Maonyo Matatu

Kama muumini wa Mungu, hamfai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla mwisho wenu haujaamuliwa, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu. Kabla Sijaendelea, mnafaa kwanza kuelewa yafuatayo: Maneno Ninayoongea ni ukweli unaoelekezwa kwa wanadamu wote, na wala si kwa mtu mahususi au aina fulani ya mtu. Kwa hiyo, mnapaswa kumakinikia kupokea maneno Yangu kutoka katika mtazamo wa ukweli, na vile vile mdumishe mtazamo wa uzingativu na uaminifu kamili. Msipuuze hata neno moja au ukweli Ninaoongea, na wala usichukulie maneno Yangu kwa dharau. Katika maisha yenu, Naona mengi ambayo mnafanya ambayo hayana uhusiano na ukweli, kwa hivyo Ninawaomba kwa dhati kuwa watumishi wa ukweli na wala si kutawaliwa na maovu na ubaya. Msikanyage ukweli na kuchafua sehemu yoyote ya nyumba ya Mungu. Hili ndilo onyo Langu kwenu. Sasa Nitaanza kuzungumza kuhusu mada ya karibu:

Kwanza, kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu mnatambua kwamba nyinyi mmehesabiwa miongoni mwa wale walio katika nyumba ya Mungu, basi mnastahili kumletea Mungu katika mambo yote utulivu wa akili na utoshelevu. Kwa maneno mengine, lazima muwe wenye maadili katika matendo yenu na kutii ukweli katika mambo kama hayo. Kama hali hii inazidi uwezo wako, basi utachukiwa na kukataliwa na Mungu na vilevile kukataliwa kwa dharau na wote. Punde utakapokuwa katika hali mbaya kama hii, basi hauwezi kuhesabiwa miongoni mwa wale walio kwenye nyumba ya Mungu. Hivi ndivyo ilivyo kutoidhinishwa na Mungu.

Pili, mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu anayo dutu ya uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Na ndiyo maana Mungu huwapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu mioyo yenu; kutomdanganya katu katika chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kufunika ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kutia mchanga wa macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinafanywa ili tu mweze kujipendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. Kile Ninachoongea ni rahisi sana lakini ni kigumu maradufu kwenu. Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu. Si ajabu kwamba Nina matendo mengine kwa wale ambao si waaminifu. Bila shaka, Ninaelewa ugumu mkuu mnaokumbana nao kwa kuwa binadamu waaminifu. Nyinyi wote ni werevu sana na stadi katika kuwahukumu wengine kutoka kwa mtazamo wenu, kwa hiyo hii hufanya kazi Yangu kuwa rahisi zaidi. Na kwa sababu kila mmoja wenu anaficha siri katika moyo wako, basi, Nitawatumeni kila mmoja wenu katika janga kupitia “jaribio” la moto, ili baadaye mtajitolea kabisa katika kuamini maneno Yangu. Hatimaye, Nitapokonya maneno “Mungu ni Mungu wa uaminifu,” kutoka kwa vinywa vyenu na kisha ndipo mtakapojigamba na kujitanua kifua na kulalama kwamba “ujanja ndio moyo wa binadamu.” Nini basi ndicho kitakachokuwa hali ya akili zenu? Ninafikiri hamtajisahau sana na majivuno kama mlivyo sasa. Na sembuse hamtakuwa “wa maana sana kiasi cha kutoeleweka” kama mlivyo sasa. Baadhi hutenda kwa ustaarabu na hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, ilhali wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika “kutangamana,” basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe unao siri nyingi usiotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye kwake wokovu hutaweza kupatikana na ambaye hataweza kuibuka kutoka kwa giza kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ndiwe unayeishi mara nyingi katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mtiifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme. Unafaa kujua kama kunayo imani ya kweli na uaminifu wa kweli ndani yako, kama katika rekodi yako umeteseka kwa ajili ya Mungu, na kama unamtii kikamilifu kwa Mungu. Kama unakosa hivi Nilivyotaja, basi ndani yako kunabaki kutotii, udanganyifu, ulafi, na kutotosheka. Kwa vile moyo wako si mwaminifu, hujawahi kupokea utambuzi mzuri kutoka kwa Mungu na hujawahi kuishi katika mwangaza. Kile ambacho jaala ya mtu kitakuwa hutegemea kama anao moyo wa uaminifu na wa kweli, na kama anayo nafsi isiyo na doa. Kama wewe ndiwe asiye mwaminifu zaidi, uliye na moyo wa kijicho na nafsi isiyo safi, basi rekodi ya majaliwa yako bila shaka ipo pale ambapo binadamu huadhibiwa. Kama unadai kwamba wewe ni mwaminifu sana, ilhali kamwe hutendi kulingana na ukweli au kuongea neno la ukweli, basi bado unatarajia Mungu kukutuza? Bado unatumai Mungu kukufikiri kama kipenzi Chake? Je, kufikiria huku si kwa upuzi? Unamdanganya Mungu katika mambo yote, basi nyumba ya Bwana inawezaje kumpa nafasi mtu kama wewe asiyekuwa na mikono safi?

Kitu cha tatu ni hiki: Wote wanaomwamini Mungu wamemkataa na kumdanganya Mungu wakati fulani katika njia zao. Baadhi ya matendo mabaya hayahitaji kurekodiwa kama kosa, lakini mengine hayasameheki; kwani mengi ni yale yanayokiuka amri za kiutawala, hali ambayo ni kosa dhidi ya tabia ya Mungu. Wengi ambao wanajali majaliwa yao binafsi wanaweza kuuliza matendo haya ni yapi. Lazima mjue kwamba nyinyi mna kiburi na wenye majivuno kiasili, na hamko radhi kutii jambo hili. Kwa hiyo, Nitawaambia kidogo kidogo baada ya nyinyi kutafakari kujihusu. Ninawashawishi kuelewa kwa njia bora zaidi yaliyomo katika amri za kiutawala na kujua tabia ya Mungu. Vinginevyo, mtapata ugumu sana kuendelea kufunga vinywa vyenu na kufyata ndimi zenu dhidi ya kuropokwa bila kizuizi kwa mazungumzo ya mbwembwe. Bila kujua mnaweza kuikosea tabia ya Mungu na kujipata kwenye giza, mkipoteza uwepo wa Roho Mtakatifu na mwangaza. Kwa sababu nyinyi ni wapotovu katika matendo yenu. Ukifanya au kusema kile ambacho hufai kufanya hivyo, basi utapokea adhabu inayokufaa. Lazima ujue kwamba ingawa wewe ni mpotovu katika maneno yako na matendo yako, Mungu ni mwenye maadili katika hali hizi zote. Sababu ya wewe kupokea adhabu ni kwa sababu umemkosea Mungu na wala si binadamu. Kama, katika maisha yako, wewe hutenda makosa mengi dhidi ya tabia ya Mungu, basi huna budi ila kuwa mtoto wa Kuzimu. Kwake binadamu inaweza kuonekana kwamba umetenda matendo machache tu yasiyolingana na ukweli na si chochote kingine. Je, una habari, hata hivyo, kwamba katika macho ya Mungu, tayari wewe ni mmoja ambaye kwake hakuna tena sadaka ya dhambi? Kwani umevunja amri za kiutawala za Mungu zaidi ya mara moja na huonyeshi ishara yoyote ya kutubu, kwa hivyo huna chaguo lolote ila kutumbukia Kuzimu pale ambapo binadamu anaadhibiwa na Mungu. Katika wakati wao wa kufuata Mungu, idadi ndogo ya watu ilitenda matendo yaliyoenda kinyume na kanuni, lakini baada ya kushughulikiwa na kuongozwa, waligundua kwa utaratibu kupotoka kwao, na kisha wakachukua njia iliyo sawa ya uhalisi, na leo wanabaki wenye msingi imara katika njia ya Bwana. Binadamu kama hawa ndio watakaobakia mwisho. Ni wale walio waaminifu ndio Ninaowatafuta; kama wewe ni mwaminifu na unatenda kwa maadili, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu. Kama katika matendo yako hukosei tabia ya Mungu, na unatafuta mapenzi ya Mungu na unao moyo wa kumcha Mungu, basi imani yako ni ya juu ya kiwango kilichowekwa. Wale wasiomcha Mungu na hawana moyo unaotetema kwa woga na huenda wakakiuka amri za kiutawala za Mungu kwa urahisi. Wengi humhudumia Mungu kwa misingi ya tamanio, na hawajui katu amri za kiutawala za Mungu, sembuse kuelewa athari za neno Lake. Na kwa hivyo, na nia zao nzuri, mara nyingi wanaishia kufanya vitu vinavyotatiza usimamizi wa Mungu. Wale wanaosababisha vurugu kubwa wanatupwa nje na hawana tena fursa ya kumfuata Mungu; wanatupwa kuzimu bila ya kuwa na uhusiano wowote mwingine na nyumba ya Mungu. Watu hawa hufanya kazi katika nyumba ya Mungu wakiwa na nia nzuri zisizojua na wanaishia kuchochea tabia ya Mungu. Watu huleta njia zao za kuwahudumia wajumbe na watawala wakuu katika nyumba ya Mungu na kujaribu kufanya yatumike, wakidhania kwa kiburi kwamba njia kama hizo zinaweza kutumika hapa. Hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu hana ile tabia ya mwanakondoo bali ile ya simba. Kwa hiyo, wanaojishirikisha na Mungu kwa mara ya kwanza wanashindwa kuwasiliana na Yeye, kwani moyo wa Mungu ni tofauti na ule wa binadamu. Ni baada tu ya kuelewa ukweli mwingi ndipo unapoweza kujua siku zote kumhusu Mungu. Maarifa haya si masomo wala falsafa, lakini yanaweza kutumika kama hazina ya kuingia katika matumaini ya karibu na Mungu na ithibati kwamba Anafurahishwa na wewe. Kama unakosa uhalisi wa maarifa na huna ukweli, basi huduma yako ya shauku itakuletea tu hali ya chuki ya kupindukia na kuchukizwa sana kwa Mungu. Sasa unafaa kuelewa kwamba imani katika Mungu si masomo tu ya thiolojia.

Ingawa onyo Langu ni la muhtasari kwa urefu, vyote Nilivyovifafanua hapa ndivyo vinachokosekana zaidi ndani yenu. Lazima mjue kwamba kile Ninachozungumzia sasa ni kwa minajili ya kazi Yangu ya mwisho miongoni mwa binadamu, kuamua hatima ya binadamu. Sipendelei kufanya kazi nyingi zaidi isiyo na kusudio lolote, na wala Sipendelei kuendelea kuongoza wale binadamu wasio na matumaini kama mbao zilizopwelewa, sembuse wale walio na nia mbaya. Pengine siku moja mtaelewa nia za dhati zinazosukuma maneno Yangu na michango Nimefanya kwa mwanadamu. Pengine siku moja mtafahamu kanuni inayowawezesha kuamua hatima yenu binafsi.