Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

(Sehemu ya Tano)

9. Bwana Yesu Atenda Miujiza

1) Bwana Yesu Awalisha Watu Elfu Tano

Yohana 6:8-13 Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema kwake, Kuna mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri nao samaki wawili wadogo: lakini ni yapi miongoni mwa watu wengi? Naye Yesu akasema, Wafanye watu waketi chini. Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano. Naye Yesu akaichukua ile mikate, na baada ya kutoa shukrani, akagawanya kwa wanafunzi, na wanafunzi wakawapa wale waliokuwa wameketi chini; na vivyo hivyo wale samaki kadiri kiasi walichotaka. Baada ya kushiba, alisema kwa wanafunzi wake, Ninyi kusanyeni vipande ambavyo vimebaki, ndiyo chochote kisipotezwe. Kwa hivyo walivikusanya pamoja, na wakavijaza vikapu kumi na mbili na vipande vya mikate mnitano ya shayiri vilivyobaki baada ya wale watu kula.

2) Kufufuka kwa Lazaro Kwampa Mungu Utukufu

Yohana 11:43-44 Na baada ya yeye kuzungumza, akasema kwa sauti kuu, Lazaro, kuja nje. Na yeye ambaye alikuwa amefariki akatoka nje, akiwa amefungwa mkono na mguu na sanda: na uso wake ulikuwa umefungwa kwa kitambaa. Yesu akasema kwao, Mfungueni yeye, na mwache aondoke.

Kati ya miujiza iliyotendwa na Bwana Yesu, tumechagua tu hii miwili kwa sababu inatosha kuwaonyesha kile ambacho Ningependa kuzungumzia hapa. Miujiza hii miwili inashangaza ajabu, na inawakilisha hasa miujiza ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.

Kwanza, hebu tuangalie ufahamu wa kwanza: Bwana Yesu Awalisha Watu Elfu Tano.

Dhana ya “mikate mitano na samaki wawili” ni ya aina gani? Ni watu wangapi ambao mikate mitano na samaki wawili hulisha kwa kawaida? Mkipima kulingana na hamu ya kula ya mtu wa kawaida, inaweza kutosha tu watu wawili. Hii ndiyo dhana ya kimsingi kabisa ya mikate mitano na samaki wawili. Hata hivyo, imeandikwa katika dondoo hii kwamba mikate mitano na samaki wawili viliwalisha watu wangapi? Imerekodiwa katika Maandiko hivi: “Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano.” Tukilinganisha na mikate mitano na samaki wawili, elfu tano ni idadi kubwa? Ni nini maana ya idadi hii kuwa kubwa sana? Kutoka kwa mtazamo wa binadamu, kugawanya mikate mitano na samaki wawili kati ya watu elfu tano haitawezekana, kwa sababu tofauti kati ya idadi hizi ni kubwa mno. Hata kama kila mtu angepata tu kipande kidogo cha kutafuna, bado mikate hiyo isingetosha watu hao elfu tano. Lakini hapa Bwana Yesu alitenda muujiza—Hakuruhusu watu elfu tano kula hadi wakashiba tu, ila kulikuwa na vyakula vilivyobaki. Maandiko yanasema: “Baada ya kushiba, alisema kwa wanafunzi wake, Ninyi kusanyeni vipande ambavyo vimebaki, ndiyo chochote kisipotezwe. Kwa hivyo walivikusanya pamoja, na wakavijaza vikapu kumi na mbili na vipande vya mikate mnitano ya shayiri vilivyobaki baada ya wale watu kula.” Muujiza huu uliwaruhusu watu kutambua utambulisho na hadhi ya Bwana Yesu, na uliwaruhusu pia kuona kwamba hakuna kisichowezekana kwa Mungu—waliuona ukweli wa kudura ya Mungu. Mikate mitano na samaki wawili viliweza kutosha kuwalisha watu elfu tano lakini kama kusingekuwa na chakula chochote, Mungu angeweza kuwalisha watu hao elfu tano? Bila shaka Angeweza! Huu ulikuwa muujiza, hivyo basi bila shaka watu walihisi hali hii kutoeleweka na wakahisi kwamba haikuaminika na iliwashangaza lakini kwa Mungu kufanya kitu kama hicho halikuwa kitu. Kwa sababu hili lilikuwa jambo la kawaida kwa Mungu, kwa nini litengwe ili liweze kufasiriwa? Kwa sababu kile kilichomo nyuma ya muujiza huu kimebeba mapenzi ya Bwana Yesu, ambayo hayajawahi kugunduliwa na wanadamu.

Kwanza, hebu tujaribu kuelewa watu hawa elfu tano walikuwa wa aina gani. Walikuwa wafuasi wa Bwana Yesu? Kutoka kwa Maandiko, tunajua kwamba hawakuwa wafuasi Wake. Walijua Bwana Yesu alikuwa nani? Bila shaka hawakujua! Kwa kiwango cha chini sana, hawakujua yule mtu aliyekuwa amesimama mbele yao alikuwa Kristo, au pengine baadhi ya watu walijua tu jina Lake lilikuwa nani, na kujua kitu kumhusu Yeye au walikuwa wamesikia kitu kuhusu mambo aliyokuwa Amefanya. Walikuwa na mshawasha tu kuhusu Bwana Yesu kutoka katika hadithi, lakini bila shaka hamwezi kusema kwamba wao walimfuata Yeye, wala hata Kumwelewa. Bwana Yesu alipowaona watu hawa elfu tano, walikuwa na njaa na Angefikiria tu kuwalisha hadi washibe, na hivyo basi ilikuwa katika muktadha huu ndipo Bwana Yesu aliporidhisha matamanio yao. Baada ya kuyaridhisha matamanio yao, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Mwelekeo Wake kwa watu hawa waliotaka tu kula hadi kushiba ulikuwa upi? Wakati huu, fikira na mwelekeo Wake Bwana Yesu lazima ungehusu tabia ya Mungu na hali Yake halisi. Kuwa mbele ya watu hawa elfu tano waliokuwa na njaa na ambao walitaka tu kula chakula hadi kushiba, kuwa mbele ya watu hawa waliojaa mshawasha na matumaini kumhusu, Bwana Yesu alifikiria tu kutumia muujiza huu ili kuwatolea neema. Hata hivyo, Hakujipa tumaini sana kwamba watakuwa wafuasi Wake, kwani Alijua walitaka kujiunga na furaha hiyo na kuweza kula hadi kushiba, hivyo basi Aliweza kutumia kwa njia bora zaidi kile Alichokuwa nacho hapo, na Akatumia mikate mitano na samaki wawili kuwalisha watu elfu tano. Aliwafumbua macho watu hawa waliofurahia burudani hiyo, waliotaka kuiona miujiza, na wakaona kwa macho yao mambo yale ambayo Mungu mwenye mwili Angeweza kukamilisha. Ingawa Bwana Yesu alitumia kitu kinachoweza kushikika ili kuridhisha mshawasha wao, tayari Alijua katika moyo Wake kwamba watu hawa elfu tano walitaka tu kuwa na mlo mzuri, hivyo basi Hakusema chochote kamwe au kuwahubiria kamwe—Aliwaacha tu kuuona muujiza ukifanyika. Bila shaka Asingeweza kuwashughulikia watu hawa kwa njia sawa ambayo aliwashughulikia wanafunzi Wake ambao walimfuata Yeye kwa kweli, lakini katika moyo wa Mungu, viumbe vyote vilikuwa katika utawala Wake, na Angeviruhusu viumbe vyote katika macho Yake kufurahia neema ya Mungu kila ilipohitajika. Hata ingawa watu hawa hawakujua Yeye alikuwa nani au kumwelewa, au kuwa na picha yoyote fulani kumhusu au kutoa shukrani Kwake hata baada ya kula mikate na samaki, hili halikuwa jambo ambalo Mungu Alijali kuhusu—Aliwapa watu hawa fursa nzuri ya kufurahia neema ya Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba Mungu ana kanuni katika kile Anachofanya, na kwamba Hawaangalii wala kuwalinda wale wasioamini, na Yeye hasa hawaruhusu kufurahia neema Yake. Je, hivyo ndivyo ilivyo kwa hakika? Machoni mwa Mungu, mradi tu viwe ni viumbe vyenye uhai ambavyo Yeye Mwenyewe aliviumba, Ataweza kuvisimamia na kuvitunza; Atavitunza, Atavipangia, na Atavitawala katika njia tofauti. Hizi ndizo fikira na mtazamo wa Mungu kwa mambo yote.

Ingawa watu hawa elfu tano walioila mikate hiyo na samaki hawakupanga kumfuata Bwana Yesu, Hakuwa mkali kwao; baada ya wao kula hadi kushiba, je, mwajua kile Alichofanya Bwana Yesu? Je, Aliwahubiria chochote? Alienda wapi baada ya haya? Maandiko hayarekodi kwamba Bwana Yesu alisema chochote kwao; Alipokamilisha kutenda muujiza Wake Aliondoka kimya kimya. Hivyo basi Aliwawekea mahitaji yoyote watu hawa? Kulikuwa na chuki yoyote? Hakukuwepo na chochote kati ya hizi—Yeye hakutaka tu kutilia maanani akili yoyote kwa watu hawa ambao wasingeweza kumfuata, na kwa wakati huu moyo Wake ulikuwa katika maumivu. Kwa sababu alikuwa Ameuona upungufu wa wanadamu na Alikuwa amehisi namna ambavyo wanadamu walivyomkataa, na Alipowaona watu hawa au Alipokuwa na wao, upumbavu wa binadamu na kutojua kwao kulimfanya awe na huzuni sana na kukamwacha na maumivu katika moyo Wake, hivyo basi Alitaka tu kuwaacha watu hawa haraka iwezekanavyo. Bwana hakuwa na mahitaji yoyote kwao katika moyo Wake, Hakutaka kuwatilia maanani, Yeye hasa hakutaka kutumia nguvu Zake zozote kwao, na Alijua kwamba wasingeweza kumfuata—licha ya haya yote, mtazamo Wake kwao ulikuwa bado wazi kabisa. Alitaka tu kuwashughulikia kwa huruma, kuwarudishia neema—huu ndio uliokuwa mtazamo wa Mungu kwa kila kiumbe kilicho katika utawala Wake: kwa kila kiumbe, kishughulikie kwa huruma, watoshelezee mahitaji yao, wawaruzuku wao. Kwa sababu hasa ambayo Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, Aliweza kwa hali ya kimaumbile sana kufichua kiini cha Mungu binafsi na kuwashughulikia watu hawa kwa huruma. Aliwatendea kwa ukarimu na moyo wa rehema na uvumilivu. Haijalishi ni vipi watu hawa walimwona Bwana Yesu, na haikujalisha ni aina gani ya matokeo ambayo yangekuwepo, Alikitendea tu kila kiumbe kutokana na nafasi Yake kama Bwana wa uumbaji wote. Kile Alichofichua kilikuwa, bila kuachwa, tabia ya Mungu, na kile Alicho nacho na kile Alicho. Kwa hivyo Bwana Yesu alifanya kitu kimya kimya, kisha Akaondoka kimya kimya—hii ni sura gani ya tabia ya Mungu? Unaweza kusema kwamba hii ni rehema ya upendo wa Mungu? Unaweza kusema kwamba Mungu ni Mwenye kujitolea? Mtu wa kawaida anaweza kufanya hivi? Bila shaka hawezi! Katika kiini, wale watu elfu tano ambao Bwana Yesu aliwalisha kwa mikate mitano na samaki wawili walikuwa kina nani? Tunaweza kusema kwamba walikuwa watu waliolingana na Yeye? Unaweza kusema kwamba wote walikuwa wakatili kwa Mungu? Inaweza kusemekana kwa uhakika kwamba hawakuwa kabisa wanaolingana na Bwana, na kiini chao halisi kilikuwa kikatili kabisa kwa Mungu. Lakini Mungu aliwashughulikia vipi? Alitumia mbinu ya kuutuliza ukatili wa watu kwa Mungu—mbinu hii inaitwa “huruma.” Yaani, ingawa Bwana Yesu aliwaona kama watendaji dhambi, machoni mwa Mungu walikuwa hata hivyo uumbaji Wake hivyo basi bado aliwashughulikia watendaji dhambi hawa kwa huruma. Huu ndio uvumilivu wa Mungu, na uvumilivu huu unaamuliwa na utambulisho na kiini cha Mungu binafsi. Hivyo basi, hili ni jambo ambalo hakuna mwanadamu aliyeumbwa na Mungu anaweza kufanya—Mungu pekee ndiye anayeweza kufanya hivi.

Unapoweza kutambua kwa kweli fikira na mtazamo wa Mungu kwa wanadamu, wakati unapoweza kuelewa kwa kweli hisia na kujali kwa Mungu kwa kila kiumbe, utaweza kuelewa kule kujitolea na upendo unaotumika kwa kila mmoja wa watu walioumbwa na Muumba. Haya yanapofanyika, utatumia maneno mawili kufafanua upendo wa Mungu—maneno hayo mawili ni yapi? Baadhi ya watu husema “mwenye kujitolea” na baadhi ya watu wakasema “kuwa na huruma nyingi ya kutoa msaada.” Kati ya kauli hizi mbili, “kuwa na huruma nyingi ya kutoa msaada” ndiyo kauli ambayo inafaa kwa kiasi kidogo zaidi kuufafanua upendo wa Mungu. Hii ni kauli ambayo watu hutumia kufafanua fikira na hisia za mtu kwa upana wa akili zake. Naichukia kweli kauli hii kwa sababu inarejelea ule utoaji wa msaada bila mpango na bila ubaguzi, bila kujali kanuni zozote. Ni maelezo ya kihisia za ziada za watu wajinga na waliochanganyikiwa. Wakati neno hili linatumika kufafanua upendo wa Mungu, bila shaka kuna nia ya kukufuru. Nina maneno mawili ambayo yanafafanua kwa usahihi zaidi upendo wa Mungu—maneno hayo mawili ni yapi? Neno la kwanza ni “kubwa.” Je, si neno hili huamsha na kuleta hisia? Neno la pili ni “pana.” Kunayo maana halisi katika maneno haya mawili mbili Ninazotumia katika kufafanua upendo wa Mungu. Kama yatachukuliwa kwa njia ya moja kwa moja, “kubwa” linafafanua ukubwa au wingi wa kitu, lakini haijalishi kitu hicho kina ukubwa gani—ni kitu ambacho watu wanaweza kugusa na kuona. Hii ni kwa sababu kipo, si kifaa cha kidhahania na kinapatia watu hisia kwamba kwa kiasi fulani kina usahihi na hali ya kimatendo. Haijalishi kama unakiangalia kutoka katika mtazamo bapa au wa pande zote tatu; huhitajiki kufikiria uwepo wake, kwa sababu ni kitu ambacho kwa kweli kipo. Hata ingawa kwa kutumia “kubwa sana” kufafanua upendo wa Mungu kunaweza kuhisiwa kana kwamba tunataka kupima wingi wa upendo Wake, lakini hata hivyo linatoa hisia kwamba hauwezi kupimwa. Nasema kwamba upendo wa Mungu unaweza kupimwa kwa sababu upendo Wake si aina fulani ya kitu kisichojulikana, wala hauchipuki tu kutoka kwa ngano yoyote. Badala yake, ni kitu cha kutumiwa kwa pamoja na vitu vyote katika utawala wa Mungu, na ni kitu cha kufurahiwa na viumbe vyote hadi kwa viwango tofauti na kutoka katika mitazamo tofauti. Ingawa watu hawawezi kukiona au kukigusa, upendo huu huleta maendelezo na maisha katika vitu vyote kwani kinafichuliwa hatua kwa hatua katika maisha yao, na wanahesabu na kushuhudia upendo wa Mungu wanaofurahia kila wakati. Nasema kwamba upendo wa Mungu hauwezi kuhesabiwa kwa sababu fumbo la Mungu la Yeye kukidhi na kuimarisha vitu vyote ni kitu ambacho ni kigumu kwa wanadamu kuelewa, kama vile tu zilivyo fikira za Mungu katika vitu vyote na hasa vile vya mwanadamu. Hivyo ni kusema hakuna anayejua damu na machozi ambayo Muumba ametoa kwa sababu ya wanadamu. Hakuna anayeweza kufahamu, hakuna anayeweza kuelewa kina au uzito wa upendo ambao Muumba anao kwa ajili ya wanadamu, aliowaumba kwa mikono Yake binafsi. Kufafanua upendo wa Mungu kama mkubwa sana ni kuwasaidia watu kutambua na kuelewa upana wake na ukweli wa uwepo wake. Iko hivyo ili watu waweze kufahamu kwa kina zaidi maana halisi ya neno “Muumba,” na ili watu waweze kupata ufahamu wa kina zaidi wa maana ya “uumbaji.” Neno “pana” kwa kawaida huwa linafafanua nini? Linatumika kwa ujumla kumaanisha bahari au ulimwengu kama vile ulimwengu mpana au bahari pana. Ule mtanuko na kina kitulivu cha ulimwengu unazidi ufahamu wa binadamu na ni kitu ambacho kinanata fikra za binadamu, ambacho kwacho wamejawa na upendezwaji. Fumbo lake na umuhimu wake vyote vimo katika uwezo wa kuonekana lakini haviwezi kufikika. Unapofikiria kuhusu bahari, unafikiria kuhusu upana wake—yaonekana isiyo na mipaka, na unaweza kuhisi ile hali ya bahari hiyo kuwa fumbo na ujumuishwaji wake pia. Ndiyo maana Nimetumia neno “pana” kufafanua upendo wa Mungu. Ni kuwasaidia watu wahisi namna neno hilo lilivyo na thamani, na ili wahisi ule urembo wa kipekee wa upendo Wake, na kwamba nguvu za upendo wa Mungu haziishi na zimeenea. Ni kwa minajili ya kuwasaidia kuhisi utakatifu wa upendo Wake, na heshima pamoja na hali ya kutoweza kukosewa ya Mungu ambayo inafichuliwa kupitia upendo Wake. Sasa unafikiri kwamba “pana” ni neno linalofaa kufafanua upendo wa Mungu? Je, upendo wa Mungu unaweza kufikia maana ya maneno haya mawili, “kubwa sana” na “pana”? Bila shaka! Katika lugha ya binadamu, maneno haya mawili tu ndiyo ambayo yanafaa kwa kiasi fulani, na kwa kiasi fulani yanakaribia kuufafanua upendo wa Mungu. Je, huoni hivyo? Kama Ningewaulizeni kuufafanua upendo wa Mungu, je, mngetumia kauli hizi mbili? Kuna uwezekano mkubwa zaidi, msingeyatumia kwa sababu ufahamu na utambuzi wenu wa upendo wa Mungu ni finyu na unafikia tu mtazamo bapa, na bado haujakwea ngazi hadi katika ule urefu wa nafasi ya pande zote tatu. Hivyo basi kama Ningetaka mfafanue upendo wa Mungu, mngehisi kwamba mnakosa maneno; huenda pengine hata mtakosa kuongea kabisa. Maneno haya mawili ambayo Nimeyazungumzia leo yanaweza kuwa magumu kwako kuelewa, au pengine kwa ufupi tu hukubali. Hali hii inaweza kuongelea tu hoja kwamba utambuzi na ufahamu wako wa upendo wa Mungu ni wa juujuu na ndani ya upana mwembamba. Nimesema awali kwamba Mungu ni mwenye kujitolea—unakumbuka neno kujitolea? Inaweza kusemekana kwamba upendo wa Mungu unaweza kufafanuliwa tu kuwa wa kujitolea? Je, si haya si mawanda membamba mno? Mnafaa kutafakari suala hili zaidi ili kuweza kufaidika kutoka kwalo.

Yale yaliyotajwa hapo juu ndiyo yale tuliyoyaona ya tabia ya Mungu na kiini Chake kutoka katika muujiza wa kwanza. Hata ingawa ni hadithi ambayo watu wameisoma kwa maelfu kadhaa ya miaka, inao mtiririko mwepesi, na inaruhusu watu kuweza kuona suala la pekee, ilhali katika mtiririko huu mwepesi tunaweza kuona kitu chenye thamani zaidi, hali ambayo ni tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Mambo haya kuwa Alicho nacho na kile Alicho yanamwakilisha Mungu Mwenyewe, na ni maelezo ya fikira za Mungu binafsi. Wakati Mungu anapoonyesha fikira Zake, ni udhihirisho wa sauti ya moyo Wake. Anatumai kwamba kutakuwa na watu wanaoweza kumwelewa Yeye, kumjua Yeye na wanafahamu mapenzi Yake, na Anatumai kutakuwa na watu wanaoweza kuisikia sauti ya moyo Wake na wataweza kushirikiana kwa bidii ili kuridhisha mapenzi Yake. Na vitu hivi ambavyo Bwana Yesu alifanya vilikuwa ni maelezo ya kimya ya Mungu.

Halafu, hebu tuuangalie dondoo hii: Kufufuka kwa Lazaro Kwatukuza Mungu.

Mnayo picha gani baada ya kusoma dondoo hii? Umuhimu wa muujiza huu ambao Bwana Yesu alitenda ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa awali kwa sababu hakuna muujiza ambao unajitokeza zaidi kuliko ule wa kufufua binadamu aliyekufa na kutoka katika kaburi. Bwana Yesu kufanya kitu kama hiki kulikuwa na umuhimu mkubwa mno katika enzi hiyo. Kwa sababu Mungu alikuwa mwili, watu waliweza kuona tu kuonekana Kwake kwa kimwili, upande Wake wa kimatendo, na upande Wake usio na umuhimu. Hata kama baadhi ya watu waliona na kuelewa hulka Yake fulani au nguvu Zake ambazo alionekana kuwa nazo, hakuna aliyejua pale ambapo Bwana Yesu alipotokea, ambaye kiini Chake cha kweli kilikuwa, na nini kingine zaidi ambacho Angeweza kufanya. Haya yote hayakujulikana kwa mwanadamu. Watu wengi mno walitaka ithibati ya kitu hiki, na kuujua ukweli. Je, Mungu angeweza kufanya kitu ili kuthibitisha utambulisho Wake Mwenyewe? Kwa Mungu, huu ulikuwa upepo mwanana—lilikuwa jambo rahisi sana. Angefanya kitu popote, wakati wowote ili kuthibitisha utambulisho na kiini Chake, lakini Mungu alifanya mambo kwa mpango, na kwa hatua. Hakufanya vitu bila mpangilio; Alitafuta muda unaofaa, na fursa inayofaa kufanya kitu chenye maana zaidi kwa wanadamu kuweza kuona. Hili lilithibitisha mamlaka Yake na utambulisho Wake. Hivyo basi, kufufuka kwa Lazaro kungeweza kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu? Hebu tuangalie kifungu hiki cha maandiko: “Na baada ya yeye kuzungumza, akasema kwa sauti kuu, Lazaro, kuja nje. Na yeye ambaye alikuwa amefariki akatoka nje.” Wakati Bwana Yesu alipofanya haya, Alisema tu jambo moja: “Lazaro, kuja nje.” Kisha Lazaro akatoka nje ya kaburi—hii ilikamilika kwa sababu ya mstari mmoja uliotamkwa na Bwana. Katika wakati huu, Bwana Yesu hakuweza kuandaa madhabahu, na Hakutekeleza hatua zote nyingine. Alisema tu jambo moja. Hili linaweza kutaitwa muujiza au amri? Au lilikuwa aina fulani wa uchawi? Kwa juujuu, yaonekana ingeweza kuitwa muujiza, na ukiangalia hali hiyo kutoka mtazamo wa kisasa, bila shaka mnaweza bado kuliita muujiza. Hata hivyo, bila shaka hali hiyo isingeweza kuitwa apizo la kuiita nafsi kurudi kutoka kwa wafu, na bila shaka si uchawi. Ni sahihi kusema kwamba muujiza huu ulikuwa ni onyesho la kawaida zaidi, dogo ajabu la mamlaka ya Muumba. Haya ndiyo mamlaka, na uwezo wa Mungu. Mungu ana mamlaka ya kumwacha mtu afe, kuruhusu nafsi yake iondoke mwilini mwake na kurudi kuzimu au popote pale itakapoenda. Mtu anapokufa, na anakokwenda baada ya kifo—haya yanaamuliwa na Mungu. Yeye anaweza kufanya haya wakati wowote na mahali popote. Yeye hazuiliwi na binadamu, matukio, vifaa, nafasi au mahali. Akitaka kulifanya Anaweza kulifanya, kwa sababu vitu vyote na viumbe vyenye uhai vinatawaliwa na Yeye, na vitu vyote vinaishi na kufa kwa neno Lake, mamlaka Yake. Anaweza kumfufua binadamu aliyekufa—pia hiki ni kitu Anachoweza kufanya wakati wowote mahali popote. Haya ndiyo mamlaka ambayo Muumbaji pekee humiliki.

Bwana Yesu alipofanya kitu kama vile kumleta Lazaro kutoka kwa wafu, lengo Lake lilikuwa ni kutoa ithibati kwa wanadamu na Shetani aweze kuona, na kuacha wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu, maisha na kifo cha wanadamu vyote vinaamuliwa na Mungu, na kwamba ingawa Alikuwa amekuwa mwili ilivyo kama siku zote, Alibaki katika mamlaka juu ya ulimwengu wa kimwili unaoweza kuonekana pamoja na ulimwengu wa kiroho ambao wanadamu hawawezi kuuona. Huku kulikuwa kuwaruhusu wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu hakiko katika amri ya Shetani. Huu ulikuwa ni ufunuo na onyesho la mamlaka ya Mungu, na ilikuwa pia njia ya Mungu kuutuma ujumbe wake kwa viumbe vyote kwamba maisha na kifo cha wanadamu kimo mikononi mwa Mungu. Bwana Yesu kumfufua Lazaro—kutenda kwa aina hii ni mojawapo ya njia za Muumba za kumfunza na kumwelekeza wanadamu. Ilikuwa ni hatua thabiti ambapo Aliutumia uwezo Wake na mamlaka Yake kuwaelekeza wanadamu, na kuwatolea wanadamu. Ilikuwa njia bila matumizi ya maneno kwa Muumba ya kuwaruhusu wanadamu kuweza kuuona ukweli wa Yeye kuwa na mamlaka juu ya viumbe vyote. Ilikuwa njia Yake ya kuwaambia binadamu kupitia kwa hatua za kimatendo kwamba hamna wokovu mbali na kupitia Yeye. Mbinu za aina hii za kimya za Yeye kuwaelekeza wanadamu zinadumu milele—hazifutiki, na iliweza kuleta katika mioyo ya wanadamu mshtuko na kupatikana kwa nuru ambayo haiwezi kufifia. Kufufuliwa kwa Lazaro kulimtukuza Mungu—hali hii inayo athari ya kina katika kila mojawapo wa wafuasi wa Mungu. Inakita mizizi kwa kila mmoja anayeelewa kwa kina tukio hili, ufahamu, maono kwamba ni Mungu tu anayeweza kuamuru maisha na kifo cha wanadamu. Ingawa Mungu ana aina hii ya mamlaka, na ingawa Aliutuma ujumbe kuhusu uhuru Wake dhidi ya maisha na kifo cha wanadamu kupitia kwa kufufuka kwa Lazaro, hii haikuwa kazi Yake ya msingi. Mungu katu hafanyi kitu bila maana. Kila kitu Anachofanya kina thamani kuu; ni hazina ya mufti. Bila shaka Yeye hatamfanya mtu kutoka katika kaburi lake kuwa sababu ya kimsingi au lengo au sababu kuu katika kazi Yake. Mungu hafanyi chochote ambacho hakina maana. Kufufuka kumoja kwa Lazaro kunatosha kuonyesha mamlaka ya Mungu. Kunatosha kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu hakurudia aina hii ya muujiza. Mungu hufanya mambo kulingana na kanuni Zake binafsi. Katika lugha ya binadamu, ingekuwa kwamba Mungu anajali kazi muhimu. Yaani, wakati Mungu anapofanya mambo Hapotoki kutoka kwenye kusudio Lake la kazi. Anajua ni kazi gani Anayotaka kutekeleza katika awamu hii, kile Anachotaka kukamilisha, na Atafanya kazi mahususi kulingana na mpango Wake. Kama mtu aliyepotoka angekuwa na aina hiyo ya uwezo, angekuwa akifikiria tu kuhusu njia za kufichua uwezo wake ili wengine wajue namna alivyokuwa thabiti, hivyo basi kumwinamia, ili aweze kuwadhibiti na kuwameza. Huu ndio uovu unaotoka kwa Shetani—huu unaitwa upotovu. Mungu hana tabia kama hiyo, na Hana kiini kama hicho. Kusudio Lake katika kufanya mambo si kujionyesha Mwenyewe, lakini kuwapa wanadamu ufunuo na mwongozo zaidi, ili watu waweze kuiona mifano michache katika Biblia kuhusu aina hii ya jambo. Hii haimaanishi kwamba uwezo wa Bwana Yesu ulikuwa finyu, au kwamba asingeweza kufanya jambo la aina hiyo. Ni kwamba Mungu hakutaka tu kulifanya jambo hilo, kwa sababu Bwana Yesu kumfufua Lazaro kulikuwa na umuhimu wa kimatendo kabisa, na pia kwa sababu kazi kuu ya Mungu kuwa mwili haikuwa ni kutenda miujiza, haikuwa ni kuwaleta watu kutoka katika kifo, lakini ilikuwa ni kazi ya ukombozi wa wanadamu. Hivyo basi, wingi wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha ilikuwa ni kuwafunza watu, kuwatoshelezea haja zao, na kuwasaidia, na mambo kama vile kumfufua Lazaro yalikuwa tu mambo madogo ya huduma ambayo Bwana Yesu alitekeleza. Hata zaidi, mnaweza kusema kwamba “kujionyesha” si sehemu ya kiini cha Mungu, hivyo basi kutoonyesha miujiza zaidi hakukuwa kujizuia kimakusudi, wala hakukuwa kwa sababu ya vizuizi vya kimazingira, na bila shaka hakukuwa kwa sababu ya ukosefu wa uwezo.

Bwana Yesu alipomleta Lazaro kutoka kwa wafu, Alitumia mstari mmoja: “Lazaro, kuja nje.” Hakusema kitu kingine mbali na hiki—maneno haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha hoja kwamba Mungu anaweza kukamilisha chochote kupitia maongezi, kukiwemo kumfufua mtu aliyekufa. Mungu alipoumba viumbe vyote, Alipouumba ulimwengu, Alifanya hivyo kwa maneno. Alitumia amri, maneno yaliyotamkwa kwa mamlaka, na hivyo tu viumbe vyote viliumbwa. Yalikamilishwa hivyo. Mstari huu mmoja uliozungumzwa na Bwana Yesu ulikuwa sawa na maneno yaliyotamkwa na Mungu alipoziumba mbingu na dunia na viumbe vyote; mstari huo pia uliweza kushikilia mamlaka ya Mungu, uwezo wa Muumba. Viumbe vyote viliumbwa na vikasimama kwa sababu ya matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu, na vivyo hivyo, Lazaro alitembea kutoka katika kaburi lake kwa sababu ya matamshi kutoka katika kinywa cha Bwana Yesu. Haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ya Mungu, yaliyoonyeshwa na kutambuliwa katika mwili Wake. Aina hii ya mamlaka na uwezo vilimilikiwa na Muumba, na kwa Mwana wa Adamu ambaye kwake Muumba alitambuliwa. Huu ndio ufahamu uliofunzwa kwa mwanadamu kwa Mungu kumleta Lazaro kutoka kwa wafu. Hayo ndiyo yote katika mada hii.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp