Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) (Sehemu ya Pili)

Mazingira ya Kuishi ya Msingi Ambayo Mungu Anawaumbia Wanadamu

3. Sauti

Kitu cha tatu ni nini? Ni kitu ambacho mazingira ya kuishi ya kawaida ya wanadamu yanatakiwa kuwa nacho. Ni kitu ambacho Mungu alishughulikia alipoumba vitu vyote. Hiki ni kitu muhimu sana kwa Mungu na pia kwa kila mtu. Kama Mungu hakushughulikia suala hilo, ingekuwa kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Hiyo ni kusema kwamba ingekuwa na athari yenye maana sana kwa mwili na maisha ya mwanadamu, kiasi kwamba wanadamu hawangeweza kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Pia inaweza kusemwa kwamba viumbe vyote vyenye uhai haviwezi kuendelea kuishi katika mazingira kama hayo. Hivyo hiki ni kitu gani? Ni sauti. Mungu aliumba kila kitu, na kila kitu kinaishi mikononi mwa Mungu. Machoni pa Mungu, vitu vyote vinasonga na vinaishi. Yaani kuwepo kwa kila mojawapo ya vitu vilivyoumbwa na Mungu kuna thamani na maana. Yaani, vyote vina umuhimu katika kuwepo kwao. Kila kitu kina uhai machoni pa Mungu; kwa kuwa vyote viko hai na vinasonga, vitatoa sauti. Kwa mfano, dunia daima inazunguka, jua daima linazunguka, na mwezi daima unazunguka pia. Sauti daima zinatolewa katika uzalishaji na kuendelea na miendo ya vitu vyote. Vitu juu ya dunia daima vinazaa, kukua na kusonga. Kwa mfano, misingi ya milima inasonga na kubadilisha nafasi, huku vitu vyote vyenye uhai katika kina cha bahari vinasonga na kuogelea. Hii inamaanisha kwamba vitu hivi vyenye uhai, vitu vyote machoni pa Mungu, vyote daima, kwa kawaida, na mara kwa mara viko katika mwendo. Hivyo ni nini kinaletwa na uzalishaji wa siri na maendeleo na miendo ya vitu hivyo? Sauti za nguvu. Mbali na dunia, kila aina ya sayari daima ziko katika mwendo, na viumbe vyenye uhai na viumbe hai juu ya sayari hizo pia daima vinazaa, vinakua na viko katika mwendo. Yaani, vitu vyote vilivyo na uhai na visivyo na uhai daima vinasonga mbele machoni pa Mungu, na pia vinatoa sauti wakati huo huo. Mungu pia ameshughulikia sauti hizi. Mnapaswa kujua sababu ya mbona sauti hizi zinashughulikiwa, sivyo? Unaposonga karibu na ndege, sauti ya kunguruma ya ndege itakufanyia nini? (Masikio yatazibwa.) Masikio yatazibwa muda unavyozidi kusonga. Je, mioyo ya watu itaweza kuistahimili? (La.) Wengine wenye mioyo hafifu hawataweza kuistahimili. Bila shaka, hata wale wenye mioyo yenye nguvu hawataweza kuistahimili ikiendelea kwa muda mrefu. Hiyo ni kusema, athari ya sauti kwa mwili wa mwanadamu, kama ni kwa masikio au moyo, ni yenye maana kabisa kwa kila mtu, na sauti ambazo ni za juu sana zitaleta madhara kwa watu. Kwa hiyo, Mungu alipoumba vitu vyote na baada ya hivyo kuanza kufanya kazi kwa kawaida, Mungu pia aliweka sauti hizi—sauti za vitu vyote vilivyo katika mwendo—kupitia kwa utendeaji wa kufaa. Hii pia ni mojawapo ya fikira muhimu alizokuwa nazo Mungu alipoumbia wanadamu mazingira.

Kwanza kabisa, kimo cha angahewa kutoka kwa uso wa dunia kitaathiri sauti. Pia, ukubwa wa utupu ndani ya mchanga, pia utaendesha na kuathiri sauti. Kisha kuna mahali mito miwili inapoungana pa mazingira mbalimbali ya kijiografia, ambapo pia pataathiri sauti. Hiyo ni kusema, Mungu hutumia mbinu fulani kuondoa sauti zingine, ili wanadamu waweze kuendelea kuishi katika mazingira ambayo masikio na mioyo yao vinaweza kustahimili. La sivyo sauti zitaleta kizuizi kikubwa kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu; zitaleta matatizo makubwa kwa maisha yao. Hili litakuwa tatizo kubwa kwao. Hiyo ni kusema, Mungu alikuwa mwenye kujali sana katika uumbaji Wake wa nchi, angahewa, na aina mbalimbali za mazingira ya kijiografia. Hekima ya Mungu iko ndani ya haya yote. Ufahamu wa wanadamu kuhusu haya hauhitaji kuwa kinaganaga sana. Kila wanachohitaji kujua ni kwamba kitendo cha Mungu kimo humo. Sasa Niambieni, je, kazi ya Mungu ya uendeshaji wa sauti ilikuwa muhimu? Je, hamwezi kuhisi umuhimu wa Mungu kufanya hili? Kazi ambayo Mungu alifanya ilikuwa kuongoza uendeshaji wa taratibu sana wa sauti ili kudumisha mazingira ya kuishi ya wanadamu na maisha yao ya kawaida. Je, kazi hii ilikuwa muhimu? (Ndiyo.) Ikiwa kazi hii ilikuwa muhimu, basi kutokana na mtazamo huu, je, inaweza kusemwa kwamba Mungu alitumia mbinu kama hii kupeana vitu vyote? Mungu aliwapa wanadamu na kuumba mazingira haya tulivu, ili kwamba mwili wa mwanadamu uweze kuishi kwa kawaida kabisa katika mazingira haya bila vizuizi vyovyote, na ili kwamba mwanadamu ataweza kuwepo na kuishi kwa kawaida. Je, hii si njia mojawapo ambayo kwayo Mungu huwapa wanadamu? Je, jambo hili alilofanya Mungu lilikuwa muhimu sana? (Ndiyo.) Lilikuwa muhimu sana. Je, ni vipi ambavyo mnashukuru hili? Hata kama hamwezi kuhisi kwamba hiki kilikuwa kitendo cha Mungu, wala hamjui vile Mungu alikifanya wakati huo, je, bado mnaweza kuhisi umuhimu wa Mungu kufanya hilo? Je, mnaweza kuhisi hekima ya Mungu au umakini na wazo Aliyoweka katika jambo hili? (Ndiyo.) Kuweza tu kuhisi hili ni sawa. Yatosha. Kuna vitu vingi ambavyo Mungu amefanya miongoni mwa vitu vyote ambavyo watu hawawezi kuhisi na kuona. Lengo la Mimi kukitaja hapa ni kuwapa tu habari kiasi kuhusu matendo ya Mungu ili muweze kuanza kumjua Mungu. Vidokezo hivi vinaweza kuwafanya mjue na kumwelewa Mungu vizuri zaidi.

4. Nuru

Kitu cha nne kinahusiana na macho ya watu—nacho ni, nuru. Hiki pia ni muhimu sana. Unapoona nuru inayong’aa, na mwangaza wa nuru hiyo ukafikia kiasi fulani, macho yako yatapofushwa. Hata hivyo, macho ya wanadamu ni macho ya mwili. Hayana kinga dhidi ya madhara. Je, kuna yeyote anayethubutu kulitazama jua moja kwa moja? (La.) Yeyote amewahi kujaribu? Watu wengine wamejaribu. Unaweza kutazama ukiwa umevaa miwani ya jua, sivyo? Hilo linahitaji usaidizi wa vifaa. Bila vifaa, macho makavu ya mwanadamu hayathubutu kutazama jua moja kwa moja. Hata hivyo, Mungu aliumba jua ili awape wanadamu nuru, na pia aliendesha nuru hii. Mungu hakuliacha tu jua na kulipuuza baada ya kuliumba. “Nani anajali iwapo macho ya mwanadamu yanaweza kulistahimili!” Mungu hafanyi vitu hivyo. Yeye hufanya vitu kwa uangalifu sana na huzingatia vipengele vyote. Mungu aliwapa wanadamu macho ili waweze kuona, lakini Mungu ametayarisha pia umbali wa mwangaza ambao wanaweza kutazama chini yake. Haitawezekana iwapo hakuna nuru ya kutosha. Iwapo kuna giza sana mpaka watu hawawezi kuona mkono wao ulio mbele yao, kisha macho yao yatapoteza kazi yake na hayatakuwa na faida yoyote. Sehemu iliyo na mwangaza mwingi itakuwa haivumiliki kwa macho ya mwanadamu na pia hawataweza kuona chochote. Hivyo katika mazingira wanayoishi ndani wanadamu, Mungu amewapa kiasi cha nuru kinachofaa macho ya wanadamu. Nuru hii haitaumiza wala kudhuru macho ya watu. Zaidi ya hayo, haitayafanya macho ya watu yapoteze matumizi yake. Hii ndiyo sababu ambayo Mungu aliongeza mawingu yanayozunguka jua na dunia, na uzito wa hewa unaweza pia kuchuja kwa kawaida nuru inayoweza kuumiza macho ya watu au ngozi. Haya yanahusiana. Kuongezea, rangi ya dunia iliyoumbwa na Mungu huakisi pia nuru ya jua na kuondoa ile sehemu ya mwangaza katika nuru inayofanya macho ya wanadamu kutokuwa na raha. Kwa njia hiyo, watu hawahitaji kila mara kuvaa miwani myeusi sana ya jua ili waweze kutembea huko nje na kufanya shughuli za maisha yao. Katika hali za kawaida, macho ya wanadamu yanaweza kuona vitu vilivyo katika eneo la kuona kwao na hayataingiliwa kati na nuru. Yaani, nuru hii haiwezi kuwa ya kuchoma sana wala ya kufifiliza, ikiwa ya kufifiliza sana, macho ya watu yatadhuriwa na hawataweza kuyatumia kwa muda mrefu sana kabla ya macho yao kuacha kutumika; ikiwa ina mwangaza sana, macho ya watu hayataweza kuistahimili, na macho yao hayataweza kutumika katika miaka ya 30 hadi 40 au miaka 40 hadi 50. Hiyo ni kusema, nuru hii inafaa kwa macho ya wanadamu kuona, na madhara yanayoletwa kwa macho ya wanadamu na nuru yamepunguzwa na Mungu kupitia kwa mbinu mbalimbali. Haijalishi ikiwa nuru huleta faida au kikwazo kwa macho ya wanadamu, inatosha kuyawezesha macho ya watu kuendelea kuishi mpaka mwisho wa maisha yao. Je, Mungu hajalifikiria hilo kikamilifu sana? Lakini wakati Shetani, ibilisi, anafanya mambo, hafikirii mambo haya. Nuru hiyo ama ina mwangaza sana au inafifiliza sana Hivi ndivyo Shetani hufanya vitu.

Mungu alifanya vitu hivi katika vipengele vyote vya mwili wa mwanadamu—kuona, kusikia, kuonja, kupumua, hisia … kuongeza hadi upeo uwezo wa kubadilisha wa kuendelea kuishi kwa wanadamu ili waweze kuishi, waweze kuishi kwa kawaida na kuendelea kuishi. Yaani ni kusema, mazingira ya kuishi kama hayo yaliyopo yaliyoumbwa na Mungu ni mazingira ya kuishi yanayofaa zaidi na yenye faida kwa kuendelea kuishi kwa wanadamu. Wengine wanaweza kufikiri kwamba hii haitoshi na kwamba yote ni ya kawaida sana. Sauti, nuru, na hewa ni vitu ambavyo watu hufikiria kwamba walizaliwa navyo, vitu wanavyoweza kufurahia tangu wakati wa kuzaliwa. Lakini kile alichofanya Mungu kinachosababisha kufurahia kwao kwa vitu hivi ni kitu wanachohitaji kujua na kuelewa. Haijalishi ikiwa unahisi kuna haja ya kuelewa au kujua vitu hivi, kwa ufupi, Mungu alipoumba vitu hivi, alikuwa ametumia fikira, Alikuwa na mpango, Alikuwa na mawazo fulani. Hakuwaweka wanadamu katika mazingira ya kuishi kama haya kwa kawaida, kwa bahati, au bila kufikiria. Huenda mkadhani kwamba kila kitu ambacho Nimezungumzia si muhimu, lakini kwa mtazamo Wangu, kila kitu ambacho Mungu aliwapa wanadamu ni muhimu kwa kuendelea kuishi kwa binadamu. Kuna tendo la Mungu katika hili.

5. Bubujiko la Hewa

Kitu cha tano ni kipi? Kitu hiki kinahusiana sana na maisha ya kila siku ya mwanadamu, na uhusiano huu thabiti. Ni kitu ambacho mwili wa mwanadamu hauwezi kuishi bila katika ulimwengu huu yakinifu. Kitu hiki ni bubujiko la hewa. “Bubujiko la hewa” ni neno ambalo watu wote labda wanaelewa. Hivyo bubujiko la hewa ni nini? Jaribuni kueleza katika maneno yenu wenyewe. (Bubujiko la hewa ni kububujika kwa hewa.) Mngesema hilo. Kububujika kwa hewa kunaitwa “bubujiko la hewa.” Bubujiko la hewa ni upepo ambao jicho la mwanadamu haliwezi kuona. Pia ni njia ambayo gesi husonga. Lakini ni bubujiko la hewa gani tunalozungumzia hapa? Mtaelewa punde Nitakaposema. Dunia hubeba milima, bahari, na vitu vyote inapogeuka, na inapogeuka kuna spidi. Hata ikiwa huwezi kuhisi kuzunguka kokote, mzunguko wake upo kweli. Mzunguko wake huleta nini? Ni nini hufanyika mtu anapokimbia? Huwa kuna upepo kando ya masikio yako unapokimbia? (Ndiyo.) Ikiwa upepo unaweza kuzalishwa unapokimbia, inawezekanaje kutokuwepo kwa nguvu za upepo dunia inapozunguka? Dunia inapozunguka, vitu vyote viko katika mwendo. Iko katika mwendo na kuzunguka katika spidi fulani, wakati vitu vyote duniani daima vinazaa na kukua. Kwa hiyo, kusonga kwa spidi fulani kwa kawaida kutaleta bubujiko la hewa. Hilo ndilo bubujiko la hewa. Bubujiko la hewa hilo litaathiri mwili wa mwanadamu kwa kiasi fulani? Taiwan na Hong Kong zote zina tufani. Tufani hizo hazina nguvu sana, lakini zinapotokea, watu hawawezi kusimama kwa utulivu na huona vigumu kutembea katika upepo huo. Ni vigumu hata kutembea hatua moja. Ina nguvu sana, baadhi ya watu wanasukumwa na upepo dhidi ya kitu na hawawezi kusonga. Hii ni mojawapo ya njia ambazo bubujiko la hewa linaweza kuathiri wanadamu. Ikiwa dunia nzima ingekuwa imejaa tambarare, ingekuwa vigumu mno kwa mwili wa binadamu kuhimili bubujiko la hewa ambalo lingezalishwa na mzunguko wa dunia na mwendo wa vitu vyote katika spidi fulani. Ingekuwa vigumu zaidi kustahimili. Ingekuwa hivyo, hili bubujiko la hewa halingeleta tu madhara kwa wanadamu, bali uharibifu. Hakuna ambaye angeweza kuendelea kuishi katika mazingira hayo. Ndio maana Mungu hutumia mazingira ya kijiografia mbalimbali kutatua aina hiyo ya bubujiko za hewa, kudhoofisha bubujiko za hewa kama hizo kwa kubadilisha mwelekeo, spidi na nguvu zake kupitia kwa mazingira mbalimbali. Ndio maana watu wanaweza kuona mazingira ya jiografia mbalimbali, kama vile milima, safu za milima, tambarare, vilima, vidimbwi, mabonde, uwanda wa juu, na mito. Mungu hutumia haya mazingira mbalimbali ya jiografia kubadilisha spidi, mwelekeo na nguvu za bubujiko la hewa, akitumia mbinu kama hiyo kupunguza au kuiendesha kuwa spidi ya upepo, mwelekeo wa upepo, na nguvu za upepo zinazofaa, ili wanadamu waweze kuwa na mazingira ya kuishi ya kawaida. Je, ni lazima kufanya hivyo? (Ndiyo.) Kufanya jambo kama hilo kunaonekana kuwa vigumu kwa wanadamu, lakini ni rahisi kwa Mungu kwa sababu Anaangalia kwa makini vitu vyote. Kwa Yeye kuumba mazingira yenye bubujiko la hewa linalofaa wanadamu ni kitu sahili sana, rahisi sana. Kwa hiyo, katika mazingira kama hayo yaliyoumbwa na Mungu, kila kitu na vitu vyote miongoni mwa vitu vyote ni vya lazima. Kuna thamani na umuhimu katika kila kuwepo kwa vitu hivyo. Hata hivyo, Shetani na wanadamu wapotovu hawaelewi aina hiyo ya falsafa. Wanaendelea kuharibu na kukuza, wakiota bure juu ya kugeuza milima kuwa ardhi tambarare, kujaza korongo kuu, na kujenga magorofa juu ya ardhi tambarare kuunda misitu ya saruji. Ni matumaini ya Mungu kwamba wanadamu wataishi kwa furaha, kukua kwa furaha, na kutumia kila siku kwa furaha katika mazingira ya kufaa zaidi Aliyowatayarishia. Ndiyo maana Mungu hajawahi kuwa mzembe inapohusu kushughulikia mazingira ya kuishi ya wanadamu. Kutoka kwa halijoto mpaka kwa hewa, kutoka kwa sauti mpaka kwa nuru, Mungu amefanya mipango na utaratibu tatanishi, ili mazingira ya kuishi ya wanadamu na miili yao visiweze kupatwa na kuharibiwa kokote kutoka kwa hali za asili, na badala yake wanadamu waweze kuishi na kuongezeka kawaida na kuishi na vitu vyote kawaida kwa kuishi pamoja kwa amani yenye kuridhisha. Hii yote inapeanwa na Mungu kwa vitu vyote na wanadamu.

Je, unaweza kuona, kutokana na jinsi Alishughulikia hali hizi tano za msingi za kuendelea kuishi kwa wanadamu, upeanaji wa Mungu kwa wanadamu? (Ndiyo.) Hiyo ni kusema kwamba Mungu aliumba msingi kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Wakati huo huo, Mungu pia anasimamia na kudhibiti vitu hivi vyote, na hata sasa, baada ya wanadamu kuwepo kwa maelfu ya miaka, Mungu bado daima anabadilisha mazingira yao ya kuishi, kupeana mazingira ya kuishi yaliyo bora zaidi na ya kufaa zaidi kwa wanadamu ili maisha yao yaweze kudumishwa kwa kawaida. Haya yatadumishwa mpaka lini? Kwa maneno mengine, Mungu ataendelea kupeana mazingira kama haya kwa muda gani? Mpaka Mungu akamilishe kabisa kazi Yake ya usimamizi. Kisha, Mungu atabadilisha mazingira ya kuishi ya wanadamu. Huenda ikawa kupitia kwa mbinu zile zile, au huenda ikawa kupitia kwa mbinu tofauti, lakini kile ambacho watu wanahitaji kujua sasa ni kwamba Mungu daima anapeana mahitaji ya wanadamu, anasimamia mazingira ya kuishi ya wanadamu, na kutunza, kuhifadhi na kudumisha mazingira ya kuishi ya wanadamu. Ni kwa sababu ya mazingira kama hayo ndiyo watu waliochaguliwa na Mungu wanaweza kuishi kwa kawaida hivyo na kukubali wokovu wa Mungu na kuadibu na hukumu. Vitu vyote vinaendelea kuwepo kwa sababu ya kanuni ya Mungu, wakati wanadamu wote wanaendelea kusonga mbele kwa sababu ya upeanaji wa Mungu kwa jinsi hii.

Je, sehemu hii ambayo Nimewasilisha sasa hivi imewaletea mawazo yoyote mapya? Je, sasa mnahisi tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu? Nani hasa ndiye bwana wa vitu vyote? Ni mwanadamu? (La.) Basi mnajua ni nini tofauti kati ya vile Mungu na wanadamu hushughulikia vitu vyote? (Mungu hutawala na kupanga vitu vyote, ilhali mwanadamu hufurahia vitu hivyo vyote.) Je, mnakubaliana na maneno hayo? (Ndiyo.) Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Kisha kutokana na mtazamo wa vitu vyote, ni nini tofauti kati ya Mungu na wanadamu? Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote. Yaani, vitu vyote vipo machoni mwa Mungu na katika eneo Lake la ukaguzi. Je, wanadamu wanaweza kuona vitu vyote? Kile ambacho wanadamu huona kimewekewa mipaka. Huwezi kuita hicho “vitu vyote”—ni tu kile wanachoona mbele ya macho yao. Ukiukwea mlima huu, unachoona ni mlima huu. Huwezi kuona kilicho upande mwingine wa mlima huo. Ukienda pwani, unaweza kuona upande huu wa bahari, lakini hujui upande ule mwingine wa bahari ulivyo. Ukiwasili katika msitu huu, unaweza kuona mimea iliyo mbele ya macho yako na inayokuzunguka, lakini huwezi kuona iliyo mbele zaidi. Wanadamu hawawezi kuona sehemu zilizo juu sana, mbali sana na kina sana. Kile wanachoweza kuona ni kilicho mbele ya macho yao na katika mpaka wa upeo wao wa kuona. Hata kama wanadamu wanajua mpangilio wa misimu minne katika mwaka na mpangilio wa ukuaji wa vitu vyote, hawawezi kusimamia au kutawala vitu vyote. Kwa upande mwingine, vile Mungu aonavyo vitu vyote ni kama vile Mungu angeona mashine Aliyotengeneza binafsi. Angejua kila kijenzi vizuri kabisa. Kanuni zake ni zipi, mipangilio yake ni ipi, na kusudi lake ni lipi—Mungu anajua vitu hivi vyote wazi na dhahiri. Kwa hiyo Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu! Hata mwanadamu akiendelea kuchunguza sayansi na sheria za vitu vyote, ni katika eneo lililowekewa mipaka pekee, ilhali Mungu anadhibiti vitu vyote. Kwa mwanadamu, hiyo ni isiyo na kikomo. Wanadamu wakichunguza kitu fulani kidogo ambacho Mungu alifanya, wangetumia maisha yao yote kukichunguza bila kupata matokeo yoyote ya kweli. Ndiyo maana ukitumia ufahamu na kile ulichojifunza kumsoma Mungu, hutaweza kamwe kujua au kuelewa Mungu. Lakini ukitumia njia ya kutafuta ukweli na kumtafuta Mungu, na kumtazama Mungu kutokana na mtazamo wa kuanza kumjua Mungu, basi siku moja utakubali kwamba matendo na hekima ya Mungu viko kila mahali, na utajua pia hasa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote na chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kadiri unavyokuwa na maarifa kama hayo, ndivyo utakavyoelewa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote. Vitu vyote na kila kitu, pamoja na wewe, daima vinapokea mtiririko thabiti wa upeanaji wa Mungu. Utaweza pia kuhisi dhahiri kwamba katika ulimwengu huu, na miongoni mwa wanadamu hawa, hakuna yeyote isipokuwa Mungu anayeweza kuwa na nguvu kama hizo na kiini kama hicho kutawala, kusimamia, na kudumisha kuwepo kwa vitu vyote. Ukitimiza ufahamu kama huo, utakubali kwa kweli kwamba Mungu ni Mungu wako. Ukifikia kiwango hiki, umemkubali Mungu kwa kweli na kumruhusu awe Mungu wako na Bwana wako. Ukiwa na ufahamu kama huo na maisha yako yakifikia kiwango kama hicho, Mungu hatakujaribu na kukuhukumu tena, wala Hatakushurutisha ufanye mambo, kwa sababu unamfahamu Mungu, unajua moyo Wake, na umemkubali Mungu kwa kweli ndani ya moyo wako. Hii ni sababu muhimu ya kuwasilisha mada hizi kuhusu utawala na usimamizi wa Mungu juu ya vitu vyote. Ni kuwapa watu maarifa na ufahamu zaidi; sio tu kukufanya ukubali, lakini kukupa maarifa zaidi na ufahamu wa utendaji wa matendo ya Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp