Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 338

Tafakarini kuhusu siku za nyuma: Ni lini macho Yangu yamekuwa na hasira, na sauti Yangu kuwa kali, kwenu? Ni wakati upi Nimegombana nanyi? Ni wakati upi Nimewakaripia bila mantiki? Ni wakati upi Nimewakemea usoni mwenu? Je, si ni kwa ajili ya kazi Yangu ndio kwamba Mimi namwomba Baba Yangu kuwaweka mbali na majaribu? Kwa nini mnanitendea Mimi hivi? Je, Nimewahi kutumia mamlaka Yangu kuipiga miili yenu? Kwa nini mnanilipa Mimi kwa njia hii? Baada ya ninyi kuwa moto na baridi Kwangu, nyinyi si moto wala baridi, na kisha mu wadanganyifu Kwangu na kuficha mambo kutoka Kwangu, na vinywa vyenu vimejaa mate ya wasio haki. Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kumdanganya Roho Wangu? Je, mnafikiri kwamba ndimi zenu zinaweza kuepuka ghadhabu Yangu? Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kupitisha hukumu kwa matendo Yangu, Yehova, jinsi zinavyopenda? Je, Mimi ni Mungu ambaye mwanadamu hupishia hukumu? Ningewezaje kuruhusu buu dogo linikufuru hivyo? Ningewezaje kudai wana wa uasi kuwa miongoni mwa baraka Zangu za milele? Maneno na matendo yenu kwa muda mrefu yamewafichua na kuwahukumu. Wakati Nilieneza mbingu na kuumba vitu vyote, Sikuruhusu kiumbe yeyote kushiriki atakavyo, sembuse kuruhusu jambo lolote kuvuruga kazi Yangu na usimamizi Wangu, vile linavyopenda. Sikuvumilia mtu au kitu chochote; Ningewezaje kuwaacha walio wakatili na wa kinyama Kwangu? Ningewezaje kuwasamehe wale ambao wanaasi dhidi ya maneno Yangu? Ningewezaje kuwaacha wanaoniasi? Je, majaliwa ya mwanadamu hayako katika mikono Yangu, Mwenyezi? Ningeuchukua vipi udhalimu wako na uasi kama vitu vitakatifu? Jinsi gani dhambi zako zingenajisi utakatifu Wangu? Mimi sijanajisika na uchafu wa wasio haki, wala kufurahia sadaka ya wasio haki. Kama ungekuwa mwaminifu Kwangu, Yehova, je, ungeweza kujichukulia sadaka kutoka katika madhabahu Yangu? Je, ungeweza kutumia ulimi wako wa sumu kukufuru jina Langu takatifu? Ungeweza kuliasi neno Langu kwa njia hii? Je, ungeweza kuuchukua utukufu Wangu na jina langu takatifu kama chombo ambacho kwalo unamtumikia Shetani, yule mwovu? Maisha Yangu yametolewa kwa ajili ya furaha ya watakatifu. Ningewezaje kukuruhusu ucheze na maisha Yangu jinsi utakavyo, na kuyatumia kama chombo kwa ajili ya migogoro kati yenu? Mngewezaje kuwa wakatili sana, na watovu sana katika njia ya wenye wema, katika jinsi mlivyo Kwangu? Je, hamjui kwamba tayari Nimeandika matendo yenu maovu katika neno hili la maisha? Jinsi gani mngeweza kuepuka siku ya ghadhabu Ninapoadibu Misri? Ningewezaje kupingwa na kukaidiwa kwa njia hii na nyinyi, mara kwa mara? Nawaambia wazi, siku itakapokuja, basi kuadibu kwenu kutakuwa kusikovumilika zaidi kuliko ile ya Misri! Mnawezaje kuitoroka siku ya ghadhabu Yangu? Nawaambia kwa kweli: Uvumilivu Wangu ulitayarishwa kwa ajili ya matendo yenu maovu, na upo kwa ajili ya kuadibu kwenu siku hiyo. Je, ninyi si wale mtakaopata hukumu ya ghadhabu Yangu punde Nifikapo mwisho wa uvumilivu Wangu? Si mambo yote yapo mikononi Mwangu, Mwenyezi? Ningewezaje kuwaruhusu mniasi hivyo, chini ya mbingu? Maisha yenu yatakuwa magumu sana kwa kuwa mmekutana na Masiha, ambaye ilisemekana Angekuja, lakini ambaye kamwe Hakuja. Je, si nyinyi ni maadui Wake? Yesu amekuwa rafiki wenu, lakini bado mu maadui wa Masiha. Je, hamjui kwamba ingawa nyinyi ni marafiki wa Yesu, matendo yenu maovu yamejaza vyombo vya wale ambao ni wa karaha? Ingawa nyinyi mu karibu sana na Yehova, je, hamjui kwamba maneno yenu mabaya yamefikia masikio ya Yehova na kuchochea ghadhabu Yake? Ingekuwaje awe karibu nawe, na jinsi gani Yeye asingevichoma hivyo vyombo vyako, ambavyo vimejaa matendo mabaya? Ingekuwaje Asiwe adui wako?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp