Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 495

Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote. Ikiwa katika maisha yako yote hujawahi kumpenda au kumtosheleza Mungu, basi kuna haja gani ya kuishi? Kuna haja gani ya imani yako kwa Mungu? Huku si kuharibu nguvu? Hii ni kusema, kama watu wanataka kuamini na kumpenda Mungu, ni sharti wagharamike. Badala ya kujaribu kuenenda kwa namna fulani kwa nje tu, wanapaswa watafute utambuzi wa kweli kutoka ndani ya mioyo yao. Ikiwa unapenda sana kuimba na kucheza lakini huwezi kuonyesha ukweli katika vitendo, unaweza kusemekana kwamba unampenda Mungu? Kumpenda Mungu kunahitaji utafutaji wa mapenzi ya Mungu katika mambo yote, na kwamba ujisaili wewe mwenyewe kwa kina jambo lolote likikutokea, kujaribu kujua mapenzi ya Mungu na kujaribu kuona mapenzi ya Mungu ni yapi katika suala hili, Anataka ufanikishe nini, na ni jinsi gani utayajali mapenzi Yake? Kwa mfano: jambo fulani linafanyika linalokutaka uvumilie hali ngumu, wakati huo unapaswa ufahamu ni nini mapenzi ya Mungu, na ni jinsi gani unapaswa kuyajali mapenzi ya Mungu. Usijiridhishe mwenyewe: Jiweke kando kwanza. Hakuna kitu kilicho duni kuliko mwili. Ni lazima udhamirie kumridhisha Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako. Katika mawazo kama hayo, Mungu atakupa nuru ya kipekee katika jambo hili, na moyo wako pia utapata faraja. Jambo lolote likikutendekea, liwe dogo au kubwa, ni sharti kwanza ujiweke pembeni na kuuona mwili kama kitu duni zaidi kuliko vitu vyote. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo unavyochukua uhuru zaidi; ukiuridhisha mara hii, wakati mwingine utataka zaidi, na jinsi hili linaendelea, ndivyo unapata kuupenda mwili hata zaidi. Mwili mara zote una tamaa kupita kiasi, mara zote mwili unakutaka uuridhishe, na kwamba uutosheleze kwa ndani, iwe ni katika chakula unachokula, unachokivaa, au kuwa na hasira katika matendo yako, au kuushawishi udhaifu na uzembe wako… Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo tamaa yake inaongezeka, na jinsi mwili unavyopotoka zaidi, hadi kufikia kiwango ambacho miili ya watu inahodhi dhana nzito, na kutomtii Mungu, na kujiinua, na kuanza kuishuku kazi ya Mungu. Kadiri unavyouridhisha mwili zaidi, ndivyo udhaifu wa mwili unavyokuwa mkubwa; daima utahisi kuwa hakuna anayekuonea huruma kwa udhaifu wako, daima utaamini kuwa Mungu amezidi sana, na utasema: Mungu anawezaje kuwa mkali namna hii? Ni kwa nini Hawezi kuwapa watu nafasi? Watu wakiudekeza sana mwili, na kuupenda kupindukia, basi watajiponza wao wenyewe. Ikiwa unampenda Mungu kwa dhati, na huuridhishi mwili, basi utaona kuwa kila anachokifanya Mungu ni chenye haki sana, na kizuri sana, na kwamba laana Yake kwa uasi wako na hukumu ya udhalimu wako ni haki. Zitakuwepo nyakati ambapo Mungu atakurudi na kukufundisha nidhamu, na kuanzisha mazingira ya kukukasirisha, na kukushurutisha uje mbele Zake—na daima utahisi kuwa anachokifanya Mungu ni cha ajabu. Hivyo utahisi kana kwamba hakuna uchungu mwingi, na kwamba Mungu anapendeza. Ukifuata udhaifu wa mwili, na kusema kwamba Mungu amezidi, basi daima utahisi uchungu na daima utahuzunika, na utakosa uwazi kuhusu kazi yote ya Mungu na itaonekana kana kwamba Mungu hana huruma kwa udhaifu wa mwanadamu, na Hatambui shida za mwanadamu. Hivyo utajihisi mnyonge na mpweke, kana kwamba umekumbwa na dhuluma kubwa, na wakati huo utaanza kulalama. Kadiri unavyoutosheleza udhaifu wa mwili, ndivyo unavyohisi kuwa Mungu anazidi, hadi inakuwa mbaya kiasi kwamba unaikana kazi ya Mungu, na kuanza kumpinga Mungu na kujaa uasi. Hivyo unafaa kuuasi mwili na usiutosheleze: Mumeo, mkeo, watoto, matarajio, ndoa, familia—hakuna hata moja kati ya haya ambalo ni la thamani. Unafaa uwe na azimio hili: “Moyoni mwangu mna Mungu pekee na nitajaribu kumridhisha Mungu kadiri ya uwezo wangu, na si kuuridhisha mwili.” Daima ukiwa na azimio hili, basi ukiuweka ukweli katika vitendo, na kujiweka kando, utaweza kufanya hivyo kwa juhudi kidogo. Inasemekana kuwa kulikuwepo na mkulima aliyeona nyoka barabarani aliyekuwa ameganda. Huyu mkulima alimchukua yule nyoka na kumweka kifuani mwake, na baada ya yule nyoka kuamka alimuuma yule mkulima hadi akafa. Miili ya wanadamu ni kama yule nyoka: asili yake ni kuyadhuru maisha yao—na ikipata mbinu yake kikamilifu, maisha yako yanapotea. Mwili ni wa Shetani. Kuna tamaa kupita kiasi ndani yake, hujithamini wenyewe, unafurahia faraja, na kushangilia burudani, kujiachilia katika uvivu na uzembe, na baada ya kuuridhisha kwa kiwango fulani mwishowe utakuangamiza. Hivi ni kusema, ukiuridhisha sasa, wakati mwingine utakuomba zaidi. Daima mwili una tamaa na matakwa kupita kiasi, na unajinufaisha kutokana na wewe kuutosheleza mwili na kukufanya uufurahie hata zaidi na kuishi katika starehe zake—na ikiwa hutaushinda, mwishowe utajipotosha. Iwapo utapata uzima mbele za Mungu, na namna hatima yako itakavyokuwa, inategemea uasi wako dhidi ya mwili utakuwa wa namna gani. Mungu amekuokoa, na kukuteua na kukuamulia kabla, bado ikiwa leo hauko radhi kumridhisha, hauko radhi kuuweka ukweli katika vitendo, hauko radhi kuuasi mwili wako kwa moyo umpendao Mungu kwa dhati, hatimaye utajiangamiza mwenyewe, na kwa hivyo utapitia mateso mengi. Ikiwa mara zote unautosheleza mwili, Shetani atakumeza hatua kwa hatua, na kukuacha bila uzima, au upako wa Roho, hadi siku itafika ambayo ndani utakuwa giza. Ukiishi katika giza, utakuwa umetekwa nyara na Shetani, hutakuwa na Mungu tena, na wakati ule utaukataa uwepo wa Mungu na kumwacha. Kwa hivyo, ikiwa unataka kumpenda Mungu, ni lazima ulipe gharama ya uchungu na kupitia shida. Hakuna haja ya hamasa za nje na shida, kusoma zaidi na kuzungukazunguka zaidi; badala yake, unafaa kuweka kando vitu vilivyomo ndani yako: mawazo kupita kiasi, maslahi ya kibinafsi, na masuala yako binafsi, dhana, na motisha. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp