Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 215
Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Loti alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Mungu hana nia mbaya kwa viumbe na anataka tu kumshinda Shetani. Kazi yote yake—iwe ni kuadibu ama hukumu—inaelekezwa kwa Shetani; inafanyika kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na ina lengo moja: kufanya vita na Shetani mpaka mwisho kabisa! Na Mungu kamwe hatapumzika kabla ya kuwa mshindi dhidi ya Shetani! Atapumzika tu punde atakapomshinda Shetani. Kwa sababu kazi yote ambayo inafanywa na Mungu inaelekezwa kwa Shetani, na kwa sababu wale waliopotoshwa na Shetani wote wamo katika udhibiti wa utawala wa Shetani na wote wanamilikiwa na Shetani, bila kupambana dhidi ya Shetani na kumvunja, Shetani hangepumzika kushika watu hawa, na hawangeweza kupatwa. Kama hawangepatwa, ingethibitisha kwamba Shetani bado hakushindwa, na ya kwamba hakutiishwa. Na kwa hivyo, katika miaka 6,000 ya mpango wa usimamizi wa Mungu, kwenye wakati wa awamu ya kwanza Yeye alifanya kazi ya sheria, wakati wa awamu ya pili Yeye alifanya kazi ya Enzi ya Neema, yaani, kazi ya kusulubiwa, na wakati wa awamu ya tatu Yeye alifanya kazi ya kumshinda mwanadamu. Kazi hizi zote zilielekezwa katika kiwango ambacho Shetani alikuwa amempotosha mwanadamu, na yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na hakuna awamu moja ambayo si kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kiini cha miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi ni vita dhidi ya joka kubwa jekundu, na kazi ya kusimamia watu pia ni kazi ya kumshinda Shetani, na kazi ya kufanya vita na Shetani. Mungu amepigana vita kwa miaka 6,000, na hivyo kufanya kazi kwa miaka 6,000, ili hatimaye kuleta mwanadamu katika ulimwengu mpya. Wakati Shetani atashindwa, mwanadamu atakuwa amewekwa huru kabisa. Je, huu si mwelekeo wa kazi ya Mungu hivi leo? Huu kwa hakika ni mwelekeo wa kazi ya leo: ukombozi kamili na kuwekwa huru kwa mwanadamu, ili kwamba asiwe chini ya sheria yoyote, wala asiwekewe mipaka na vifungu au vikwazo vyovyote. Kazi hii yote inafanywa kwa mujibu wa kimo chenu na kwa mujibu wa mahitaji yenu, kwa maana kuwa nyinyi mnapewa mnachoweza kutimiza. Sio namna ya “kuendesha bata kwenye sangara,” ya kuwalazimisha kufanya mambo zaidi ya uwezo wenu; badala yake, kazi hii yote inafanywa kwa mujibu wa mahitaji yenu ya ukweli. Kila awamu ya kazi ni kwa mujibu wa mahitaji halisi na matakwa ya mwanadamu, na ni kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kwa kweli, hapo mwanzo hapakuwa na vikwazo kati ya Muumba na viumbe vyake. Zote zinasababishwa na Shetani. Mwanadamu ameanza kuwa asiyeweza kuona au kugusa chochote kwa sababu ya usumbufu wa Shetani na upotovu wake. Mwanadamu ndiye mwaathirika, yule ambaye amedanganywa. Punde tu Shetani anaposhindwa, viumbe watamtazama Muumba, na Muumba ataangalia viumbe na kuweza kuwaongoza binafsi. Haya ndiyo tu maisha ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo duniani. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu kimsingi ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na punde tu Shetani anaposhindwa, mambo yote yatakuwa yametatuliwa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Loti alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma...
Umati unanishangilia, umati unanisifu; watu wote wanalitaja jina la Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanayainua macho yao kuviangalia...
Uzao: Awamu ya Tano Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa...
Mungu anafanya mengi kando na kuhakikisha usalama wa watu, kuhakikisha kwamba hawatamezwa na Shetani; pia hufanya kazi nyingi sana kwa...