Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 146

Mat 4:8-11 Tena, Ibilisi akampeleka hadi kwenye mlima mrefu sana, na kumwonyesha falme zote za dunia, na fahari yao; Na akasema kwake, Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu. Kisha Yesu akamwambia, Ondoka uende zako, Shetani; kwa kuwa imeandikwa, Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia. Basi akawachwa na Ibilisi, na, tazama, malaika wakaja na wakamhudumia.

Shetani, ibilisi, baada ya kushindwa katika hila zake mbili za awali, alijaribu nyingine tena: Alionyesha falme zote duniani na utukufu wa falme hizi kwa Bwana Yesu na kumwambia amwabudu ibilisi. Unaona nini kuhusu sura za ukweli za ibilisi kutoka kwa hali hii? Si Shetani ibilisi hana haya kabisa? (Ndiyo.) Anaweza kukosa haya namna gani? Kila kitu kiliumbwa na Mungu, lakini Shetani anakigeuza na kumwonyesha Mungu akisema, “Angalia utajiri na utukufu wa falme hizi zote. Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu.” Je, si hili ni mabadiliko ya jukumu? Si Shetani hana haya? Mungu aliumba kila kitu, lakini kilikuwa cha raha Zake? Mungu alimpa mwanadamu kila kitu, lakini Shetani alitaka kunyakua vyote na baadaye akasema, “Niabudu! Niabudu na nitakupa Wewe haya yote.” Huu ni uso usiopendeza wa Shetani; hana haya kabisa, siyo? Shetani hata hajui maana ya neno “haya,” na huu ni mfano mwingine tu wa uovu wake. Hata hajui haya ni nini. Shetani anajua vyema kwamba Mungu aliumba kila kitu na kwamba Anavisimamia na Anavitawala. Kila kitu ni cha Mungu, si cha mwanadamu, sembuse Shetani, lakini Shetani ibilisi bila haya alisema kwamba angempa Mungu kila kitu. Si tena Shetani anafanya kitu cha ujinga na kisicho na aibu? Mungu anamchukia Shetani hata zaidi sasa, siyo? Lakini licha ya kile Shetani alijaribu kufanya, Bwana Yesu alikiamini? (La.) Bwana Yesu alisema nini? (“Muabudu Bwana Mungu wako.”) Je, kirai hiki kina maana ya utendaji? (Ndiyo.) Maana gani ya utendaji? Tunaona uovu na kutokuwa na aibu kwa Shetani katika matamshi yake. Kwa hivyo iwapo mwanadamu angemwabudu Shetani, hitimisho lingekuwa nini? Angepokea utajiri na utukufu wa falme zote? (La.) Angepokea nini? Je, wanadamu wangekuwa wasio na haya na wa kuchekwa kama tu Shetani? (Ndiyo.) Hawangekuwa tofauti na Shetani basi. Kwa hivyo, Bwana Yesu alisema kirai hiki ambacho ni muhimu kwa kila mtu: “Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia,” kinachosema kwamba isipokuwa Bwana, isipokuwa Mungu Mwenyewe, ukimhudumia mwingine, ukimwabudu Shetani ibilisi, basi utagaagaa katika uchafu sawa na Shetani. Kisha utashiriki kutokuwa na haya na uovu wa Shetani, na kama tu Shetani ungemjaribu Mungu na kumshambulia Mungu. Na basi mwisho wako ungekuwa upi? Ungechukiwa na Mungu, kuangushwa na Mungu na kuangamizwa na Mungu, sivyo? Baada ya Shetani kumjaribu Bwana Mungu mara kadhaa bila mafanikio, alijaribu tena? Shetani hakujaribu tena na kisha akaondoka. Hii inathibitisha nini? Inathibitisha kwamba asili ovu ya Shetani, kuonea kijicho kwake, na ujinga na upuuzi wake yote hayastahili kutajwa mbele ya Mungu. Bwana Yesu alimshinda Shetani kwa sentensi tatu tu, na baadaye akatoroka na mkia wake katikati ya miguu yake, kuaibika sana asiweze kuonyesha uso wake tena, na hakumjaribu Bwana Yesu tena. Kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amelishinda jaribio hili la Shetani, Angeweza kuendelea kwa urahisi kazi ambayo Alipaswa kufanya na kuanza kazi zilizokuwa mbele Yake. Je, yote aliyoyasema Bwana Yesu na kufanya katika hali hii yanabeba maana kiasi ya vitendo kwa kila mtu yakitumika sasa? (Ndiyo.) Maana ya utendaji ya aina gani? Je, kumshinda Shetani ni kitu rahisi kufanya? (La.) Ingekuwa nini basi? Ni lazima watu wawe na uelewa wazi wa asili ovu ya Shetani? Ni lazima watu wawe na uelewa sahihi wa majaribu ya Shetani? (Ndiyo.) Ukiwahi kupitia majaribu ya Shetani katika maisha yako, na iwapo unaweza kuona hadi kwa asili ovu ya Shetani, utaweza kumshinda? Iwapo unajua kuhusu ujinga na upuuzi wa Shetani, bado unaweza kusimama kando ya Shetani na kumshambulia Mungu? (La, hatungeweza.) Ikiwa unaelewa jinsi kuwa na kijicho na kutokuwa na aibu kwa Shetani vinafichuliwa kupitia kwako—iwapo unatambua wazi na kujua mambo haya—bado ungemshambulia na kumjaribu Mungu kwa njia hii? (La, hatungeweza.) Utafanya nini? (Tutaasi dhidi ya Shetani na kumwacha.) Hili ni jambo rahisi kufanya? (La.) Hili si rahisi, kufanya hivi, watu wanalazimika kuomba mara nyingi, ni lazima wajiweke mbele ya Mungu, na lazima wajichunguze. Lazima watii nidhamu ya Mungu na hukumu Yake na kuadibu Kwake na kwa njia hii tu ndipo watu wataweza kujitoa polepole kutoka kwa udanganyifu na udhibiti wa Shetani.

Tunaweza kuweka pamoja mambo yanayojumuisha kiini cha Shetani kutoka kwa mambo haya ambayo amesema. Kwanza, kiini cha Shetani kwa jumla kinaweza kusemwa kuwa ovu, ambacho ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Kwa nini Nasema kiini cha Shetani ni ovu? Mtu anapaswa kuangalia matokeo ya kile Shetani anafanyia watu ili kuona haya. Shetani anapotosha na kudhibiti mwanadamu, na mwanadamu anatenda chini ya tabia potovu ya Shetani, na anaishi katika dunia iliyopotoshwa na Shetani na kuishi miongoni mwa watu potovu. Wengi wanamilikiwa na kusimilishwa na Shetani bila kusudi; mwanadamu hivyo ana tabia potovu ya Shetani, ambayo ni asili ya Shetani. Kutoka kwa yote Shetani amesema na kufanya, umeona kiburi chake? Umeona udanganyifu na kijicho chake? Kiburi cha Shetani kimsingi kinaonekana vipi? Je, Shetani daima anataka kuchukua nafasi ya Mungu? Shetani daima anataka kuharibu kazi ya Mungu na nafasi ya Mungu na kuyachukua kuwa yake ili watu waunge mkono na kuabudu Shetani; hii ni asili ya kiburi ya Shetani. Wakati Shetani anapotosha watu, huwaambia moja kwa moja kile wanachopaswa kufanya? Wakati Shetani anamjaribu Mungu, je, hatoki na kusema, “Nakujaribu, nitakushambulia”? Hakika hafanyi hivyo. Ni mbinu gani hivyo Shetani anatumia? Anashawishi, anajaribu, anashambulia, na anaweka mitego yake, na hata kwa kutaja maandiko, Shetani anazungumza na kutenda kwa njia mbalimbali ili kutimiza nia zake mbaya. Baada ya Shetani kufanya hivi, ni nini kinachoweza kuonekana kutoka kile kilichojitokeza kwa mwanadamu? Je, si watu wana kiburi? Mwanadamu ameteseka kutoka kwa upotovu wa Shetani kwa maelfu ya miaka na hivyo mwanadamu amekuwa mwenye kiburi mdanganyifu, mwenye kijicho, na asiyefikiri. Haya mambo yote yametokana kwa sababu ya asili ya Shetani. Kwa sababu asili ya Shetani ni ovu, amempa mwanadamu asili hii ovu na kumletea mwanadamu tabia hii potovu. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi chini ya tabia potovu ya kishetani na, kama Shetani, mwanadamu anaenda kinyume na Mungu, anamshambulia Mungu, na kumjaribu Yeye hadi kwa kiwango ambacho mwanadamu hamwabudu Mungu na hamheshimu katika moyo wake.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp