Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 163

Kuna njia sita za msingi ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu.

Ya kwanza ni kudhibiti na kulazimisha. Yaani, Shetani atafanya vyovyote vile kudhibiti moyo wako. “Kulazimisha” kunamaanisha nini? (Kunamaanisha shurutisho.) Hukutishia na kukulazimisha kumtii, kukufanya kufikiria matokeo usipomtii. Unaogopa na huthubutu kumpinga, kwa hivyo basi unamtii.

Ya pili ni kudanganya na kulaghai. “Kudanganya na kulaghai” yanahusisha nini? Shetani hutunga baadhi ya hadithi na uongo, kukulaghai wewe kuziamini. Hakwambii kamwe kwamba mwanadamu aliumbwa na Mungu, wala hasemi pia moja kwa moja kwamba hukuumbwa na Mungu. Hatumii jina “Mungu” kabisa, lakini badala yake hutumia kitu kingine mbadala, akitumia kitu hiki kukudanganya ili kimsingi usiwe na wazo la kuwepo kwa Mungu. Huu ulaghai bila shaka unahusisha vipengele vingi, sio tu hiki kimoja.

Ya tatu ni kufunza kwa nguvu. Je, kuna kufunza kwa nguvu? (Ndiyo.) Kufunza nini kwa nguvu? Je, kufunzwa kwa nguvu kunafanywa kwa hiari ya mwanadamu mwenyewe? Je, kunafanywa na idhini ya mwanadamu? (La.) Haijalishi kama hukuidhinisha. Katika kutojua kwako, humwaga ndani yako, kuweka ndani yako kufikiria kwa Shetani, kanuni zake za maisha na kiini chake.

Ya nne ni vitisho na vivutio. Yaani, Shetani hutumia mbinu mbalimbali ili umkubali, umfuate, ufanye kazi katika Huduma yake; hujaribu kufikia malengo yake kwa vyovyote vile. Saa zingine hukupa fadhili ndogo lakini bado hukushawishi kufanya dhambi. Usipomfuata, atakufanya uteseke na kukuadhibu na atatumia njia mbalimbali kukushambulia na kukutega.

Ya tano ni uongo na kiharusi. “Uongo na kiharusi” ni kwamba Shetani hutunga kauli na mawazo yanayosikika kuwa matamu ambayo yako pamoja na dhana za watu kufanya ionekane kwamba anatilia maanani miili ya watu ama anafikiria kuhusu maisha yao na siku zao za baadaye, wakati hakika anakudanganya tu. Kisha anakupooza ili usijue kile kilicho sahihi na kile kilicho makosa, ili udanganywe bila kujua na hivyo kuja chini ya udhibiti wake.

Ya sita ni uangamizi wa mwili na akili. Shetani huharibu kipi cha mwanadamu? (Akili yao, nafsi yao yote.) Shetani huharibu akili yako, kukufanya kutokuwa na nguvu za kupinga, kumaanisha kuwa polepole sana moyo wako unageuka kwa Shetani licha ya wewe mwenyewe. Huingiza mambo haya ndani yako kila siku, kila siku akitumia mawazo na utamaduni huu kukushawishi na kukuelimisha, polepole akiharibu utashi wako, kukufanya kutotaka kuwa mtu mzuri tena, kukufanya kutotaka tena kutotetea kile unachoita cha haki. Bila kujua, huna tena utashi wa kuogelea kinyume na mkondo dhidi ya bamvua, lakini badala yake kububujika chini pamoja nayo. “Uangamizi” unamaanisha kwamba Shetani hutesa watu sana hadi wanakuwa sio kama wanadamu wala pepo, kisha anachukua fursa ya kuwameza.

Kila ya hizi njia zote Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu inaweza kumfanya mwanadamu kutokuwa na nguvu ya kupinga; yoyote inaweza kuwa ya kufisha kwa watu. Kwa maneno mengine, chochote anachofanya Shetani na njia yoyote anayotumia inaweza kukufanya kupotoka, inaweza kukuleta chini ya udhibiti wa Shetani na inaweza kukuzamisha katika bwawa la uovu. Hizi ndizo njia Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp