Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza)

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu. Kwa njia hii, ingawa watu tofauti kila mmoja hufuatilia malengo yao binafsi, lengo la harakati zao na motisha yao yote ni sawa, na, zaidi ya hayo, kwa wengi wao, malengo yao ya ibada kwa kiasi kikubwa ni sawa. Katika kipindi cha elfu kadhaa za miaka iliyopita, waumini wengi wamekufa, na wengi wamekufa na kuzaliwa tena. Sio mtu mmoja au wawili ambao humtafuta Mungu, wala hata watu elfu moja au mbili, ilhali harakati ya wengi wa watu hawa ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe ama matumaini yao tukufu ya siku zijazo. Wale ambao ni waaminifu kwa Kristo ni wachache na nadra. Waumini wengi wanaomcha Mungu bado wamekufa wakiwa wametegwa na nyavu zao wenyewe, na zaidi ya hayo, idadi ya watu ambao wamekuwa na mafanikio, ni ndogo mno. Hadi siku ya leo, sababu za watu kushindwa, au siri ya mafanikio yao, bado haijulikani. Wale ambao wamejawa na hamu ya kumtafuta Kristo bado hawajapata wakati wao wa ufahamu wa ghafla, hawajafikia kina cha mafumbo haya, kwa sababu hawajui. Ingawa wao wanafanya juhudi za mchwa katika harakati zao, njia ambayo wanatembelea ni njia ya kushindwa ambayo ilitembelewa na watangulizi wao, na si njia ya mafanikio. Kwa njia hii, bila kujali jinsi wanavyotafuta, je, si wao wanatembea katika njia ambayo inaelekea gizani? Je, si wanachopata ni matunda machungu? Ni vigumu vya kutosha kutabiri ikiwa watu ambao huiga wale waliofaulu katika nyakati za zamani hatimaye watapata utajiri au msiba. Uwezekano ni mbaya kiasi gani, basi, kwa watu ambao hutafuta kwa kufuata nyayo za wale ambao hawakufaulu? Je, si wao wana uwezekano mkubwa zaidi wa kutofaulu? Ni thamani gani iliyoko katika njia wanayoipitia? Je, wao si wanapoteza wakati wao? Bila kujali iwapo mtu hufaulu ama hufeli katika harakati yake, kuna, kwa kifupi, sababu kwa nini wao wanafanya hivyo, na si kweli kuwa kufaulu kwao ama kushindwa kwao kunaamuliwa na kutafuta vyovyote watakavyo.

Mahitaji ya msingi ya imani ya mtu kwa Mungu ni kuwa ni sharti awe na moyo mwaminifu, na kwamba ajitolee mwenyewe, na kutii kwa kweli. Kile kigumu sana kwa mwanadamu ni kupeana mwili wake ili abadilishe na imani ya kweli, ambapo kupitia hii anaweza kupata ukweli mzima, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Hili haliwezi kupatikana na wale ambao wanafeli, na haliwezi kupatikana hata zaidi na wale ambao hawawezi kumpata Yesu. Kwa sababu mwanadamu si hodari kwa kujitolea mwenyewe kwa Mungu kabisa, kwa sababu mwanadamu hayuko tayari kutekeleza wajibu wake kwa Muumba, kwa sababu mwanadamu ameona ukweli lakini anauepuka na kutembea katika njia yake mwenyewe, kwa sababu mwanadamu daima anatafuta kwa kufuata njia ya wale walioshindwa, kwa sababu mwanadamu daima anaasi Mbingu, hivyo, mwanadamu daima hushindwa, huchukuliwa na hila za Shetani, na anakamatwa kwa hila na wavu wake. Kwa sababu mwanadamu hamjui Kristo, kwa sababu mwanadamu hana ustadi katika kuelewa na kushuhudia ukweli, kwa sababu mwanadamu ni wa kuabudu Paulo sana na mwenye tamaa nyingi ya mbinguni, kwa sababu mwanadamu daima anadai kuwa Kristo awe akimtii yeye na kuagiza kuhusu Mungu, hivyo mashujaa hao wakuu na wale ambao wamepitia mabadiliko mabaya ya dunia bado wamo na ubinaadamu, na bado hufa kwa kuadibu kwa Mungu. Yote Ninayoweza kusema kuhusu watu kama hawa ni kuwa wanakufa kifo cha kutisha, na athari yao—kifo chao—si bila haki. Je, si kushindwa kwao hakuvumiliki hata zaidi kwa sheria ya Mbinguni? Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu. Ilhali Kristo hutoa ukweli tu; Yeye haji kuamua ikiwa mwanadamu atafanikiwa katika harakati yake ya kufuata ukweli. Hivyo, kinachofuata ni kuwa mafanikio au kushindwa kwa kweli yote yanategemea harakati ya mwanadamu. Mafanikio au kushindwa kwa mwanadamu kwa kweli kamwe hakuna uhusiano na Kristo, lakini kwa mbadala kunategemea harakati yake. Hatima ya mwanadamu na mafanikio yake ama kushindwa haiwezi kurundikwa kichwani pa Mungu, ili Mungu mwenyewe afanywe wa kuibeba, kwa sababu sio jambo la Mungu mwenyewe, lakini linahusiana moja kwa moja na wajibu ambao viumbe wa Mungu wanapaswa kutekeleza. Watu wengi wana maarifa madogo ya harakati na hatima za Paulo na Petro, lakini watu hawajui lolote ila matokeo ya Petro na Paulo, na hawajui kuhusu siri ya mafanikio ya Petro, au mapungufu yaliyosababisha kushindwa kwa Paulo. Na kwa hivyo, kama ninyi hamwezi kabisa kuelewa kiini cha harakati zao basi harakati ya wengi wenu bila shaka haitafaulu, na hata kama wachache wenu watafaulu, bado hawatakuwa sawa na Petro. Ikiwa njia unayopitia katika kutafuta ni ya kweli, basi una matumaini ya mafanikio. Kama njia unayopitia katika kufuatilia ukweli ni mbaya, basi wewe milele hutaweza kufanikiwa, na utakuwa na hatima sawa na Paulo.

Petro alikuwa mtu aliyefanywa mkamilifu. Ni baada tu ya kupitia kuadibu na hukumu, na hivyo kupata upendo safi wa Mungu, ndipo alifanywa mkamilifu kabisa; njia ambayo alipitia ilikuwa ni njia ya kukamilishwa. Ambayo ni kusema kuwa, tangu hapo mwanzo kabisa, njia ambayo Petro alipitia ilikuwa ya haki, na motisha ya kumwamini Mungu ilikuwa sahihi, na kwa hivyo akawa mtu aliyekuwa amefanywa kamili. Yeye alifuata njia mpya ambayo mwanadamu kamwe hajawahi kuitembelea hapo awali, ilhali njia ambayo Paulo alitembea tangu mwanzo ilikuwa njia ya upinzani kwa Kristo, na ni kwa sababu tu Roho Mtakatifu alitaka kumtumia, na kufaidika na vipaji vyake na ustahili wake wote kwa kazi yake, kwamba alifanya kazi kwa ajili ya Kristo kwa miongo mingi. Alikuwa mtu tu ambaye alitumiwa na Roho Mtakatifu, na hakutumika kwa sababu Yesu alitazama ubinadamu wake kwa mapendeleo, lakini ni kwa sababu ya vipaji vyake. Aliweza kufanya kazi ya Yesu kwa sababu alipigwa, na sio kwa sababu alifurahia kufanya hivyo. Aliweza kufanya kazi kama hiyo kwa sababu ya kupata nuru na uongozi wa Roho Mtakatifu, na kazi aliyoifanya haiwakilishi harakati yake kwa njia yeyote, au ubinaadamu wake. Kazi ya Paulo inawakilisha kazi ya mtumishi, ambayo ni kusema kuwa yeye alifanya kazi ya mtume. Petro, hata hivyo, alikuwa tofauti: Yeye pia alifanya baadhi ya kazi, na ingawa haikuwa kuu kama kazi ya Paulo, alifanya kazi huku akiwa na harakati ya kuingia kwake mwenyewe, na kazi yake ilikuwa tofauti na kazi ya Paulo. Kazi ya Petro ilikuwa utekelezaji wa wajibu wa kiumbe wa Mungu. Yeye hakufanya kazi katika nafasi ya mtume, lakini wakati wa ufukuziaji wake wa upendo wa Mungu. Mwendo wa kazi ya Paulo pia ulikuwa na harakati yake binafsi. Harakati yake ilikuwa tu kwa ajili ya matumaini yake ya siku za baadaye, na shauku yake ya hatima nzuri. Yeye hakukubali usafishaji wakati wa kazi yake, wala hakukubali upogoaji na ushughulikaji. Yeye aliamini kuwa ilmradi kazi aliyoifanya iliridhisha mapenzi ya Mungu, na yote aliyofanya yalimpendeza Mungu, basi tuzo hatimaye ilikuwa unamsubiri. Hakukuwa na matukio ya kibinafsi katika kazi yake—yote yalikuwa kwa ajili yake mwenyewe, na hayakufanyika huku kukiwa na harakati ya mabadiliko. Kila kitu katika kazi yake kilikuwa shughuli, na hakukuwa na wajibu wowote au kujisalimisha kwa kiumbe cha Mungu. Wakati wa safari ya kazi yake, hakuna mabadiliko yaliyotokea katika tabia ya zamani ya Paulo. Kazi yake ilikuwa tu ya kufanya huduma kwa ajili ya wengine, na haikuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko katika tabia yake. Paulo alifanya kazi yake moja kwa moja, bila ya kufanywa mkamilifu ama kushughulikiwa, na alivutiwa na thawabu. Petro alikuwa tofauti: alikuwa mtu ambaye alikuwa amepitia upogoaji, na alikuwa amepitia ushughulikiaji na usafishaji. Lengo na motisha za kazi ya Petro zilikuwa tofauti kimsingi na zile za Paulo. Ingawa Petro hakufanya sehemu kubwa ya kazi, tabia yake ilipitia mabadiliko mengi, na alichotafuta ni ukweli, na mabadiliko ya kweli. Kazi yake haikufanyika tu kwa ajili ya kazi yenyewe. Ingawa Paulo alifanya kazi nyingi, yote ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu, na ingawa Paulo alishirikiana katika kazi hii, yeye, hakuipitia. Kwamba Petro alifanya kazi ndogo ilikuwa tu kwa ajili Roho Mtakatifu hakufanya kazi kubwa kupitia yeye. Wingi wa kazi zao haukuamua iwapo walikuwa wamefanywa wakamilifu; harakati ya mmoja ilikuwa ili kupokea tuzo, na ile ya mwingine ilikuwa ili kufikia upendo wa mwisho wa Mungu na kutimiza wajibu wake kama kiumbe cha Mungu, kwa kiasi kwamba angeweza kuishi kwa kudhihirisha picha inayopendeza ili kukidhi mapenzi ya Mungu. Nje walikuwa tofauti, na pia vile vile viini vyao vilikuwa tofauti. Huwezi kuamua ni nani kati yao alifanywa mkamilifu kwa msingi wa kazi waliyofanya. Petro alitafuta kuishi kwa kudhihirisha picha ya yule ambaye hupenda Mungu, kuwa mtu ambaye alimtii Mungu, kuwa mtu ambaye alikubali ushughulikaji na upogoaji, na kuwa mtu aliyetekeleza wajibu wake kama kiumbe wa Mungu. Aliweza kujitolea kwa Mungu, kuweka nafsi yake kamilifu katika mikono ya Mungu, na kumtii hadi kifo. Hilo ndilo alilokuwa ameamua kufanya na, zaidi ya hayo, hilo ndilo alilotimiza. Hii ndiyo sababu ya msingi ya kwani hatima yake ilikuwa tofauti na ile ya Paulo. Kazi ambayo Roho Mtakatifu alifanya ndani ya Petro ilikuwa kumfanya mkamilifu, na kazi ambayo Roho Mtakatifu alifanya ndani ya Paulo ilikuwa kumtumia. Hii ni kwa sababu asili zao na mitazamo yao kuhusu harakati hazikuwa sawa. Wote walikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Petro alitumia kazi hii kwake mwenyewe, na pia akawapa watu wengine; Paulo, kwa upande mwingine, aliwapa wengine kazi nzima ya Roho Mtakatifu, na mwenyewe hakufaidika na chochote kutoka kwa kazi hiyo. Kwa njia hii, baada ya yeye kushuhudia kazi ya Roho Mtakatifu kwa miaka mingi, mabadiliko ndani ya Paulo yalikuwa karibu na kutokuwepo. Yeye bado alibaki karibu katika hali yake ya asili, na bado alikuwa Paulo wa awali. Ni baada tu ya kuvumilia ugumu wa miaka mingi ya kazi, ndivyo alikuwa amejifunza jinsi ya kufanya kazi, na kujifunza uvumilivu, lakini asili yake ya zamani—ushindani wake mkuu na asili wa kimamluki—bado ilibaki. Baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi, hakufahamu asili yake potovu, wala hakuwa amejiondoa mwenyewe kutoka kwa asili yake ya zamani, na bado ilikuwa inaonekana katika kazi yake. Kwake, kulikuwepo tu na uzoefu wa kazi zaidi, lakini uzoefu mdogo kiasi hicho pekee haukuwa na uwezo wa kumbadilisha, na hukuweza kubadilisha maoni yake kuhusu kuwepo au umuhimu wa harakati yake. Ingawa alimfanyia Kristo kazi kwa miaka mingi, na hakumtesa tena Bwana Yesu, ndani ya Moyo wake hakukuwa na mabadiliko katika elimu kuhusu Mungu. Ambayo ina maana kuwa hakufanya kazi ili awe mwaminifu kwa Mungu, lakini alikuwa, badala yake, amelazimika kufanya kazi kwa ajili ya hatima yake ya siku zijazo. Kwa kuwa, hapo mwanzo, alimtesa Kristo, na hakumtii Kristo; kiasili yeye alikuwa mwasi ambaye alimpinga Kristo kimakusudi, na mtu ambaye hakuwa na elimu kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hitimisho la kazi yake, yeye bado hakujua kazi ya Roho Mtakatifu, na yeye tu alitenda kwa hiari yake mwenyewe kwa mujibu wa asili yake mwenyewe, bila hata kidogo kutilia maanani mapenzi ya Roho Mtakatifu. Na hivyo asili yake ilikuwa katika uhasama na Kristo na haikutii ukweli. Mtu kama huyu, ambaye alikuwa ameachwa na kazi ya Roho Mtakatifu, ambaye hakujua kazi ya Roho Mtakatifu, na ambaye pia alimpinga Kristo—je, ni jinsi gani mtu kama huyu angeokolewa? Iwapo mtu ataweza kuokolewa au la haitegemei kiasi cha kazi anayoifanya, au ni kiasi gani anajitolea, lakini badala yake kuamuliwa na iwapo anajua au hajui kazi ya Roho Mtakatifu, iwapo anaweza kuweka ukweli kwenye vitendo au la, na iwapo maoni yake kuhusu harakati yanalingana na ukweli au la.

Ingawa ufunuo wa asilia ulitokea baada ya Petro kuanza kumfuata Yesu, katika asili alikuwa, tangu mwanzo kabisa, mtu ambaye alikuwa tayari kujiwasilisha kwa Roho Mtakatifu na kumtafuta Kristo. Utiifu wake wa Roho Mtakatifu ulikuwa safi: hakutafuta umaarufu na mali, lakini badala yake alikuwa amepewa motisha na utii wa ukweli. Ingawa kuna nyakati tatu ambapo Petro alikana kumjua Kristo, na ingawa alimjaribu Bwana Yesu, udhaifu kidogo kama huu wa kibinadamu haukubeba uhusiano wa asilia yake, na haukuathiri harakati zake za mbeleni, na huwezi kuthibitisha kikamilifu ya kuwa majaribu yake yalikuwa kitendo cha mpinga Kristo. Udhaifu wa kawaida wa kibinadamu ni kitu ambacho kimo kwa watu wote duniani—je, unatarajia Petro kuwa tofauti vyovyote vile? Je, si watu wana mtazamo fulani kuhusu Petro kwa sababu alifanya makosa mengi ya kijinga? Na je, si watu wanampenda Paulo kwa sababu ya kazi yote aliyoifanya, na nyaraka zote alizoandika? Itakuwaje mtu kuwa na uwezo wa kuona kupitia kiini cha mwanadamu? Hakika, je, wale ambao kwa kweli wana hisia wanaweza kuona kitu chenye thamani ndogo kama hiyo?

Ingawa miaka mingi ya matukio ya uchungu ya Petro hayajanakiliwa katika Biblia, hii haithibitishi kuwa Petro hakuwa na matukio halisi, au kwamba Petro hakufanywa mkamilifu. Ni jinsi gani kazi ya Mungu inaweza kueleweka na mwanadamu? Kumbukumbu kwenye Biblia hazikuchaguliwa binafsi na Yesu, lakini zilikusanywa na vizazi vya baadaye. Kwa njia hii, si yote ambayo yaliandikwa katika Biblia yalichaguliwa kulingana na mawazo na mwanadamu? Zaidi ya hayo, hatima ya Petro na Paulo hazijaelezwa kwa dhati katika nyaraka, kwa hivyo mwanadamu anawahukumu Petro na Paulo kulingana na mtazamo wake mwenyewe, na kulingana na matakwa yake mwenyewe. Na kwa kuwa Paulo alifanya kazi kubwa sana, kwa sababu “michango” yake ilikuwa mikuu sana, yeye alipata imani ya umma. Je, si mwanadamu anamakinika tu na vitu vya juu juu tu. Inakuwaje mwanadamu kuwa na uwezo wa kuona kupitia kwa kiini cha mwanadamu? Bila kutaja, kwa kuwa Paulo amekuwa mlengwa wa ibada kwa maelfu ya miaka, ni nani ambaye atathubutu kukana kazi yake kwa haraka? Petro alikuwa mvuvi tu, hivyo ni jinsi gani mchango wake ungekuwa mkubwa kama ule wa Paulo? Kwa msingi wa mchango, Paulo angepaswa kuzawadiwa kabla ya Petro, na inapaswa kuwa yeye ndiye angekuwa amehitimu vyema zaidi kupata kibali cha Mungu. Nani angeweza kufikiri kuwa, katika kumtendea Paulo, Mungu alimfanya tu afanye kazi kupitia vipawa vyake, ilhali Mungu alimfanya Petro kuwa mkamilifu. Si kwa njia yoyote kweli ya kwamba Bwana Yesu alikuwa amefanya mpango kwa ajili ya Petro na Paulo tangu mwanzo kabisa: Badala yake, walifanywa wakamilifu au kuwekwa kazini kulingana na tabia zao za kiasili. Na kwa hivyo, kitu ambacho wanadamu wanachoona kama michango ya nje ya mwanadamu tu, ilhali anachoona Mungu ni kiini cha mtu, na vile vile kama njia ambayo mwanadamu hufuatilia tangu mwanzo, na motisha inayosukuma harakati ya mwanadamu. Watu hupima mwanadamu kulingana na dhana zao, na kulingana na mitazamo yao wenyewe, na bado hatima ya mwisho ya mwanadamu haiamuliwi kulingana na mambo ya nje ya mwanadamu. Na kwa hivyo Mimi ninasema kwamba kama njia unayochukua tangu mwanzo ni njia ya mafanikio, na mtazamo wako kuhusu harakati ni sahihi tangu mwanzo, basi wewe ni kama ya Petro; kama njia ambayo unatembea ni njia ya kushindwa, basi gharama yoyote ambayo unalipa, hatima yako itakuwa sawa na ile ya Paulo. Yawayo yoyote, hatima yako, na kama utafaulu ama hautafaulu, yote yanaamuliwa na kama njia unayotafuta ni sahihi ama si sahihi, badala ya kujitolea kwako, au gharama ambayo wewe hulipa. Kiini cha Petro na kiini cha Paulo, na malengo ambayo walifuatilia, yalikuwa tofauti; mwanadamu hana uwezo wa kugundua vitu hivi, na Mungu pekee anaweza kuyajua kwa ujumla wao. Kwa kuwa kitu ambacho Mungu huona ni kiini cha mwanadamu, ilhali mwanadamu hajui chochote kuhusu kiini chake mwenyewe. Mwanadamu hana uwezo wa kukitazama kiini ndani ya mwanadamu ama kimo chake halisi, na hivyo hana uwezo wa kutambua sababu za kutofaulu ama kufaulu kwa Paulo na Petro. Sababu ya wanadamu wengi kumuabudu Paulo na wala si Petro ni kuwa Paulo alitumika katika kazi ya umma, na mwanadamu anaweza kutambua kazi hii, na hivyo watu wanakiri “mafanikio” ya Paulo. Matukio ya Petro, wakati huo huo, hayaonekani na mwanadamu, na kwamba kile alichotafuta hakipatikani na mwanadamu, na hivyo mwanadamu hana moyo wa kutaka kumjua Petro.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp