Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) (Sehemu ya Pili)

Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingeweza kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo. Kwa aina hiyo ya mazingira yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni ya kufaa na yapo katika mpangilio, aina zote za watu duniani, aina zote za jamii zinaweza kuishi ndani ya mawanda yao husika. Hakuna anayeweza kwenda zaidi ya mawanda haya au mipaka hii kwa sababu ni Mungu ambaye ameichora. Kwa nini Mungu aichore kwa namna hii? Hii ni muhimu sana kwa binadamu wote—ni muhimu sana! Mungu alichora mawanda ya kila aina ya kiumbe hai na aliweka mbinu ya kuendelea kuishi kwa kila aina ya binadamu. Pia aligawanya aina mbalimbali za watu na jamii mbalimbali duniani na akaweka mawanda yao. Hiki ndicho tunachotaka kujadili wakati ujao.

Nne, Mungu alichora mipaka kati ya jamii za rangi tofautitofauti. Duniani kuna watu weupe, watu weusi, watu wa kahawia na watu wa njano. Hawa ni aina tofauti za watu. Mungu pia aliweka mawanda kwa ajili ya maisha ya aina hizi tofauti za watu, na bila kutambua, watu wanaishi ndani ya mazingira yao stahiki kwa kuendelea kuishi chini ya usimamizi wa Mungu. Hakuna anayeweza kwenda nje ya hapa. Kwa mfano, wazungu, ni maeneo gani ambayo wanaishi kwa kiasi kikubwa? Kwa kiasi kikubwa wanaishi Ulaya na Marekani. Watu weusi kimsingi wanaishi Afrika. Na watu wa rangi ya kahawia wanaishi ndani ya eneo gani? (Asia Kusini-mashariki.) Kama vile Thailand, India, Myanmar, Vietnam na Laos. Hasa wanaishi Kusini-mashariki mwa Asia na Asia Kusini. Watu wa njano kimsingi wanaishi Asia, yaani, China, Japan, Korea ya Kusini na nchi nyinginezo kama hizo. Mungu amegawanya aina hizi tofautitofauti za jamii kwa usawa kiasi kwamba jamii hizi tofautitofauti zimegawanywa katika sehemu tofautitofauti za dunia. Katika sehemu tofautitofauti hizi za dunia, Mungu aliandaa zamani sana mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yanayofaa kwa ajili ya kila jamii tofauti ya binadamu. Ndani ya aina hizi za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi, Mungu amewaandalia rangi na vijenzi vya udongo. Kwa maneno mengine, vijenzi katika miili ya watu weupe havifanani na vile vilivyo ndani ya miili ya watu weusi, na pia ni tofauti na vijenzi vya miili ya watu wa jamii nyinginezo. Mungu alipoumba viumbe vyote, tayari Alikuwa ameandaa mazingira ya namna hiyo kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa jamii hiyo. Lengo Lake katika hili lilikuwa kwamba pale ambapo aina hiyo ya watu inaanza kuongezeka, watakapoanza kuongezeka kwa idadi, wangeweza kuwekwa ndani ya mawanda hayo. Kabla Mungu hajawaumba binadamu alikuwa amekwishatafakari yote—Angeweza kutoa Ulaya na Amerika kwa watu weupe na kuwaruhusu kuliendeleza na kuendelea kuishi. Kwa hiyo Mungu alipokuwa anatengeneza dunia tayari Alikuwa na mpango, alikuwa na nia na kusudi katika kile alichokuwa anakiweka katika kipande hicho cha ardhi, na kile ambacho kingelelewa katika kipande hicho cha ardhi. Kwa mfano, Mungu zamani sana aliandaa mlima upi, tambarare ngapi, vyanzo vya maji vingapi, ni aina gani ya ndege na wanyama, samaki gani, na mimea gani ingeweza kuwepo katika ardhi hiyo. Alipokuwa anaandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina ya binadamu, kwa ajili ya jamii, Mungu aliangalia vipengele vingi vya masuala: mazingira ya kijiografia, vijenzi vya udongo, aina ya ndege na wanyama, ukubwa wa aina tofautitofauti za samaki, vijenzi katika samaki, ubora tofauti wa maji, vilevile aina tofauti za mimea…. Mungu alikuwa ameandaa yote hayo zamani sana. Aina hiyo ya mazingira ni mazingira ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaumba na kuyaandaa kwa ajili ya watu weupe. Mmeweza kuona kwamba Mungu alipoviumba viumbe vyote Alitafakari sana na Alifanya vitu kwa mpango? (Ndiyo.) Mmeona nini? (Fikira za Mungu kwa aina mbalimbali za watu zilikuwa ni za uangalifu sana. Kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina tofautitofauti za binadamu, aliandaa aina za ndege na wanyama na aina za samaki, milima mingapi na tambarare ngapi zitakuwepo. Yote haya yalifikiriwa kwa uangalifu sana na kwa usahihi.) Kwa mfano, vyakula wanavyokula wazungu hasa ni vipi? Vyakula ambavyo watu weupe wanakula ni tofauti sana na vyakula ambavyo watu wa Asia wanakula. Vyakula vikuu ambavyo watu weupe wanakula hasa ni nyama, mayai, maziwa, na kuku. Nafaka kama vile mkate na mchele kwa ujumla sio chakula kikuu ambacho kinawekwa pembeni mwa sahani. Hata pale wanapokula kachumbari ya mboga, wanaweka kiasi cha nyama ya kukaanga au kuku ndani yake. Hata kama wanakula vyakula vinavyotokana na ngano, wanaongeza siagi, mayai, au nyama kwenye chakula hicho. Hiyo ni kusema, vyakula vyao vikuu havijumuishi hasa vyakula vinavyotokana na ngano au mchele; wanakula sana nyama na siagi. Mara nyingi wanakunywa maji ya barafu kwa sababu wanakula vyakula vyenye kalori ya juu sana. Kwa hiyo watu weupe ni wenye afya kweli. Hivi ndivyo vyanzo vya maisha yao, mazingira yao kwa ajili ya kuishi yaliandaliwa na Mungu kwa ajili yao, yanawafanya wawe na aina hiyo ya mtindo wa maisha. Mtindo huo wa maisha ni tofauti na mitindo ya maisha ya watu wa jamii nyingine. Hakuna baya au zuri katika mtindo huu wa maisha—ni wa kuzaliwa, uliamuliwa kabla na Mungu na kwa sababu ya kanuni ya Mungu na mipangilio Yake. Aina hii ya mbari ina mtindo fulani wa maisha na vyanzo fulani vya riziki zao kitu ambacho ni kwa sababu ya mbari yao, vilevile ni kwa sababu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoandaliwa na Mungu kwa ajili yao. Mngeweza kusema kwamba mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaandaa kwa ajili ya watu weupe na chakula cha kila siku wanachokipata kutoka katika mazingira hayo ni kingi na kimejaa tele.

Mungu pia aliandaa mazingira faafu kwa ajili ya mbari nyingine kuendelea kuishi. Pia kuna watu weusi—watu weusi wanapatikana wapi? Hasa wanapatikana katikati na kusini mwa Afrika. Mungu aliwaandalia nini kwa ajili ya kuishi katika aina hiyo ya mazingira? Misitu ya kitropiki, aina zote za ndege na wanyama, pia majangwa, na aina zote za mimea ambayo inaambatana nao. Wana vyanzo vya maji, riziki zao, na chakula. Mungu hakuwabagua. Bila kujali kile walichowahi kukifanya, kuendelea kuishi kwao hakujawahi kuwa tatizo. Pia wanachukua mahali fulani maalumu na eneo fulani katika sehemu ya dunia.

Sasa, hebu tuzungumze kidogo kuhusu watu wa njano. Watu wa njano hasa wanapatikana nchi za Mashariki. Kuna tofauti gani kati ya mazingira na sehemu za kijiografia za nchi za Mashariki na nchi za Magharibi? Katika nchi za Mashariki, eneo kubwa la ardhi ni la rutuba, na zina hazina kubwa ya vitu na madini. Yaani, aina zote za rasilimali za juu ya ardhi na za chini ya ardhi zimejaa tele. Na kwa kundi hili la watu, kwa mbari hii, Mungu pia aliandaa udongo, hali ya hewa inayofanana nao, na mazingira mbalimbali ya kijiografia ambayo yanawafaa. Ingawa kuna tofauti kubwa kati ya mazingira hayo ya kijiografia na mazingira ya nchi za Magharibi, chakula cha lazima cha watu, riziki, na vyanzo kwa ajili ya kuendelea kuishi viliandaliwa na Mungu. Ni mazingira tofauti tu kwa ajili ya kuishi kuliko yale ambayo watu weupe wanayo katika nchi za Magharibi. Lakini kitu kimoja ni kipi ambacho Ninahitaji kuvuta usikivu wenu, ambacho Ninahitaji kuwaambia? Idadi ya mbari ya Mashariki kiasi fulani ni kubwa, hivyo Mungu aliongeza vipengele vingi katika kipande hicho cha ardhi ambavyo ni tofauti na vya Magharibi. Katika upande huo wa dunia, Aliongeza mandhari mengi mbalimbali na aina zote za vitu vingi. Huko rasilimali za asili ni tele; mandhari pia yanatofautiana na anuwai, yanatosha kwa ajili ya kulea idadi kubwa ya mbari ya Mashariki. Kitu fulani ambacho ni tofauti na Magharibi ni kwamba Mashariki—kutoka kusini kwenda kaskazini, kutoka mashariki kwenda magharibi—hali ya hewa ni nzuri kuliko ya Magharibi. Misimu minne imeoneshwa kinaganaga, hali ya joto ni nzuri, rasilimali za asili zipo tele, mazingira ya asili na aina za mandhari ni mazuri zaidi kuliko ya Magharibi. Kwa nini Mungu alifanya hivi? Mungu alitengeneza uwiano razini kabisa kati ya watu weupe na watu wa njano. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuwa kila kipengele cha chakula chao, vitu ambavyo wanatumia, kile ambacho watu weupe wanacho cha kujifurahisha ni kizuri zaidi kuliko kile ambacho watu wa njano wanaweza kukifurahia. Hata hivyo, Mungu habagui mbari yoyote. Mungu aliwapatia watu wa njano mazingira mazuri na bora zaidi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hii ni uwiano. Kwa hiyo mnaelewa, siyo?

Mungu ameamua kabla ni aina gani ya watu waishi katika sehemu ipi ya dunia na binadamu hawawezi kwenda nje ya mawanda haya. Hili ni jambo la ajabu! Hata kama kuna vita au uvamizi katika enzi mbalimbali au nyakati fulani, vita hivi, uvamizi huu, hakika hauwezi kuharibu mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaamua kabla kwa ajili ya kila mbari. Yaani, Mungu amewaweka aina fulani ya watu katika eneo fulani la dunia na hawawezi kwenda nje ya mawanda hayo. Hata kama watu wana lengo la kubadilisha au kuongeza eneo lao, bila ruhusa ya Mungu, hii itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Kwa mfano, watu weupe walitaka kuongeza maeneo yao na wakazitawala kwa mabavu baadhi ya nchi. Wajerumani walivamia baadhi ya nchi, Uingereza waliitwaa India. Matokeo yalikuwa ni nini? Mwishowe walishindwa. Tunaona nini kutokana na kushindwa huku? Kile ambacho Mungu amekiamua kabla hakiwezi kuharibiwa. Kwa hiyo, haijalishi ni nguvu kubwa kiasi gani ambayo umeweza kuiona katika upanuzi wa Uingereza, mwishowe matokeo ni kwamba bado walitakiwa kuondoka na ardhi hiyo bado ni ya India. Wale ambao wanaishi katika ardhi hiyo bado ni Wahindi, na si Waingereza. Hii ni kwa sababu ni kitu ambacho Mungu haruhusu. Baadhi ya wale ambao wanatafiti historia au siasa wametoa tasnifu juu ya hili. Wanatoa sababu kwa nini Uingereza ilishindwa, wanasema kwamba pengine ilikuwa ni kwa sababu mbari fulani isingeweza kushindwa, au pengine ni kwa sababu ya sababu nyinginezo za kibinadamu…. Hizi sio sababu za kweli. Sababu ya kweli ni kwa sababu ya Mungu—Haruhusu hilo! Mungu anaamua mbari waishi katika nchi fulani na Anawaweka hapo, na kama Mungu hawaruhusu kuhama hawataweza kuhama kamwe. Ikiwa Mungu ataamua mawanda kwa ajili yao, wataishi ndani ya mawanda hayo. Binadamu hawezi kuvunja bure au kwenda nje ya mawanda haya. Hii ni hakika. Haijalishi nguvu za wavamizi ni kubwa kiasi gani, au jinsi gani wale wanaovamiwa ni dhaifu, mafanikio yao mwishowe yanamtegemea Mungu. Ameshaliamua hili tayari na hakuna anayeweza kulibadilisha.

Hivi ndivyo Mungu alivyogawanya mbari mbalimbali. Ni kazi gani ambayo Mungu amefanya kuzigawanya mbari? Kwanza, aliandaa mazingira makubwa ya kijiografia, Akiwapa watu maeneo tofautitofauti, na kisha kizazi baada ya kizazi kinaendelea kuishi pale. Hii imeamuliwa—mawanda ya kuendelea kuishi kwao yameamuliwa. Na maisha yao, kile wanachokula, kile wanachokunywa, riziki zao—Mungu aliamua hayo yote zamani sana. Na Mungu alipokuwa anaumba viumbe vyote, Alifanya maandalizi tofautitofauti kwa ajili ya aina tofauti za watu: Kuna vijenzi tofautitofauti vya udongo, hali ya hewa tofauti, mimea tofauti, na mazingira tofauti ya kijiografia. Maeneo tofautitofauti yana hata ndege na wanyama tofauti, maji tofauti yana aina tofauti za samaki wao spesheli na bidhaa za majini. Hata aina ya wadudu inaamuliwa na Mungu. Kwa mfano, shorewanda wa Marekani ni tofauti na shorewanda wa China bara. Vitu ambavyo vinakua katika bara la Marekani vyote ni vikubwa sana, virefu sana na vyenye nguvu sana. Mizizi ya miti msituni yote haina kina kirefu kabisa, lakini inakua mirefu sana. Inaweza kurefuka hadi kufikia zaidi ya mita mia moja, lakini miti katika misitu ya Asia kwa kiasi kikubwa si mirefu kiasi hicho. Nina uhakika wote mmekwishawahi kusikia juu ya mimea ya mshubiri. Japan ni midogo sana, membamba sana, lakini mimea ya mshubiri Marekani ni mikubwa sana. Hii ni tofauti. Ni aina ile ile ya mmea ikiwa na jina lile lile, lakini katika bara la Marekani ni kubwa hasa. Tofauti katika vipengele hivi tofautitofauti zinaweza zisionekane au kufahamika kwa watu, lakini Mungu alipokuwa anaumba viumbe vyote, alivionyesha kinaganaga na aliandaa mazingira tofauti ya kijiografia, mandhari tofauti, na viumbe hai tofauti kwa ajili ya mbari mbalimbali. Hiyo ni kwa sababu Mungu aliumba aina tofautitofauti za watu, na Anajua kile ambacho kila mmoja anahitaji na mitindo yao ya maisha ni nini.

Baada ya kuzungumza juu ya baadhi ya vitu hivi, sasa mna uelewa fulani wa mada kuu ambayo tumeijadili hivi punde? Je, mmeielewa kwa kiasi fulani? Kuna sababu ambayo nimeongea kuhusu mambo haya ndani ya mada pana—sasa mnapaswa kuwa mmeelewa angalau kwa muhtasari. Mnaweza kuniambia mmeelewa kwa kiasi gani. (Binadamu wote wamelelewa kwa sheria tu ambazo ziliamuliwa na Mungu kwa ajili ya vitu vyote. Mungu alipokuwa anaamua sheria hizi, Aliandaa mbari tofautitofauti zikiwa na mazingira tofauti, mitindo tofauti ya maisha, vyakula tofauti, na hali ya hewa na halijoto tofauti. Hii ilikuwa hivyo ili binadamu wote waweze kuishi duniani na kuendelea kuishi. Kutokana na hili naweza kuuona mpango wa usimamizi wa Mungu na mipango yake angalifu na sahihi vilevile hekima na ukamilifu Wake.) (Sheria na mawanda yaliyoamuliwa na Mungu hayawezi kubadilishwa kabisa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Yote ipo chini ya kanuni Yake.) Tukiangalia kwa mtazamo wa sheria zilizoamriwa na Mungu kwa ukuaji wa vitu vyote, yote hii si kwa ajili ya mwanadamu, haijalishi ni wa aina gani, anaishi chini ya uangalizi wa Mungu—je, wote hawaishi chini ya malezi Yake? Ikiwa sheria hizi zingeharibiwa au Mungu hakuanzisha aina hizi za sheria kwa ajili ya binadamu, majaliwa yao yangekuwa ni nini? Baada ya binadamu kupoteza mazingira yao ya msingi kwa ajili ya kuendelea kuishi, je, wangekuwa na chanzo chochote cha chakula? Inawezekana kwamba vyanzo vya chakula vingekuwa tatizo. Ikiwa watu wangepoteza vyanzo vyao vya chakula, yaani, ikiwa hawangeweza kupata kitu chochote cha kula, ni siku ngapi wangeweza kuvumilia? Pengine wasingeweza kuvumilia hata kwa mwezi mmoja, na kuendelea kuishi kwao kungekuwa ni tatizo. Kwa hiyo kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa ajili ya watu kuendelea kuishi, kwa ajili ya wao kuendelea kuwepo, kuongezeka, na ruzuku ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya miongoni mwa vitu vyote vinahusiana kwa karibu na haviwezi kutenganishwa na watu kuendelea kuishi. Ikiwa kuendelea kuishi kwa binadamu kulikuwa tatizo, je, usimamizi wa Mungu ungeweza kuendelea? Je, usimamizi wa Mungu bado ungekuwepo? Usimamizi wa Mungu unakwenda sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu wote ambao Anawalea, kwa hivyo haijalishi Mungu anaandaa kitu gani kwa ajili ya vitu vyote na kile Anachofanya kwa ajili ya binadamu, hii yote ndiyo lazima Kwake, na ni muhimu sana kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ikiwa sheria zote hizi ambazo Mungu aliziamua kwa ajili ya vitu vyote zingekuwa zimeachwa, ikiwa sheria hizi zingekuwa zimevunjwa au zimeharibiwa, vitu vyote visingeweza kuwepo, mazingira ya binadamu ya kuendelea kuwepo yasingekuwepo, na wala riziki zao za kila siku, na wala wao wenyewe. Kwa sababu hii, Usimamizi wa Mungu wa wokovu wa binadamu wala nao usingekuwepo pia.

Kila kitu ambacho tumejadili, kila kitu, kila kipengele kimeungana kikamilifu na kuendelea kuishi kwa kila mtu. Mnaweza kusema, “Unachokizungumzia ni kikubwa sana, hatuwezi kukiona,” na pengine kuna watu ambao wangeweza kusema “Unachokizungumzia hakinihusu.” Hata hivyo, usisahau kwamba unaishi kama sehemu tu ya vitu vyote; wewe ni mshirika wa vitu vyote ndani ya kanuni ya Mungu. Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake. Baadhi ya watu wanasema: “Mimi sio mkulima, sipandi mazao kwa ajili ya kuishi. Sitegemei mbingu ili nipate chakula changu, kwa hiyo naweza kusema kwamba siendelei kuishi katika mazingira ambayo aliyaanzisha Mungu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Aina hiyo ya mazingira haijanipatia kitu chochote.” Hii ni kweli? Unasema kwamba hupandi mazao kwa ajili ya kuishi, lakini huli nafaka? Huli nyama na mayai? Je, huli mbogamboga na matunda. Kila kitu unachokula, vitu hivi vyote unavyovitaka havitenganishwi na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoanzishwa na Mungu kwa ajili ya binadamu. Na chanzo cha kila kitu ambacho binadamu anahitaji hakiwezi kutenganishwa na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, aina hizo za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Maji unayokunywa, nguo unazovaa, na vitu vyote unavyotumia—ni kitu gani kati ya hivi ambacho hakipatikani kutoka katika vitu hivi vyote? Baadhi ya watu husema: “Kuna baadhi ya vitu ambavyo havipatikani kutoka katika vitu vyote hivi. Unaona, plastiki haitokani na vitu vyote hivi. Ni kitu cha kemikali, kitu kilichotengenezwa na mwanadamu.” Hii ni sahihi? Plastiki imetengenezwa na mwanadamu, ni kitu cha kemikali, lakini vijenzi asilia vya plastiki vilitoka wapi? Vijenzi asilia vilipatikana kutoka katika vitu ambavyo kwa asili vilitengenezwa na Mungu. Vitu ambavyo unavifurahia, ambavyo unaona, kila kitu ambacho unatumia, vyote vinapatikana kutoka katika vitu vyote ambavyo vilitengenezwa na Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, haijalishi ni mbari gani, haijalishi ni riziki gani, au ni katika aina gani ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo watu wanaishi, hawawezi kujitenganisha na uangalizi wa Mungu. Kwa hiyo mambo haya tuliyoyajadili leo yanahusiana na mada yetu ya “Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote”? Je, vitu tulivyovijadili leo vinaangukia chini ya mada hii kubwa? (Ndiyo.) Pengine baadhi ya ambayo nimeyazungumzia leo ni ya kidhahania kidogo na ni vigumu kidogo kuweza kuyajadili. Hata hivyo, Nadhani kwamba sasa mnaelewa vizuri kidogo.

Nyakati chache hizi katika ushirika, kiwango cha mada ambazo tumekuwa nazo katika ushirika ni kipana sana, na mawanda yao ni mapana, kwa hiyo unapaswa uwe na jitihada kiasi fulani ili uweze kuzielewa zote. Hii ni kwa sababu mada hizi ni vitu ambavyo watu hawajawahi kukabiliana navyo katika imani yao kwa Mungu. Baadhi ya watu wanaisikia kama muujiza na baadhi ya watu wanaisikia kama hadithi—mtazamo gani ni sahihi? Unasikia haya yote kutoka katika mtazamo gani? (Tumeyaona matendo ya Mungu, vilevile kwa mbinu gani Amepangilia vitu vyote na kwamba vitu vyote vina sheria hizi na kupitia maneno haya tunaweza kuelewa zaidi juu ya matendo ya Mungu na mpangilio wake angalifu na sahihi kwa ajili ya kumwokoa binadamu.) Kupitia nyakati hizi katika ushirika, Mmeona mawanda ya usimamizi wa Mungu wa vitu vyote ni nini? (Binadamu wote, kila kitu.) Je, Mungu ni Mungu wa mbari moja? Je, ni Mungu wa aina moja ya watu? Je, ni Mungu wa eneo dogo la binadamu? (Hapana, hayupo hivyo.) Kwa kuwa Hayupo hivyo, katika maarifa ya watu juu ya Mungu, ikiwa angekuwa ni Mungu wa sehemu ndogo tu ya binadamu, au ikiwa unaamini kwamba Mungu ni Mungu wako tu, je, mtazamo huu upo sahihi? Kwa kuwa Mungu anasimamia na kutawala vitu vyote, watu wanapaswa kuona matendo Yake, hekima Yake, na ukuu Wake ambavyo vimefunuliwa katika utawala Wake wa vitu vyote. Hiki ni kitu ambacho watu wanapaswa kufahamu. Ikiwa unasema kwamba Mungu anasimamia viumbe vyote, na Anatawala binadamu wote, lakini kama huna uelewa wowote au umaizi katika utawala Wake kwa binadamu, je, unaweza kutambua kwamba Anatawala vitu vyote? Unaweza kufikiri moyoni mwako, “Ninaweza, kwa sababu ninaona kwamba maisha yangu haya yote yanatawaliwa na Mungu.” Je, kweli Mungu ni mdogo kiasi hicho? Hayupo hivyo! Unaona tu wokovu wa Mungu kwa ajili yako na kazi yake kwako, na kutokana na vitu hivi unauona utawala Wake. Hayo ni mawanda finyu sana, na yana athari katika maarifa yako halisi juu ya Mungu. Pia yanaweka mipaka kwenye maarifa yako halisi juu ya utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Ikiwa unayawekea mipaka maarifa Yake kwenye mawanda ya kile ambacho Mungu anatoa kwa ajili yako na wokovu Wake kwa ajili yako, hutaweza kutambua kwamba anatawala kila kitu, kwamba anatawala vitu vyote, na anatawala binadamu wote. Unaposhindwa kutambua haya yote, je, kweli unaweza kutambua ukweli kwamba Mungu anatawala majaliwa yako? Huwezi. Moyoni mwako hutaweza kutambua kipengele hicho—hutoweza kutambua kiwango hicho. Unaelewa, siyo? Kwa kweli, Ninajua ni kwa kiwango gani mnaweza kuelewa mada hizi, maudhui haya ninayoyazungumzia, sasa kwa nini Naendelea kuizungumzia? Ni kwa sababu mada hizi ni mambo ambayo yanapaswa kueleweka kwa kila mfuasi wa Mungu, kila mtu ambaye anataka kuokolewa na Mungu—anapaswa kuelewa mada hizi. Ingawa, kwa kipindi hiki ambacho huzielewi, siku moja, ambapo maisha yako na uzoefu wako wa ukweli utafikia kiwango fulani, pale ambapo mabadiliko yako ya tabia yako ya maisha yanafikia kiwango fulani na kimo chako kinaongezeka kwa kiwango fulani, ni wakati huo tu ndio mada hizi ambazo naziwasilisha kwako katika ushirika zitakimu na kuridhisha utafutaji wako wa maarifa ya Mungu. Kwa hiyo maneno haya yalikuwa ni kwa ajili ya kuweka msingi, kuwaandaa kwa ajili ya uelewa wenu wa baadaye kwamba Mungu anatawala vitu vyote na kwa ajili ya uelewa wenu wa Mungu Mwenyewe.

Vyovyote vile uelewa juu ya Mungu ulivyo mkubwa katika mioyo ya watu, unaamua nafasi kubwa kiasi gani Anachukua katika mioyo yao. Vyovyote vile kiwango cha maarifa ya Mungu kilivyo katika mioyo yao ndivyo kwa kiwango kikubwa Mungu alivyo katika mioyo yao. Ikiwa Mungu unayemfahamu yupo tupu na ni yule asiye yakini, basi yule Mungu unayemwamini pia ni tupu na ni yule asiye yakini. Ikiwa Mungu unayemfahamu anaishia ndani ya mipaka ya mawanda yako, basi Mungu wako ni Mungu mdogo kweli na hajaunganishwa na Mungu wa kweli. Kwa hiyo, kuyajua matendo ya Mungu, kuujua uhalisi wa Mungu na uweza Wake, kuujua utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, kujua kile Anacho na alicho kujua kile Alichokuonyesha miongoni mwa vitu vyote—haya ni muhimu sana kwa kila mtu anayetafuta maarifa ya Mungu. Haya yana uhusiano wa moja kwa moja na iwapo watu wanaweza kuingia kwa uhalisi wa ukweli. Ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako juu ya Mungu katika maneno tu, ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako mdogo tu, Neema ya Mungu unayoihesabu, au shuhuda zako ndogo kwa Mungu, basi Ninasema kwamba yule Mungu unayemwamini si Mungu wa kweli kabisa. Kabisa si Mungu Mwenyewe wa kweli, na inaweza pia kusemwa kuwa Mungu unayemwamini si Mungu. Hii ni kwa sababu Mungu ambaye Ninamzungumzia ni yule ambaye Anatawala kila kitu, ambaye Anatembea miongoni mwa kila kitu, ambaye Anasimamia kila kitu. Yeye ndiye Anashikilia majaliwa ya binadamu wote—ambaye anashikilia majaliwa ya kila kitu. Kazi na matendo ya Mungu ambaye Ninamzungumzia hayaishii kwa sehemu ndogo tu ya watu. Yaani, haiishii tu kwa watu tu ambao sasa wanamfuata. Matendo Yake yameonyeshwa miongoni mwa vitu vyote, katika vitu vyote kuendelea kuishi, na katika sheria za mabadiliko ya vitu vyote.

Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, na yupo ndani ya akili yako finyu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya aina hiyo ya Mungu, basi Mungu hataisifu imani yako. Unapokuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu, ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha. Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaongoza binadamu wote kwa njia ya utawala Wake wa vitu vyote, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Sasa unaelewa yote haya, sio? Lengo Langu ni nini kusema yote haya? Iko hivyo ili usiweze kulichukulia hili kirahisi, ili msiamini kwamba mada hizi Nilizozizungumzia hazina uhusiano na kuingia kwenu binafsi katika maisha, na ili msichukue mada hizi kama tu aina ya maarifa au mafundisho. Ikiwa unasikiliza ukiwa na mtazamo kama huo, hutapata kitu hata kimoja. Utapoteza fursa kubwa hii ya kumjua Mungu. Unaweza kukumbuka hayo sasa, siyo?

Lengo Langu la kuzungumza juu ya mambo haya yote ni nini? Lengo langu ni kuwafanya watu wamjue Mungu, kuwafanya watu waelewe matendo halisi ya Mungu. Mara utakapomuelewa Mungu na ukaelewa matendo Yake, ni baada ya hapo tu ndipo utakuwa na fursa au uwezekano wa kumjua Mungu. Kwa mfano, ikiwa unataka kumwelewa mtu, ni jinsi gani unaweza kumwelewa? Je, inaweza kuwa kupitia kuangalia umbo lao la nje? Je, inaweza kuwa kupitia kile wanachokivaa, jinsi wanavyovaa? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia jinsi wanavyotembea? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia mawanda ya maarifa yao? (Hapana.) Kwa hiyo unamwelewaje mtu? Unafanya hukumu kupitia maneno na tabia ya mtu, kupitia mawazo zake, kupitia kile anachokionyesha na kile anachokifichua. Hivyo ndivyo unavyomjua mtu, unavyomwelewa mtu. Kwa njia ile ile, ikiwa mnahitaji kumjua Mungu, ikiwa mnataka kuelewa upande Wake wa vitendo, upande Wake wa kweli, mnapaswa kumjua Yeye kupitia matendo Yake na kupitika kila kitu halisi Anachofanya. Hii ndiyo njia bora zaidi na ndiyo njia pekee.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp