Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na wakati hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambapo watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo Zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu dunia katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza nafsi Yangu na wanafaa kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu. Kama sehemu kubwa ya maneno Yangu haingeelekezwa kwa udhaifu wa mwanadamu, angejigamba na kutia mambo chumvi, na angehubiri na kubuni nadharia zenye kuvutia, ni kama aliye na maarifa yote na anayejua yote kuhusu masuala duniani. Nani bado huthubutu kujigamba kati ya wale waliokuwa waaminifu Kwangu hapo awali, na ambao leo hii wanasimama imara mbele Yangu? Ni nani asiyefurahia matarajio yake mwenyewe kisiri? Wakati Sikufichua waziwazi, mwanadamu hakuwa na mahali pa kujificha na aliteswa na aibu. Ingekuwa mbaya zaidi kiasi gani Mimi Ninapozungumza kupitia njia nyingine? Wanadamu wangekuwa na hisia kubwa zaidi za kuwa wadeni, wangeamini kwamba hakuna kitu kingeweza kuwatibu, na wote wangefungwa vizuri na kutokuwa na hisia kwao. Mwanadamu anapopoteza matumaini, saluti ya ufalme husikika kwa urasmi, ambayo ni “wakati ambapo Roho aliyeongezwa nguvu mara saba Huanza kufanya kazi,” kama lilivyoongelewa na mwanadamu, kwa maneno mengine, wakati maisha ya ufalme huanza kwa urasmi duniani, yaani, wakati uungu Wangu huja kufanya kazi moja kwa moja (bila kufikiriwa na ubongo). Watu wote wanakuwa na shughuli nyingi kama nyuki; inaonekana ni kama wamefufuliwa, ni kama wameamshwa kutoka katika ndoto, na punde wanapoamka, wanapigwa na butwaa kwa kujikuta katika hali kama hiyo. Katika siku za awali, Nilisema mengi kuhusu ujenzi wa kanisa, Nilifichua siri nyingi, na wakati ujenzi wa kanisa ulifikia kilele chake, ulifikia kikomo cha ghafla. Hata hivyo, ujenzi wa ufalme ni tofauti. Wakati vita katika ulimwengu wa kiroho vinapofika hatua yake ya mwisho tu ndipo Nianzapo upya duniani. Hiyo ni kusema, ni wakati tu mwanadamu anapotaka kurudi nyuma ndipo Ninaanza kwa urasmi na kuinua kazi Yangu mpya. Tofauti kati ya ujenzi wa ufalme na ujenzi wa kanisa ni kwamba, katika ujenzi wa kanisa, Nilifanya kazi katika ubinadamu ulioongozwa na uungu. Nilishughulika moja kwa moja na asili ya zamani ya mwanadamu, moja kwa moja Nilifichua nafsi mbaya ya mwanadamu, na kuweka wazi kiini cha mwanadamu. Kwa sababu hii mwanadamu alikuja kujijua mwenyewe kwa msingi huu, na hivyo aliridhishwa katika moyo na kwa neno. Katika ujenzi wa ufalme Ninatenda moja kwa moja katika hali ya uungu Wangu, na kuruhusu watu wote kujua kile Nilicho nacho na nilicho kwa msingi wa maarifa ya maneno Yangu, hatimaye kuwaruhusu kupata ufahamu Wangu Mimi Niliye katika mwili. Hivyo hukomesha harakati zote za wanadamu kutafuta Mungu asiye dhahiri, na hukomesha nafasi ya Mungu mbinguni katika moyo wa mwanadamu, ambayo ni kusema, linaruhusu mwanadamu kujua matendo Yangu katika mwili Wangu, na hivyo linahitimisha wakati Wangu duniani.

Ujenzi wa ufalme unalenga ulimwengu wa kiroho moja kwa moja. Kwa maneno mengine, vita vya ulimwengu wa kiroho vimewekwa wazi miongoni mwa watu Wangu wote, na kutoka kwa hii inaweza kuonekana kwamba watu wote daima wamo vitani, sio tu katika kanisa, lakini hata zaidi katika wakati wa ufalme, na kwamba hata ingawa mwanadamu yuko katika mwili, ulimwengu wa kiroho unafichuliwa moja kwa moja, na mwanadamu anajihusisha na maisha ya ulimwengu wa kiroho. Hivyo, mnapoanza kuwa waaminifu, lazima mjiandae vizuri kwa ajili ya hatua ya kazi Yangu inayofuata. Mnapaswa kutoa moyo wenu wote, na ni kwa kufanya hivi tu ndio mnaweza kukidhi Moyo Wangu. Sijali kuhusu chochote ambacho mwanadamu alifanya hapo awali katika kanisa; leo, Najali kuhusu yanayotendeka katika ufalme. Katika mpango Wangu, Shetani amewahi kushindana na kila hatua, na, kama foili[a] ya hekima Yangu amejaribu siku zote kutafuta njia na namna ya kuvuruga mpango Wangu wa awali. Lakini Ningeweza kukabiliwa na miradi yake ya udanganyifu? Vyote mbinguni na duniani vinanitumikia—njama za udanganyifu za shetani zingeweza kuwa tofauti? Huku ndiko hasa kukutana kwa hekima Yangu, ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu matendo Yangu, na ni kanuni ambayo mpango Wangu wa usimamizi mzima unafanywa kupitia. Wakati wa ujenzi wa ufalme, bado Mimi Siepuki njama za udanganyifu za Shetani, ila Naendelea kufanya kazi ambayo lazima Nifanye. Kati ya vitu vyote katika ulimwengu, Nimechagua matendo ya Shetani kama foili[a] Yangu. Je, hii si hekima Yangu? Je, si haya ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu kazi yangu? Katika tukio la kuingia katika wakati wa ufalme, mabadiliko makubwa hutokea katika mambo yote mbinguni na duniani, na wao husherehekea na kufurahi. Je, nyinyi mna tofauti yoyote? Ni nani asiyejisikia mtamu kama asali katika moyo wake? Ni nani asiyebubujikwa na furaha katika moyo wake? Ni nani asiyecheza kwa furaha? Ni nani asiyesema maneno ya sifa?

Katika yote Niliyonena na kusema kuhusu hapo juu, je, mnapata kufahamu malengo na asili ya matamko Yangu, au la? Kama Singeuliza swali hili, watu wengi wangeamini kuwa Ninabubujikwa na maneno tu, na hawangeweza kutambua chanzo cha maneno Yangu. Mkiyatafakari kwa makini, mtajua umuhimu wa maneno Yangu. Ungefanya vyema kwa kuyasoma kwa karibu: Ni yapi kati ya maneno hayo yasiyo ya faida kwako? Ni yapi yasiyo kwa ajili ya ukuaji wa maisha yako? Ni yapi yasiyozungumzia hali halisi ya ulimwengu wa kiroho? Watu wengi sana wanaamini hakuna maana katika maneno Yangu, ya kuwa hayana maelezo yoyote na tafsiri. Je, maneno Yangu kweli ni dhahania sana na yasiyoeleweka? Je, mnatii kwa kweli maneno Yangu? Je, mnayakubali maneno Yangu kwa kweli? Je, hamyachukulii kama kidude cha watoto kuchezea? Je, huyatumii kama mavazi ya kuficha uchi wa sura yako mbaya? Katika dunia hii kubwa, ni nani amechunguzwa na Mimi binafsi? Ni nani ameyasikia mwenyewe maneno ya Roho Wangu? Watu wengi sana hututusa tu gizani, wengi sana huomba wakiwa na shida, wengi sana hutazama kwa matumaini wakiwa na njaa na baridi, wengi sana wamefungwa na Shetani, ilhali wengi sana bado hawajui wanakofaa kugeukia, wengi sana hunisaliti wakiwa katika furaha, wengi sana hawana shukrani, na wengi sana ni waaminifu kwa njama za udanganyifu za shetani. Nani kati yenu ni Ayubu? Petro ni nani? Kwa nini Nimetaja mara kwa mara jina la Ayubu? Na mbona Nimemtaja Petro mara nyingi? Je, mmewahi kufahamu matumaini Yangu kwenu? Mnapaswa kuchukua muda zaidi kuwaza mambo ya aina hii.

Petro alikuwa mwaminifu Kwangu kwa miaka mingi, ilhali hakunung’unika kamwe wala kuwa na moyo wa kulalamika, na hata Ayubu hakuwa wa kulinganishwa naye. Kwa miaka na dahari watakatifu, pia, wamekuwa wenye upungufu kuliko yeye. Yeye hakufuatilia kunijua Mimi tu lakini pia alinijua wakati ambapo Shetani alikuwa anaendeleza njama zake za udanganyifu. Hii ilisababisha miaka mingi ya huduma iliyoupendeza nafsi Yangu, na kwa sababu hii Shetani hakuweza kumnyonya. Petro alitumia imani ya Ayubu, bado pia alifahamu wazi upungufu wake. Ingawa Ayubu alikuwa na imani kubwa, alikosa ujuzi wa masuala katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo alisema maneno mengi ambayo hayakulingana na hali halisi; hii inaonyesha kwamba maarifa yake bado hayakuwa ya kina, na hayakuwa na uwezo wa kufanywa kuwa kamilifu. Na hivyo, Petro siku zote alitazamia kupata hisia ya roho, na daima alilenga kuchunguza mienendo ya ulimwengu wa kiroho. Kwa sababu hii, hakuwa tu na uwezo wa kutambua kitu cha matakwa Yangu, lakini pia alielewa kidogo juu ya njama za udanganyifu za Shetani, na hivyo elimu yake ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyingine yoyote katika enzi.

Kutokana na matukio ya Petro si vigumu kuona kwamba mtu akitaka kunijua, lazima awe makini kwa kuzingatia kwa uangalifu katika roho. Sikuulizi kwamba “utoe” kiasi kikubwa Kwangu kwa nje; hili ni la umuhimu wa ziada. Iwapo hunijui, basi imani yote, upendo na uaminifu unaozungumzia ni ndoto tu, ni povu, na wewe hakika utakuwa mtu ambaye ana majivuno makubwa mbele Zangu lakini hajijui mwenyewe, ndipo wewe utanaswa tena na Shetani na hutaweza kujitoa; utakuwa mwana wa kuteseka milele, na utakuwa chombo cha uharibifu. Lakini kama wewe huna hisia na hujali kuhusu maneno Yangu, basi bila shaka unanipinga Mimi. Hii ni kweli, na ingekuwa vyema utazame kupitia lango la ulimwengu wa kiroho uone roho nyingi na tofauti tofauti zilizoadibiwa na Mimi. Ni wapi kati yao hawakukaa tu na hawakujali, na hawakuyakubali maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuwa na shaka kwa maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakujaribu kuyashika maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakutumia maneno Yangu kama silaha ya kujikinga itakayotumiwa kujilinda? Wao hawakutafuta maarifa Yangu kwa njia ya maneno Yangu, lakini waliyatumia kama vitu vya kuchezea. Katika hili, je, wao si walinipinga moja kwa moja? Maneno Yangu ni nani? Ni nani Roho Yangu? Mara nyingi Mimi Nimeyanena maneno haya kwenu, lakini maono yenu yamewahi kuwa ya kiwango cha juu na yenye uwazi? Matukio yenu yamewahi kuwa ya kweli? Ninawakumbusha mara nyingine: Iwapo hamyajui maneno Yangu, hamyakubali, na wala hamyaweki katika matendo, basi bila shaka mtakuwa chombo cha kuadibu Kwangu! Nyinyi kwa hakika mtakuwa waathirika wa Shetani!

Februari 29, 1992

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Kumi Na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa Waovu Lazima Waadhibiwe Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu Jinsi ya Kuujua Uhalisi Amri za Enzi Mpya Ufalme wa Milenia Umewasili Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe Kuijua Kazi ya Mungu Leo Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania? Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika" Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne Je, Umekuwa Hai Tena? Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili) Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili Je, Utatu Mtakatifu Upo? Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza) Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili) Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali? Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi? Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi Unajua Nini Kuhusu Imani? Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe” Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia Kazi katika Enzi ya Sheria Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza) Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili) Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu? Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza) Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili) Kiini cha Mwili Ulio na Mungu Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza) Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili) Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu? Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako Wewe U Mwaminifu kwa Nani? Maonyo Matatu Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu Kutanafusi kwa Mwenye Uweza Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

00:00
00:00

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji