Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani. Suala hili si lile ambalo ni geni sana kwenu, lakini inaonekana kwamba hamwelewi au hamjazoea maana iliyomo kwenye suala hili. Wengi wanayo dalili ya ufahamu tu na mara nyingi maarifa ya juujuu kuhusu suala hili. Ili kuwasaidia kutenda kwa njia bora zaidi ukweli, yaani, kuwasaidia kuweka kwa njia bora zaidi maneno Yangu katika matendo, Nafikiri kwamba ni suala hili ambalo lazima kwanza mlijue. Vinginevyo, imani yenu itabakia isiyo wazi, ya unafiki, na iliyopambwa sana na dini. Kama huelewi tabia ya Mungu, basi itakuwa haiwezekani kwako wewe kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, ndivyo pia haitawezekana kubakiza hali ya kumcha na kumwogopa Yeye, utakuwa ni uzembe na kuepuka kusema ukweli wote kwa kutojali, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, ilhali hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakinifu au kudadisi suala hili. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuuzilia mbali amri za kiutawala Nilizozitoa. Kama hamuelewi tabia ya Mungu, basi mtaweza kukosea kwa urahisi sana tabia Yake. Kosa kama hilo ni sawa na kumkasirisha Mungu Mwenyewe, na tunda la msingi la tendo lako linakuwa ni uhalifu dhidi ya amri ya kiutawala. Sasa unafaa kutambua kwamba unaweza kuelewa tabia ya Mungu unapokuja kujua dutu Yake, na kuelewa tabia ya Mungu ni sawa na kuelewa amri za kiutawala. Bila shaka, wingi wa amri za kiutawala zinahusu tabia ya Mungu, lakini uzima wa tabia Yake bado haujaweza kuonyeshwa ndani yao. Hili linawahitaji kuzoea zaidi tabia ya Mungu.

Ninaongea nanyi leo si katika hali ya mazungumzo ya kawaida, kwa hiyo lazima myajali maneno Yangu kwa bidii na, zaidi, kuyatafakari kwa kina. Kile Ninachomaanisha na haya ni kwamba mmetoa jitihada ndogo sana kwa maneno ambayo Nimeyazungumza. Tunapokuja kwa tabia ya Mungu, hamko radhi zaidi kutafakari juu ya suala hili, na wachache sana wanajitolea kufanya hili. Kwa hiyo, Nasema kwamba imani yenu ni maneno ya kujionyesha tu. Hata sasa, hakuna hata mmoja wenu ametoa jitihada yoyote ya kweli kwa udhaifu wenu mkuu zaidi. Mmenisikitisha baada ya maumivu yote Niliyoyapitia kwa ajili yenu. Si ajabu kwamba nyote hamjali Mungu na mnaishi maisha yasiyo na ukweli. Ni vipi watu kama hawa wanaweza kuchukuliwa kama watakatifu? Sheria ya mbinguni haitaweza kuvumilia kitu kama hiki! Kwa sababu mnao uelewa mdogo sana, basi itabidi Nitumie pumzi zaidi.

Tabia ya Mungu ni mada ambayo inaonekana kuwa dhahania sana na ambayo haikubaliwi kwa urahisi, kwani tabia Yake ni tofauti na hulka ya binadamu. Mungu, vilevile, anazo hisia za anasa, hasira, huzuni, na furaha, lakini hisia kama hizo zinatofautiana pia na zile za binadamu. Mungu anayo nafsi Yake mwenyewe na kile Anachokimiliki. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukionyesha ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Nafsi Yake, kile Anachomiliki, pamoja na dutu na utambulisho vyote haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, kumtuliza binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa mwanadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini mema, changamfu, au ngumu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa wale walio hai miongoni mwa vitu vyote, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia yake ni ishara ya mamlaka na kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, na kizuri. Aidha, ni ishara ya namna ambavyo Mungu hawezi[a] kukandamizwa au kushambuliwa na giza na kikosi chochote cha adui, pamoja na ishara ya namna ambavyo hawezi kuwa (na kwa kweli haruhusiwi kuwa)[b] kukasirishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanaoweza au wanaweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini hulka ya binadamu si zaidi ya ishara tu ya hali ya kuwa na mamlaka ya juu zaidi kiasi cha binadamu dhidi ya wanyama. Binadamu mwenyewe hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuzidi nafsi, bali ni dutu tu inayotii kwa njia ya woga kutawaliwa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Anasa ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa hali ya kuwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa mwanadamu; furaha Yake ni ile ya hali ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi ya yote, ishara ya msaada. Hasira ya Mungu inatokana na uwepo wa dhuluma na vurugu inayosababisha ambayo inamdhuru mwanadamu Wake; kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na cha kupendeza. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya mwanadamu, ambaye kwake Ana matumaini lakini ambaye ameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya mwanadamu asiye na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule binadamu mzuri lakini mwenye hisia kinzani. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya urembo na wema Wake. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na mwanadamu kupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na furaha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko furaha. Furaha Yake ni ishara ya mwanadamu kuwa huru dhidi ya mateso na kuingia katika ulimwengu wa mwangaza. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote zipo kwa makusudio ya masilahi yake mwenyewe, na wala si za haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, na kidogo kati ya vyote neema ya Mbinguni. Hisia za mwanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo si za mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo binadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa kwa pumzi moja. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na mwenye heshima kila wakati, huku naye binadamu siku zote akiwa chini na kila wakati akikosa thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa mwanadamu; binadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na hufanya kazi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia uwepo wa mwanadamu, ilhali binadamu hachangii kitu katika mwangaza au haki. Hata kama binadamu anashughulika kwa muda, yeye ni mnyonge na hawezi kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake na wala si wengine. Binadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mbinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo na haki, wema, na urembo, huku naye binadamu akiwa mrithi na mwonyeshaji wa vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na urembo, ilhali binadamu anaweza, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa njia ya Mungu.

Kila sentensi Niliyoizungumza inaendeleza tabia ya Mungu. Mngefanya vizuri zaidi endapo mngetafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka katika maneno haya. Dutu ya Mungu ni ngumu sana kuelewa, lakini Ninaamini kwamba nyinyi nyote mnayo angalau baadhi ya maarifa kuhusu tabia ya Mungu. Ninatumai, basi, kwamba mtanionyesha Mimi na kufanya mengi zaidi ya yale ambayo hayakosei tabia ya Mungu. Kisha Nitatuliza moyo. Kwa mfano, mhifadhi Mungu katika moyo wako siku zote. Unapochukua hatua, timiza neno Lake. Tafuta fikira Zake katika kila kitu, na usifanye kile ambacho kitavunjia heshima na kumdhalilisha Mungu. Vilevile, usimweke Mungu nyuma ya akili zako ili ukajaze uwazi wa baadaye katika moyo wako. Ukifanya hivyo, basi utakuwa umekosea tabia ya Mungu. Kama kamwe hutamki matamshi ya kukufanya kukufuru au kulalamika dhidi ya Mungu na unaweza kufanya kikamilifu kila kitu ambacho amekuaminia wewe katika maisha yako yote, pamoja na kutii maneno yote ya Mungu, basi umeweza kuepuka kwa ufanisi kukosea amri za kiutawala. Kwa mfano, kama umewahi kusema “Kwa nini sifikirii kwamba Yeye ni Mungu?” “Nafikiri kwamba maneno haya si zaidi ya kutiwa nuru fulani na Roho Mtakatifu,” “Sifikirii kwamba kila kitu Mungu anachokifanya ni cha kweli,” “Ubinadamu wa Mungu hauna ukubwa zaidi kuliko wangu,” “Neno la Mungu haliaminiki tu,” au matamshi mengine kama hayo ya kuhukumu, basi Nakushawishi wewe kukiri dhambi zako na kutubu. Vinginevyo, hutawahi kuwa na fursa ya msamaha, kwani unakosea sio binadamu tu lakini Mungu Mwenyewe. Unaweza kuamini kwamba wewe unahukumu mtu tu, lakini Roho Mtakatifu wa Mungu hachukulii hivyo. Wewe kutoheshimu mwili Wake ni sawa na kumvunjia heshima Yeye mwenyewe. Kama hali ni hivi, basi si kweli kwamba umekosea tabia ya Mungu? Lazima mkumbuke kwamba kila kitu kinachofanywa na Roho wa Mungu ni kusaidia kazi Yake katika mwili na kufanya kazi kama hiyo vizuri. Ukiyapuuza haya, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye kamwe hutaweza kufaulu katika kumwamini Mungu. Kwani umechochea hasira ya Mungu, na kwa hivyo lazima Atumie adhabu inayofaa ili kukufunza adabu.

Kuzoea dutu ya Mungu si jambo dogo. Lazima uelewe tabia Yake. Katika njia hii, polepole utaanza kuzoea dutu ya Mungu Wakati umeingia katika maarifa haya, na hivyo basi kusonga mbele wakati uo huo katika hali kubwa zaidi na ya kupendeza zaidi. Hatimaye, utaaibika kutokana na nafsi yako ya kuchukiza, kiasi kwamba unaaibika kuuonyesha uso wako. Wakati huo, ndipo utakapokosea tabia ya Mungu kwa kiwango kidogo na kidogo; moyo wako utakuwa karibu zaidi na zaidi na ule wa Mungu, na polepole upendo wako Kwake utaweza kukua ndani ya moyo wako. Hii ni ishara ya mwanadamu kuingia katika hali nzuri. Lakini kufikia sasa bado hamjapata hili. Nyinyi hujichosha mkisafiri huku na kule kwa ajili ya hatima yenu, kwa hiyo ni nani angefikiria kujaribu na kuzoea zaidi dutu ya Mungu? Kama hali hii itaendelea, nyinyi mtaweza kuikosea bila kujua amri ya kiutawala kwani mnajua kidogo sana kuhusu tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kile mfanyacho sasa hakiweki msingi kwa sababu ya makosa yenu dhidi ya tabia ya Mungu? Kwamba Ninawaomba muweze kuelewa tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkienda kinyume cha amri za kiutawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, kazi Yangu haingekuwa bure kabisa? Kwa hivyo, Ningali Naomba kwamba pamoja na kuchunguza matendo yenu binafsi, kwamba muwe makini zaidi na hatua mnazochukua. Hili ndilo ombi kubwa zaidi ambalo Nitawaomba, na Ninatumai kwamba nyote mtalitilia maanani kwa umakinifu na kuliona kuwa muhimu. Endapo siku itawahi kufika ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa yenu pekee kufikiria, na hakuna mwingine yeyote atakayevumilia adhabu hiyo kwa niaba yenu.

Tanbihi:

a. Maandishi asilia yanasoma “kutoweza kuwa.”

b. Maandishi asilia yanasoma “kutoweza kuwa (na kwa hakika kutoruhusiwa kuwa).”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp