Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 150
Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Kile ambacho watu wanajua...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Kwa kuwa maneno Yangu yametimilika, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu. Naenda Nikipitia dunia nzima, Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida. Leo hii, nyote mko hai mbele Yangu: kesho nyote mtakua hai ndani ya ufalme Wangu. Je, si hii ndiyo baraka kubwa zaidi ambayo Nimempa mwanadamu? Kwa sababu ya gharama ambayo mnalipa leo, mtarithi baraka za wakati ujao na mtaishi ndani ya utukufu Wangu. Je, si bado mnataka kujihusisha na kiini cha Roho Wangu? Je, bado mnataka kujiua wenyewe? Watu wako tayari kufuata ahadi ambazo wanaweza kuziona, hata kama ni za muda mfupi, lakini hakuna aliye tayari kukubali ahadi za kesho, hata kama ni za milele. Vitu vinavyoonekana kwa mwanadamu ni vitu ambavyo Nitaangamiza, na vitu visivyoweza kushikika na mwanadamu ndivyo Nitakavyotimiza. Hii ndiyo tofauti ya Mungu na mwanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 20
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Kile ambacho watu wanajua...
Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu (Vifungu teule) Ayubu 1:6-11 Sasa kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja...
Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima...
Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni...