu angechukua kila kitu alichokuwa nacho, na ndio uliokuwa mwelekeo wake wa utiifu kwa Mungu ndani ya moyo wake; yaani, hakuwa na madai au malalamiko kuhusu ni lini au kama Mungu angechukua kutoka kwake, na wala hakuuliza sababu, lakini alilenga tu kutii mipango ya Mungu. Tatu, hakuwahi kusadiki kwamba rasilimali zake zilitokana na jitihada zake, lakini kwamba alipewa yeye na Mungu. Hii ilikuwa imani ya Ayubu kwa Mungu, na onyesho la imani yake. Je, ubinadamu wa Ayubu na ufuatiliaji wake wa kweli wa kila siku umefanywa kuwa wazi katika muhtasari huu wa hoja tatu kumhusu yeye? Ubinadamu na ufuatiliaji wa Ayubu ni vitu vilivyokuwa muhimu katika mwenendo wake mtulivu alipokabiliwa na hali ya kupoteza mali yake. Ilikuwa hasa kwa sababu ya ufuatiliaji wake wa kila siku ndipo Ayubu akawa na kimo na imani ya kusema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” kwenye majaribio ya Mungu. Maneno haya hayakupatwa kwa mkesha mmoja, na wala hayakujitokeza tu kwa ghafla kwenye kichwa chake Ayubu. Yalikuwa yale ambayo alikuwa ameona na kupata kwa miaka mingi ya kupitia safari ya maisha. Akilinganishwa na wale wote wanaotafuta tu baraka za Mungu na wanaoogopa Mungu atachukua kutoka kwao, nao wanachukia hali hio na wanalalamikia kuhusu hali hiyo, je utiifu wa Ayubu ni wa kweli haswa? Tukilinganisha na wale wote wanaosadiki kwamba Mungu yupo, lakini ambao hawajawahi kusadiki kwamba Mungu anatawala mambo yote, Ayubu anamiliki uaminifu na unyofu mkubwa?

Urazini wa Ayubu

Uzoefu halisi wa Ayubu na ubinadamu wake wenye unyofu na uaminifu ulimaanisha kwamba alifanya uamuzi na uchaguzi wenye urazini zaidi alipozipoteza rasilimali zake na watoto wake. Machaguo kama hayo ya kirazini yasingeweza kutenganishwa na shughuli zake za kila siku na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa amejua kwenye maisha yake ya siku baada ya siku. Uaminifu wa Ayubu ulimfanya kuweza kusadiki kwamba mkono wa Yehova Mungu unatawala mambo yote; imani yake ilimruhusu kujua ukweli wa ukuu wa Yehova Mungu juu ya vitu vyote; maarifa yake yalimfanya kuwa radhi na kuwa na uwezo wa kutii ukuu na mipangilio ya Yehova Mungu juu ya vitu vyote; utiifu wake ulimwezesha kuwa mkweli na mkweli zaidi katika kumcha kwake kwa Yehova Mungu; kumcha kwake kulimfanya kuwa halisi zaidi na zaidi katika kujiepusha kwake na maovu; hatimaye, Ayubu alikuwa mtimilifu kwa sababu alimcha Mungu na kujiepusha na maovu; na ukamilifu kwake kulimfanya kuwa na hekima zaidi na kukampa urazini wa kipekee.

Tunafaa kulielewa vipi neno hili “urazini”? Ufasiri wa moja kwa moja unamaanisha kwamba kuwa mwenye hisia nzuri, kuwa mwenye mantiki na wa kueleweka katika kufikiria kwako, kuwa na maneno ya kueleweka, vitendo na hukumu ya kueleweka, na kumiliki viwango visivyo na makosa na maadili ya mara kwa mara. Lakini urazini wa Ayubu hauelezwi sana kwa urahisi. Inaposemekana hapa kwamba Ayubu alimiliki urazini wa kipekee, inahusiana na ubinadamu wake na mwenendo wake mbele ya Mungu. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwaminifu, aliweza kuusadiki na kuutii ukuu wa Mungu, uliompa maarifa ambayo yasingeweza kupatikana na wengine na maarifa haya yalimfanya kuweza kutambua, kuhukumu, na kufafanua kwa usahihi zaidi yale yaliyompata, na yaliyomwezesha kuchagua ni nini cha kufanya na ni nini cha kushikilia kwa usahihi na wepesi zaidi wa kukata ushauri. Hivi ni kusema kwamba maneno, tabia, na kanuni zake ziliandamana na hatua zake, na msimbo ambao aliufanyia kazi, ulikuwa wa mara kwa mara, ulio wazi, na mahususi na haukukosa mwelekeo, wenye uamuzi wa haraka au wa kihisia. Alijua namna ya kushughulikia chochote kile kilichompata yeye, alijua namna ya kusawazisha na kushughulikia mahusiano kati ya matukio magumu, alijua namna ya kushikilia mambo kwa njia ambayo mambo hayo yalifaa kushikiliwa, na, vilevile, alijua namna ya kushughulikia ule utoaji na uchukuaji wa Yehova Mungu. Huu ndio uliokuwa urazini wenyewe wa Ayubu. Ilikuwa hasa kwa sababu Ayubu alijihami na urazini kama huu ndiposa akasema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” alipozipoteza rasilimali zake na watoto wake wa kiume na kike.

Wakati Ayubu alipokabiliwa na maumivu makali ya mwili, na malalamiko ya watu wa ukoo na marafiki zake, na wakati alipokabiliwa na kifo, mwenendo wake halisi kwa mara nyingine tena ulionyesha kimo chake kwa mambo yote.

Asili Halisi ya Ayubu: Mkweli, Aliyetakaswa, na Asiye na Uongo

Hebu tusome Ayubu 2:7-8: “Hivyo Shetani akatoka mbele za uwepo wa Yehova, na akamgonga Ayubu kwa majipu ya kuuma kutoka kwenye wayo wa mguu wake hadi utosini mwa kichwa chake. Na akachukua kigae kwa ajili ya kujikuna nacho; naye akakaa chini kwenye majivu.” Huu ni ufafanuzi wa mwenendo wa Ayubu wakati ambapo majipu yawashayo yalipoota kwenye mwili wake. Wakati huu, Ayubu aliketi kwenye majivu huku akiyavumilia. Hakuna aliyemtibu yeye, na hakuna aliyemsaidia kupunguza maumivu kwenye mwili wake; badala yake, alitumia kigaye cha chungu kukwaruza sehemu ya juu ya majipu yake yenye maumivu. Juu juu, hii ilikuwa awamu tu ya mateso ya Ayubu na haina uhusiano wowote na ubinadamu wake na kumcha Mungu kwake, kwani Ayubu hakuongea maneno yoyote kuonyesha hali na maoni yake wakati huo. Lakini matendo na mwenendo wake Ayubu bado ni onyesho la kweli la ubinadamu wake. Kwenye rekodi za sura ya awali tunasoma kwamba Ayubu alikuwa ndiye mkuu zaidi kati ya wanaume wote wa mashariki. Kifungu hiki cha sura ya pili, nayo, inatuonyesha kwamba binadamu huyu mkuu wa mashariki anafaa kuchukua kigae cha chungu na kujikwaruza nacho huku akiwa ameketi kwenye jivu. Je, hakuna ulinganuzi wowote wa wazi kati ya fafanuzi hizi mbili? Ni ulinganuzi unaotuonyesha nafsi ya kweli ya Ayubu: Licha ya nafasi na hadhi yake ya kifahari, hakuwahi kuzipenda wala kuzitilia maanani yoyote; hakujali namna wengine walivyoangalia nafasi yake wala kuhusu kama hatua au mwenendo wake ungekuwa na athari mbaya kwa nafasi yake; hakujihusisha katika utajiri wa hali, wala hakufurahia utukufu uliokuja pamoja na hadhi na nafasi yake katika jamii. Alijali tu kuhusu thamani yake na umuhimu wa kuishi kwake mbele ya macho ya Yehova Mungu. Nafsi ya kweli ya Ayubu ilikuwa kiini chake: Hakupenda umaarufu na utajiri, na wala hakuishi kwa ajili ya umaarufu na utajiri; alikuwa mkweli, na aliyetakaswa, na aliye bila ya uongo wowote.

Utenganisho wa Ayubu kati ya Upendo na Chuki

Upande mwingine wa ubinadamu wa Ayubu unaonyeshwa katika mazungumzo yake na mke wake: “Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe. Lakini yeye akasema kwake, Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” (Ayubu 2:9-10). Kuona mateso aliyokuwa akipitia, mke wa Ayubu alijaribu kumshauri Ayubu ili amsaidie kutoroka mateso yake—lakini zile “nia nzuri” hazikupata idhini ya Ayubu; badala yake, ziliamsha ndani yake hasira, kwani alikataa imani yake katika na utiifu wake kwa Yehova Mungu na pia akakataa uwepo wa Yehova Mungu. Hali hii isingeweza kuvumilika kwa Ayubu, kwani hakuwahi kujiruhusu kufanya chochote ambacho kingepinga au kingemdhuru Mungu, bila kusema chochote kuhusu wengine. Angewezaje kubakia vilevile bila kujali chochote wakati alipowaona wengine wakiongea maneno yaliyomkufuru na kumtukana Mungu? Hivyo basi akamuita mke wake “mwanamke mjinga.” Mwelekeo wa Ayubu kwa mke wake ulikuwa ule wa hasira na chuki, pamoja na ule wa kushutumu na kukemea. Haya ndiyo yaliyokuwa maonyesho ya kiasili ya ubinadamu wa Ayubu ambayo yalitofautisha kati ya upendo na chuki na yalikuwa uwakilishi wa kweli wa ubinadamu wake uliokuwa na unyofu. Ayubu alimiliki hali fulani ya haki—hali ambayo ilimfanya kuchukia upepo na mawimbi ya maovu, na kumfanya kuchukia, kushutumu, na kukataa uzushi wa ajabu, mabishano ya kijinga na madai yasiyokuwa na msingi, na ikamruhusu kushikilia kanuni zake sahihi, za kweli kwake yeye mwenyewe na msimamo ule aliochukua wakati alipokuwa amekataliwa na wengi na kuachwa na wale walio kuwa karibu na yeye.

Ukarimu na Uaminifu wa Ayubu

Kwa sababu, katika mwenendo wa Ayubu, tunaweza kuona maonyesho ya vipengele mbalimbali vya ubinadamu wake, tunauona ubinadamu wa Ayubu upi anapokifunua kinywa chake kuilaani siku aliyozaliwa? Hii ndiyo mada tutakayozungumzia hapa chini.

Hapo juu, Nimezungumzia asili ya laana la Ayubu ya siku ya kuzaliwa kwake. Mnaona nini katika haya? Kama Ayubu asingekuwa mkarimu na asiye na upendo, kama angekuwa mnyama na asiye na hisia, na mpungufu wa ubinadamu, angejali kuhusu tamanio la moyoni mwa Mungu? Na je angedharau siku ya kuzaliwa kwake kutokana na kuutunza moyo wa Mungu? Kwa maneno mengine kama Ayubu alikuwa hana ukarimu na aliyepungukiwa na ubinadamu, angedhikishwa na maumivu ya Mungu? Angeilaani siku yake ya kuzaliwa kwa sababu Mungu alikuwa amedhulumiwa na yeye? Jibu ni, bila shaka la! Kwa sababu alikuwa mkarimu, Ayubu aliutunza moyo wa Mungu; kwa sababu aliutunza moyo wa Mungu, Ayubu alihisi maumivu ya Mungu; kwa sababu alikuwa mkarimu, alipata maumivu makali zaidi kutokana na kuyahisi maumivu ya Mungu; kwa sababu aliyahisi maumivu ya Mungu, alianza kuichukia siku ya kuzaliwa kwake, na hivyo akailaani siku yake ya kuzaliwa. Kwa watu wa nje, mwenendo wote wa Ayubu wakati wa majaribio yake ni wa kupigiwa mifano. Kulaani kwake tu kwa siku ya kuzaliwa ndiko kunakoweka picha ya kiulizo juu ya utimilifu na unyofu wake, au kutoa utathmini tofauti. Kwa hakika, haya ndiyo yaliyokuwa maonyesho ya kweli zaidi ya kiini cha ubinadamu wa Ayubu. Kiini cha ubinadamu wake hakikufichwa au kubadilishwa, au kudurusiwa na mtu mwingine. Alipoilaani siku yake ya kuzaliwa, alionyesha ukarimu na uaminifu uliokuwa ndani ya moyo wake; alikuwa kama chemichemi ya maji ambayo maji yake yalikuwa safi sana na angavu kiasi cha kufichua sehemu ya chini kabisa ya chemichemi hio.

Baada ya kujifunza haya yote kuhusu Ayubu, watu wengi zaidi bila shaka watakuwa na utathmini sahihi kwa kiasi fulani na usiopendelea kuhusu kiini cha ubinadamu wa Ayubu. Wanafaa pia kuwa na uelewa na kina kikuu cha kimatendo, na uliopevuka zaidi wa utimilifu na unyofu wa Ayubu kama ulivyozungumzwa na Mungu. Ni tumaini langu kwamba, uelewa na kina hiki kitawasaidia watu kuanza kushughulikia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Uhusiano Kati ya Mungu kumpa Shetani Ayubu na Malengo ya Kazi ya Mungu

Ingawaje watu wengi sasa wanatambua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, utambuzi huu hauwapi uelewa mkubwa zaidi wa nia ya Mungu. Wakati huohuo wakionea wivu ubinadamu na ushughulikaji wa Ayubu, wanamuuliza Mungu swali lifuatalo: Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu sana, watu walimpenda sana, kwa hivyo kwa nini Mungu akamkabidhi kwa Shetani na kumpitishia maumivu haya makali? Maswali kama hayo yanatarajiwa kuwepo katika mioyo ya watu wengi—au, kushuku huku ndiko hasa swali katika mioyo ya watu wengi. Kwa sababu kushuku huku kumeshangaza watu wengi sana, lazima tuliwasilishe swali hili waziwazi na kulielezea kikamilifu.

Kila kitu ambacho Mungu anafanya kinahitajika, na kina umuhimu usio wa kawaida, kwani kila kitu anachofanya ndani ya binadamu kinahusu usimamizi wake na wokovu wa wanadamu. Kiasili kazi ambayo Mungu alimfanyia Ayubu si tofauti, ingawaje Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu mbele ya macho ya Mungu. Kwa maneno mengine, licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kufanya, licha ya gharama, au lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili[c] na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, Shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemletea Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribio na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaoibuka katika majaribio na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda Shetani ni wale waliookolewa na Mungu. Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribio ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumtunza Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawatekwi bakunja, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani, wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa. Ayubu alikuwa mtu kama huyo mwenye uhuru na huu ndio umuhimu hasa wa kwa nini Mungu alikuwa amemkabidhi kwa Shetani.

Ayubu alidhulumiwa na Shetani, lakini pia aliweza kupata uhuru na ukombozi wa milele, na kupata haki ya kutowahi kukabidhiwa tena kwa upotovu, unyanyasaji, na mashtaka ya Shetani, na badala yake kuishi katika nuru ya udhibiti wa Mungu usio na pingamizi na kuishi katikati ya baraka kutoka kwa Mungu. Hakuna ambaye angechukua au kuangamiza, au kupata haki hii. Ilipewa kwa Ayubu kutokana na imani, bidii, na utiifu wake kwa na kumcha Mungu; Ayubu alilipia gharama ya maisha yake ili kuweza kupata shangwe na furaha duniani, ili kufanikiwa kupata haki na kuweza kustahili, kama ilivyoamriwa mbinguni na kutambuliwa na dunia, ili kumwabudu Muumba bila ya uingiliaji kati kama kiumbe wa kweli wa Mungu duniani. Hivyo pia ndivyo yalivyokuwa matokeo makubwa zaidi ya majaribio yaliyovumiliwa na Ayubu.

Wakati watu bado hawajaokolewa, maisha yao mara nyingi yanaingiliwa kati na hata kudhibitiwa na, Shetani. Kwa maneno mengine, watu ambao hawajaokolewa ni wafungwa wa Shetani, hawana uhuru, hawajaachiliwa na Shetani, hawajafuzu wala kustahili kumwabudu Mungu, na wanafuatiliwa kwa karibu na kushambuliwa kwa ukali na Shetani. Watu kama hawa hawana furaha ya kuzungumzia, hawana haki ya uwepo wa kawaida wa kuzungumzia, na zaidi hawana heshima ya kuzungumzia. Ni pale tu unaposimama imara na kupigana na Shetani, kwa kutumia imani yako katika Mungu na utiifu kwake, pamoja na kumcha Mungu kama silaha ambazo utatumia kupigana vita vya maisha na mauti dhidi ya Shetani, kiasi cha kwamba utamshinda kabisa Shetani na kumsababisha kukata tamaa na kuwa mwoga kila anapokuona wewe, ili aache kabisa mashambulizi na mashtaka yake dhidi yako—hapo tu ndipo utakapookolewa na kuwa huru. Kama umeamua kutengana kabisa na Shetani lakini huna silaha zitakazokusaidia kupigana na Shetani, basi bado utakuwa katika hatari; kwa kadri muda unaposonga, baada ya wewe kuteswa na Shetani kiasi cha kwamba huna hata usuli wa nguvu uliobakia ndani mwako, lakini bado hujaweza kuwa na ushuhuda, bado hujajifungua kabisa kuwa huru dhidi ya mashtaka na mashambulizi ya Shetani dhidi yako, basi utakuwa na tumaini dogo la wokovu. Mwishowe, wakati hitimisho la kazi ya Mungu itakapotangazwa, bado utakuwa katika mashiko ya Shetani, usiweze kujiachilia kuwa huru, na hivyo hutawahi kuwa na fursa au tumaini. Matokeo yake, hivyo basi, ni kwamba watu kama hao watakuwa mateka kabisa wa Shetani.

Kubali Mitihani ya Mungu, Shinda Majaribio ya Shetani, na Mruhusu Mungu Kupata Nafsi Yako Nzima

Wakati wa kazi wa utoaji Wake wa kudumu na msaada kwa binadamu, Mungu anaambia binadamu kuhusu mapenzi Yake na mahitaji Yake yote, na anaonyesha vitendo Vyake, tabia, na kile Anacho na alicho kwa binadamu. Lengo ni kuweza kumtayarisha binadamu ili awe na kimo, na kumruhusu binadamu kupata ukweli mbalimbali kutoka kwa Mungu wakati anaendelea kumfuata Yeye—ukweli ambao ni silaha alizopewa binadamu na Mungu ambazo atatumia kupigana na Shetani. Hivyo akiwa na silaha hizo, binadamu lazima akabiliane na mitihani ya Mungu. Mungu anazo mbinu na njia nyingi za kumjaribu binadamu, lakini kila mojawapo inahitaji “ushirikiano” wa adui wa Mungu: Shetani. Hivi ni kusema, baada ya kumpa binadamu silaha ambazo atatumia kupigana na Shetani, Mungu anamkabidhi binadamu kwa Shetani na kuruhusu Shetani “kujaribu” kimo cha binadamu. Kama binadamu anaweza kufanikiwa dhidi ya uundaji wa vita vya Shetani, kama anaweza kutoroka mizunguko ya Shetani na bado akaishi, basi mwanadamu atakuwa ameupita mtihani. Lakini kama binadamu atashindwa kuondoka kwenye uundaji wa vita vya Shetani, na kujinyenyekeza kwa Shetani, basi hatakuwa ameupita mtihani. Haijalishi ni kipengele kipi cha binadamu ambacho mungu anachunguza, kigezo cha uchunguzi Wake ni kama binadamu atasimama imara katika ushuhuda wake atakaposhambuliwa na Shetani au la, kujua kama amemuacha Mungu au la na akajisalimisha na akajinyenyekeza kwa Shetani baada ya kunaswa na Shetani. Inaweza kusemekana kwamba, iwapo binadamu anaweza kuokolewa au la yote haya yanategemea kama anaweza kumzidi na kumshinda Shetani, na kama ataweza kupata uhuru au la yanategemea kama anaweza kuinua, yeye binafsi, silaha alizopewa na Mungu ili kushinda utumwa wa Shetani, na kumfanya Shetani kuwacha kabisa tumaini na kumwacha pekee. Kama Shetani ataliacha tumaini na kumwachilia mtu, hii inamaanisha kwamba Shetani hatawahi tena kujaribu kuchukua mtu huyu kutoka kwa Mungu hatawahi tena kumshtaki na kuingilia kati mtu huyu, hatawahi tena kutaka kumtesa au kumshambulia; mtu kama huyu tu ndiye atakuwa kwa kweli amepatwa na Mungu. Huu ndio mchakato mzima ambao Mungu anapata watu.

Onyo na Nuru Iliyotolewa kwa Vizazi vya Baadaye Na Ushuhuda wa Ayubu

Huku wakielewa mchakato ambao Mungu anampata kabisa mtu, watu wataweza pia kuelewa nia na umuhimu wa Mungu kumpeleka Ayubu kwa Shetani. Watu hawasumbuliwi tena na maumivu makali ya Ayubu, na wanatambua upya umuhimu wake. Hawawi na wasiwasi tena kuhusu kama wao wenyewe watapitia majaribio sawa na yale ya Ayubu, na hawapingi tena au kukataa tena ujio wa majaribio ya Mungu. Imani, utiifu, na ushuhuda wake Ayubu wa kushinda Shetani, vyote hivi vimekuwa ni chanzo cha msaada mkubwa na himizo kwa watu. Kwa Ayubu, wanaona tumaini la wokovu wao binafsi, na wanaona kwamba kupitia kwa imani na utiifu kwa na kumcha Mungu, inawezekana kabisa kushinda Shetani, na kumshinda Shetani. Wanaona kwamba mradi tu waukubali ukuu na mipangilio ya Mungu, na kumiliki uamuzi na imani ya kutomwacha Mungu baada ya kupoteza kila kitu, basi wanaweza kumletea Shetani aibu na hali ya kushindwa, na kwamba wanahitaji tu kumiliki uamuzi na ustahimilivu wa kusimama imara katika ushuhuda wao—hata kama itamaanisha kupoteza maisha yao—ili Shetani aweze kuaibika na kurejea nyuma haraka. Ushuhuda wa Ayubu ni onyo kwa vizazi vya baadaye, na onyo hili linawaambia kwamba kama hawatamshinda Shetani, basi hawatawahi kuweza kujiondolea mashtaka na uingiliaji kati wa Shetani, na wala hawatawahi kuweza kutoroka dhulma na mashambulizi ya Shetani. Ushuhuda wa Ayubu ulipatia nuru vizazi vya baadaye. Upatiaji Nuru huu unafunza watu kwamba ni pale tu wanapokuwa watimilifu na wanyofu ndipo watakapoweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; unawafunza kwamba ni pale tu wanapomcha Mungu na kujiepusha na maovu ndipo watakapoweza kuwa na ushuhuda wenye udhabiti na wa kipekee kwa Mungu; pale tu watakapokuwa na ushuhuda dhabiti na wakipekee wa Mungu ndipo hawatawahi kudhibitiwa na Shetani, na kuishi katika mwongozo na ulinzi wa Mungu—na hapo tu ndipo watakapokuwa wameokolewa kwa kweli. Hulka ya Ayubu na ufuatiliaji wake wa maisha unafaa kuigwa na kila mmoja anayefuata wokovu. Kile alichoishi kwa kudhihirisha katika maisha yake yote na mwenendo wake wakati wa majaribio yake ni hazina yenye thamani kwa watu wote wanaotaka kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Tanbihi:

a. Maandishi asilia yameacha “kupotezwa kwa.”

b. Maandishi asilia yameacha “yaliyo kuwa yameenda.”

c. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp