Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 37
Mungu anafanya kazi Yake katika ulimwengu mzima. Wote wanaoamini katika Yeye lazima walikubali neno Lake, na kula na kunywa neno Lake;...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Mara nyingi watu husema kuwa wamemfanya Mungu kuwa maisha yao, lakini bado wangali kupitia hatua hii. Wanasema tu kuwa Mungu ndiye maisha yao, kuwa Anawaongoza kila siku, kuwa wanakula na kunywa maneno Yake kila siku, na kuwa wanamwomba kila siku, na hivyo Amekuwa ndiye maisha yao. Ufahamu wa wanaosema hili ni wa juu juu. Ndani ya watu wengi hakuna msingi; maneno ya Mungu yamepandwa ndani yao, lakini bado hayajaota, au hata kuzaa tunda lolote. Hadi leo, umepitia uzoefu wa kiwango gani? Ni saa hii, baada ya Mungu kukulazimisha kuja umbali huu, ndio unahisi kuwa huwezi kumuacha Mungu. Siku moja ukishakuwa na uzoefu hadi kiwango fulani, Mungu akitaka kukuacha, hutaweza kufanya hivyo. Daima utahisi kuwa huwezi kuishi bila Mungu ndani yako; waweza kuwa bila mume, mke, au watoto, bila familia, bila mama au baba, bila kufurahia kwa mwili, lakini huwezi kuishi bila Mungu. Kuwa bila Mungu itakuwa kama kupoteza uhai wako, hutaweza kuishi bila Mungu. Unapopitia hadi kiwango hiki, utakuwa umefanikisha imani yako kwa Mungu, na kwa njia hii Mungu atakuwa maisha yako, atakuwa msingi wa kuishi kwako, na hutaweza tena kumuacha Mungu. Unapokuwa umepitia hadi kiwango hiki, utakuwa umefurahia upendo wa Mungu kwelikweli, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa karibu mno, Mungu atakuwa maisha yako, upendo wako, na wakati huo utaomba kwa Mungu na kusema: Ee Mungu! Siwezi kukuacha, wewe ndiwe maisha yangu, naweza kuishi bila vitu vingine vyote—lakini bila Wewe siwezi kuendelea kuishi. Hiki ni kimo halisi cha watu; ni maisha halisi. Watu wengine wamelazimika kufika walipo siku ya leo: lazima waendelee wapende wasipende, na daima huhisi kuwa wako katika hali ngumu. Lazima ugundue kuwa Mungu yupo maishani mwako, kiasi kwamba kama Mungu angekuondoa kutoka katika upendo huo itakuwa kama umepoteza uhai wako; Mungu lazima awe maisha yako, na lazima uwe huwezi kumwacha. Kwa njia hii utakuwa umekutana na Mungu, na kwa wakati huu, unapompenda Mungu tena, utampenda Mungu kwa kweli, na utakuwa upendo wa kipekee, upendo safi. Siku moja matukio unayopitia yatakapokuwa kwamba maisha yako yamefikia kiwango fulani, utamwomba Mungu, utakula na kunywa maneno ya Mungu, na hutaweza kumwacha Mungu ndani, na hata kama ungetaka, hutaweza kumsahau. Mungu atakuwa maisha yako, waweza kuusahau ulimwengu, waweza kumsahau mkeo na watoto, lakini itakuwia vigumu kumsahau Mungu—hilo haliwezekani, haya ndiyo maisha yako halisi, na upendo wako wa ukweli kwa Mungu. Upendo wa watu kwa Mungu ufikiapo kiwango fulani, hakuna chochote wanachokipenda kinachoweza kulinganishwa na upendo wao kwa Mungu, Yeye ndiye mpenzi wao wa kwanza, na hivi ndivyo wanaweza kuacha vitu vingine vyote, na wawe tayari kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Unapopata pendo kutoka kwa Mungu ambalo linazidi mengine yote, utaishi katika uhalisi, na katika upendo wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Mungu anafanya kazi Yake katika ulimwengu mzima. Wote wanaoamini katika Yeye lazima walikubali neno Lake, na kula na kunywa neno Lake;...
Tafakarini kuhusu siku za nyuma: Ni lini macho Yangu yamekuwa na hasira, na sauti Yangu kuwa kali, kwenu? Ni wakati upi Nimegombana nanyi?...
Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni...
Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hufai Kufuata lile Wazo la Imani ya Kuabudu Miungu Wengi Ingawaje mbinu na uwezo wa Shetani ni...