Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

(Sehemu ya Tatu)

Kisha, tutazungumzia hadithi ya Nuhu na namna ambavyo inahusiana na mada ya kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe.

Mnaona Mungu akimfanya nini Nuhu kwenye sehemu hii ya maandiko? Pengine kila mmoja aliyeketi hapa anajua kitu kuhusu hayo baada ya kusoma maandiko: Mungu alimfanya Nuhu kujenga safina, kisha Mungu akatumia gharika kuangamiza ulimwengu. Mungu alimruhusu Nuhu kujenga safina ili kuokoa familia yake ya wanane, kuwaruhusu kuweza kuishi, ili kuwa babu wa kizazi kifuatacho cha wanadamu. Sasa hebu tuyasome maandiko.

2. Nuhu

1) Mungu Anuia kuangamiza Ulimwengu kwa Gharika, Amwagiza Nuhu Kuijenga Safina

Mwa 6:9-14 Hivi ni vizazi vyake Nuhu: Nuhu alikuwa mtu mwenye haki na mtimilifu katika vizazi vyake, naye Nuhu alitembea na Mungu. Naye Nuhu akapata watoto watatu wa kiume, Shemu, Hamu, na Yafethi. Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, nayo dunia ilijaa vurugu. Naye Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani. Naye Mungu akasema kwake Nuhu, Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia. Ujitengenezee safina ya mbao wa mvinje; utatengeneza vyumba ndani ya safina, na uipake lami ndani na nje.

Mwa 6:18-22 Lakini na wewe nitaliimarisha agano langu; na utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako, na mke wako, na wake zao wana wako pamoja na wewe. Na kwa kila kilicho na uhai chenye mwili, utawaleta wawili wa kila aina katika safina, kuwaweka hai pamoja nawe; watakuwa wa kiume na wa kike. Kila ndege arukaye kwa aina yake, na mifugo kwa aina yake, kila kinachotambaa duniani kwa aina yake, wawili wa aina yote watakuja kwa wewe, ili uwaweke hai. Na ujichukulie chakula cha kila aina kinacholika, nawe ukikusanye kwako; na kitakuwa kwa ajili ya chakula cha ninyi, na cha wao. Nuhu alifanya hivyo; kulingana na vyote ambavyo Mungu alimwamrisha, alifanya hivyo.

Je sasa mnaelewa kwa jumla Nuhu ni nani baada ya kuzisoma fahamu hizi? Nuhu ni mtu wa aina gani? Maandishi asilia ni: “Nuhu alikuwa mtu mwenye haki na mtimilifu katika vizazi vyake.” Kulingana na uelewa wa watu wa kisasa, mtu mwenye haki wakati huo wa nyuma alikuwa mtu wa aina gani? Mtu mwenye haki anafaa kuwa mtu mtimilifu. Je, mnajua kama mtu huyu mtimilifu ni mtimilifu machoni mwa binadamu au ni mtimilifu machoni mwa Mungu? Bila shaka mtu huyu mtimilifu ni mtu mtimilifu machoni mwa Mungu na wala si machoni mwa binadamu. Haya yote ni kweli! Hii ni kwa sababu binadamu ni kipofu na hawezi kuona, na Mungu tu ndiye anayeiangalia nchi nzima na kila mmoja wetu, Mungu pekee ndiye anayejua Nuhu ni mtu mtimilifu. Hivyo basi, mpango wa Mungu wa kuuangamiza ulimwengu kwa gharika ulianza pindi tu Alipomuita Nuhu.

Katika enzi hiyo, Mungu alinuia kumuita Nuhu ili kufanya kitu muhimu sana. Kwa nini ilikuwa lazima Afanye hivyo? Kwa sababu Mungu alikuwa na mpango kwa moyo Wake wakati huo. Mpango Wake ulikuwa kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Kwa nini auangamize ulimwengu? Maandiko yanasema hivi: “Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, nayo dunia ilijaa vurugu.” Mnaona nini kutoka kwenye kauli “dunia ilijaa vurugu”? Ni ajabu duniani wakati ulimwengu na watu wake wanapotoka kwa kupindukia, na ni hivi: “dunia ilijaa vurugu.” Katika lugha ya leo, “ikajaa dhuluma” inamaanisha kila kitu kimechanganyika. Kwa binadamu, inamaanisha kwamba katika nyanja zote za maisha hakuna mpangilio, na mambo yamejaa fujo kweli na ni magumu kudhibiti. Katika macho ya Mungu, inamaanisha watu wa ulimwengu wamepotoka sana. Wamepotoka hadi kiwango gani? Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu hawezi tena kuvumilia kuangalia na hawezi tena kuwa na subira kuhusu hali hiyo. Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu anaamua kuwaangamiza. Wakati Mungu alipoamua kuuangamiza ulimwengu, Alipanga kupata mtu wa kuijenga safina. Kisha Mungu akamchagua Nuhu kufanya kitu hicho, ambacho ni kumruhusu Nuhu kuijenga safina. Kwa nini Mungu alimchagua Nuhu? Katika macho ya Mungu, Nuhu ni mtu mwenye haki na haijalishi kile ambacho Mungu atamwagiza yeye kufanya, atafanya vivyohivyo. Hii inamaanisha atafanya chochote anachoambiwa kufanya na Mungu. Mungu alitaka kumtafuta mtu kama huyu ili afanye kazi na Yeye, kukamilisha kile alichokuwa amemwaminia kufanya, kuikamilisha kazi Yake hapa duniani. Hapo nyuma, kulikuwa na mtu mwingine kando na Nuhu ambaye angekamilisha kazi hiyo? Bila shaka la! Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa pekee ambaye angeweza kukamilisha kile ambacho Mungu alikuwa amemwaminia kufanya, na hivyo Mungu alimchagua yeye. Lakini je upana na viwango vya Mungu vya kuwaokoa watu hapo nyuma vilikuwa sawa na vile vya sasa? Jibu ni bila shaka kunayo tofauti! Kwa nini Nauliza hivi? Nuhu alikuwa ndiye mwanaume pekee mwenye haki katika macho ya Mungu wakati huo, kwa dokezo watoto wake wa kiume na mke na wakwe wake wote hawakukuwa watu wenye haki, lakini Mungu aliwalinda watu hawa kwa sababu ya Nuhu. Mungu hakuwataka wao kufanya kile anachowataka watu kufanya leo, na badala yake Aliwaweka hai wanachama wote wanane wa familia ya Nuhu. Walipata baraka za Mungu kwa sababu ya Nuhu kuwa mwenye haki. Kama Nuhu asingekuwepo, hakuna yeyote kati yao ambaye angekamilisha kile ambacho Mungu alikuwa amemwaminia kufanya. Hivyo basi Nuhu alikuwa ndiye mtu wa pekee ambaye alitakikana kubakia hai baada ya ulimwengu kuangamizwa wakati huo, na wale wengine walikuwa tu wafadhiliwa wa ziada. Hii inaonyesha kwamba, katika enzi kabla ya Mungu kuanza rasmi kazi Yake ya usimamizi, kanuni na viwango ambavyo Alishughulikia watu na kuwadai mahitaji vilikuwa vimelegezwa kidogo. Kwa watu wa leo, namna ambavyo Mungu alivyoshughulikia familia ya Nuhu ya watu wanane yaonekana kukosa haki. Lakini tukilinganisha na wingi wa kazi ambayo Yeye Anafanya kwa watu na kiwango cha neno Lake Analopitisha, namna Mungu alivyoshughulikia familia ya Nuhu ya watu wanane ilikuwa tu ni kanuni ya kazi Yake aliyoifanyia katika usuli wa kazi Yake wakati huu. Kwa kulinganisha, familia ya Nuhu ya watu wanane ndio ilipokea mengi zaidi kutoka kwa Mungu au ni watu wa Mungu ndio waliopokea?

Kwamba Nuhu aliitwa ni ukweli mdogo, lakini hoja kuu ya kile tunachozungumzia sasa—tabia ya Mungu, mapenzi Yake kiini Chake halisi katika rekodi hii—si rahisi. Ili kuelewa dhana hizi mbalimbali za Mungu lazima kwanza tuelewe ni mtu wa aina gani ambaye Mungu hutamani kuita, nakupitia hii, tuweze kuelewa tabia yake, mapenzi yake na kiini chake halisi. Kufanya hivi ni muhimu. Hivyo katika macho ya Mungu, mtu huyu ni wa aina gani ambaye yeye humwita? Huyu lazima awe ni mtu anayeweza kuyasikiza maneno Yake. Wakati huohuo, lazima mtu huyu awe yule wa kuwajibika, mtu atakayetekeleza neno la Mungu kwa kuliona kuwa jukumu na wajibu ambao anahitajika kukamilisha. Basi mtu huyu anahitajika kuwa mtu anayemjua Mungu? La. Hapo nyuma, Nuhu hakuwa ameyasikia sana mafundisho ya Mungu wala kupitia kazi yoyote ile ya Mungu. Hivyo basi, maarifa ya Nuhu kumhusu Mungu yalikuwa madogo mno. Ingawaje imerekodiwa hapa kwamba Nuhu alitembea na Mungu, aliwahi kuiona nafsi ya Mungu? Jibu ni bila shaka la! Kwa sababu katika siku hizo, wajumbe wa Mungu tu ndio waliowaendea watu. Ingawa waliweza kuwakilisha Mungu katika kusema na kufanya mambo, walikuwa wakipitisha tu mapenzi na nia Zake. Nafsi ya Mungu haikufichuliwa kwa binadamu uso kwa macho. Kwenye sehemu hii ya maandiko, chote tunachoona tu ni kile ambacho mtu huyu Nuhu alilazimika kufanya na maagizo ya Mungu kwake yalikuwa gani. Hivyo basi ni kiini kipi kilichoonyeshwa na Mungu hapa? Kila kitu anachofanya Mungu kimepangiliwa kwa uhakika. Anapoona jambo au hali ikitokea, kutakuwa na kiwango cha kulipima jambo hilo katika macho Yake, na kiwango hiki kitaamua kama Ataanza mpango wa kulishughulikia au namna ya kuchukulia jambo na hali hii. Yeye anajali na ana hisia kwa kila kitu. Kwa hakika ni kinyume kabisa cha mambo. Kunao mstari hapa ambao Mungu alimwambia Nuhu: “Kikomo cha kila aliye na mwili kimekuja mbele zangu Mimi; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia.” Katika maneno ya Mungu wakati huu, Alisema kwamba Angeangamiza binadamu tu? La! Mungu Alisema kwamba Angeangamiza viumbe wote hai wenye mwili. Kwa nini Mungu alitaka kuangamiza? Kunao ufunuo mwingine wa tabia ya Mungu hapa: Katika macho ya Mungu, kunayo mipaka ya subira yake kwa kupotoka kwa binadamu, kwa uchafu, vurugu, na kutotii kwa mwili wote. Mipaka Yake ni ipi? Ni kama vile alivyosema Mungu: “Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani.” Kauli hii “kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani” inamaanisha nini? Inamaanisha kiumbe yeyote hai, wakiwemo wale waliofuata Mungu, wale walioita jina la Mungu, wale waliowahi kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu, wale waliomtambua Mungu kwa vinywa vyao na hata kumsifia Mungu—pindi tabia yao ilipojaa upotovu na kufikia macho ya Mungu, basi ingemlazimu kuwaangamiza. Hiyo ndiyo ilikuwa mipaka ya Mungu. Hivyo basi ni hadi kiwango kipi Mungu alibakia kuwa mwenye subira kwa binadamu na upotovu wa mwili wote? Hadi katika kiwango ambacho watu wote, wawe wafuasi wa Mungu au wasioamini, walikuwa hawatembelei njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu alikuwa hajapotoshwa tu katika maadili na mwenye wingi wa maovu, lakini pia pale ambapo hakukuwa na mtu aliyesadiki uwepo wa Mungu, tupilia mbali yeyote aliyesadiki kuwa ulimwengu unatawaliwa na Mungu na kwamba Mungu anaweza kuwaletea watu nuru na njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu aliudharau uwepo wa Mungu, na hakumruhusu Mungu kuwepo. Pindi upotovu wa mwanadamu ulipofikia kiwango hiki, Mungu asingeweza tena kuwa na subira. Ni nini kingechukua nafasi yake? Kuja kwa hasira ya Mungu na adhabu ya Mungu. Huu haukuwa ufunuo kiasi wa tabia ya Mungu? Katika enzi hii ya sasa, yupo bado binadamu mwenye haki katika macho ya Mungu? Yupo bado binadamu mtimilifu katika macho ya Mungu? Enzi hii ndiyo ile ambayo tabia ya miili yote duniani imepotoka mbele ya macho ya Mungu? Katika siku na enzi hii, mbali na wale Mungu anataka kuwafanya kuwa kamili, wale wanaoweza kumfuata Mungu na kuukubali wokovu Wake, huoni kwamba watu wote wa mwili wanapatia changamoto ile mipaka ya subira ya Mungu? Si kila kitu kinachofanyika kando yenu, kila mnachoona kwa macho yenu, na kusikia kwa masikio yenu, na kupitia ninyi binafsi kila siku katika ulimwengu huu kimejaa vurugu? Katika macho ya Mungu, si ulimwengu kama huu, enzi kama hii, inafaa kukomeshwa? Ingawaje usuli wa enzi ya sasa ni tofauti kabisa na usuli wa enzi ya Nuhu, hisia na hasira Alizo nazo Mungu kwa kupotoka kwa binadamu inabakia ileile sawa na ilivyokuwa wakati huo. Mungu anaweza kuwa mwenye subira kwa sababu ya kazi Yake, lakini kulingana na hali na masharti ya aina yote, ulimwengu huu unafaa kuwa uliangamizwa kitambo katika macho ya Mungu. Hali imepita na kupitiliza ile iliyokuwa hapo nyuma wakati ulimwengu uliangamizwa na gharika. Lakini tofauti ni nini? Hili ndilo jambo jingine linalohuzunisha moyo wa Mungu zaidi, na pengine kitu ambacho hakuna yeyote kati yenu anaweza kutambua.

Alipokuwa akiuangamiza ulimwengu kwa gharika, Mungu angemwita Nuhu ili kuijenga safina na kufanya baadhi ya kazi ya matayarisho. Mungu angemwita binadamu mmoja—Nuhu—kumfanyia misururu hii ya mambo. Lakini kwenye enzi ya sasa, Mungu hana mtu yeyote wa kumuita. Kwa nini hivyo? Kila mmoja aliyeketi hapa pengine anaelewa na kujua sababu vizuri sana. Je, mngependa Mimi niweze kuiweka wazi? Kuitaja kwa sauti huenda kukawaaibisha na kufanya kila mmoja kukasirika. Baadhi ya watu wanaweza kusema: “Ingawaje sisi si watu wenye haki na wala sisi si watu watimilifu kwenye macho ya Mungu, kama Mungu atatuelekeza sisi kufanya kitu, bado tutaweza kukifanya. Kabla, Aliposema janga kuu lilikuwa likija, tulianza kutayarisha chakula na vitu ambavyo tungehitaji wakati wa janga hilo. Si haya yote yalifanywa kulingana na mahitaji ya Mungu? Si tulikuwa tukishirikiana kwa hakika na kazi ya Mungu? Mambo haya tuliyofanya hayawezi kulinganishwa na kile Nuhu alifanya? Kwani kufanya kile tulichofanya si utiifu wa kweli? Kwani hatukuwa tunafuata maagizo ya Mungu? Kwani hatukufanya kile Mungu alichosema kwa sababu tunayo imani katika maneno ya Mungu? Basi kwa nini Mungu angali na huzuni? Kwa nini Mungu anasema Hana mtu wa kumwita?” Kunao tofauti wowote kati ya vitendo vyenu na vile vya Nuhu? Tofauti ni nini? (Kutayarisha chakula leo kwa minajili ya janga kulikuwa nia yetu binafsi.) (Matendo yetu hayawezi kufikia yale ya “haki,” ilhali Nuhu ni mtu mwenye haki mbele ya macho ya Mungu.) Kile mlichosema hakiko mbali sana na ukweli. Kile alichofanya Nuhu ni tofauti sana kulingana na kile watu wanafanya sasa. Wakati Nuhu alipofanya kama vile Mungu alivyomwagiza hakujua nia za Mungu zilikuwa nini. Hakujua ni nini ambacho Mungu Alitaka kukamilisha. Mungu alikuwa amempa tu amri, Akamwagiza afanye kitu, lakini bila ya maelezo mengi, na akaendelea mbele na kukifanya. Hakujaribu kuelewa kwa siri nia za Mungu zilikuwa nini, wala hakumpinga Mungu au kuwa na fikira mbili kuhusu jambo hilo. Alienda tu na kuifanya vilivyo kwa moyo safi na rahisi. Chochote ambacho Mungu alimruhusu kufanya alifanya, na kutii na kusikiliza neno la Mungu vyote vilikuwa ni imani yake ya kufanya mambo. Hivyo ndivyo alivyokuwa mnyofu na mwepesi wa kushughulikia kile ambacho Mungu alimwaminia kufanya. Kiini chake—kiini cha vitendo vyake kilikuwa ni utiifu, sio kutarajia kwa kukisia, sio kupinga, na zaidi; kutofikiria kuhusu maslahi yake binafsi na faida zake na hasara zake. Zaidi ya hayo, wakati Mungu Aliposema angeuangamiza ulimwengu kwa mafuriko, hakuuliza ni lini au kujaribu kulielewa jambo hilo kwa ujumla, na bila shaka hakumuuliza Mungu namna hasa alivyopanga kuangamiza ulimwengu. Alifanya tu kama Mungu alivyomwagiza. Njia yoyote ile aliyotaka Mungu, safina hiyo iweze kujengwa na hasa kujengwa na nini, alifanya tu vile ambavyo Mungu alimwomba na pia akaanza kazi mara moja. Alifanya hivyo kwa mwelekeo wa kutaka kutosheleza Mungu. Je, alikuwa akifanya hivyo kujisaidia yeye kuepuka janga? La. Je, alimwuliza Mungu ni baada ya muda gani zaidi kabla ulimwengu ungeangamizwa? Hakuuliza. Je, alimwuliza Mungu au alijua ingechukua muda gani kuijenga safina? Hakujua hilo pia. Alitii tu, akasikiliza, na kufanya hivyo inavyohitajika. Watu wa sasa si sawa: Pindi tu taarifa fulani inapojitokeza kupitia kwa neno la Mungu, pindi tu watu wanapohisi ishara ya kutatizwa au matatizo, wote watachukua hatua mara moja, haijalishi ni nini, au gharama husika, ili kutayarisha kile ambacho watakula, kunywa, na kutumia athari za baadaye, hata kupanga njia za wao kutoroka wakati janga litakapovamia. Hata ya kuvutia zaidi ni kwamba, wakati huu muhimu, akili za binadamu zinakuwa zenye “manufaa sana.” Katika hali ambazo Mungu hajanipa maagizo yoyote, binadamu anaweza kupanga kila kitu kwa njia inayofaa. Mngeweza kutumia neno “sahihi” ili kuielezea. Na kuhusiana na kile Mungu anachosema, nia za Mungu ni nini, au kile Mungu anataka ni nini, hakuna anayejali na hakuna anayejaribu kukitambua. Je, hii siyo tofauti kubwa zaidi kati ya watu wa leo na Nuhu?

Katika rekodi hii ya hadithi ya Nuhu, mnaona sehemu ya tabia ya Mungu? Kunacho mpaka kwa subira ya Mungu kwa upotovu, uchafu, na vurugu la binadamu. Anapofikia ule mpaka, Hatawahi tena kuwa na subira na badala yake Ataanza usimamizi Wake mpya na mpango mpya, kuanza kufanya kile ambacho lazima Afanye, kufichua matendo Yake na upande ule mwingine wa tabia Yake. Kitendo hiki Chake si cha kuonyesha kwamba lazima Asiwahi kukosewa na binadamu au kwamba Yeye amejaa mamlaka na hasira, na wala si kuonyesha kwamba Anaweza kuangamiza binadamu. Ni kwamba tabia Yake na kiini chake takatifu ambacho hakiwezi tena kuruhusu, hakina tena subira kwa aina hii ya binadamu kuishi mbele Yake, kuishi chini ya utawala Wake. Hivyo ni kusema, wakati wanadamu wote wako dhidi Yake, wakati hakuna mtu yeyote Anayeweza kuokoa katika ulimwengu mzima, Hatakuwa tena na subira kwa binadamu kama hawa, na Ataweza, bila ya utundu wowote, kutekeleza mpango Wake—kuangamiza binadamu wa aina hii. Kitendo kama hicho cha Mungu kinaamuliwa na tabia Yake. Hii ni athari inayohitajika, na athari ambayo kila kiumbe aliyeumbwa chini ya utawala wa Mungu lazima ashuhudie. Je, haya hayaonyeshi kwamba katika enzi ya sasa, Mungu hawezi kusubiri kukamilisha mpango Wake na kuokoa watu Anaotaka kuokoa? Katika hali hizi, Mungu anajali kuhusu nini zaidi? Si vile wale wasiomfuata Yeye kabisa au wale wanaompinga Yeye kwa vyovyote vile wanamshughulikia Yeye au kumpinga Yeye, au namna ambavyo mwanadamu anamdanganya Yeye. Anajali tu kuhusu kama wale wanaomfuata Yeye, walengwa wa wokovu Wake katika mpango Wake wa usimamizi, wamewekwa kamili na Yeye, na kama wametimiza utoshelezi Wake. Kuhusiana na watu wale wengine bali na wale wanaomfuata Yeye, Anawatolea tu adhabu kidogo mara kwa mara ili kuonyesha ghadhabu Yake. Kwa mfano tsunami, mitetemeko ya ardhi, kuibuka kwa volkano na kadhalika. Wakati huohuo, Anawalinda kwa dhati na kuwashughulikia wale wanaomfuata Yeye na karibu wanaokolewa na Yeye. Tabia ya Mungu ni hii: Kwa mkono mmoja, Anaweza kuwapatia watu Anaonuia kutekeleza subira na ustahimilivu kamili wa kupindukia na kuwasubiria wao kwa muda mrefu Anavyoweza; kwa mkono mwingine, Mungu anachukia na kuchukizwa kwa dhati na watu wa aina ya Shetani wasiomfuata Yeye na wanaompinga Yeye. Ingawaje Hajali kama hawa watu wa aina ya Shetani wanamfuata au wanamwabudu Yeye, bado Anawachukia wao huku akiwa na subira na wao katika moyo Wake, na Anapoamua mwisho wa hawa watu wa aina ya Shetani, Yeye pia anasubiria kufika kwa hatua za mpango Wake wa usimamizi.

Hebu tuangalie kifungu kinachofuata.

2) Baraka za Mungu kwa Nuhu Baada ya Gharika

Mwa 9:1-6 Naye Mungu akawabariki Nuhu na wana wake, na akasema kwao, Ninyi Zaeni, na muongezeke, na muijaze tena dunia. Na wanyama wote wa dunia watawaogopa na kuwa na hofu nanyi, na ndege wote wa angani, na vyote vitembeavyo duniani, na kila samaki wa baharini; wamewekwa katika mikono yenu. Kila kisongacho kilicho na uhai kitakuwa chakula chenu, jinsi ambavyo nimewapa mboga ndivyo ninavyowapa vitu vyote. Lakini nyama iliyo na uhai, ambayo ni damu yake, ninyi msiile. Na bila shaka nitahitaji damu yenu ya uhai wenu, nitaihitaji kwa mkono wa kila mnyama, na kwa mkono wa mwanadamu, nitahitaji uhai wa mwanadamu kwa mkono wa ndugu wa kila mwanadamu. Yeyote ambaye atamwaga damu ya mwanadamu, damu yake itamwagika na mwanadamu: kwa kuwa Mungu alimfanya mwanadamu kwa mfano wake.

Ni nini mnachoona katika kifungu hiki? Kwa nini Nikachagua mistari hii? Kwa nini Sikuchukua dondoo la Nuhu na maisha ya familia yake kwenye safina? Kwa sababu maelezo haya hayana muunganisho mwingi na mada ambayo tunawasiliana leo. Kile tunachotilia maanani ni tabia ya Mungu. Kama mnataka kujua kuhusu maelezo hayo, basi mnaweza kuchukua Biblia ili muweze kujisomea wenyewe. Hatutaizungumzia hiyo hapa. Kitu kikuu tunachozungumzia leo ni kuhusu namna ya kujua matendo ya Mungu.

Baada ya Nuhu kukubali maagizo ya Mungu na kujenga safina na kuishi katika siku zile husika Mungu alitumia gharika ili kuangamiza ulimwengu, familia yake nzima ya wanane ilinusurika. Mbali na familia ya Nuhu ya wanane, wanadamu wote waliangamizwa, na viumbe wote nchini wakaangamizwa. Kwa Nuhu, Mungu alimpa baraka, na akasema baadhi ya mambo kwake na watoto wake wa kiume. Mambo haya yalikuwa yale ambayo Mungu alikuwa akimpa yeye na pia baraka zake kwake yeye. Hizi ndizo baraka na ahadi Mungu humpa yule ambaye anaweza kumsikiliza Yeye na kuyakubali maagizo Yake, na pia namna anavyotuza watu. Hivi ni kusema, haijalishi kama Nuhu alikuwa binadamu mtimilifu au alikuwa binadamu mwenye haki mbele ya macho ya Mungu, na haijalishi ni kiwango kipi alichomjua Mungu, kwa ufupi, Nuhu na watoto wake wa kiume watatu wote waliyasikiliza maneno ya Mungu, wakaratibu na kazi ya Mungu, na kufanya kile walichofaa kufanya kulingana na maagizo ya Mungu. Kutokana na hayo, walimsaidia Mungu kuweza kubakiza binadamu na aina mbalimbali za viumbe walio na uhai baada ya kuangamizwa kwa ulimwengu na gharika, na hivyo wakawa wamefanya mchango mkubwa kwa hatua iliyofuata ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Kwa sababu ya kila kitu alichokuwa amefanya, Mungu alimbariki. Pengine kwa watu wa leo, kile alichofanya Nuhu hakikuwa sana na thamani ya kutajwa. Baadhi wanaweza hata kufikiria: Nuhu hakufanya chochote; Mungu alikuwa ameamua akilini Mwake kumhifadhi, hivyo kwa hakika angehifadhiwa. Kuwepo kwake si kwa sababu yake. Hili ndilo jambo ambalo Mungu alitaka lifanyike, kwa sababu binadamu ni mtulivu. Lakini hicho sicho Mungu alikuwa anafikiria. Kwa Mungu, haijalishi kama mtu ni mkubwa au asiye wa maana, mradi tu aweze kumsikiliza Yeye, kutii maagizo Yake na kile anachomwaminia na aweze kushirikiana na kazi Yake, mapenzi Yake, na mpango Wake, ili mapenzi Yake na Mpango Wake iweze kukamilika vizuri, basi mwenendo wake unastahili kukumbukwa na Yeye na kustahili kupokea baraka Zake. Mungu huthamini sana watu kama hao, na Yeye Hupenda sana vitendo vyao na upendo wao na huba yao Kwake. Huu ndio mwelekeo wa Mungu. Hivyo kwa nini Mungu alimbariki Nuhu? Kwa sababu hivi ndivyo Mungu anavyoshughulikia vitendo kama hivyo na utiifu wa mwanadamu.

Kuhusiana na baraka za Mungu kwa Nuhu, baadhi ya watu watasema: “Kama binadamu atamsikiliza Mungu na kumtosheleza Mungu, basi Mungu anafaa kumbariki binadamu. Je, hilo halifanyiki hivyo bila kusema?” Tunaweza kusema hivyo? Baadhi ya watu husema: “La.” Kwa nini hatuwezi kusema hivyo? Baadhi ya watu husema: “Binadamu hastahili kufurahia baraka za Mungu.” Hilo si sahihi kabisa. Kwa sababu wakati mtu anapokubali kile Mungu amemwaminia, Mungu anacho kiwango cha kuhukumu kama vitendo vya mtu huyu ni vizuri au vibaya na kama mtu huyu amemtii, na kama mtu huyu ametosheleza mapenzi ya Mungu na kama kile anachofanya kimeruhusiwa. Kile anachojali Mungu ni kuhusu moyo wa mtu huyu, si vitendo vyake vya juujuu. Si jambo kwamba Mungu anafaa kubariki mtu mradi tu afanye hivyo, licha ya namna anavyofanya hivyo. Huku ni kutoelewa kwa watu kumhusu Mungu. Mungu huangalia tu mwisho wa matokeo ya mambo, lakini Anatilia mkazo zaidi kuhusu namna moyo wa mtu ulivyo na namna mwelekeo wa mtu ulivyo wakati wa maendeleo ya mambo, na Anaangalia kama kunao utiifu, utiliaji maanani, na tamanio ya kumtosheleza Mungu ndani ya moyo wake. Nuhu alijua kiasi kipi kumhusu Mungu wakati huo? Kiasi hicho kilikuwa kingi kama mafundisho ya dini mnayojua sasa? Kuhusu dhana za ukweli kama vile dhana na maarifa ya Mungu, alipokea kunyunyizia na uchungaji kama ninyi? La, hakupokea! Lakini kunao ukweli mmoja ambao haupingiki: Katika fahamu, akili, na hata kina cha mioyo ya watu wa leo, dhana zao na mwelekeo wao kwa Mungu umejaa ukungu na haueleweki. Mnaweza hata kusema kwamba sehemu fulani ya watu inashikilia mwelekeo mbaya kwa uwepo wa Mungu. Lakini katika moyo wa Nuhu na fahamu yake, uwepo wa Mungu ulikuwepo na bila shaka, na hivyo basi utiifu wake kwa Mungu ulikuwa haujatiwa doa wala toa na ungeweza kustahimili majaribio. Moyo wake ulikuwa safi na wazi kwa Mungu. Hakuhitaji maarifa ya mafundisho ya dini mengi mno ili kujishawishi kufuata kila neno la Mungu, wala hakuhitaji ukweli mwingi kuthibitisha uwepo wa Mungu, ili akubali kile Mungu alimwaminia na kuweza kufanya chochote kile ambacho Mungu angemruhusu kufanya. Hii ni tofauti muhimu kati ya Nuhu na watu wa leo, na pia ndio ufasili wa kweli hasa kuhusu binadamu mtimilifu alivyo machoni mwa Mungu. Kile anachotaka Mungu ni watu kama Nuhu. Yeye ni aina ya mtu anayesifiwa na Mungu, na pia hasa mtu wa aina ile ambaye Mungu hubariki. Mmepokea nuru yoyote kutoka haya? Watu huangalia watu kutoka nje, huku naye Mungu anaangalia mioyo ya watu na kiini chao. Mungu hamruhusu yeyote kuwa na moyo wowote wa kukosa ari au shaka kwake Yeye, wala Hawaruhusu watu kushuku au kumjaribu Yeye kwa njia yoyote ile. Hivyo, ingawaje watu wa leo wako uso kwa uso na neno la Mungu, au mnaweza hata sema kwamba wako uso kwa uso na Mungu, kutokana na kitu kilicho ndani ya mioyo yao, uwepo wa kiini chao potovu, na mwelekeo wao wenye ukatili kwake Yeye, wamezuiliwa kutoka kwa imani yao ya kweli kwa Mungu na kuzibwa kutoka kwa utiifu wao kwake Yeye. Kwa sababu ya haya, ni vigumu sana kwao kutimiza baraka sawa ambazo Mungu alikabidhi Nuhu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp