Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) (Sehemu ya Tatu)

Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho

3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na wanaitwa tu “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni kwamba kila wakati Mungu anafanya kazi muhimu ni lazima waje—ambacho ni kitu cha kwanza kati ya vinavyowafanya maalum. Na umuhimu wao ni gani? Kuchaguliwa kwao na Mungu kunamaanisha kuwa wana umuhimu mkubwa. Yaani, Mungu angelipenda kuwafanya hawa watu timilifu, na kuwafanya wakamilifu, na baada ya kazi Yake ya usimamizi kuisha, Atawachukua watu hawa. Je, umuhimu huu si mkubwa? Kwa hiyo, hawa wateule ni wa umuhimu mkubwa kwa Mungu, kwa kuwa ni wale ambao Mungu anakusudia kuwapata. Lakini watendaji huduma—vyema, hebu tuachane na uamuzi uliokwisha kufanywa na Mungu, na kwanza tuzungumzie asili yao. Maana ya kawaida ya “mtendaji huduma” ni mtu anayehudumu. Wanaohudumu ni wa kupita; hawahudumu kwa muda mrefu, au milele, ila wanaajiriwa au kuandikwa kwa muda mfupi. Wengi wao wanachaguliwa kutoka miongoni mwa wasioamini. Wajapo duniani ndipo inapoamriwa kwamba watachukua nafasi ya watendaji huduma katika kazi ya Mungu. Wanaweza kuwa walikuwa mnyama katika maisha yao yaliyopita, lakini pia wanaweza kuwa walikuwa mmoja wa wasioamini. Hiyo ndiyo asili ya watendaji huduma.

Hebu turejee kwa wateule wa Mungu. Wanapokufa, wateule wa Mungu huenda sehemu fulani tofauti kabisa na wasioamini na watu mbalimbali wenye imani. Ni sehemu ambayo wanaambatana na malaika na wajumbe wa Mungu, na ambayo inaendeshwa na Mungu binafsi. Japo katika sehemu hii, wateule wa Mungu hawawezi kumwona Mungu kwa macho yao wenyewe, si kama sehemu nyingine yoyote katika milki ya kiroho; ni sehemu ambayo hili kundi la watu huenda baada ya kufa. Wakifa, wao pia hupitia uchunguzi mkali kutoka kwa wajumbe wa Mungu. Na ni nini kinachochunguzwa? Wajumbe wa Mungu huchunguza njia zilizopitiwa na hawa watu katika maisha yao yote katika imani yao kwa Mungu, ikiwa waliwahi au hawakuwahi kumpinga Mungu wakati huo, au kumlaani, na ikiwa walitenda au hawakutenda dhambi mbaya au maovu. Uchunguzi huu unajibu swali la ikiwa mtu fulani ataondoka au atabaki. “Kuondoka” kunarejelea nini? Na “kubaki” kunarejelea nini? “Kuondoka” kunarejelea ikiwa, kulingana na mienendo yao, watabaki miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu. “Kubaki” kunarejelea kuwa wanaweza kubaki miongoni mwa watu ambao wanafanywa na Mungu kuwa kamili katika siku za mwisho. Mungu ana mipango maalum kwa wale wanaobaki. Katika kila kipindi cha kazi Yake, Mungu atatuma watu kufanya kazi kama mitume au kufanya kazi ya kuyaamsha makanisa, au kuyahudumia. Lakini watu ambao wana uwezo wa kazi kama hizo hawapati miili mara kwa mara kama wasioamini, ambao wanazaliwa upya tena na tena; badala yake, wanarudishwa duniani kulingana na mahitaji na hatua ya kazi ya Mungu, na si wale wapatao mwili mara kwa mara. Je, kuna amri kuhusu ni lini wapate mwili? Je, wanakuja mara moja baada ya kila miaka michache? Je, wanakuja na hiyo haraka? Hawafanyi hivyo. Hii inategemea nini? Inategemea kazi ya Mungu, hatua ya kazi ya Mungu, na mahitaji Yake, na hakuna amri. Amri moja tu ni kwamba Mungu akifanya hatua ya mwisho ya kazi Yake katika siku za mwisho, wateule hawa wote watakuja. Wakija wote, hii itakuwa mara ya mwisho ambapo wanapata mwili. Na kwa nini hivyo? Hii inategemea matokeo yatakayopatikana katika hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu—kwani katika hatua hii ya mwisho ya kazi, Mungu atawafanya wateule hawa kuwa kamili kabisa. Hili linamaanisha nini? Ikiwa, katika hii awamu ya mwisho, watu hawa watafanywa kuwa kamili, na kufanywa wakamilifu, basi hawatapata mwili kama awali; mchakato wa kuwa wanadamu utakamilika kabisa, sawa na mchakato wa kupata mwili. Hili linawahusu wale watakaobaki. Je, wale ambao hawawezi kubaki huenda wapi? Wasioweza kubaki wanakuwa na sehemu mwafaka ya kwenda. Kwanza kabisa kwa sababu ya maovu yao, makosa waliyofanya, na dhambi walizofanya, wao pia wanaadhibiwa. Baada ya kuadhibiwa, Mungu anawatuma miongoni mwa wasioamini; kulingana na hali ilivyo, Atafanya mpango wawe miongoni mwa wasioamini, vinginevyo miongoni mwa watu mbalimbali wenye imani. Yaani, wana chaguzi mbili: Moja ni labda waishi miongoni mwa watu wa dini fulani baada ya adhabu, na nyingine ni wawe wasioamini. Kama watakuwa wasioamini, basi watapoteza kila fursa. Lakini wakiwa watu wa imani—kwa mfano, wakiwa Wakristo—bado wangali na nafasi ya kurudi miongoni mwa madaraja ya wateule wa Mungu; kwa hili kuna uhusiano changamano sana. Kwa ufupi, ikiwa mmoja wa wateule wa Mungu atafanya kitu kitakachomkosea Mungu, wataadhibiwa sawa tu na watu wengine. Chukulia Paulo, kwa mfano, ambaye tulizungumzia awali. Paulo ni mfano wa wale wanaoadhibiwa. Je, mnapata picha ya yale ninayozungumzia? Je, mipaka ya wateule wa Mungu ni ya kudumu? (Kwa kiasi kikubwa ni ya kudumu.) Kiasi kikubwa chake ni cha kudumu, lakini sehemu ndogo si ya kudumu. Kwa nini hivyo? (Kwa sababu wametenda maovu.) Nimerejelea hapa mfano mmoja dhahiri: kutenda maovu. Wanapotenda maovu, Mungu hawataki, na wakati Mungu hawataki, anawatupa miongoni mwa makabila na aina mbalimbali za watu, kitu ambacho kinawaacha bila tegemeo na kufanya kurudi kwao kuwe kugumu. Haya yote yanahusu mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wa Mungu.

Kinachofuata ni mzunguko wa uhai na mauti wa watendaji huduma. Tulisema asili za watendaji huduma ni gani? (Wengine walikuwa wasioamini, wengine walikuwa wanyama.) Hawa watendaji huduma walipata mwili baada ya kuwa wasioamini au wanyama. Na ujio wa hatua ya mwisho ya kazi, Mungu amechagua kundi la watu hawa kutoka kwa wasioamini, na ni kundi ambalo ni maalum. Nia ya Mungu ya kuchagua watu hawa ni kuhudumia kazi Yake. “Huduma” si neno la jamala kutamka, wala si kitu ambacho mtu yeyote angependa, lakini tunapaswa kuona ambao linawalenga. Kuna umuhimu maalum katika uwepo wa watendaji huduma wa Mungu. Hamna mwingine awezaye kuchukua nafasi yao, kwa kuwa walichaguliwa na Mungu. Na ni ipi nafasi ya watendaji huduma? Kuwahudumia wateule wa Mungu. Kwa ujumla, kazi yao ni kuihudumia kazi ya Mungu, kushirikiana na kazi ya Mungu, na kushirikiana na ukamilisho wa Mungu wa wateule Wake. Haijalishi kama wanafanya kazi ngumu, wanafanya kazi fulani, au wanajiandaa kufanya kazi fulani, ni yapi mahitaji ya Mungu kwa hawa watu? Je, anawadai sana kwa masharti Yake kwao? (La, Mungu anawataka wawe waaminifu.) Watendaji huduma pia wanapaswa kuwa waaminifu. Haijalishi asili zako, au kwa nini Mungu alikuchagua, ni lazima uwe mwaminifu: Ni lazima uwe mwaminifu kwa Mungu, kwa kile anachokuagiza, na vilevile kazi unayoiwajibikia na jukumu unalolifanya. Ikiwa watendaji huduma wanaweza kuwa waaminifu, na kumridhisha Mungu, basi hatima yao itakuwaje? Wataweza kubaki. Je, ni baraka kuwa mtendaji huduma anayebaki? Kubaki kunamaanisha nini? Hii baraka inamaanisha nini? Kihadhi, hawafanani na wateule wa Mungu, wanaonekana tofauti. Kwa hakika, hata hivyo, wakipatacho katika maisha haya siyo sawa na wakipatacho wateule wa Mungu? Angalau, katika haya maisha ni sawa. Hamlipingi hili, naam? Matamko ya Mungu, neema ya Mungu, riziki ya Mungu, baraka za Mungu—ni nani hafurahii vitu hivi? Kila mtu anafurahia wingi wa haya. Kitambulisho cha mtendaji huduma ni mtendaji huduma, lakini kwa Mungu, ni miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba—tofauti ni kwamba tu nafasi yao ni ile ya watendaji huduma. Kama mmoja wa viumbe wa Mungu, kuna tofauti kati ya watendaji huduma na wateule wa Mungu? Kwa hakika, hakuna. Kwa mazungumzo ya kawaida, kuna tofauti, katika kiini kuna tofauti, kwa kurejelea nafasi wanazoshika kuna tofauti, ila Mungu hawabagui hawa watu. Hivyo ni kwa nini hawa watu wanatambuliwa kama watendaji huduma? Unapaswa kuelewa hili. Watendaji huduma wanatokana na wasioamini. Kutaja wasioamini kunatuambia kuwa maisha yao ya awali ni mabaya: Wote ni wakana Mungu, katika maisha yao ya nyuma walikuwa wakana Mungu, hawakumwamini Mungu, na walikuwa mahasimu wa Mungu, wa ukweli, na vitu vizuri. Hawakumwamini Mungu, hawakuamini kuwa kuna Mungu, hivi wana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu? Ni haki kusema kwamba, kwa kiwango kikubwa, hawana. Sawa tu na wanyama wasivyo na uwezo wa kuelewa maneno ya mwanadamu, watendaji huduma hawaelewi Mungu anasema nini, Anahitaji nini, kwa nini Ana mahitaji kama hayo—hawaelewi, hivi vitu havieleweki kwao, wanabaki bila nuru. Na kwa sababu hii, watu hawa hawana uhai tuliouzungumzia. Je, bila uhai, watu wanaweza kuelewa ukweli? Je, wana ukweli? Je, wana uzoefu na ufahamu wa maneno ya Mungu? (La.) Hizo ndizo asili za watendaji huduma. Lakini kwa kuwa Mungu anawafanya hawa watu watendaji huduma, bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo; Hawadharau, na Hawachukulii kwa uzembe. Japo hawaelewi maneno yake, na hawana uhai, bado Mungu ni mwema kwao, na bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo. Mmevizungumzia hivi viwango hivi karibuni: Kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kufanya Asemacho. Katika huduma yako ni lazima uhudumu unapohitajika, na ni lazima uhudumu hadi mwisho. Kama unaweza kuhudumu hadi mwisho, ikiwa unaweza kuwa mtendaji huduma mwaminifu, unaweza kuhudumu hadi mwisho, na unaweza kukamilisha kazi upewayo na Mungu kikamilifu, basi utaishi maisha ya thamani, na utaweza kubaki. Ukitia bidii kidogo, ukijaribu kwa nguvu, ukiongeza maradufu jitihada zako za kumjua Mungu, ukiweza kuongea kidogo kuhusu ufahamu wa Mungu, ukiweza kumshuhudia Mungu, na zaidi, ukielewa kitu kuhusu mapenzi ya Mungu, ukiweza kushirikiana katika kazi ya Mungu, na ukiyazingatia kidogo mapenzi ya Mungu, basi wewe, mtendaji huduma, utapata bahati. Na hili litakuwa badiliko gani katika bahati? Hutaweza kubaki tu. Kutegemea tabia yako na malengo na juhudi zako binafsi, Mungu atakufanya mmoja wa wateule. Hii itakuwa bahati yako. Kwa watendaji huduma, ni nini kizuri kuhusu hili? Ni kwamba unaweza kuwa mmoja wa wateule wa Mungu. Inamaanisha nini ukiwa mmoja wa wateule wa Mungu? Inamaanisha kuwa hawatapata tena mwili kama wanyama au wasioamini. Je, hiyo ni habari njema? Ndiyo, na ni habari njema. Inamaanisha, watendaji huduma wanaweza kufinyangwa. Si kwamba kwa mtendaji huduma, Mungu akimpangia awali kuhudumu, daima atahudumu; si lazima iwe hivyo. Kutegemea tabia yake binafsi, Mungu atamtendea tofauti, na kumjibu tofauti.

Lakini kuna watendaji huduma ambao hawana uwezo wa kumtumikia Mungu hadi mwisho; wakati wa huduma yao, kuna wale ambao wanajitoa nusu na kutelekeza Mungu, kuna wale ambao hufanya mambo mengi mabaya, na hata wale ambao wanasababisha madhara makubwa na kufanya uharibifu mkubwa kwa Kazi ya Mungu, kuna hata watendaji huduma ambao humlaani Mungu, na kadhalika—na ni nini maana ya matokeo haya yasiyorekebishika? Matendo maovu yoyote kama hayo humaanisha kufikia mwisho kwa huduma yao. Kwa sababu matendo yako wakati wa huduma yamekuwa maovu sana, kwa sababu umevuka mipaka yako, wakati Mungu anaona huduma yako haijafikia kiwango Atakutoa ustahiki wa kutoa huduma, Hatakubali ufanye huduma, Atakutoa mbele ya macho Yake, na kutoka katika nyumba ya Mungu. Au ni kwamba hutaki kufanya huduma? Je, siku zote hutamani kufanya maovu? Je, siku zote wewe si mwaminifu? Sawa basi, kuna suluhisho rahisi: Utanyang’anywa ustahiki wako wa kuhudumu. Kwa Mungu, kunyang’anya mtendaji huduma ustahiki wa kufanya huduma kuna maana kuwa mwisho wa mtendaji huduma huyu umetangazwa, na hatakuwa anastahili kufanya huduma kwa Mungu tena, Mungu hahitaji huduma zake tena, na haijalishi ni vitu vipi vizuri atasema, maneno haya yatabaki ya bure. Mambo yanapofikia kiwango hiki, hii hali itakuwa isiyorekebishika; watendaji huduma kama hawa hawana njia ya kurudi nyuma. Na Mungu huwafanyia nini watendaji huduma kama hawa? Anawaachisha tu kutoa huduma? La! Je, Anawazuia tu wasibaki? Au anawaweka katika upande mmoja. Na kuwangoja wabadilike? Hafanyi hivyo. Kwa kweli Mungu hana upendo sana kwa watendaji huduma. Iwapo mtu ana aina hii ya mwelekeo katika huduma yake kwa Mungu, Mungu, kutokana na matokeo ya mwelekeo huu, Atawanyang’anya ustahiki wao wa kutoa huduma, na kwa mara nyingine kuwatupa tena miongoni mwa wasioamini. Na ni ipi hatima ya watendaji huduma waliorudishwa tena kati ya wasioamini? Ni sawa na ile ya wasioamini; kupata mwili kama wanyama na kupokea adhabu ya wasioamini katika ulimwengu wa kiroho. Na Mungu hatakuwa na maslahi ya kibinafsi katika adhabu yao, kwa kuwa hawana umuhimu wowote tena katika kazi ya Mungu. Huu si mwisho tu wa maisha yao ya imani kwa Mungu, ila mwisho wa hatima yao pia, kutangazwa kwa hatima yao. Kwa hiyo watendaji huduma wakihudumu vibaya, watapata matokeo wao wenyewe. Kama mtendaji huduma hana uwezo wa kufanya huduma hadi mwisho kabisa, au amenyang’anywa ustahiki wake wa kutoa huduma katikati ya njia, basi watatupwa miongoni mwa wasioamini—na kama watatupwa miongoni mwa wasioamini watashughulikiwa sawa na jinsi mifugo wanavyoshughulikiwa, sawa na watu wasio na akili au urazini. Ninapoielezea namna hiyo, unaelewa, naam?

Hivyo ndivyo Mungu anavyoushughulikia mzunguko wa uhai na mauti wa wateule wake na watendaji huduma. Mnajihisi vipi baada ya kusikia haya? Nimewahi kuzungumza kuhusu mada ambayo Nimeitaja sasa hivi, mada ya wateule wa Mungu na watendaji huduma? Kwa kweli Nimewahi, lakini hamkumbuki. Mungu ni mwenye haki kwa wateule wake na watendaji huduma. Kwa vyovyote vile Yeye ni mwenye haki, siyo? Kuna mahali popote unaweza kupata makosa? Wapo watu ambao watasema: “Kwa nini Mungu ni mvumilivu sana kwa wateule? Na kwa nini anawavumilia kidogo sana watendaji huduma?” Kuna yeyote angependa kuwatetea watendaji huduma? “Je, Mungu anaweza kuwapa watendaji huduma muda zaidi, na kuwa mstahimilivu na mvumilivu zaidi kwao?” Haya maneno yako sahihi? (Hapana, hayapo sahihi.) Na ni kwa nini hayapo sahihi? (Kwa kuwa tumeonyeshwa neema kweli kwa kufanywa kuwa watendaji huduma.) Watendaji huduma wameonyeshwa neema kwa kuruhusiwa kufanya huduma! Bila ya dhana “watendaji huduma,” na bila Kazi ya watendaji huduma, hawa watendaji huduma wangekuwa wapi? Miongoni mwa wasioamini, wakiishi na kufa pamoja na mifugo. Ni neema iliyoje wanayoifurahia leo, kuruhusiwa kuja mbele za Mungu, na kuja katika nyumba ya Mungu! Hii ni neema kubwa! Kama Mungu hakukupa nafasi ya kutoa huduma, usingekuwa na nafasi ya kuja mbele za Mungu. Kwa kusema machache, hata kama wewe ni Mbudha na umepata maisha ya milele, sanasana wewe ni mtumwa katika ulimwengu wa kiroho; hutaweza kamwe kumwona Mungu, au kusikia sauti Yake, au kusikia maneno Yake, au kuhisi upendo Wake na baraka Zake kwako, na hata isingewezekana kamwe kuonana na Yeye uso kwa uso. Kilicho tu mbele ya wafuasi wa Budha ni kazi rahisi. Hawawezi kamwe kumjua Mungu, na wanaitikia na kutii kiupofu tu, wakati ambapo watendaji huduma wanafaidi mengi sana katika hatua hii ya kazi. Kwanza, wanaweza kuonana na Mungu uso kwa uso, kusikia sauti Yake, kuyasikia maneno Yake, na kupitia neema na baraka Anazowapa watu. Zaidi ya hayo, wanaweza kufurahia maneno na ukweli unaotolewa na Mungu. Wanapata mengi zaidi! Mengi zaidi! Hivyo, kama mtendaji huduma, huwezi hata kufanya juhudi zilizo za kweli, je, Mungu bado atakuweka? Hawezi kukuweka. Hataki mengi kutoka kwako lakini hufanyi chochote Anachotaka vizuri, hujawajibika ipasavyo—na kwa hivyo, bila shaka, Mungu hawezi kukuweka. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Mungu hakudekezi, lakini wala Hakubagui. Mungu anafanya kazi na kanuni hizo. Mungu hutekeleza mambo jinsi hii kwa watu na viumbe wote.

Inapokuja katika ulimwengu wa kiroho, kama viumbe mbalimbali waliomo watafanya kitu kibaya, kama hawafanyi kazi yao inavyostahili, Mungu pia ana sheria za peponi na amri zifaazo kuwashughulikia—hili halipingwi. Basi, katika maelfu kadhaa ya miaka ya kazi ya usimamizi ya Mungu, wasimamizi wengine ambao walifanya maovu wameangamizwa, wengine, leo, wangali wanazuiliwa na kuadhibiwa. Hili ndilo linafaa kukabiliwa na kila kiumbe aliye katika ulimwengu wa kiroho. Kama watafanya kitu kibaya au kutenda maovu, wanaadhibiwa—ambayo ni sawa na jinsi Mungu anatenda kwa wateule Wake na watendaji huduma. Na kwa hivyo, iwe ni katika ulimwengu wa kiroho au ulimwengu yakinifu, kanuni ambazo Mungu hutekeleza matendo hazibadiliki. Bila kujali kama unaweza kuona matendo ya Mungu au la, kanuni zao hazibadiliki. Daima, Mungu amekuwa na kanuni sawa kwa jinsi Anavyotekeleza matendo kwa vitu vyote na kuvishughulikia vitu vyote. Hili halibadiliki. Mungu atakuwa mkarimu kwa wale walio miongoni mwa wasioamini ambao angalau wanaishi ipasavyo, na kuwapa nafasi wale walio katika kila dini ambao wana tabia nzuri na hawatendi maovu, kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao katika vitu vyote vinavyosimamiwa na Mungu, na kufanya kile ambacho wanafaa kufanya. Vivyo hivyo, kati ya wale wanaomfuata Mungu, kati ya wateule Wake, Mungu habagui mtu yeyote kulingana na kanuni Zake hizi. Ni mwema kwa kila mtu anayeweza kumfuata kwa dhati, na kupenda kila mtu anayemfuata kwa dhati. Ni kwamba tu kwa aina hizi mbalimbali za watu—wasioamini, aina tofauti za watu wenye imani, na wateule wa Mungu—anachowazawadia wao ni tofauti. Chukulia wasioamini: hata kama hawamwamini Mungu, na Mungu huwaona kama mifugo, miongoni mwa kila kitu kila mmoja wao ana chakula, mahali pao wenyewe, na mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti. Wanaotenda maovu wanaadhibiwa, na wanaofanya mazuri wanabarikiwa na hupokea wema wa Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo? Kwa watu wenye imani, kama wanaweza kutii hasa maadili ya kidini, kizazi baada ya kizazi, basi baada ya hivi vizazi vyote Mungu hatimaye atatoa uamuzi Wake kwao. Vivyohivyo, kwa wewe leo, awe mmoja wa wateule wa Mungu au mtendaji huduma, Mungu vilevile atakuwazisha na kuamua mwisho wako kulingana na kanuni na amri za utawala ambazo Ameziweka. Miongoni mwa aina hizi kadhaa za watu—aina tofauti za watu wa imani, walio katika dini tofauti—je, Mungu amewapa nafasi ya kuishi? Uko wapi Uyahudi? Mungu ameingilia katika imani yao? Hajaingilia, siyo? Na vipi kuhusu Ukristo? Hajaingilia pia? Anawaruhusu kufuata mipangilio yao wenyewe, na Hasemi nao, au kuwapa nuru yoyote, na, zaidi ya hayo, Hawafichulii kitu chochote: “Kama unafikiria ni sahihi, basi amini hivyo!” Wakatoliki wanamwamini Maria, na kwamba ni kupitia kwa Maria ambapo habari zilimfikia Bwana Yesu; hiyo ndiyo aina yao ya imani. Na Mungu amewahi kurekebisha imani yao? Mungu huwapa uhuru, Mungu hawasikizi, na huwapa sehemu fulani ambapo wataishi. Na kwa Waisilamu na wafuasi wa Budha, je, Yuko hivyo pia? Ameweka mipaka kwa ajili yao, pia, na kuwaruhusu kuwa na mahali pao wenyewe pa kuishi, bila ya kuingilia imani zao. Yote yamepangwa vizuri. Na unaona nini katika haya yote? Kwamba Mungu ana mamlaka, lakini hatumii vibaya mamlaka Yake. Mungu hupanga vitu vyote katika mpangilio taratibu, na ni mwenye utaratibu, na katika hili busara na kudura Zake vinadhihirika.

Leo tumezungumzia mada mpya na maalum, ambayo inahusu masuala ya ulimwengu wa kiroho, ambayo ni sehemu mojawapo ya uendeshaji na utawala wa Mungu juu ya ulimwengu wa kiroho. Mlipokuwa hamyaelewi mambo haya, huenda mlisema; “Chochote kinachohusiana na haya ni mafumbo, na hayahusiani na kuingia kwetu katika uhai; mambo haya yametenganishwa na jinsi watu wanaishi hasa, na hatutaki kuyaelewa, wala hatutamani kuyasikia. Hayana uhusiano wowote na kumfahamu Mungu.” Sasa, mnafikiria kuna shida na aina hiyo ya mawazo? Ni sahihi? (La.) Mawazo kama hayo sio sahihi, na yana matatizo makubwa. Hii ni kwa sababu, kama unatamani kujua jinsi Mungu anatawala juu ya vitu vyote, huwezi tu kuelewa kile ambacho unaweza kuona na kile unachokipata kutoka kwa mawazo yako. Ni lazima pia ufahamu ya ulimwengu ule mwingine ambao hauonekani kwako, ambao umeunganishwa kwa njia isiyochanganulika na huu ulimwengu ambao unaweza kuuona. Haya yanahusu ukuu wa Mungu, yanahusu mada ya “Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote”; ni taarifa kuhusu hayo. Bila ya hii taarifa, kungekuwepo na dosari na upungufu katika ufahamu kuhusu jinsi Mungu alivyo chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Hivyo, kile ambacho tumeongea leo kinaweza kusemwa kuwa kimetamatisha yale tuliyoyaongelea kabla, pamoja na maudhui ya “Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Baada ya kuelewa haya, mna uwezo wa kumjua Mungu kupitia maudhui haya? Na kilicho muhimu zaidi ni kwamba leo, Nimewapitisha ujumbe muhimu sana: kuhusu watendaji huduma. Ninajua mnapenda sana kusikia mada kama hizi, kwamba mnayatilia maanani sana mambo haya, basi mnahisi mmeridhika na yale Nimezungumzia leo? (Ndiyo, tumeridhika.) Mwaweza kuwa hamvutiwi sana na vitu vingine, lakini haswa mnavutiwa na mazungumzo kuhusu watendaji huduma, kwa kuwa hii mada inagusia kila moyo wa mmoja wenu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp