Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 333

Kama sasa Ningeweka utajiri mbele yenu na kuwaambia kuwa mchague kwa uhuru, huku Nikijua kwamba sitawahukumu, basi wengi wangechagua utajiri na kuacha ukweli. Wazuri miongoni mwenu wangeacha utajiri na kuchagua ukweli shingo upande, ilhali wale ambao wako katikati wangekumbatia utajiri kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine kuukumbatia ukweli. Kwa njia hii, je, rangi zenu halisi si zingejidhihirisha? Unapochagua ukweli kwa kulinganisha na kitu chochote ambacho u mwaminifu kwacho, wote mtafanya maamuzi kama hayo, na tabia yenu itabakia kuwa ile ile. Si ndivyo ilivyo? Je, hakuna watu wengi miongoni mwenu waliobadilika badilika katika kuchagua baina ya wema na ubaya? Katika mashindano kati ya mazuri na mabaya, nyeusi na nyeupe, mna uhakika na uchaguzi mlioufanya kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, amani na vurugu, utajiri na umasikini, hadhi na kuwa mtu wa kawaida, kusaidiwa na kutupiliwa mbali, na kadhalika. Kati ya familia yenye amani na familia iliyovunjika, nyinyi huchagua ya kwanza bila kusita; kati ya utajiri na wajibu, safari hii pia mnachagua ya kwanza, bila kuwa na nia ya kurudi ufuoni kati ya starehe na umasikini, tena mlichagua ya kwanza; kati ya watoto, mke, mume na Mimi, mnachagua za kwanza; na kati ya dhana na ukweli, kwa mara nyingine tena mlichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, karibu sana Nimepoteza imani Yangu kwenu. Ninashangazwa sana na kwamba mioyo yenu inapinga kulainishwa. Miaka mingi ya kujitolea na jitihada Yangu imeniletea kuvunjika moyo tu nanyi kupoteza imani Nami. Hata hivyo, matumaini Yangu juu yenu yanakua kila siku inayopita, kwa kuwa siku Yangu tayari imekwisha kuwekwa wazi kwa kila mtu. Lakini, bado mnaendelea kuyafuata yale ambayo ni ya giza na maovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu. Kwa kufanya hivyo, mtapata matokeo gani? Mmewahi kutafakari kwa makini kuhusu hili? Kama mngetakiwa kuchagua tena, msimamo wenu ungekuwa upi? Bado lingekuwa ni chaguo la kwanza? Je, yale ambayo mngenipatia bado yangekuwa maudhi na huzuni ya majuto? Je, mioyo yenu bado ingekuwa migumu? Je bado mngekuwa hamjui cha kufanya ili kuufariji moyo Wangu? Kwa wakati wa sasa, chaguo lenu ni nini? Mtayakubali maneno Yangu, au yatawachosha? Siku Yangu imewekwa wazi kabisa mbele ya macho yenu, na kile mnachokiona ni maisha mapya na mwanzo mpya. Hata hivyo, ni lazima niwaambie kwamba huu mwanzo mpya si mwanzo wa kazi mpya iliyopita, bali ni mwisho wa ya kale. Yaani, hili ni tendo la mwisho. Ninaamini nyote mtaelewa kitu ambacho si cha kawaida kuhusu mwanzo huu mpya. Lakini siku moja hivi karibuni, mtaelewa maana halisi ya huu mwanzo mpya, kwa hivyo hebu sote tuipite na kuikaribisha tamati inayofuata! Hata hivyo, kitu ambacho Ninaendelea kutofurahishwa nacho ni kwamba pale mnapokabiliwa na mambo ambayo si ya haki na mambo ya haki, daima mmekuwa mkichagua chaguo la kwanza. Lakini hayo yote yako katika maisha yenu ya zamani. Pia Ninatumai kuyasahau yale yote yaliyotokea katika maisha yenu ya zamani, kitu kimoja baada ya kingine, ingawa hili ni gumu sana kufanya. Lakini bado nina njia nzuri sana ya kulitimiza. Aacha maisha ya baadaye yachukue nafasi ya maisha ya zamani na kuacha kivuli cha maisha yenu ya zamani kiondolewe badala ya utu wenu halisi wa leo. Hii ina maana kwamba nitawasumbua tena ili uweze kufanya maamuzi kwa mara nyingine tena na kuona uaminifu wenu uko kwa nani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp