Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 142
Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Tayari Nimeshasema kuwa wale wanaonifuata ni wengi lakini wanaonipenda kwa moyo wa kweli ni wachache. Huenda ikawa wengine wanasema, “Ningeweza kujinyima mengi kiasi hicho ikiwa sikupendi Wewe? Ningeendelea bado kukufuata ikiwa sikupendi?” Unazo sababu nyingi kwa hakika. Kwa hakika, upendo wako ni mkubwa, lakini nini umuhimu wa mapenzi yako Kwangu? “Upendo,” kama unavyoitwa, unaashiria hisia safi isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi, na kuwa na mawazo. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi na hakuna kutenga. Katika upendo hakuna shaka, hakuna uongo na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna kukaa mbali na hakuna kitu kisicho safi. Ukipenda, basi hudanganyi, hulalamiki, huasi na hupeani au kuchukua rushwa. Ukipenda, basi unajinyima bila kusononeka, unavumilia hali ngumu, na unaambatana na Mimi. Ungeacha vitu vyako vyote kwa sababu Yangu: familia yako, siku zako za baadaye, ujana wako, na ndoa yako. La sivyo, basi upendo wako si upendo hata kidogo, bali ni uongo na usaliti! Upendo wako ni upendo wa aina gani? Je, ni upendo wa kweli? Je, ni wa uongo? Umejinyima kiasi gani? Umejitolea kiasi gani? Je, Nimepata upendo kiasi gani kutoka kwako? Je, unajua? Moyo wenu umejaa maovu, usaliti na uongo. Kwa hivyo kiwango kipi cha upendo wenu ni kichafu? Mnaamini kuwa mmewacha kila kitu kwa ajili Yangu; Mnaamini kuwa upendo wenu Kwangu tayari umetosha, ila ni kwa nini maneno yenu na matendo yenu huambatana na uasi na uongo? Mnanifuata, ilhali hamkubali neno Langu. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, kisha mnanitenga na kuniweka kando. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali mko na shaka na Mimi. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, ilhali hamkubali kuwepo Kwangu. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali hamnitendei vile Ninavyopaswa kutendewa na mnafanya mambo yawe magumu Kwangu katika kila hatua. Je, hii inachukuliwa kama mapenzi? Mnanifuata, ilhali mnanichukua kama mjinga na kunidanganya Mimi katika kila jambo. Je, haya ni mapenzi? Mnanihudumia, ilhali hamnichi. Je, huu ni upendo? Mnanipinga katika kila hali na kila jambo. Je, yote haya yanachukuliwa kama upendo? Mmejinyima mengi, huu ni ukweli, ilhali hamjawahi kuyafanya Ninayowaagiza mfanye. Je, huu unaweza kuwa upendo? Uchunguzi wa makini unaashiria kuwa hamna upendo Kwangu ndani yenu. Baada ya miaka hii mingi ya kazi na maneno mengi Niliyosambaza, ni kiasi kipi mlichopokea kwa hakika? Je, hii haistahili mtazamo mwangalifu wa nyuma? Ninawaonya: Wale Niwaitao sio wale ambao hawajapotoshwa, bali wale Ninaowachagua ni wale wanaonipenda kwa ukweli. Kwa hivyo, mnapaswa kuwa makini na maneno na matendo yenu, na muichunguze azma na mawazo yenu ili vitu hivi visije vikavuka mipaka. Wakati wa mwisho, fanyeni jitihada ili muonyeshe mapenzi yenu Kwangu, isije ghadhabu yangu ikabaki kwenu milele!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika...
Maisha ya kiroho ni maisha ya aina gani? Maisha ya kiroho ni yale ambayo kwayo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na unaweza kuwa...
Kwa hakika, tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haijafichika, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi...
Leo, nani kati yenu anathubutu kusema kwamba maneno yote yaliyotamkwa na wale waliotumiwa na Roho Mtakatifu yalitoka kwa Roho Mtakatifu?...