Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatua Tatu za Kazi | Dondoo 34

Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria, ama kurudia kazi ya awali, ama kuhisi hali ya kumbukumbu kwa vitu vilivyopita; ni Mungu ambaye ni mpya kila wakati na hazeeki, na kila siku anazungumza maneno mapya. Lazima uyafuate yale ambayo lazima yafuatwe leo; haya ni majukumu na kazi ya mwanadamu. Ni muhimu kwamba utendaji uwekwe katika nuru iliyopo na maneno ya Mungu katika siku ya leo. Mungu hafuati masharti, na Anaweza kuzungumza kutoka kwa mitazamo mingi tofauti ili kufanya wazi hekima Yake na uwezo. Haijalishi ikiwa Anazungumza kutoka kwa mtazamo wa Roho, ama mwanadamu, ama mtu wa tatu—Mungu ni Mungu kila wakati na huwezi kusema kuwa yeye si Mungu kwa sababu ya mtazamo wa mwanadamu ambao Anazungumzia kutoka. Kati ya baadhi ya watu dhana zimetokea kutokana na mitazamo tofauti tofauti ambayo Mungu Anazungumza. Watu hao hawana maarifa ya Mungu, na pia maarifa ya kazi Yake. Iwapo Mungu angezungumza kila wakati kutumia mtazamo mmoja, je mwanadamu hangeweka masharti kuhusu Mungu? Je Mungu Anaweza kukubali mwanadamu kutenda kwa njia hiyo? Haijalishi ni mtazamo gani ambao Mungu Anaongelea, Mungu Ana malengo Yake kwa kila moja. Iwapo Mungu Angeongea kila wakati kwa mtazamo wa Roho, ungeweza kushiriki na Yeye? Hiyvo, Anazungumza kupitia mtu wa tatu ili kukupatia maneno Yake na kukuongoza kwa ukweli. Kila kitu Atendacho Mungu kinafaa. Kwa ufupi, yote yanafanywa na Mungu, na hupaswi kuwa na shaka kuyahusu. Bora tu kwamba Yeye ni Mungu, basi haijalishi kuwa ni mtazamo gani Anaongelea kutoka, Yeye bado ni Mungu. Huu ni ukweli usiobadilika. Njia yoyote Afanyayo kazi, Yeye bado ni Mungu, na dutu Yake haiwezi kubadilika! Petro alimpenda Mungu sana na alikuwa mtu aliyetaka kumridhisha Mungu, lakini Mungu hakumshuhudia kama Bwana ama Kristo, kwani dutu ya kiumbe ni vile ilivyo, na haiwezi badilika. Katika kazi Yake, Mungu hafuati masharti, lakini Anatumia mbinu tofauti kufanya kazi Yake ifanikiwe na kuongeza maarifa ya mwanadamu kumhusu. Kila mbinu Yake ya kazi inamsaidia mwanadamu kumjua, na ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu kamili. Haijalishi ni mbinu gani ya kufanya kazi Yeye hutumia, kila ni ili kumwongeza mwanadamu na kumfanya mtimilifu. Ingawa moja ya mbinu Zake za kazi ilikaa kwa muda mrefu, ni kwa ajili ya kupunguza imani ya mwanadamu Kwake. Hivyo hampaswi kuwa na shaka. Hizi zote ni hatua za kazi ya Mungu, na mnapaswa kuzitii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp