Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 364
Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu?...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Mwanadamu amepotoshwa na Shetani, na yeye ndiye kiumbe wa juu kabisa kuliko viumbe wote wa Mungu, hivyo mwanadamu anahitaji wokovu wa Mungu. Mlengwa wa wokovu wa Mungu ni mwanadamu, si Shetani, na kile kitakachookolewa ni mwili wa mwanadamu, na roho ya mwanadamu, na si mwovu. Shetani ni mlengwa wa uharibifu wa Mungu, mwanadamu ni mlengwa wa wokovu wa Mungu, na mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, kwa hivyo kitu cha kwanza kuokolewa ni mwili wa mwanadamu. Mwili wa mwanadamu umepotoshwa kwa kiasi kikubwa, na umekuwa kitu cha kumpinga Mungu, ambacho kinapinga na kukana waziwazi uwepo wa Mungu. Mwili huu uliopotoka ni vigumu sana kushughulika nao, na hakuna kitu ambacho ni kigumu sana kushughulika nacho au kukibadilisha kuliko silika potovu ya mwili. Shetani anaingia katika mwili wa mwanadamu ili kuchochea usumbufu, na anatumia mwili wa mwanadamu kuisumbua kazi ya Mungu, na kuharibu mpango wa Mungu, na hivyo mwanadamu amekuwa Shetani, na adui wa Mungu. Ili mwanadamu aweze kuokolewa, kwanza ni lazima achukuliwe mateka. Ni kwa sababu hii ndiyo maana Mungu anainuka na kuingia katika vita na Anaingia katika mwili ili afanye kazi, Amekusudia kufanya vita na Shetani. Lengo lake ni wokovu wa mwanadamu, mwanadamu ambaye amepotoshwa, na kushindwa na kuangamizwa kwa Shetani, ambaye ameasi dhidi Yake. Anamshinda Shetani kupitia kazi Yake ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo anamwokoa mwanadamu aliyeanguka. Hivyo, Mungu anatatua matatizo mawili kwa wakati mmoja. Anafanya kazi katika mwili, na Anazungumza katika mwili, na Anafanya kazi zote katika mwili ili aweze kujihusisha vizuri na mwanadamu, na kumdhibiti mwanadamu vizuri. Wakati wa mwisho ambapo Mungu Atakuwa mwili, kazi Yake katika siku za mwisho itahitimishwa katika mwili. Atawaainisha wanadamu wote kulingana na aina, na kuhitimisha usimamizi wake wote, na pia kuhitimisha kazi Yake yote katika mwili. Baada ya kazi Yake yote duniani kwisha, atakuwa mshindi kikamilifu. Kufanya kazi katika mwili, Mungu atakuwa amemshinda mwanadamu kikamilifu na atakuwa amempata mwanadamu kikamilifu. Hii haimaanishi kuwa usimamizi Wake wote utakuwa umekoma? Mungu anapohitimisha kazi Yake katika mwili, ilivyo kwamba amemshinda shetani kikamilifu, na amekuwa mshindi, Shetani hatakuwa na fursa zaidi ya kumpotosha mwanadamu. Kazi ya Mungu mwenye mwili wa kwanza ilikuwa ni wokovu na msamaha wa dhambi za mwanadamu. Sasa ni kazi ya kumshinda na kumpata mwanadamu, ili kwamba Shetani asiweze tena kufanya kazi yake, na atakuwa amepotea kabisa, na Mungu atakuwa ameshinda kabisa. Hii ni kazi ya mwili, na ni kazi inayofanywa na Mungu Mwenyewe.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu?...
Mungu mwenye mwili hawezi kukaa na mwanadamu milele kwa sababu Mungu Ana kazi zingine nyingi za kufanya. Yeye hawezi kufungwa katika mwili;...
Kazi ya Mungu katika mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na...
Katika kila hatua ya kazi ya Mungu yapo matakwa sawia kwa mwanadamu. Wale wote walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikishwa na...