Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 2

Miliki na uwepo wa Mungu, kiini cha Mungu, tabia ya Mungu—yote yamewekwa wazi katika maneno Yake kwa binadamu. Anapopitia maneno ya Mungu, katika mchakato wa kuyatekeleza mwanadamu atapata kuelewa kusudi la maneno Anayonena Mungu, na kuelewa chemichemi na usuli wa maneno ya Mungu, na kuelewa na kufahamu matokeo yaliotarajiwa ya maneno ya Mungu. Kwa binadamu, haya ni mambo yote ambayo mwanadamu lazima ayapitie, ayatambue, na kuyafikia ili kuufikia ukweli na uzima, kutambua nia ya Mungu, kubadilishwa katika tabia yake, na kuweza kutii mamlaka ya Mungu na mipango. Katika wakati huo ambao mwanadamu anapitia, anafahamu, na kuvifikia vitu hivi, atakuwa kupata kumwelewa Mungu polepole, na katika wakati huu atakuwa pia amepata viwango tofauti vya ufahamu kumhusu Yeye. Kuelewa huku na maarifa havitoki katika kitu ambacho mwanadamu amefikiria ama kutengeneza, ila kutoka kwa kile ambacho anafahamu, anapitia, anahisi, na anashuhudia ndani yake mwenyewe. Ni baada tu ya kufahamu, kupitia, kuhisi, na kushuhudia vitu hivi ndipo ufahamu wa mwanadamu kumhusu Mungu utapata ujazo, ni maarifa anayopata katika wakati huu pekee ndio ulio halisi, wa kweli na sahihi, na mchakato huu—wa kupata kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu kwa kuelewa, uzoefu, kuhisi, na kushuhudia maneno Yake—sio kingine ila ushirika wa kweli kati ya mwanadamu na Mungu. Katikati ya aina hii ya ushirika, mwanadamu anakuja kuelewa kwa dhati na kufahamu nia za Mungu, anakuja kuelewa kwa dhati na kujua miliki na uwepo wa Mungu, anakuja na kuelewa kujua kwa kweli kiini cha Mungu, anakuja kuelewa na kujua tabia ya Mungu polepole, anafikia uhakika wa kweli kuhusu, na ufafanuzi sahihi wa, ukweli wa mamlaka ya Mungu juu ya vitu vyote vilivyoumbwa, na kupata mkondo kamili kwa na ufahamu wa utambulisho wa Mungu na nafasi Yake. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu anabadilika, hatua kwa hatua, mawazo yake kuhusu Mungu, bila kumwaza pasi na msingi, ama kuipa nafasi tashwishi yake kumhusu Yeye, ama kutomwelewa, ama kumshutumu, ama kupitisha hukumu Kwake, ama kuwa na shaka Naye. Kwa sababu hii, mwanadamu atakuwa na mijadala michache na Mungu, atakuwa na uhasama kiasi kidogo na Mungu, na kutakuwa na matukio machache ambapo atamuasi Mungu. Kwa upande mwingine, kujali kwa mwanadamu na utii kwa Mungu kutakua kwa kiasi kikubwa, na uchaji wake Mungu utakuwa wa kweli zaidi na pia mkubwa zaidi. Katika ya aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kupewa ukweli pekee na ubatizo wa uzima, bali wakati uo huo pia atapata maarifa ya kweli ya Mungu. Katika aina hii ya ushirika, mwanadamu hatapata kubadilishwa kwa tabia yake na kupata wokovu pekee, bali pia kwa wakati huo atafikia uchaji na ibada ya kweli ya kiumbe aliyeumbwa kwa Mungu. Baada ya kuwa na aina hii ya ushirika, imani ya mwanadamu katika Mungu haitakuwa tena ukurasa tupu wa karatasi, ama ahadi ya maneno matupu, ama harakati na tamanio lisilo na lengo na kuabudu kama mungu; katika aina hii ya ushirika pekee ndio maisha ya mwanadamu yatakua kuelekea ukomavu siku baada ya siku, na ni wakati huu ndio tabia yake itabadilika polepole, na imani yake kwa Mungu, hatua kwa hatua, itatoka kwenye imani ya wasiwasi na kutoeleweka na imani isiyo ya hakika mpaka katika utii wa kweli na kujali, na kuwa katika uchaji Mungu wa kweli; mwanadamu pia katika kumfuata Mungu, ataendelea polepole kutoka kuwa mtazamaji na kuwa na hali ya utendaji, kutoka yule anayeshughulikwa na kuwa anayechukua nafasi ya kutenda; kwa aina hii ya ushirika pekee ndipo mwanadamu atafikia kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu, kwa ufahamu wa kweli wa Mungu. Kwa sababu watu wengi hawajawahi kuiingia katika ushirika wa kweli na Mungu, ufahamu wao wa Mungu unakomea kiwango cha nadharia, katika kiwango cha barua na kanuni. Hivyo ni kusema, watu wengi, haijalishi ni miaka mingapi wamemwamini Mungu, ikija kwa kumjua Mungu bado wako mahali walipoanzia, wamekwama katika msingi wa aina za heshima, na mitego yao ya hadhi na kabaila za kishirikina. Kwamba maarifa ya mwanadamu kumhusu Mungu yanapaswa kukomea yalipoanzia ina maana kwamba hayapo kabisa. Mbali na uthibitisho wa mwanadamu kuhusu nafasi ya Mungu na utambulisho, imani ya mwanadamu kwa Mungu bado iko katika hali ya kutoeleweka na kutokuwa na uhakika. Hii ikiwa hivyo, ni kiasi gani ambacho mwanadamu anaweza kuwa nacho kuhusu uchaji Mungu wa kweli?

Haijalishi kiwango cha imani yako katika uwepo Wake, hili haliwezi kuchukua mahali pa ufahamu wako wa Mungu, wala uchaji wako wa Mungu. Haijalishi kiwango ambacho umefurahia baraka Zake na neema Yake, hii haiwezi kuchukua nafasi ya ufahamu wako wa Mungu. Haijalishi ni kiwango gani unataka na kutamani kuweka wakfu kila kitu chako na kugharimika kwa ajili Yake, hii haiwezi kuchukua nafasi ya maarifa yako kuhusu Mungu. Ama labda umeyazoea sana maneno ambayo Amenena mpaka unayajua kimoyomoyo na unaweza kuyasema upesi kinyumenyume; hata hivyo, hii haiwezi kuchukua nafasi ya maarifa yako kuhusu Mungu. Haijalishi kiwango cha dhamira ya mwanadamu katika kumfuata Mungu, iwapo hajawahi kuwa na ushirika wa kweli na Mungu, ama kuwa na uzoefu wa kweli wa maneno ya Mungu, basi ufahamu wake wa Mungu utakuwa utupu tu au ndoto isiyo na mwisho; kwa kuwa yote yale unaweza kuwa “umekumbana” na Mungu kwa kupita, au kukutana Naye uso kwa uso, ufahamu wako wa Mungu bado utakuwa sufuri, na uchaji wako wa Mungu utakuwa tu kidahizo ama njozi.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp