Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 366
Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Wakati mtu hana maarifa yaliyo wazi na hajapitia ukuu wa Mungu na mipangilio Yake, maarifa ya mtu kuhusu hatima na yale ya kifo yatakuwa yale yasiyoeleweka. Watu hawawezi kuona waziwazi kwamba haya yote yamo kwenye kiganja cha mkono wa Mungu, hawatambui kwamba Mungu ameushika usukani na Anashikilia ukuu juu yao, hawatambui kwamba binadamu hawezi kutupa nje au kutoroka ukuu kama huo; na kwa hivyo wakati wanapokabiliwa na kifo hakuna mwisho wowote katika maneno yao ya mwisho, wasiwasi wao, na hata majuto. Wanalemewa sana na mambo mengi, wanajivuta ajabu, kunakuwa na mkanganyo mkubwa, na haya yote yanawafanya kuogopa kifo. Kwani mtu yeyote aliyezaliwa ulimwenguni humu, kuzaliwa kwake kunahitajika, na kuaga kwake hakuwezi kuepukika, na hakuna mtu anayeweza kuupiga chenga mkondo huu. Kama mtu atataka kuondoka ulimwenguni humu bila maumivu, kama mtu atataka kukabiliana na awamu ya mwisho ya maisha bila kusitasita au wasiwasi, njia pekee ni kutokuwa na majuto. Na njia pekee ya kuondoka bila majuto ni kujua ukuu wa Muumba, kujua mamlaka yake, na kunyenyekea mbele zake. Ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuwa mbali na mahangaiko ya binadamu, maovu, utumwa wa Shetani; ni kwa njia hii ndipo mtu anaweza kuishi maisha kama ya Ayubu, akiongozwa na akibarikiwa na Muumba, maisha yaliyo huru na yaliyokombolewa, maisha yenye thamani na maana, maisha yenye uaminifu na moyo wazi; ni kupitia kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kunyenyekea, kama Ayubu, kujaribiwa na kunyang’anywa na Muumba, kunyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Muumba; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kumwabudu Muumba maisha yake yote na kuweza kupata pongezi Lake, kama Ayubu alivyopata, na kusikia sauti Yake, kumwona akionekana; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi na kufa kwa furaha, kama Ayubu, bila ya maumivu, bila wasiwasi, bila majuto; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi kwa nuru, kama Ayubu, kupita kila mojawapo ya awamu ya maisha kwa nuru, na kukamilisha vizuri safari yake kwa nuru, kutimiza kwa ufanisi kazi yake maalum—kupitia, kujifunza, na kujua ukuu wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa—na kuiaga dunia kwa nuru, na milele hadi milele kusimama upande wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa, kilichopongezwa na Yeye.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata...
Baada ya kutekeleza kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, kimsingi kumshinda Shetani na kuwaokoa...
Duniani, Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe katika mioyo ya watu; mbinguni, Mimi Ndiye Mkuu wa viumbe vyote. Nimepanda milima na kuvuka...
Hakuna aliye na imani kwamba atauona utukufu Wangu, na Mimi simlazimishi, badala yake Nauondoa utukufu Wangu kutoka miongoni mwa wanadamu...