Kuijua Kazi ya Mungu Leo
Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (katika siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Anazungumza tu ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, ili kila mtu awe amepewa na kutiwa nuru maneno Yake, na ili roho ya mwanadamu iamshwe na aweze kuona vizuri kuhusu maono yake. Wakati wa siku za mwisho, Mungu katika mwili Amekuja duniani hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno. Yesu Alipokuja, Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni, na Akatimiza kazi ya wokovu wa msalaba. Alihitimisha Enzi ya Sheria, na Akakomesha mambo yote ya kale. Ujio wa Yesu ulihitimisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema. Ujio wa Mungu katika mwili wa siku za mwisho umehitimisha Enzi ya Neema. Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, kutumia maneno ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, kumwangazia na kumpa nuru mwanadamu, na kumwondoa Mungu asiye yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii sio hatua ya kazi ambayo Yesu Aliifanya Alipokuja. Yesu Alipokuja, Alifanya miujiza mingi, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alifanya kazi ya wokovu ya msalaba. Na matokeo yake ni kwamba, katika dhana za mwanadamu, mwanadamu anaamini kwamba hivi ndivyo Mungu Anapaswa kuwa. Maana Yesu Alipokuja, hakufanya kazi ya kuondoa taswira ya Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu; Alipokuja, Alisulubishwa, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni. Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho.
Kile unachopaswa kujua:
1. Kazi ya Mungu si ya kimiujiza, na hupaswi kuhifadhi dhana juu yake.
2. Unapaswa kuelewa kazi kuu ambayo Mungu katika mwili Amekuja kufanya wakati huu.
Hakuja kuponya wagonjwa, au kutoa mapepo, au kufanya miujiza, na Hajakuja kueneza injili ya toba, au kumpatia mwanadamu ukombozi. Hiyo ni kwa sababu Yesu Amekwishafanya kazi hii, na Mungu Harudii kazi ile ile. Leo, Mungu Amekuja kuhitimisha Enzi ya Neema, na kuzitupilia mbali desturi zote za Enzi ya Neema. Mungu wa vitendo Amekuja hasa kuonyesha kuwa Yeye ni halisi. Yesu Alipokuja Alizungumza maneno machache; hasa Alionyesha miujiza, Akafanya ishara na maajabu, na Akaponya wagonjwa na kutoa mapepo, au wakati mwingine Alizungumza unabii ili kumshawishi mwanadamu, na kumfanya mwanadamu aone kwamba ni kweli Alikuwa Mungu, na Alikuwa Mungu Asiyependelea. Hatimaye, Akakamilisha kazi ya msalaba. Mungu wa leo Haonyeshi ishara na maajabu, wala Haponyi wagonjwa na kutoa mapepo. Yesu Alipokuja, kazi Aliyoifanya iliwakilisha upande mmoja wa Mungu, lakini wakati huu Mungu Amekuja kufanya hatua ya kazi ambayo imetazamiwa, maana Mungu Harudii kazi ile ile; ni Mungu ambaye siku zote ni mpya na Hawezi kuzeeka kamwe, na hivyo yale yote unayoyaona leo ni maneno na kazi ya Mungu wa vitendo.
Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika maisha ya mwanadamu, kuonyesha yale ambayo mwanadamu anapaswa kuingia kwayo, kumwonesha mwanadamu matendo ya Mungu, na kumwonesha mwanadamu hekima, uweza na uajabu wa Mungu. Kupitia njia nyingi ambazo Mungu Anazungumza, mwanadamu anatazama ukuu wa Mungu, aidha, unyenyekevu na usiri wa Mungu. Mwanadamu anatazama kwamba Mungu ni mkuu, lakini ni mnyenyekevu na msiri, na Anaweza kuwa mdogo kuliko vitu vyote. Baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa Roho, baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu, na baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu. Katika hili inaweza kuonekana kwamba namna ya kazi ya Mungu inatofautiana kwa kiasi kikubwa na ni kwa njia ya maneno ndipo Anamruhusu mwanadamu kuiona. Kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho ni ya kawaida na halisi, na hivyo kundi la watu wa siku za mwisho wanakumbwa na majaribu makubwa kuliko yote. Kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu, watu wote wameingia katika majaribu hayo; kwamba mwanadamu ameingia katika majaribu ya Mungu ni kwa sababu ya ukawaida na uhalisia wa Mungu. Wakati wa enzi ya Yesu, hakukuwa na dhana au majaribu. Kwa sababu kazi kubwa iliyofanywa na Yesu ilikuwa ni kulingana na dhana za mwanadamu, watu walimfuata, na hawakuwa na dhana juu Yake. Majaribu ya leo ni makubwa sana ambayo yamewahi kukabiliwa na mwanadamu, na inaposemwa kwamba watu hawa wametoka katika dhiki kuu, hii ndiyo dhiki inayoongelewa. Leo, Mungu Ananena ili kusababisha imani, upendo, ustahimilivu na utii kwa watu hawa. Maneno yaliyozungumzwa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho ni kutokana na hulka ya asili ya mwanadamu, kulingana na tabia ya mwanadamu, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia kwacho leo. Mbinu Yake ya kuzungumza[a] ni halisi na ya kawaida: Hazungumzi juu ya kesho, wala Haangalii nyuma, jana; Anazungumza kile tu ambacho kinapaswa kuingiwa kwacho, kuwekwa katika vitendo, na kueleweka leo. Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na ana uwezo wa kutoa mapepo, na kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine; mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Unapaswa kuelewa vizuri mambo haya. Kwa nini kazi ya Mungu leo ni tofauti na kazi ya Yesu? Kwa nini Mungu leo Haonyeshi ishara na maajabu, Hatoi mapepo, na Haponyi wagonjwa? Ikiwa kazi ya Yesu ingekuwa sawa na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Sheria, je, Angekuwa Amemwakilisha Mungu wa Enzi ya Neema? Je, Yesu Angekuwa Amemaliza kazi ya msalaba? Ikiwa, kama katika Enzi ya Sheria, Yesu Angeingia hekaluni na kuitunza Sabato, basi Asingeteswa na mtu yeyote na Angekumbatiwa na wote. Kama ingekuwa hivyo, je, Angesulubiwa? Je, Angekuwa Amemaliza kazi ya ukombozi? Je, ingekuwa na maana gani ikiwa Mungu katika mwili wa siku za mwisho Angeonyesha ishara na maajabu kama Yesu? Ikiwa tu Mungu Atafanya sehemu nyingine ya kazi Yake wakati wa siku za mwisho, kazi inayowakilisha sehemu ya mpango wa usimamizi Wake, ndipo mwanadamu anaweza kupata maarifa ya kina ya Mungu, na baada ya hapo tu ndipo mpango wa usimamizi wa Mungu unaweza kukamilika.
Wakati wa siku za mwisho Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu. Mara tu taswira ya Mungu ndani ya mwanadamu inapozeeka, basi inakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hii ya kazi, Hakuwakilisha Mungu kikamilifu. Alifanya baadhi ya ishara na maajabu, Alizungumza maneno kadhaa, na hatimaye Akasulubishwa, na Aliwakilisha upande mmoja wa Mungu. Hakuweza kuwakilisha yale yote ambayo ni ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya upande mmoja wa kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu, na ni wa ajabu sana, na Haeleweki, na kwa sababu Mungu Anafanya upande mmoja tu wa kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Akazungumza maneno fulani kwa Wanaisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu yaliwekwa wazi, lakini kwa sababu ubora wa tabia ya mwanadamu ulikuwa finyu na hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kukamilika, Mungu Aliendelea kuzungumza na kufanya kazi. Wakati wa Enzi ya Neema, mwanadamu aliweza kuona tena sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu Aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kutoa mapepo, na kusulubishwa, siku tatu baadaye. Akafufuka na Akawatokea watu Akiwa katika mwili. Kumhusu Mungu, mwanadamu hakujua chochote zaidi ya hiki. Mwanadamu anajua tu kile ambacho Mungu Amemwonyesha, na kama Mungu Asingeonyesha chochote zaidi kwa mwanadamu, basi hicho kingekuwa kiwango cha mwanadamu kumwekea mipaka Mungu. Hivyo, Mungu Anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu juu Yake yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili taratibu aweze kuijua hulka ya Mungu. Mungu anatumia maneno yake kumkamilisha mwanadamu. Tabia yako iliyoharibika imewekwa wazi kwa maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinaondolewa na uhalisia wa Mungu. Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kutimiza maneno haya kwamba “Neno Lafanyika kuwa mwili, Neno Lakuwa mwili, na Neno Laonekana katika mwili,” na kama huna maarifa ya kina kuhusu hili, basi hutaweza kusimama imara; wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa Mungu wa usimamizi. Hivyo, maarifa yako yanapaswa kuwa wazi; bila kujali namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, Mungu Hamruhusu mwanadamu kumwekea mipaka. Ikiwa Mungu Asingefanya kazi hii wakati wa siku za mwisho, basi maarifa ya mwanadamu juu Yake yasingeweza kwenda popote. Ungeweza kujua tu kwamba Mungu Anaweza kusulubiwa na Anaweza kuiangamiza Sodoma, na kwamba Yesu Anaweza kufufuliwa kutoka katika wafu na kumtokea Petro…. Lakini usingeweza kusema kwamba maneno ya Mungu yanaweza kutimiza yote, na yanaweza kumshinda mwanadamu. Ni kwa njia tu ya kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu ndipo unaweza kuzungumza juu ya maarifa hayo, na kadri unapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu zaidi, ndivyo maarifa yako yanavyokuwa ya kina zaidi kumhusu Yeye. Ni baada ya hapo tu ndipo utaacha kumwekea Mungu mipaka ndani ya dhana zako binafsi. Mwanadamu anakuja kumjua Mungu kwa kupitia kazi Yake, na hakuna njia nyingine sahihi ya kumjua Mungu. Leo, kuna watu wengi ambao hawafanyi chochote bali wanasubiri kuona ishara na maajabu na wakati wa maangamizi. Je, unamwamini Mungu, au unaamini katika maangamizi? Ukisubiri hadi wakati wa maangamizi utakuwa umechelewa sana, na ikiwa Mungu Hataleta maangamizi, basi Atakuwa si Mungu? Je, unaamini ishara na maajabu, au unamwamini Mungu Mwenyewe? Yesu Hakuonyesha ishara na maajabu wakati Alipobezwa na wengine; je, Hakuwa Mungu? Je, unaamini ishara na maajabu, au unaamini katika hulka ya Mungu? Mitazamo ya mwanadamu kuhusu imani kwa Mungu ni makosa! Yehova Alizungumza maneno mengi wakati wa Enzi ya Sheria, lakini hata leo baadhi yake bado hayajatimizwa. Je, unaweza kusema kwamba Yehova Hakuwa Mungu?
Leo, inapaswa kueleweka kwenu wote kwamba, katika siku za mwisho, ni kwa kiasi kikubwa ukweli wa “Neno linakuwa mwili” ambao unakamilishwa na Mungu. Kupitia kazi yake halisi duniani, Anafanya mwanadamu kumfahamu, na kushirikiana Naye, na kuona matendo Yake halisi. Anamsababisha mwanadamu kuona kwa wazi kwamba Yeye Anaweza kuonyesha ishara na maajabu na pia kuna nyakati ambapo Hawezi kufanya hivyo, na hii inategemea enzi. Kutokana na hili unaweza kuona kwamba Mungu sio kwamba Hawezi kuonyesha ishara na maajabu, lakini badala yake Anabadilisha kufanya kazi Kwake kulingana na kazi Yake, na kulingana na enzi. Katika hatua ya sasa ya kazi, Haonyeshi ishara na maajabu; kuonyesha kwake baadhi ya ishara na maajabu katika enzi ya Yesu, ilikuwa ni kwa sababu kazi Yake katika enzi hiyo ilikuwa tofauti. Mungu Hafanyi kazi hiyo leo, na baadhi ya watu wanaamini Hana uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, au wanafikiri kwamba kama Haonyeshi ishara na maajabu, basi Yeye si Mungu. Hii sio hoja ya uwongo? Mungu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, lakini Anafanya kazi katika enzi tofauti, na hivyo Hafanyi kazi hiyo. Kwa kuwa hii ni enzi tofauti, na kwa kuwa hii ni hatua tofauti ya kazi ya Mungu, matendo yaliyowekwa wazi na Mungu pia ni tofauti. Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio imani katika ishara na maajabu, wala imani katika miujiza, bali ni imani katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya. Mwanadamu anamjua Mungu kupitia namna ambavyo Mungu Anafanya kazi, na maarifa haya yanamfanya mwanadamu amwamini Mungu, ambavyo ni kusema, imani katika kazi na matendo ya Mungu. Katika hatua hii ya kazi, Mungu Anazungumza hasa. Usisubiri kuona ishara na maajabu; hutayaona! Maana hukuzaliwa katika Enzi ya Neema. Kama ungezaliwa katika Enzi ya Neema, ungeweza kuona ishara na maajabu, lakini umezaliwa katika siku za mwisho, na hivyo unaweza kuona tu uhalisia na ukawaida wa Mungu. Usitarajie kumwona Yesu wa kimiujiza wakati wa siku za mwisho. Unaweza kumwona tu Mungu katika mwili wa vitendo, Ambaye si tofauti na mwanadamu yeyote wa kawaida. Katika kila enzi, Mungu Anaweka wazi matendo mbalimbali. Katika kila enzi Anaweka wazi sehemu ya matendo ya Mungu, na kazi ya kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu, na inawakilisha sehemu moja ya matendo ya Mungu. Matendo Anayoyaweka wazi yanatofautiana na enzi ambayo kwayo Anafanya kazi, lakini yote yanampatia mwanadamu maarifa ya Mungu ambayo ni ya kina, imani kwa Mungu ambayo ni yenye kuhusika na mambo halisi sana, na ambayo ni ya kweli zaidi. Mwanadamu anamwamini Mungu kwa sababu ya matendo yote ya Mungu, na kwa sababu Mungu ni wa ajabu ni mkuu sana, kwa sababu Yeye ni mwenyezi, na ambaye Hapimiki kina. Ikiwa unamwamini Mungu kwa kuwa Anaweza kufanya ishara na maajabu na Anaweza kuponya wagonjwa na kuwatoa mapepo, basi mtazamo wako si sahihi, na baadhi ya watu watakwambia, “Je, pepo wachafu pia hawawezi kufanya mambo hayo?” Je, hii sio kuielewa vibaya taswira ya Mungu kwa kuilinganisha na taswira ya Shetani? Leo, imani ya mwanadamu kwa Mungu ni kwa sababu ya matendo Yake mengi na njia nyingi ambazo kwazo Anafanya kazi na kuzungumza. Mungu Anatumia matamshi yake kumshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu. Mwanadamu anamwamini Mungu, kwa sababu ya matendo Yake mengi, na si kwa sababu Anaweza kuonyesha ishara na maajabu, na wanadamu wanamwelewa tu kwa sababu wanaona matendo Yake, Ni kwa kujua tu matendo halisi ya Mungu, namna Anavyofanya kazi, njia ambazo Anaonyesha hekima Yake, vile Anavyozungumza, na jinsi Anavyomfanya mwanadamu kuwa mkamilifu—ni kwa kujua tu vipengele hivi—ndipo unaweza kufahamu uhalisia wa Mungu na kuelewa tabia Yake. Kile Anachopenda, kile Anachochukia, namna Anavyomfanyia kazi mwanadamu—kwa kuelewa yale ambayo Mungu Anayapenda na Asiyoyapenda, unaweza kutofautisha kati ya kile ambacho ni chanya na kile ambacho ni hasi, na kupitia maarifa yako juu ya Mungu kunakuwa na maendeleo katika maisha yako. Kwa ufupi unapaswa kuwa na maarifa ya kazi ya Mungu, na unapaswa kuweka sahihi mitazamo yako kuhusu kuwa na imani kwa Mungu.
Tanbihi:
a. Matini halisia inasomeka “Hicho.”
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?