Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 152

Shetani hutumia mbinu hizi nyingi kumpotosha mwanadamu. Mwanadamu ana maarifa na baadhi ya nadharia za kisayansi, mwanadamu anaishi na ushawishi wa desturi ya kitamaduni, na kila mtu anarithi desturi ya kitamaduni. Mwanadamu ataendeleza desturi ya kitamaduni aliyopewa kutoka kwa Shetani na pia kutenda pamoja na mienendo ya kijamii ambayo Shetani anawapa wanadamu. Binadamu hawezi kutengana na Shetani, kushiriki na kile ambacho Shetani anafanya wakati wote, kukubali udanganyifu, kiburi, kijicho, na uovu wake. Mwanadamu alipomiliki tabia hizi za Shetani, amekuwa na furaha ama huzuni kuishi miongoni mwa wanadamu hawa na katika dunia hii? (Huzuni.) Mbona unasema hivyo? (Amefungwa na vitu hivi na maisha yake ni mapambano machungu.) Hmm. Mtu fulani ambaye ana miwani na anaonekana wa hekima; pengine kamwe hapigi kelele, awe daima na lugha ya kushawishi, wa busara, na zaidi ya hayo, kwa sababu ya umri wake mkubwa, pengine amepitia vitu vingi na kuwa na uzoefu mkubwa; pengine anaweza kuzungumza kwa undani kuhusu masuala makubwa na madogo na kuwa na msingi dhabiti wa kile anachosema; pengine pia ana seti ya nadharia ya kutathmini uhalisi na sababu ya vitu; na watu pengine wanaweza kuangalia tabia yake, sura yake, na kuona jinsi anavyotenda na kuona uadilifu wake na hulka yake na kutopata dosari kwake. Watu kama hawa hasa wanashughulika na mienendo ya kijamii ya sasa na hawachukuliwi kuwa wa mtindo wa kizamani Ingawa mtu huyu anaweza kuwa mzee, kamwe hayuko nyuma ya nyakati na kamwe si mzee sana kufunzwa. Juujuu, hakuna anayeweza kupata dosari kwake, lakini ndani amepotoshwa na Shetani kabisa na kikamilifu. Juujuu hakuna chochote kibaya, yeye ni mpole, ni muungwana, anayo maarifa na maadili fulani; ana uadilifu na vitu anavyojua vinalingana na vile wanavyojua vijana. Hata hivyo, kuhusu asili na kiini chake, mtu huyu ni mfano kamili na unaoishi wa Shetani, ana usawa kabisa na Shetani. Hili ni “tunda” la upotovu wa Shetani kwa mwanadamu. Kile Nilichosema kinaweza kuwaumiza, lakini chote ni ukweli. Maarifa ambayo mwanadamu anasoma, sayansi anayoelewa, na mbinu anazochagua kuingiliana na mienendo ya jamii, bila ubaguzi, ni vyombo vya upotovu wa Shetani. Huu ni ukweli kabisa. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi miongoni mwa tabia ambayo imepotoshwa kabisa na Shetani na mwanadamu hana njia ya kujua utakatifu wa Mungu ni nini na kiini cha Mungu ni nini. Hii ni kwa sababu juujuu mtu hawezi kupata dosari kwa njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu; hakuna anayeweza kuamua kutoka kwa tabia ya mtu kwamba kuna chochote kibaya. Kila mtu anaendelea na kazi yake kwa kawaida na kuishi maisha ya kawaida; wanasoma vitabu na magazeti kwa kawaida, wanasoma na kuzungumza kwa kawaida; watu wengine hata wamejifunza kuwa na sura ya kinafiki ya maadili ili waweze kusema salamu zao, kuwa na heshima, kuwa na adabu, kuwaelewa wengine, kuwa na urafiki, kuwasaidia wengine, kuwa wenye hisani, na wataepuka kulalamika kwa wengine na kuepuka kutumia watu kwa manufaa yao. Hata hivyo, tabia yao iliyopotoka ya kishetani imekita mizizi ndani yao; kiini hiki hakiwezi kubadilishwa kwa kutegemea juhudi za nje. Mwanadamu hana uwezo wa kujua utakatifu wa Mungu kwa sababu ya kiini hiki, na licha ya kiini cha utakatifu wa Mungu kuwekwa wazi kwa mwanadamu, mwanadamu hakichukulii kwa umakini. Hii ni kwa sababu Shetani tayari amemiliki kabisa hisia, fikira, mitazamo, na mawazo ya mwanadamu kupitia njia mbalimbali. Huu umiliki na upotovu si wa muda mfupi ama wa mara kwa mara; upo kila mahali na kila wakati. Kwa hivyo, watu wengi ambao wamemwamini Mungu kwa miaka mitatu au minne—hata miaka sita na saba—bado wanashikilia mawazo na mitazamo ambayo Shetani amewaekea kana kwamba wanashikilia hazina. Kwa sababu mwanadamu ameukubali uovu, kiburi, na mambo kutoka kwa asili ya kijicho ya Shetani, bila kuepukika kwa mahusiano ya ana kwa ana ya mwanadamu mara nyingi kuna migogoro, mara nyingi kuna magombano na kutokuwa na uwiano, mambo ambayo yameumbwa kwa sababu ya asili ya kiburi ya Shetani. Iwapo Shetani angempa mwanadamu vitu vyema—kwa mfano, iwapo Uconfucius na Utao wa desturi ya kitamaduni ambayo mwanadamu alikubali ilichukuliwa kuwa vitu vizuri—watu wa aina sawa wanapaswa kuweza kupatana na wengine baada ya kukubali vitu hivyo, siyo? Hivyo mbona kuna mgawanyiko mkubwa kati ya watu waliokubali vitu sawa? Mbona hivyo? Ni kwa sababu viti hivi vimetoka kwa Shetani na Shetani husababisha mgawanyiko miongoni mwa watu. Vitu ambavyo Shetani anapatiana, bila kujali jinsi vinavyoonekana kuwa vya heshima na vikubwa juujuu, vinamletea mwanadamu na vinaleta katika maisha ya mwanadamu kiburi pekee, na si chochote ila udanganyifu wa asili ovu ya Shetani. Sivyo? Mtu ambaye angeweza kujificha, kumiliki maarifa mengi, ama kuwa na malezi mazuri angekuwa na wakati mgumu kusitiri tabia yao potovu ya kishetani. Hiyo ni kusema, haijalishi mtu huyu atajificha kwa njia ngapi, kama ulimfikiri kuwa mtakatifu, ama kama ulifikiri ni mkamilifu, ama kama ulifikiri ni malaika, haijalishi ulifikiri ni mtu safi vipi, maisha yake yangekuwaje nyuma ya pazia? Utaona asili ipi katika ufunuo wa tabia yake? Bila shaka ungeona asili ovu ya Shetani. Mtu anaweza kusema hivyo? (Ndiyo.) Kwa mfano, tuseme mnamjua mtu wa karibu nanyi ambaye mlifikiri kuwa mtu mzuri, ama ulimfikiri kuwa mtu mzuri, pengine mtu uliyemwabudu kama Mungu. Kwa kimo chako cha sasa, unawafikiri vipi? Kwanza, unaangalia iwapo mtu wa aina hii ana ama hana ubinadamu, iwapo ni mwaminifu, iwapo ana upendo wa kweli kwa watu, iwapo maneno na vitendo vyao vinafaidi na kusaidia wengine. (La.) Yaitwayo wema, upendo na uzuri unaofichuliwa hapa, ni nini kweli? Yote ni uongo, yote ni sura ya kinafiki. Hii sura ya kinafiki ya nyuma ya pazia ina madhumuni maovu ya chinichini: Ni ya kumfanya mtu huyo apendwe na kuabudiwa kama Mungu. Je, mnaona jambo hili kwa dhahiri? (Ndiyo.)

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp