Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hukumu Katika Siku za Mwisho | Dondoo 81

Mungu harudii kazi yake katika kila enzi mpya. Kwa kuwa siku za mwisho zimewadia, Yeye Atafanya kazi ya siku za mwisho, na kufichua tabia yake yote siku za mwisho. Siku za mwisho ni enzi tofauti, enzi ambayo Yesu Alisema lazima mteseke kwa maafa, na ukabiliwe na mitetemeko ya ardhi, njaa, na baa, ambavyo vitaonyesha kuwa hii ni enzi mpya, na sio tena Enzi ya Neema ya zamani. Kama, watu wanavyosema, Mungu daima habadiliki, tabia yake daima ni ya huruma na ya upendo, na Yeye anampenda mwanadamu jinsi Anavyojipenda, na Anampa kila mwanadamu wokovu na kamwe hamchukii mwanadamu, basi Angekuwa na uwezo wa kukamilisha kazi yake? Wakati Yesu Alikuja, Alisulubishwa msalabani, na Yeye Alijitoa kama sadaka kwa sababu ya wote wenye dhambi na kwa kujitoa Yeye mwenyewe madhabahuni. Yeye tayari Alikuwa Amemaliza kazi ya ukombozi na tayari Alikuwa Ametamatisha Enzi ya Neema, na hivyo ni nini kiini cha kurudia kazi ya enzi hiyo katika siku za mwisho? Je, kufanya kitu kimoja haitakuwa kukanusha kazi ya Yesu? Iwapo Mungu hatafanya kazi ya kusulubiwa awamu hii itakapofika, lakini Yeye Asalie mwenye mapenzi na Mungu wa huruma, je, anaweza kufikisha enzi hii mwisho? Je, Mungu mwenye upendo na mwenye huruma, si Angeweza kuhitimisha enzi hii? Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitabainishwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua hatima ya wanadamu na kikomo cha safari yao. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa wakati, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kumkabili hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki, basi kungekuwepo na mwisho wa usimamizi wa Mungu? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kubainisha mwanadamu na kuleta mwanadamu katika utawala mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp