Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili)

Kwanza Mungu alimwumba Adamu na Hawa, na pia Alimwumba nyoka. Miongoni mwa mambo haya yote, nyoka ndiye aliyekuwa mwenye sumu zaidi; mwili wake ulikuwa na sumu, na Shetani aliitumia sumu hiyo ili kufaidika. Ni nyoka aliyemjaribu Hawa hadi akatenda dhambi. Adamu alitenda dhambi baada ya Hawa kutenda, na wawili hawa waliweza kutofautisha kati ya mema na maovu. Kama Yehova Alikuwa Amejua kwamba nyoka angemjaribu Hawa, na kwamba Hawa angemjaribu Adamu, kwa nini Akawaweka wote pale katika bustani? Kama Aliweza kutabiri mambo haya kwa nini Akamwumba nyoka na kumweka ndani ya Bustani ya Edeni? Kwa nini Bustani ya Edeni ilikuwa na tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Alinuia wao walile hilo tunda? Wakati Yehova alipokuja, Adamu wala Hawa hawakuthubutu kumkabili Yeye, na ulikuwa tu wakati huu ambapo Yehova alijua kwamba walikuwa wamelila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kujipata katika ujanja wa yule nyoka. Hatimaye Alimlaani nyoka, na Akamlaani Adamu na Hawa. Yehova hakuwa na habari wakati wawili hawa walipolila tunda lile la mti. Binadamu walipotoka hadi kufikia kiwango cha kuwa na uovu na uasherati wa kimapenzi, hadi kufikia awamu ya mambo haya yote waliyoyahifadhi katika mioyo yao yakawa maovu na yasiyo ya haki; yote yalikuwa machafu. Yehova hivyo basi alijutia kwa kuumba binadamu. Baadaye Alitekeleza kazi Yake ya kuharibu ulimwengu kwa gharika, ambayo Nuhu na watoto wake wa kiume walinusurika. Baadhi ya mambo kwa hakika hayajaendelea na kuzidi maumbile ya kawaida kama vile watu wanavyoweza kufikiria. Baadhi wanauliza: Kwa sababu Mungu alijua malaika mkuu angemsaliti Yeye, kwa nini alimwumba? Hizi ndizo hoja: Wakati nchi haikuwepo, malaika mkuu ndiye aliyekuwa malaika mkuu zaidi mbinguni. Alikuwa na mamlaka juu ya malaika wote kule mbinguni; haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ambayo Mungu alimpa. Kando na Mungu, ndiye aliyekuwa malaika mkubwa zaidi mbinguni. Wakati Mungu alipouumba binadamu baadaye, malaika mkuu alitekeleza usaliti mkuu zaidi dhidi ya Mungu nchini. Nasema kwamba alimsaliti Mungu kwa sababu alitaka kuwasimamia binadamu na kumzidi Mungu katika mamlaka. Ni malaika mkuu ambaye alimjaribu Hawa hadi akatenda dhambi; alifanya hivyo kwa sababu alipenda kuanzisha ufalme wake nchini na kuwafanya binadamu kumsaliti Mungu na kumtii badala yake. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi ambavyo vilimtii; malaika walimtii sawa na vile ambavyo watu walivyomtii duniani. Ndege na wanyama, miti, misitu, milima, mito na viumbe vyote vilivyo nchini vilikuwa katika utunzaji wa binadamu—yaani, Adamu na Hawa—huku nao Adamu na Hawa wakimtii. Malaika mkuu hivyo basi alitamani kuzidi mamlaka ya Mungu na kumsaliti Mungu. Baadaye aliwaongoza malaika wengi kumsaliti Mungu, ambao baadaye walikuja kuwa pepo wachafu mbalimbali. Je, huoni kwamba maendeleo ya binadamu hadi siku ya leo yamesababishwa na upotoshaji wa malaika mkuu? Binadamu wako tu namna walivyo leo kwa sababu malaika mkuu alimsaliti Mungu na kuwapotosha binadamu. Kazi hii ya hatua kwa hatua haipo popote pale karibu na dhahania na nyepesi kama vile watu wanavyofikiria. Shetani alitekeleza usaliti wake kwa sababu fulani, ilhali watu hawawezi kufahamu kitu chepesi kama hicho. Kwa nini Mungu akaiumba mbingu na nchi na viumbe vyote, na pia kumwumba Shetani? Kwa sababu Mungu anamdharau Shetani sana, naye Shetani ni adui Wake, kwa nini akamwumba Shetani? Kwa kumwumba Shetani, hakuwa anamwumba adui? Mungu kwa hakika hakuumba adui; badala yake, Alimwumba malaika, na baadaye malaika akamsaliti Yeye. Hadhi yake ilikuwa kubwa mno kiasi cha kwamba alitaka kumsaliti Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba hali hii ilikuwa ya sadfa, lakini ulikuwa pia mtindo usiokwepeka. Ni sawa na vile ambavyo mtu atakufa akiwa na umri fulani bila uwezo wa kuzuia hali hiyo; mambo yamefikia tayari katika awamu fulani. Kunao hata baadhi ya wale wa kipumbavu wanaosema: “Kwa sababu Shetani ni adui Yako, kwa nini Ukamwumba? Kwani hukujua kuwa malaika huyu mkuu angekusaliti Wewe? Kwani Huwezi kukazia macho kutoka kwa milele moja hadi nyingine? Kwani Wewe huijui asili yake? Kwa sababu ulijua waziwazi kuwa angekusaliti Wewe, basi kwa nini ukamfanya kuwa malaika mkuu? Hata kama mtu atapuuza suala la usaliti wake, aliweza bado kuwaongoza malaika wengi na akashuka hadi kwa ulimwengu wa binadamu wasiodumu ili kuwapotosha binadamu; hadi siku ya leo umeshindwa kukamilisha mpango Wako wa usimamizi wa miaka elfu sita.” Hayo ni kweli? Je, huoni kwamba unajiweka kwenye matatizo mengi zaidi kuliko inavyohitajika? Wengine bado husema: Kama Shetani asingewapotosha binadamu hadi siku ya leo, Mungu asingewaokoa binadamu kwa njia hii. Katika mfano huu, hekima na uweza wa Mungu vyote vingekuwa havionekani; hekima Yake ingewezaje kujionyesha? Hivyo basi Mungu alikiumba kizazi cha binadamu kwa minajili ya Shetani; katika siku za usoni, Mungu angefichua uweza Wake—vinginevyo, binadamu angewezaje kugundua hekima Yake? Kama binadamu asingempinga Yeye na kuchukua hatua ya kumwasi Yeye, isingehitajika kwa vitendo Vyake kujionyesha. Kama uumbaji wote ungemwabudu Yeye na kumtii Yeye, Asingekuwa na kazi ya kufanya. Hali hii nayo ni mbali zaidi na uhalisia wa mambo, kwani hakuna uchafu wowote kuhusu Mungu, na hivyo basi Hawezi kuumba uchafu. Yeye hufichua tu vitendo Vyake ili kuweza kuwashinda kabisa adui Zake, ili kuokoa binadamu, ambao aliuumba, ili kuyashinda mapepo na Shetani, ambao wanamchukia, wanamsaliti Yeye na wanampinga Yeye, ambao walikuwa katika utawala Wake na walimilikiwa na Yeye mwanzo kabisa; Anataka kuwashinda hawa mapepo na katika kufanya hivyo kuufichua uweza Wake kwa viumbe vyote. Binadamu na viumbe vyote vilivyomo nchini sasa hivi vimemilikiwa na Shetani na katika utawala wa waovu. Mungu anataka kuvifichua vitendo Vyake kwa viumbe vyote ili watu waweze kumjua Yeye, na hivyo kuishia kumshinda Shetani na kuangamiza kabisa adui Zake. Uzima wa kazi hii unakamilishwa kupitia matendo Yake yanayofichua. Viumbe Vyake vyote vimemilikiwa na Shetani, na hivyo basi Anapenda kuufichua uweza Wake kwa viumbe hivyo, kwa hivyo kumshinda Shetani. Kama Shetani asingekuwepo, Asingehitaji kuvifichua matendo Yake Kama usingekuwa unyanyasaji wa Shetani, angewaumba binadamu na kuuongoza kuishi katika Bustani ya Edeni. Kwa nini Hakuwahi kufichua vitendo Vyake vyote kwa malaika au malaika mkuu kabla ya kusalitiwa na Shetani? Kama malaika na malaika mkuu wangalimjua Yeye, na pia kumtii Yeye pale mwanzoni, basi Asingewahi kutekeleza vile vitendo vya kazi visivyo na maana. Kwa sababu ya uwepo wa Shetani na mapepo, watu humpinga na wanajazwa hadi pomoni na tabia ya uasi, na hivyo basi Mungu angependa kufichua vitendo Vyake. Kwa sababu Angependa kupigana vita na Shetani, lazima Atumie mamlaka Yake kumshinda Shetani na kutumia vitendo Vyake vyote kumshinda Shetani; kwa njia hii, kazi Yake ya wokovu Anayotekeleza miongoni mwa binadamu itawafanya watu waone hekima na uwezo Wake. Kazi anayofanya Mungu leo ni yenye maana na haifanani kwa vyovyote vile na ile baadhi watu wanayoisema: “Je, kazi hii Unayofanya haihitilafiani? Je, huu mfuatano wa kazi si mazoezi ya kujitatiza Wewe tu? Ulimwumba Shetani, kisha baadaye ukamruhusu Akakusaliti na kukupinga Wewe. Uliwaumba binadamu, na kisha ukamkabidhi Shetani, na Ukaruhusu Adamu na Hawa kujaribiwa. Kwa sababu uliyafanya mambo haya yote kimakusudi, kwa nini Unawachukia binadamu? Kwa nini Unachukia Shetani? Mambo haya si ya kujitungia Wewe? Ni nini kipo cha Wewe kuchukia?” Watu wengi wa kipumbavu watasema hayo. Wanatamani kumpenda Mungu, lakini mioyoni mwao wanalalamika kumhusu Mungu—ukinzani jinsi gani! Wewe huelewi ukweli, unazo fikira nyingi sana za kimiujiza, na pia unadai kwamba hili ni kosa la Mungu—wewe ni mpumbavu kiasi kipi! Ni wewe unayecheza na ukweli; si kosa la Mungu! Baadhi ya watu wataweza hata kulalamika na kulalamika: Ni wewe uliyemwumba Shetani, na ni Wewe uliyempa Shetani binadamu. Binadamu wanamiliki tabia ya kishetani; badala ya kuwasamehe, Unauchukia kwa kiwango fulani. Mwanzo Uliupenda binadamu kwa kiwango fulani. Ulimtimua Shetani hadi ulimwenguni mwa binadamu, na sasa Unawachukia binadamu. Ni wewe unayewachukia na kuwapenda binadamu—maelezo ya kauli hii ni yapi? Je, huu si ukinzani? Bila kujali ni vipi mnavyoangalia suala hili, hivi ndivyo ilivyofanyika mbinguni; malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa njia hii, nao binadamu wakapotoshwa kwa njia hii, na ukaendelea mpaka leo kwa njia hii. Bila kujali ni vipi mnavyopangilia kauli hizi, hii ndiyo hadithi yote. Hata hivyo, lazima muelewe kwamba Mungu anaifanya kazi ya leo ili kuwaokoa nyinyi, na ili kumshinda Shetani.

Kwa sababu malaika hasa alikuwa mnyonge na hakumiliki uwezo wowote, alikuwa mwenye kiburi wakati alipewa mamlaka, hasa malaika mkuu, ambaye hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi kuliko ile ya wale malaika wengine. Malaika mkuu alikuwa ndiye mfalme wa malaika wote. Aliwaongoza mamilioni ya malaika, na kwa usimamizi wa Yehova mamlaka yake yalizidi yale ya malaika yeyote mwingine. Alitaka kufanya hivi na vile, na kuwaongoza malaika hadi ulimwenguni mwa binadamu ili kuutawala ulimwengu. Mungu alisema kwamba Yeye huutawala ulimwengu; malaika mkuu akasema kwamba ulimwengu ulikuwa wake wa kutawala, na kuanzia hapo akamsaliti Mungu. Mbinguni, Mungu alikuwa ameuumba ulimwengu mwingine. Malaika mkuu akataka kuutawala ulimwengu huu na pia kushuka chini kwenye himaya ya binadamu. Je, Mungu angemruhusu kufanya hivi? Hivyo basi, Alimtimua hadi chini na akawa angani. Tangu hapo alipowapotosha binadamu, Mungu amefanya vita dhidi yake ili kuwaokoa binadamu; Ametumia milenia hizi sita kumshinda. Dhana yenu ya Mwenyezi Mungu hailingani na kazi ambayo Mungu anatekeleza sasa; haifanyi kazi katika kutenda na ni ya upumbavu ajabu! Kwa hakika, Mungu alitangaza malaika mkuu kuwa adui Yake baada tu ya malaika mkuu kumsaliti Yeye. Ilikuwa kutokana tu na kusaliti kwake Mungu ndiposa aliwadhalilisha binadamu baada ya kuwasili katika ulimwengu wa binadamu, na ilikuwa kwa sababu hii ndiposa binadamu waliendelea hadi kiwango hiki. Kufuatia haya, Mungu alikula kiapo na Shetani: Nitakushinda wewe na kuwaokoa binadamu, uumbaji Wangu. Shetani hakushawishika wakati wa mwanzo na akasema, ni nini kwa hakika unachoweza kunifanyia mimi? Wewe unaweza kunifukuza hadi katika anga kweli? Wewe unaweza kwa kweli kunishinda mimi? Baada ya Mungu kumtimua hadi angani, Hakumtilia maanani tena na kisha Alianza kuwaokoa binadamu na kufanya kazi Yake mwenyewe, licha ya unyanyasaji ulioendelea kutoka kwa Shetani. Kila kitu ambacho Shetani angeweza kufanya kilitokana na nguvu alizopewa na Mungu; alichukua vitu hivi pamoja naye hadi angani na amevihifadhi vitu hivi hadi leo. Mungu alimtimua hadi angani lakini hakuchukua mamlaka yake, na hivyo basi aliendelea kuwapotosha binadamu. Mungu, kwa mkono mwingine, Alianza kuwaokoa binadamu, ambao Shetani alikuwa amepotosha baada ya kuumbwa kwao. Mungu hakufichua vitendo Vyake wakati akiwa mbinguni; hata hivyo, kabla ya kuiumba dunia, Aliwaruhusu watu katika ulimwengu Aliouumba mbinguni kuona vitendo Vyake na hivyo kuwaongoza watu juu mbinguni. Aliwapa hekima na busara, na kuwaongoza watu hao kuishi kwenye ulimwengu huo. Kiasili, hakuna kati yenu ambaye amewahi kusikia haya awali. Baadaye, baada ya Mungu kuumba binadamu, malaika mkuu alianza kuwapotosha binadamu; duniani, binadamu wote walikuwa katika fujo. Ulikuwa ni wakati huu tu ambapo Alianza vita Vyake dhidi ya Shetani, na ulikuwa ni katika wakati huu tu ambapo watu waliona vitendo Vyake. Mwanzo vitendo Vyake vilifichwa kutoka kwa binadamu. Baada ya Shetani kutimuliwa hadi angani, alijishughulisha na masuala yake, naye Mungu akajishughulisha Mwenyewe na kazi Yake binafsi, mara kwa mara Akifanya vita dhidi ya Shetani, kila wakati mpaka siku za mwisho. Sasa ndio wakati ambao Shetani anafaa kuangamizwa. Mwanzoni Mungu alimpa mamlaka, na baadaye Mungu alimtimua hadi angani, lakini Shetani alibaki mwasi. Baadaye, alipofika nchini, aliwapotosha binadamu, lakini Mungu alikuwa kwa hakika ulimwenguni akiwasimamia binadamu. Mungu hutumia usimamizi Wake wa watu kumshinda Shetani. Kwa kuwapotosha watu, Shetani huleta hutamatisha hatima ya watu na kuinyanyasa kazi ya Mungu. Kwa upande mwingine, kazi ya Mungu ndiyo wokovu wa binadamu. Ni hatua gani ya kazi yenyewe ya Mungu ambayo hainuii kuwaokoa binadamu? Ni hatua gani hainuii kutakasa watu, ili kuwafanya kuwa wenye haki na kuwafanya kuishi kwa njia ambayo huunda taswira inayoweza kupendwa? Shetani, hata hivyo, hafanyi hivi. Yeye huwapotosha binadamu; siku zote anatekeleza kazi zake za kuwapotosha binadamu kote ulimwenguni. Bila shaka, Mungu pia hufanya kazi Yake. Hamtilii maanani Shetani. Haijalishi ni mamlaka kiasi kipi Shetani anayo, mamlaka yake bado yalitoka kwa Mungu; Mungu kwa hakika hakumpa mamlaka Yake yote tu, na hivyo basi haijalishi ni nini afanyacho Shetani, hawezi kuzidi Mungu na siku zote huwa kwenye udhibiti wa Mungu. Mungu hakufichua vitendo Vyake vyovyote akiwa mbinguni. Alimpa Shetani kiwango kidogo tu cha mamlaka ili kumruhusu kutekeleza udhibiti wake dhidi ya malaika. Hivyo basi, haijalishi ni nini hufanya, hawezi kuzidi mamlaka ya Mungu kwa sababu mamlaka ambayo Mungu alimpa awali ni finyu. Huku Mungu akifanya kazi, Shetani hunyanyasa. Katika siku za mwisho, atamaliza unyanyasaji wake; vilevile, kazi ya Mungu itakamilika, na aina ya mtu ambaye Mungu angependa kumkamilisha atakuwa amekamilika. Mungu huwaelekeza watu kwa njia nzuri; maisha Yake ni maji yenye uzima, yasiyopimika na yasiyo na mipaka. Shetani amepotosha binadamu hadi kiwango fulani; hatimaye, yale maji hai ya uzima yatamkamilisha binadamu, na haitawezekana kwa Shetani kuingilia kati na kutekeleza kazi yake. Hivyo basi, Mungu ataweza kuwapata kabisa watu wake. Shetani angali anakataa kukubali haya sasa; siku zote hupambana na Mungu, lakini Mungu hamtilii maanani. Amesema, Nitakuwa mshindi dhidi ya nguvu zote za giza za Shetani na dhidi ya ushawishi wote wa giza. Hii ndiyo kazi ambayo lazima ifanywe kwa mwili, na ndiyo pia maana ya kupata mwili kwa Yesu Kristo. Ni kukamilisha awamu ya kazi ya kumshinda Shetani katika siku za mwisho, kuondoa vitu vyote vinavyomilikiwa na Shetani. Ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani ni mtindo usioepukika! Shetani kwa hakika alishindwa kitambo sana. Wakati injili ilipoanza kuenezwa kote nchini mwa joka kubwa jekundu, yaani, wakati Mungu mwenye mwili alipoanza kufanya kazi na kazi hii ikafanywa kuendelea, Shetani aliweza kushindwa kabisa, kwani kupata mwili wa Kristo kulimaanisha kumshinda Shetani. Shetani aliona kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na alikuwa ameanza kutekeleza kazi Yake, na akaona kwamba hakuna nguvu ambazo zingeweza kukomesha kazi hii. Hivyo basi, alipigwa na bumbuazi alipoona kazi hii na hakuthubutu kufanya kazi yoyote nyingine zaidi. Kwanza Shetani alifikiria kwamba pia alimiliki hekima nyingi, na akaingilia kati na kunyanyasa kazi ya Mungu; hata hivyo, hakutarajia kwamba Mungu alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili, na kwamba katika kazi Yake, Mungu alikuwa ametumia uasi Wake kuhudumu kama ufunuo na hukumu kwa binadamu; na hivyo basi kushinda binadamu na kumshinda Shetani. Mungu ni mwerevu kumshinda, na kazi Yake inamzidi Shetani. Hivyo basi, Niliwahi kutaja awali kwamba: Kazi Ninayoifanya inatekelezwa kutokana na ujanja wa Shetani. Mwishowe Nitafichua uweza Wangu na hali ya kutoweza kwa Shetani. Wakati Mungu anapofanya kazi Yake, Shetani anamfuata unyo kwa unyo kutoka nyuma mpaka mwishowe anaangamizwa—hatajua hata kilichomgonga! Ataweza kutambua tu ukweli baada ya kuvunjwa na kupondwapondwa; na wakati huo atakuwa tayari amechomwa kwenye ziwa la moto. Hatakuwa ameshawishika kabisa wakati huo? Kwani hatakuwa na njama zozote zingine za kutumia!

Ni kazi hii ya kihalisi ya hatua kwa hatua ambayo mara nyingi inalemea moyo wa Mungu kwa huzuni ya binadamu, ili vita Vyake na Shetani vimedumu kwa sasa miaka 6,000. Hivyo basi Mungu alisema hivi: Sitawahi tena kuumba binadamu, wala kuwahi tena kuwapa malaika mamlaka. Kuanzia hapo, wakati malaika walipokuja kazini duniani, walimfuata tu Mungu ili kufanya kazi fulani. Hakuwahi kuwapatia malaika mamlaka. Je, malaika ambao Waisraeli waliwaona walitekeleza vipi kazi yao? Walijifichua katika ndoto na kupitisha maneno ya Yehova. Wakati Yesu alipofufuka siku tatu baada ya kusulubishwa, ni malaika ndio waliolisukuma jiwe kando; Roho wa Mungu hakufanya kazi hii yeye binafsi. Malaika waliweza kufanya tu kazi ya aina hii; waliweza kuwa na wajibu wa usaidizi na hawakuwa na mamlaka, kwani Mungu hatawahi tena kuwapatia mamlaka. Baada ya kufanya kazi kwa muda fulani, watu ambao Mungu alitumia hapa duniani walichukua nafasi ya Mungu na kusema, Nataka kuzidi ulimwengu! Nataka kusimama kwenye mbingu ya tatu! Tunataka hatamu za nguvu ya ukuu! Wangekuwa na kiburi baada ya siku kadhaa za kazi; walitaka nguvu ya ukuu duniani, walitaka kuanzisha taifa jingine, walitaka vitu vyote katika utawala wao na walitaka kusimama katika mbingu ya tatu. Je, kwani hujui kwamba wewe ni binadamu tu unayetumiwa na Mungu? Unawezaje kupaa hadi kwenye mbingu ya tatu? Mungu huja duniani kufanya kazi, kimyakimya na bila ya kujitangaza, na Huondoka kimyakimya baada ya kukamilisha kazi Yake. Hajitangazi kama vile binadamu wanavyofanya, lakini badala yake Anatekeleza kwa kiuhalisia kazi Yake. Wala haingii kanisani na kujitangaza, Nitawamaliza nyinyi nyote! Nitawalaani na kuwaadibu! Anatekeleza tu kazi Yake binafsi, na kuondoka mara Anapomaliza. Wale wachungaji wa kidini wanaowaponya wagonjwa na kupunga mapepo, wanawasomea wengine kutoka kwenye madhabahu, na kutoa hotuba ndefu na zenye makuu na kuzungumzia masuala yasiyo ya kihalisi, wana kiburi hadi moyoni! Wao ni vizazi vya malaika mkuu!

Baada ya kutekeleza kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, kimsingi kumshinda Shetani na kuwaokoa binadamu wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Huchukua fursa ya kumshinda Shetani ili kufichua vitendo Vyake kwa binadamu na kuwaruhusu watu kuweza kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu nchini, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya wokovu Wake kwa binadamu. Uumbaji wote wa Mungu humletea utukufu, humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio lake si kumshinda Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia kushindwa kwa Shetani kuwaokoa binadamu; Anakutumia kushindwa kwa Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote. Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza pia kushuhudia utukufu Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio nchini na uumbaji wote ulio nchini utauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo. Viumbe vyake kule mbinguni na nchini wote utauona utukufu Wake, na atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na kuruhusu binadamu kumsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi vipengele hivi viwili. Mwishowe binadamu wote watashindwa na Yeye, na atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa wale wote wanaomilikiwa na Shetani. Unaviona vitendo hivi vyote vya Mungu sasa, ilhali ungali unapinga na unakuwa mwasi na hutaki kunyenyekea; unayahifadhi mambo mengi ndani yako na unafanya utakacho; unafuata ashiki zako, na kile upendacho—huu ni uasi; huu ni upingaji. Kusadiki Mungu ambako kunatekelezwa kwa ajili ya mwili, kwa ajili ya ashiki za mtu, na kwa ajili ya kile anachopenda mtu, kwa ajili ya ulimwengu, na kwa ajili ya Shetani ni kuchafu; ni upinzani na uasi. Kunazo aina zote tofauti za kusadiki sasa: Baadhi hutafuta hifadhi dhidi ya janga, na wengine hutafuta kupokea baraka, huku baadhi wakitamani kuelewa mafumbo na bado wengine hujaribu kupata pesa. Hiyo yote ni mifumo ya upinzani; hiyo yote ni kukufuru! Kusema kwamba mtu anapinga au anaasi—huku si kwa mujibu wa mambo haya? Watu wengi sasa hivi wanalalamika, wanatamka manung’uniko au kutoa hukumu. Mambo haya yote yanafanywa na waovu; wao ni binadamu wapinzani na waasi; watu kama hao wamemilikiwa na kujawa na Shetani. Watu ambao Mungu huwapata ni wale wanaonyenyekea Kwake kabisa, wale waliopotoshwa na Shetani lakini kuokolewa na kushindwa na kazi Yake sasa, wale waliovumilia majaribu na hatimaye wamepokelewa kabisa na Mungu na hawaishi tena katika utawala wa Shetani na wamevunja minyororo ya udhalimu, walio radhi kuishi kwa kudhihirisha utakatifu—hawa ndio watu watakatifu zaidi; hawa ndio wale watakatifu. Kama matendo yako ya sasa hayalingani na sehemu moja ya mahitaji ya Mungu utaondolewa. Hii haipingiki. Kila kitu kinafanywa kulingana na leo; ingawa Amekuamulia awali na kukuchagua wewe, hatua zako leo bado zitaamua matokeo yako. Kama huwezi kuendelea kwa mwendo sawa sasa, utaondolewa. Kama huwezi kuendelea kwa mwendo sawa sasa, hata unawezaje kutumaini[a] kuendelea kwa mwendo sawa baadaye? Vile sasa muujiza mkubwa kama huo umekufanyikia wewe, bado huamini. Hebu Niambie, utamwamini vipi baadaye wakati Atakapomaliza kazi Yake na Hafanyi tena kazi kama hiyo? Wakati huo itakuwa vigumu zaidi kwako wewe kumfuata Yeye! Baadaye Mungu atategemea mwelekeo na maarifa yako katika kazi ya Mungu kuwa mwili na kile ulichopitia wewe ili kuamua kama wewe ni mwenye dhambi au mwenye haki, au kuamua kama wewe ndiwe uliyefanywa kuwa mtimilifu ama wewe ni yule aliyeondolewa. Lazima uweze kuona wazi sasa. Roho Mtakatifu hufanya kazi hivyo: Yeye huamua matokeo yako kulingana na tabia yako leo. Nani huongea maneno ya leo? Nani hufanya kazi ya leo? Nani huamua kama utaondolewa leo? Nani huamua kukufanya kuwa mtimilifu? Hivi sivyo Ninavyofanya Mimi mwenyewe? Mimi Ndimi ninayeongea maneno haya; Mimi Ndimi ninayetekeleza kazi hii. Kulaani, kuadibu na kuhukumu watu vyote ni sehemu ya kazi Yangu mimi binafsi. Hatimaye, kukuondoa kutakuwa pia kazi Yangu binafsi. Yote ni kazi Yangu binafsi! Kukufanya kuwa mtimilifu ni shughuli Yangu binafsi, na kukuruhusu kufurahia baraka ni shughuli Yangu binafsi pia. Hii yote ni kazi Yangu binafsi. Matokeo yako hayakuamuliwa awali na Yehova; yanaamuliwa leo na Mungu wa leo. Yanaamuliwa sasa; hayakuamuliwa kabla ya ulimwengu kuumbwa. Baadhi ya watu wapumbavu husema, Pengine kuna jambo mbaya na macho Yako, na Hunioni mimi kama vile Unavyofaa kuniona. Hatimaye mtaona namna Roho atakavyoonyesha kila kitu! Yesu kwanza Alimchagua Yuda kama mwanafunzi Wake. Watu hufikiria kwamba Yesu alikuwa amefanya kosa kwa kumchagua yeye. Angewezaje kumchagua mwanafunzi ambaye angemsaliti? Mwanzo Yuda hakuwa na nia ya kumsaliti Yesu. Hili jambo lilifanyika tu baadaye. Wakati huo Yesu alikuwa amemchukua Yuda kwa upendo; Alimfanya mwanamume huyo kumfuata Yeye na kumfanya kuwajibikia masuala yao ya kifedha. Kama Angejua kwamba Yuda angebadhiri pesa, Asingemwacha kusimamia pesa hizo. Mtu anaweza kusema kwamba Yesu hakujua mwanzo kwamba mwanamume huyu alikuwa asiye mwaminifu na mdanganyifu, na kwamba aliwadanganya ndugu zake. Baadaye Yuda alipokwisha kumfuata kwa muda fulani, Yesu alimwona akiwadanganya ndugu zake na akidanganya Mungu. Watu waligundua pia kwamba siku zote angetumia pesa kutoka kwenye mfuko wa fedha na kisha wakamwambia Yesu. Yesu alipata habari tu kuhusu haya yote wakati huu. Kwa sababu Yesu alikuwa atekeleze kazi ya kusulubishwa na Alihitaji mtu wa kumsaliti Yeye, na Yuda alitokea tu kuwa mhusika mzuri wa wajibu huu, Yesu akasema, kutakuwepo miongoni mwenu ambaye atanisaliti Mimi. Mwana wa adamu atatumia usaliti huu kuweza kusulubishwa na baada ya siku tatu atafufuka. Wakati huo Yesu hakuchagua hasa Yuda ili aweze kumsaliti Yeye; kinyume cha mambo ni kwamba, Alipenda kwamba Yuda awe mwanafunzi mtiifu. Kwa mshangao Wake, Yuda aligeuka kuwa mlafi na mwenye sifa mbaya aliyemsaliti Bwana, na akatumia hali hii kumchagua Yuda kwa kazi hii. Kama wanafunzi wote kumi na wawili wa Yesu wangekuwa watiifu, na hakuna mtu kama Yuda angekuwa miongoni mwao, yule mtu wa kumsaliti Yesu angekuwa hatimaye mtu kutoka nje ya wale wanafunzi. Hata hivyo, wakati huo ilifanyika tu kwamba kulikuwa na mmoja miongoni mwao aliyefurahia kuchukua hongo—Yuda. Yesu kwa hivyo basi alimtumia mwanamume huyu kukamilisha kazi Yake. Jambo hili liweje rahisi hivyo! Yesu hakuliamua awali mwanzoni mwa kazi Yake; alifanya tu uamuzi huu punde tu mambo yalipoimarika hadi hatua fulani. Huu ulikuwa ni uamuzi wa Yesu, yaani, uamuzi wa Roho wa Mungu Mwenyewe. Wakati huo ni Yesu aliyemchagua Yuda; wakati Yuda alipomsaliti Yesu baadaye, haya yalikuwa ni matendo ya Roho Mtakatifu ili kuhudumu hatima Zake mwenyewe; ilikuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo. Wakati Yesu alipomchagua Yuda, Hakuwa na wazo lolote kwamba Angemsaliti. Alijua tu kwamba alikuwa Yuda Iskariote. Matokeo yenu yanaamuliwa pia kulingana na kiwango chenu cha kunyenyekea leo na kulingana na kiwango chenu cha ukuzi wa maisha, na wala si kulingana na wazo miongoni mwa dhana za binadamu kwamba ilikuwa imepangiwa awali katika uumbaji wa ulimwengu. Lazima uelewe mambo haya waziwazi. Kazi hii nzima haitekelezwi kulingana na kufikiria kwako.

Tanbihi:

a. Maandishi asilia yameacha “hata unawezaje kutumaini.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp