Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 589

Muumba anakusudia kupanga viumbe vyote. Wewe ni lazima usitupe au kutokaidi chochote ambacho Yeye anakifanya, wala usiwe na uasi kwake. Kazi ambayo Yeye hufanya hatimaye itahitimisha nia yake, na katika hii atapata utukufu. Leo, ni kwa nini haisemwi kwamba nyinyi ni wa uzao wa Moabu, au watoto wa joka kuu jekundu? Je, ni kwa nini hakuna mazungumzo ya wateule, na mazungumzo pekee ni ya viumbe? Kiumbe—hili lilikuwa jina la asili la mwanadamu, na ni hili ndilo utambulisho wake wa asili. Majina yanatofautiana tu kwa sababu nyakati na vipindi ni tofauti; kwa kweli, mwanadamu ni kiumbe wa kawaida. Viumbe wote, ikiwa ni wapotovu zaidi ama ni watakatifu sana, ni lazima watekeleze wajibu wa kiumbe. Wakati Yeye anafanya kazi ya ushindi, Mungu hakudhibiti kwa kutumia matarajio yako, majaliwa au hatima. Kwa kweli hakuna haja ya kufanya kazi kwa namna hii. Lengo la kazi ya ushindi ni kumfanya mwanadamu atekeleze wajibu wa kiumbe, kumfanya aabudu Muumba, na ni baada ya hii tu ndivyo ataweza kuingia kwenye hatima ya kustaajabisha. Majaliwa ya mwanadamu yanadhibitiwa na mikono ya Mungu. Wewe huna uwezo wa kujidhibiti mwenyewe: Licha ya mwanadamu yeye mwenyewe daima kukimbilia na kujishughulisha, anabakia bila uwezo wa kujidhibiti. Kama ungejua matarajio yako mwenyewe, kama ungeweza kudhibiti majaliwa yako mwenyewe, ingekuwa wewe bado ni kiumbe? Kwa kifupi, bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi, kazi yote yake ni kwa ajili ya mwanadamu. Chukua, kwa mfano, mbingu na nchi na vitu vyote ambavyo Mungu aliviumba ili kumhudumia mwanadamu: mwezi, jua, na nyota ambazo Yeye alimuumbia mwanadamu, wanyama na mimea, majira ya machipuko, majira ya joto, vuli na baridi, na kadhalika—yote ni kwa ajili ya kuwepo kwa mwanadamu. Na kwa hivyo, bila kujali ni jinsi gani anavyoadibu na kuhukumu mwanadamu, yote ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Japokuwa yeye humnyang’anya mwanadamu matumaini yake ya kimwili, ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, na utakaso wa mwanadamu ni kwa ajili ya kuishi kwake. Hatima ya mwanadamu iko mikononi mwa Muumba, hivyo ni jinsi gani mwanadamu anaweza kujidhibiti mwenyewe?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp