Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 350

Mimi Nitamshinda mwanadamu kwa sababu waliumbwa na Mimi wakati mmoja na pia, kilicho cha ziada, walifurahia vitu vyote karimu vya uumbaji Wangu. Hata hivyo, wamenikataa Mimi, na nyoyo zao haziko na Mimi ndani yao, na wao huniona kama mzigo maishani mwao, hadi kwa kiwango ambacho, wakiwa kwa kweli wameniona, watu bado wananikataa, na wanawaza kila njia inayoweza kuwawezesha kunishinda Mimi. Watu huwa hawaniruhusu Mimi kuwachukulia kwa umakini au kuweka madai kali juu yao, wala kukubali hukumu au kuadibu Kwangu wa udhalimu wao. Hawaoni kuchukuliwa kwa namna hiyo kuwa ya kuvutia, lakini badala yake, wanaona ni kama kero kwao. Hivyo Kazi Yangu ni kushinda mwanadamu ambaye anakula, anakunywa kwa ajili Yangu na kusherehekea Kwangu, lakini hanijui. Nitawapokonya zana wanadamu, na kisha, Nitarejea kwenye makao Yangu pamoja na malaika Wangu na utukufu Wangu. Kwa kuwa tabia ya watu imenivunja moyo kabisa na kuitawanya kazi Yangu kwa vipande muda mrefu uliopita. Nataka kuumiliki tena utukufu uliokuwa umeibwa na yule mwovu kabla ya kuondoka kwa furaha, na kuwaacha wanadamu waendelee na maisha yao, waendelee na “maisha na kazi yao kwa amani,” waendelee “kulima mashamba yao,” wawe huru kutokana na kuingilia kati Kwangu katika maisha yao. Lakini Mimi sasa kwa ukamilifu Nitaumiliki tena utukufu Wangu kutoka kwa mkono wa yule mwovu, niurejeshe ukamilifu wa utukufu Niliouumba ndani ya mwanadamu wakati wa kuumbwa kwa dunia, na kamwe tena sitauweka juu ya mwanadamu wa dunia. Kwa kuwa binadamu hawajashindwa tu kuuhifadhi utukufu Wangu, bali pia wao wameugeuza kuwa mfano wa Shetani. Watu hawathamini kuwasili Kwangu, wala hawangetuza siku za utukufu Wangu. Wao hawasherehekei kukubali kwa kuadibu Kwangu, wala kuwa tayari kuurejesha utukufu Wangu Kwangu. Wala hawako tayari kutupa mbali sumu ya yule mwovu. Wanadamu bado wananidanganya kwa njia ile ile ya zamani, na wao bado huvaa tabasamu za kung’aa na nyuso zenye furaha kwa njia ile ile ya zamani. Wao hawajui kina cha huzuni ambao wanadamu watakabiliwa nao baada ya utukufu Wangu kuondoka miongoni mwao, na hasa hawajui kwamba siku Yangu itakapokuja kwa wanadamu wote, watakuwa na wakati mgumu zaidi kuliko watu katika nyakati za Nuhu. Kwa maana wao hawajui kuwa wakati utukufu Wangu ulitoweka kutoka Israeli kulikuwa na huzuni nyingi, kwa kuwa mwanadamu husahau kunapokucha jinsi ilivyokuwa vigumu kupita katika giza la usiku wa manane. Jua linaporejea mafichoni tena na giza kumshukia mwanadamu, ataanza tena kuomboleza na kusaga meno yake gizani. Je, umesahau kwamba wakati utukufu Wangu ulipotoweka kutoka Israeli, ilivyokuwa vigumu kwa watu wake kupitia mateso hayo? Huu ndio wakati ambao utaweza kuuona utukufu Wangu, na pia ndio wakati ambapo utashiriki siku ya utukufu Wangu. Mwanadamu ataomboleza katika giza wakati utukufu Wangu unaondoka kutoka katika nchi chafu. Sasa ndio siku ya utukufu Ninapofanya kazi Yangu, na pia ndio siku ambapo Namwondoa mwanadamu kutoka kwa mateso, kwa kuwa sitapita katika nyakati za uchungu na ugumu nao. Mimi Nataka tu ushindi kamili juu ya wanadamu na kumshinda kikamilifu yule mwovu wa wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp