Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
(Sehemu ya Nne)
6. Ibada Mlimani
Sifa na Heri (Mat 5:3-12)
Chumvi na Nuru (Mat 5:13-16)
Sheria (Mat 5:17-20)
Kuhusu Hasira (Mat 5:21-26)
Kuhusu Uzinzi (Mat 5:27-30)
Kuhusu Talaka (Mat 5:31-32)
Kuhusu Viapo (Mat 5:33-37)
Kuhusu Kulipiza Kisasi (Mat 5:38-42)
Upendo kwa Adui (Mat 5:43-48)
Kuhusu Utoaji Sadaka (Mat 6:1-4)
Kuhusu Maombi (Mat 6:5-8)
7. Mifano ya Bwana Yesu
Mfano wa Mpanzi (Mat 13:1-9)
Mfano wa Magugu katikati ya Ngano (Mat 13:24-30)
Mfano wa Punje ya Haradali (Mat 13:31-32)
Mfano wa Chachu (Mat 13:33)
Mfano wa Magugu Umeelezwa (Mat 13:36-43)
Mfano wa Hazina (Mat 13:44)
Mfano wa Lulu (Mat 13:45-46)
Mfano wa Wavu (Mat 13:47-50)
8. Amri
Mat 22:37-39 Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda.
Hebu kwanza tuangalie katika kila sehemu ya “Ibada Mlimani.” Haya yote yanahusiana na nini? Yaweza kusemekana kwa uhakika kwamba haya yote yameinuliwa zaidi, yana uthabiti zaidi na karibu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.
Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Mnafaa kuzielewa vipi hali hizi za heri? Ni nini mnachofaa kujua kuhusu sheria? Ghadhabu inafaa kufasiliwa vipi? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Ni nini kinachosemwa, na ni sheria aina gani zipo kuhusu talaka, na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, viapo, jicho kwa jicho, kuwapenda adui zako, maagizo kuhusu sadaka, n.k? Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na ufuataji wao wa Mungu. Baadhi ya desturi hizi zinatumika leo, lakini bado yapo katika hali ya kimsingi kuliko mahitaji ya sasa ya watu. Kwa kiasi kikubwa uko katika hali ya kimsingi ambao watu wanakumbana nao katika kuamini kwao katika Mungu. Tangu wakati Bwana Yesu alianza kufanya kazi, Alikuwa tayari anaanza kufanya kazi kwa tabia ya maisha ya binadamu, lakini yalitokana na msingi wa sheria. Je, sheria na misemo kuhusu mada hizi ilikuwa na uhusiano wowote na ukweli? Bila shaka zilikuwa nao! Taratibu, kanuni na ibada zote zingine za awali katika Enzi ya Neema zilikuwa na uhusiano, na tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho na bila shaka kwa ukweli. Haijalishi ni nini ambacho Mungu anaonyesha, kwa njia gani Anaonyesha, au Akitumia lugha gani, asili yake, na mwanzo wake, vyote vinatokana na kanuni za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hili halina kosa. Kwa hivyo ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika ibada hayaambatani na ukweli? Huwezi! Kila mojawapo ya mambo haya ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu; yote yalikuwa kanuni na mawanda yaliyotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kuwa na mwenendo, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha wakati huo, waliweza tu kukubali na kuyafahamu mambo haya. Kwa sababu dhambi ya mwanadamu ilikuwa bado haijatatuliwa, Bwana Yesu angeweza tu kuyatoa maneno haya, na Angeweza kutumia mafundisho mepesi kama hayo miongoni mwa aina hii ya upana ili kuwaambia watu wa wakati huo namna ambavyo walifaa kutenda, kile walichofaa kufanya, ndani ya kanuni na upana gani walifaa kufanya mambo, na vipi walivyofaa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha mwanadamu wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi katika sheria kuyakubali mafundisho haya, hivyo basi kile Alichofunza Bwana Yesu lazima kingebaki ndani ya mawanda haya.
Halafu, hebu tuangalie ni nini kilicho katika “Mifano ya Bwana Yesu.”
Mfano wa kwanza ni mfano wa mpanzi. Huu ni mfano wa kusisimua kweli; upanzi wa mbegu ni tukio maarufu sana katika maisha ya watu. Mfano wa pili ni mfano wa magugu. Kulingana na jinsi magugu yalivyo, yeyote ambaye amewahi kupanda mimea na watu wazima watajua. Wa tatu ni mfano wa punje ya haradali. Nyinyi nyote mnajua haradali ni nini, sivyo? Kama hujui, unaweza kupekuapekua katika Biblia. Nao mfano wa nne ni mfano wa chachu, watu wengi wanajua kwamba chachu inatumiwa katika kutia chachu; ni kitu ambacho watu wanatumia katika maisha yao ya kila siku. Mifano yote iliyotajwa hapa chini ukiwemo mfano wa sita, mfano wa hazina, mfano wa saba, mfano wa lulu, na wa nane mfano wa wavu; ni mifano iliyotolewa katika maisha ya watu; inatoka katika maisha ya watu halisi. Ni picha ya aina gani inayoonyeshwa na mifano hii? Hii ni picha ya Mungu akigeuka kuwa mtu wa kawaida na kuishi pamoja na mwanadamu, Akitumia lugha ya maisha ya kila siku, Akitumia lugha ya mwanadamu ili kuwasiliana na binadamu na kuwapa kile wanachohitaji. Wakati Mungu alikuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa muda mrefu, baada ya kupitia na kushuhudia hali ya maisha mbalimbali ya watu, hali hii Aliyopitia kilikuwa kitabu Chake cha kiada cha kubadilisha lugha Yake ya kiungu kuwa lugha ya binadamu. Bila shaka, mambo haya Aliyoyaona na kuyasikia katika maisha yaliweza pia kumwimarisha Mwana wa Adamu kupitia yale Aliyopitia akiwa binadamu. Alipowataka watu waelewe ukweli fulani, ili kuwaelewesha mapenzi fulani ya Mungu, Angetumia mifano inayofanana na ile iliyotajwa hapo juu ili kuwaeleza watu kuhusu mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake kwa binadamu. Mifano hii yote ilihusiana na maisha ya watu; hakukuwa na hata mmoja ambao haukuwa na mguso wa maisha ya binadamu. Bwana Yesu alipoishi na binadamu, Aliwaona wakulima wakilima mashamba yao; Alijua magugu yalikuwa nini na kutia chachu kulikuwa nini; Alielewa kwamba binadamu wanapenda hazina na hivyo basi Alitumia sitiari za hazina na hata lulu; mara kwa mara Aliwaona wavuvi wakizirusha nyavu zao na kadhalika. Bwana Yesu aliziona shughuli hizi katika maisha ya binadamu na pia Alipitia aina hiyo ya maisha. Alikuwa sawa na kila mtu mwingine wa kawaida Akipitia milo mitatu kwa siku ya binadamu na mazoea yale mengine ya kila siku. Aliweza kupitia kibinafsi maisha ya mtu wa kawaida na akashuhudia maisha ya wengine. Aliposhuhudia na kupitia haya yote binafsi, kile Alichofikiria kilikuwa si namna ya kuwa na maisha mazuri au namna ambavyo Angeishi kwa uhuru zaidi au kwa utulivu zaidi. Alipokuwa akipitia maisha halisi ya binadamu Bwana Yesu aliuona ugumu katika maisha ya watu, Aliuona ugumu, ule ufukara, huzuni ya watu waliopotoshwa na Shetani, wakiishi katika utawala wa Shetani na walioishi katika dhambi. Huku akiyapitia maisha ya binadamu Yeye binafsi aliweza pia kushuhudia namna ambavyo watu waliokuwa wakiishi ndani ya upotovu walivyokuwa wasioweza kujisaidia, na Akawaona kupitia ule umaskini wa wale walioishi katika dhambi, wale waliopotea katika mateso ya Shetani, ya mwovu. Bwana Yesu alipoyaona mambo haya, Aliyaona kwa macho Yake ya uungu au macho Yake ya ubinadamu? Ubinadamu Wake ulikuwepo kwa kweli—ulikuwepo waziwazi—Angeweza kuyapitia na kuyaona haya yote na bila shaka Aliyaona katika kiini Chake halisi, katika uungu Wake. Yaani, Kristo Mwenyewe, Bwana Yesu, binadamu Aliyaona haya na kila kitu Alichokiona kilimfanya kuhisi umuhimu na haja ya kazi Aliyokuwa Ameamua kuifanya wakati huu akiwa mwili. Hata ingawa Yeye Mwenyewe Alijua kwamba jukumu Alilohitaji kushughulikia Akiwa mwili lilikuwa kubwa mno, na namna ambavyo Angepitia maumivu ya kikatili, Alipomwona mwanadamu asiyejiweza ndani ya dhambi, Alipoona umaskini wa maisha yao na mapambano hafifu chini ya sheria, Alihuzunika zaidi na zaidi, na Akawa na hamu kubwa zaidi na zaidi ya kumwokoa binadamu kutoka dhambini. Haijalishi ni ugumu wa aina gani ambao Angepitia au ni aina gani ya maumivu Angehisi, Alikuwa shupavu zaidi na zaidi katika kuwakomboa wanadamu wanaoishi katika dhambi. Wakati wa mchakato huu, unaweza kusema kwamba Bwana Yesu alianza kuelewa waziwazi kazi Aliyohitajika kufanya na kile Alichokuwa Ameaminiwa kutekeleza. Alikuwa pia mwenye hamu kubwa zaidi ya kukamilisha kazi ambayo Alikuwa Aichukue—kushughulikia dhambi zote za mwanadamu, upatanisho wa Mungu na binadamu ili wasiishi tena katika dhambi naye Mungu Angeweza kusahau dhambi za binadamu kwa sababu ya sadaka ya dhambi, na hivyo basi kumruhusu kuendeleza kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu. Yaweza kusemwa kwamba katika moyo wa Bwana Yesu, Alikuwa radhi kujitoa kwa ajili ya mwanadamu, kujitoa Mwenyewe. Alikuwa radhi pia kuchukua nafasi ya sadaka ya dhambi, kusulubishwa msalabani, na Alikuwa na hamu ya kukamilisha kazi hii. Alipoona hali za kusikitisha za maisha ya binadamu, Alitaka hata zaidi kukamilisha misheni Yake haraka iwezekanavyo, bila ya kuchelewa hata dakika au sekunde moja. Alipokuwa na hisia hii ya dharura, Alikuwa hafikirii namna ambavyo maumivu Yake binafsi yangekuwa wala hakufikiria kwa muda wowote zaidi kuhusu ni kiwango kipi cha udhalilishaji ambacho Angevumilia—Alishikilia azimio moja tu moyoni Mwake: Mradi tu Alijitoa Mwenyewe, mradi tu Angesulubishwa msalabani kama sadaka ya dhambi, mapenzi ya Mungu yangetendeka na Angeweza kuanza kazi mpya. Maisha ya wanadamu katika dhambi, hali yao ya kuwepo katika dhambi ingebadilika kabisa. Imani yake na kile Alichoamua kufanya vyote vilihusiana na kumwokoa binadamu, na Alikuwa na lengo moja tu: kufanya mapenzi ya Mungu ili Aweze kuanza kwa ufanisi hatua ambayo ingefuata katika kazi Yake. Haya ndiyo yaliyokuwa katika akili ya Bwana Yesu wakati huo.
Akiishi katika mwili, Mungu mwenye mwili Alimiliki ubinadamu wa kawaida; Alikuwa na hisia na kule kuwaza kwa mtu wa kawaida. Alijua furaha ilikuwa nini, maumivu yalikuwa nini na Alipowaona wanadamu katika hali hii ya maisha, Alihisi kwa kina kwamba kuwapatia watu kiasi cha mafunzo tu, kuwapatia kitu au kuwafunza kitu kusingewaongoza kutoka katika dhambi. Wala kuwafanya kutii amri pia kusingewakomboa kutoka katika dhambi—pale tu Alipozichukua dhambi za binadamu na kuwa mfano wa mwili wenye dhambi ndipo Alipoweza kuibadilisha na uhuru wa mwanadamu na kuibadilisha na msamaha wa Mungu kwa binadamu. Kwa hivyo baada ya Bwana Yesu kupitia na kushuhudia maisha ya binadamu katika dhambi, kulikuwa na tamanio kuu lililojionyesha katika moyo Wake—kuwaruhusu wanadamu kujiondoa kutoka katika maisha yao ya kupambana na dhambi. Tamanio hili lilimfanya kuhisi zaidi na zaidi kwamba lazima Aende katika msalaba na kuzichukua dhambi za binadamu haraka iwezekanavyo, kwa dharura. Hizi ndizo zilizokuwa fikira za Bwana Yesu wakati huo, baada ya Yeye kuishi na watu na kuwaona, kuwasikia, na kuhisi umaskini wa maisha yao ndani ya dhambi. Kwamba Mungu mwenye mwili Angekuwa na nia ya aina hii kwa mwanadamu, kwamba Angeweza kueleza na kufichua tabia ya aina hii—je, hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida angekuwa nalo? Mtu wa kawaida angeona nini akiishi katika mazingira ya aina hii? Angefikiria nini? Kama mtu wa kawaida angekumbwa na haya yote, angeangalia matatizo haya kwa mtazamo wa juu? Bila shaka hapana! Ingawa kuonekana kwa Mungu mwenye mwili ni kama mwanadamu, Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuongea lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine Anaonyesha hata mawazo Yake kwa jinsi na hisia za mwanadamu, namna Anavyowaona wanadamu, kiini cha vitu, na namna ambavyo watu waliopotoka wanavyomwona mwanadamu na kiini cha vitu kwa hakika si sawa kabisa. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka. Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. Kwa watu waliopotoka, kile Anachoeleza katika mwili ni matoleo ya ukweli na maisha. Matoleo haya si ya mtu mmoja tu lakini kwa wanadamu wote. Kwa mtu yeyote aliyepotoka, katika moyo wake kunao tu wale watu wachache ambao wanahusiana na yeye. Kunao tu hao watu kadhaa ambao anawatunza ambao anajali kuwahusu. Wakati janga linakaribia, anafikiria kwanza kuhusu watoto wake binafsi, mume au mke au wazazi, na mtu mwenye moyo wa kujitoa zaidi kuhusu mwanadamu angefikiria zaidi kuhusu baadhi ya watu wa ukoo au rafiki mzuri; je yeye huwafikiria wengine? La hasha! Kwa sababu binadamu ni, kwa hakika, binadamu, na wanaweza tu kuangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo na kutoka katika kimo cha mtu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti kabisa na mtu aliyepotoka. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa binadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya binadamu na masharti na nadharia za binadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya mawanda ya kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho kama kipimo. Mawanda haya yanajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu na vya Mungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo. Je, unaona udhihirisho na ufichuzi wa Mungu Mwenyewe ndani ya Bwana Yesu? Unaweza kusema kwamba kile ambacho Bwana Yesu alifanya na kusema kilihusiana na huduma Yake na kazi ya usimamizi ya Mungu binafsi, kwamba yote hayo yalikuwa ni udhihirisho na ufichuzi wa kiini cha Mungu. Ingawa Alikuwa na udhihirisho wa binadamu, kiini Chake cha kiungu na ufichuzi Wake wa kiungu hauwezi kukataliwa. Je, udhihirisho huu wa wanadamu ulikuwa udhihirisho wa kweli wa ubinadamu? Udhihirisho Wake wa ubinadamu ulikuwa, kwa kiini chake, tofauti kabisa na udhihirishaji wa ubinadamu wa watu waliopotoka. Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, na kama Angekuwa kweli mmojawapo wa wale wa kawaida, watu waliopotoka, Angeweza kuyaona maisha ya wanadamu ndani ya dhambi kutoka katika mtazamo wa kiungu? La hasha! Hii ndiyo tofauti kati ya Mwana wa Adamu na watu wa kawaida. Watu wote waliopotoka wanaishi ndani ya dhambi na wakati mtu yeyote anaiona dhambi, hana hisia zozote kuihusu hiyo dhambi; wako sawa tu, kama vile nguruwe anayeishi kwenye matope na hahisi chochote kamwe kuhusu kutokuwa na utulivu, au uchafu—anakula vizuri na kulala vizuri. Kama mtu anasafisha nyumba ya nguruwe, nguruwe kwa hakika hatahisi utulivu, na hatabakia akiwa msafi. Baada ya muda mfupi tu atakuwa tena akijigaragaza katika matope akiwa mtulivu kabisa, kwa sababu yeye ni kiumbe mchafu. Wakati binadamu wanapomwona nguruwe wanahisi kwamba anao uchafu na ukimsafisha yule nguruwe hahisi vyema zaidi—ndio maana hakuna anayemfuga nguruwe ndani ya nyumba yake. Namna ambavyo wanadamu wanavyomwona nguruwe itakuwa tofauti siku zote na namna ambavyo nguruwe wenyewe wanavyojihisi, kwa sababu wanadamu na nguruwe si wa aina moja. Na kwa sababu Mwana wa Adamu kwa mwili si wa aina moja na wanadamu waliopotoka, Mungu mwenye mwili tu ndiye Anayeweza kusimama kutoka kwa mtazamo wa kiungu, na kusimama kutoka katika kimo cha Mungu ili kuwaona wanadamu, ili kuona kila kitu.
Mungu anapokuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu, ni mateso yapi Anayopitia katika mwili? Yupo yeyote anayeelewa kwa kweli? Baadhi ya watu husema kwamba Mungu huteseka pakubwa, na ingawa Yeye ni Mungu Mwenyewe, watu hawaelewi kiini Chake na siku zote wanamchukulia Yeye kama mtu, hali ambayo humfanya Yeye kuhisi vibaya na kuona kwamba Amekosewa—wanasema kwamba mateso ya Mungu kwa kweli ni makubwa. Baadhi ya watu husema kwamba Mungu hana hatia na hana dhambi, lakini Yeye huteseka sawa na wanavyoteseka wanadamu, na Yeye hupitia mateso, matusi, na kuvunjiwa heshima pamoja na wanadamu; wanasema Yeye pia huvumilia kutoelewana na kutotiiwa na wafuasi Wake—kuteseka kwa Mungu kwa kweli hakuwezi kupimwa. Yamkini humwelewi Mungu kwa kweli. Kwa hakika, mateso haya unayoyaongelea hayaonekani kuwa mateso ya kweli kwake Mungu, kwa sababu kunayo mateso makubwa zaidi ya haya. Basi mateso ya kweli kwa Mungu Mwenyewe ni yapi? Mateso ya kweli ya mwili wa Mungu ni yapi? Kwa Mungu, wanadamu kutomwelewa Yeye haihesabiki kuwa ni mateso, na kwa watu kuwa kutokuwa na uelewano fulani wa Mungu na kwa kutomwona Yeye kama Mungu hakuhesabiki kuwa mateso. Hata hivyo, mara nyingi watu huhisi kwamba Mungu lazima alipitia dhuluma kubwa sana, kwamba wakati Mungu yumo katika mwili Hawezi kuionyesha nafsi Yake kwa wanadamu na kuwaruhusu kuuona ukubwa Wake, na Mungu anajificha kwa unyenyekevu katika mwili duni na hivyo basi hali hii lazima ilikuwa ya kumpa Yeye maumivu makali. Watu hushikilia moyoni kile wanachoweza kuelewa na kile wanachoweza kuona kuhusu mateso ya Mungu, na kuweka aina zote za huruma kwake Mungu na mara nyingi hata wataisifia kidogo hali hiyo. Kwa uhakika, kunayo tofauti, kuna pengo kati ya kile watu wanachoelewa, kile watu wanachoelewa kuhusu mateso ya Mungu na kile Anachohisi kwa kweli. Nakwambia ukweli—kwa Mungu haijalishi kama ni Roho wa Mungu au mwili wa Mungu, mateso hayo si mateso ya kweli. Basi ni nini hasa ambacho kwa kweli Mungu huteseka? Hebu tuzungumze kuhusu mateso ya Mungu kutoka katika mtazamo wa Mungu mwenye mwili pekee.
Wakati Mungu anapokuwa mwili, kuwa mtu wa wastani, mtu wa kawaida akiishi miongoni mwa wanadamu, pamoja na watu, hawezi kuona na kuhisi mbinu za watu, sheria na falsafa zao za kuishi? Ni vipi ambavyo mbinu na sheria hizi zinamfanya Yeye kuhisi? Je, Anahisi kuwa na chuki katika moyo Wake? Kwa nini Ahisi chuki? Mbinu na sheria za kuishi za wanadamu ni gani? Zimekita mizizi katika kanuni gani? Ziko katika msingi upi? Mbinu, sheria, n.k za kuishi kwa wanadamu—zote hizi zimeundwa kwa misingi ya mantiki, maarifa na falsafa ya Shetani. Wanadamu wanaoishi chini ya aina hizi za sheria hawana ubinadamu, hawana ukweli—wote wanaukataa ukweli, na ni wakatili kwa Mungu. Tunapoangalia kiini cha Mungu tunaona kwamba kiini Chake ni kinyume kabisa na mantiki, maarifa na falsafa ya Shetani. Kiini Chake kimejaa haki, ukweli, na utakatifu na uhalisi mwingine wa mambo yote mazuri. Mungu, akimiliki kiini hiki na Akiishi miongoni mwa wanadamu—Anahisi vipi katika moyo Wake? Je, haujajaa maumivu? Moyo Wake umo katika maumivu, na maumivu haya ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kuelewa wala kutambua. Kwa sababu kila kitu Anachokumbana nacho, kukabiliana nacho, kusikia, kuona na kupitia vyote ni upotovu wa wanadamu, uovu, na uasi wao dhidi ya, na upinzani wa ukweli. Kila kitu kinachotoka kwa wanadamu ndicho chanzo cha mateso Yake. Hivi ni kusema kwa sababu kiini Chake halisi si sawa na wanadamu waliopotoka, kupotoka kwa wanadamu kunakuwa ndiko chanzo cha mateso Yake makuu. Wakati Mungu anapokuwa mwili, Anaweza kupata mtu anayetumia lugha moja na Yeye? Hili haliwezi kupatikana miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayeweza kupatikana anayeweza kuwasiliana, anayeweza kuwa na mabadilishano haya na Mungu—unaweza kusema Mungu anayo hisia aina gani? Yale mambo ambayo watu huzungumza ambayo wanapenda, ambayo wanafuatilia na kutamani yote yanahusu dhambi, na yana mielekeo ya uovu. Wakati Mungu anapokabiliana na haya, haya si kama kisu katika moyo Wake? Akiwa Amekabiliwa na mambo haya, Anaweza kuwa na furaha katika moyo Wake? Anaweza kupata kitulizo? Wale wanaoishi na Yeye ni wanadamu waliojaa uasi na uovu—je, moyo Wake utakosaje kuteseka? Mateso haya kwa kweli ni makubwa vipi, na ni nani anayeyajali? Ni nani anayeyasikiliza? Na ni nani anayeweza kuyatambua? Watu hawana njia yoyote ya kuuelewa moyo wa Mungu. Mateso Yake ni kitu ambacho watu hawawezi hasa kutambua, na ubaridi, na kutojua kwa binadamu kunayafanya mateso ya Mungu kuwa yenye kina zaidi.
Kunao baadhi ya watu ambao huonea huruma hali ya Kristo kwa sababu kunao mstari katika Biblia unaosema: “Mbweha wana mashimo, na ndege wa hewani wanavyo viota; lakini Mwana wa Adamu hana pahali pa kupumzisha kichwa chake.” Wakati watu wanaposikia haya, wanayatia moyoni na kuamini kwamba haya ndiyo mateso makubwa zaidi ambayo Mungu huvumilia, na mateso makubwa zaidi ambayo Kristo huvumilia. Sasa, tukiangalia katika mtazamo wa ukweli, hivyo ndivyo ilivyo? Mungu haamini kwamba ugumu huu ni mateso. Hajawahi kulia dhidi ya dhuluma hizi kwa ajili ya ugumu wa mwili, na hajawahi kuwalipizia kisasi wanadamu au Kujitoza na chochote. Hata hivyo, Anaposhuhudia kila kitu cha wanadamu, maisha yaliyopotoka na uovu wa wanadamu waliopotoka, Anaposhuhudia kwamba wanadamu wamo katika ung’amuzi wa Shetani na wamefungwa na Shetani na hawawezi kukwepa, kwamba wanaoishi ndani ya dhambi hawajui ukweli ni nini—Hawezi kuvumilia dhambi hizi zote. Chuki Yake kwa binadamu huongezeka siku baada ya siku, lakini lazima Avumilie yote haya. Haya ni mateso makuu ya Mungu. Mungu hawezi kujieleza kikamilifu hata sauti ya moyo Wake au hisia Zake miongoni mwa wafuasi Wake, na hakuna yeyote miongoni mwa wafuasi Wake anayeweza kuelewa kwa kweli mateso Yake. Hakuna yule ambaye hujaribu kuyaelewa au kuutuliza moyo Wake—moyo Wake huvumilia mateso haya siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, mara kwa mara. Unaona nini katika yote haya? Mungu hahitaji chochote kutoka kwa wanadamu kama malipo kwa kile Alichokitoa, lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, Hawezi kuvumilia kamwe uovu, upotovu na dhambi ya wanadamu, lakini Anahisi chukizo na chuki kupindukia, hali ambayo husababisha moyo wa Mungu na mwili Wake kuvumilia mateso yasiyoisha. Je, ungeyaona yote haya? Kuna uwezekano, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeyaona kwa sababu hakuna yeyote kati yenu anayeweza kumwelewa Mungu kwa kweli. Baada ya muda mnaweza kuyapitia haya wenyewe kwa utaratibu.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?