Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Utakatifu wa Mungu (III) (Sehemu ya Tatu)

Najua kwamba sasa watu wengi wananitarajia kusema ni nini hasa utakatifu wa Mungu, lakini Ninapozungumza kuhusu utakatifu wa Mungu Nitaongea kwanza kuhusu matendo ambayo Mungu anafanya. Nyinyi nyote mnapaswa kusikiza kwa makini, kisha nitawauliza utakatifu wa Mungu ni nini hasa. Sitawaeleza moja kwa moja, lakini badala yake nitawaacha mjaribu kuutambua, kuwapa nafasi ya kuutambua. Mnafikiri nini kuhusu mbinu hii? (Ni nzuri.) Kwa hivyo sikizeni kwa makini.

Wakati wowote Shetani anampotosha mwanadamu ama anashughulika na madhara yasiyodhibitiwa, Mungu hasimami bila kazi, wala haweki kando ama kupuuza wale ambao amechagua. Yote ambayo Shetani anafanya ni wazi kabisa na yanaeleweka na Mungu. Haijalishi anachofanya Shetani, haijalishi mwenendo anaosababisha kuibuka, Mungu anajua yote ambayo Shetani anajaribu kufanya, na Mungu hawawachi wale ambao amechagua. Badala yake, bila kuvuta macho hata kidogo, kwa siri, kwa ukimya, Mungu anafanya yote yanayohitajika. Mungu Anapoanza kufanya kazi kwa mtu, wakati amemchagua mtu, Haambii yeyote, wala Hamwambii Shetani, wala hata kufanya maonyesho makubwa. Anafanya tu kwa ukimya, kwa asili kile ambacho kinahitajika. Kwanza, Anakuchagulia familia; usuli ambao hiyo familia inao, wazazi wako ni nani, mababu zako ni nani—haya yote tayari yaliamuliwa na Mungu. Kwa maneno mengine, haya hayakuwa uamuzi wa mvuto wa ghafla yaliyofanywa na Yeye, lakini badala yake hii ilikuwa kazi iliyoanza kitambo. Baada ya Mungu kukuchagulia familia, pia Anachagua tarehe ambayo utazaliwa. Kwa sasa, Mungu anaangalia unapozaliwa katika dunia hii ukilia, Anatazama kuzaliwa kwako, Anatazama unapotamka maneno yako ya kwanza, Anatazama unapoanguka na kutembea hatua zako za kwanza, ukijifunza kutembea. Kwanza unachukua hatua moja na kisha unachukua nyingine … sasa unaweza kukimbia, sasa unaweza kuruka, sasa unaweza kuongea, sasa unaweza kuonyesha hisia zako. Mwanadamu anavyokuwa, macho ya Shetani yamewekwa kwa kila mmoja wao, kama chui mkubwa mwenye milia anavyomwangalia nyara wake. Lakini kwa kufanya kazi Yake, Mungu hajawahi kuteseka mapungufu yoyote ya watu, matukio ama mambo, ya nafasi ama wakati; Anafanya kile anachopaswa kufanya na Anafanya kile Anacholazimika kufanya. Katika mchakato wa kukua, unaweza kukutana na mambo mengi ambayo hupendi, kukutana na magonjwa na kuvunjika moyo. Lakini unapotembea njia hii, maisha yako na bahati zako ziko chini ya ulinzi wa Mungu kabisa. Mungu anakupa hakikisho halisi litakalodumu maisha yako yote, kwani Yeye yuko kando yako, anakulinda na kukutunza. Bila kujua haya, unakua. Unaanza kukutana na mambo mapya na unaanza kujua dunia hii na wanadamu hawa. Kila kitu ni kipya kwako. Unapenda kufanya mambo yako na unapenda kufanya kile unachopenda. Unaishi katika ubinadamu wako mwenyewe, unaishi katika nafasi yako ya kuishi na huna hata kiasi kidogo cha mtazamo kuhusu kuwepo kwa Mungu. Lakini Mungu anakulinda katika kila hatua ya njia unapokua, na Anakutazama unapoweka kila hatua mbele. Hata unapojifunza maarifa, ama kusoma sayansi, Mungu hajawahi toka upande wako kwa hatua hata moja. Wewe ni sawa na watu wengine kwamba, katika harakati za kuja kujua na kukutana na dunia, umeanzisha mawazo yako mwenyewe, una mambo yako mwenyewe ya kupitisha muda, mambo unayopenda mwenyewe, na pia unayo matamanio ya juu. Wakati mwingi unafikiria siku zako za baadaye, wakati mwingi ukichora muhtasari wa jinsi siku zako za baadaye zinapaswa kuwa. Lakini haijalishi kitakachofanyika njiani, Mungu anaona vyote na macho wazi. Labda wewe mwenyewe umesahau siku zako za nyuma, lakini kwa Mungu, hakuna anayeweza kukuelewa bora kuliko Yeye. Unaishi chini ya macho ya Mungu, unakua, unapevuka. Wakati huu, jukumu muhimu la Mungu ni kitu ambacho hakuna yeyote kamwe hufahamu, kitu ambacho hakuna yeyote anajua. Mungu hakika hakuambii kukihusu. Hiki kitu muhimu ni nini? Je, mnajua? (Kuleta watu mbele Yake.) Kwa hivyo Mungu anafanya nini kuleta watu mbele Yake? Analeta watu mbele Yake wakati upi? Je, mnajua? Hii ni kazi muhimu zaidi ya Mungu? Hiki ni kitu muhimu zaidi ambacho Mungu anafanya? Mtu anaweza kusema kwamba ni hakikisho kuwa Mungu atamwokoa mtu. Hii inamaanisha kwamba Mungu anataka kumwokoa mtu huyu, kwa hivyo lazima Afanye hivi, na kazi hii ni muhimu sana kwa mwanadamu na Mungu. Je, mnajua hili? Inaonekana kwamba hamna hisia yoyote kuhusu hili, ama dhana yoyote kuhusu hili, kwa hivyo nitawaambia. Kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu amefanya kazi nyingi sana kwako, lakini Hakupi maelezo moja baada ya nyingine ya kila kitu Amefanya. Mungu hakukuruhusu kujua, na Hakukwambia sivyo? Hata hivyo, kwa mwanadamu, kila kitu anachofanya Mungu ni muhimu. Kwa Mungu, ni kitu ambacho lazima Afanye. Katika moyo wake kuna kitu muhimu Anapaswa kufanya ambacho kinazidi yoyote ya mambo haya. Ni nini hicho? Yaani, kutoka alipozaliwa mwanadamu hadi sasa, Mungu lazima ahakikishe usalama wa kila mmoja wao. Baada ya kusikia maneno haya, mnaweza kuhisi kana kwamba hamwelewi kikamilifu, kusema "usalama huu ni muhimu sana?" Kwa hivyo ni nini maana halisi ya "usalama"? Labda mnauelewa kumaanisha amani ama pengine mnauelewa kumaanisha kutopitia maafa ama msiba wowote, kuishi vyema, kuishi maisha ya kawaida. Lakini katika mioyo yenu lazima mjue kwamba si rahisi hivyo. Kwa hivyo ni nini hasa kitu hiki ambacho Nimekuwa nikizungumzia, ambacho Mungu anapaswa kufanya? Usalama unamaanisha nini kwa Mungu? Kuna hakikisho lolote la usalama wenu? Kama sasa hivi? La. Kwa hivyo ni nini hiki ambacho Mungu anafanya? Usalama huu unamaanisha humezwi na Shetani. Je, jambo hili ni muhimu? Wewe humezwi na Shetani, kwa hivyo hili linahusisha usalama wako, au la? Hili linahusisha usalama wako binafsi, na hakuwezi kuwa na lolote muhimu zaidi. Baada ya wewe kumezwa na Shetani, nafsi yako wala mwili wako si vya Mungu tena. Mungu hatakuokoa tena. Mungu huacha nafsi kama hiyo na huacha watu kama hao. Kwa hivyo Nasema kitu muhimu sana ambacho Mungu anapaswa kufanya ni kuhakikishia usalama wako, kuhakikisha kwamba hutamezwa na Shetani. Hili ni muhimu kiasi, silo? Kwa hivyo mbona hamwezi kujibu? Inaonekana kwamba hamwezi kuhisi wema mkubwa wa Mungu!

Mungu anafanya mengi kando na kuhakikisha usalama wa watu, kuhakikisha kwamba hawatamezwa na Shetani; pia hufanya kazi nyingi sana kwa kutayarisha kumchagua mtu na kumwokoa. Kwanza, una tabia gani, utazaliwa kwa familia ya aina gani, wazazi wako ni nani, una kaka na dada wangapi, hali na hadhi ya kiuchumi ya familia yako ni gani, hali ya familia yako ni gani—haya yote yanapangiwa wewe kwa uangalifu na Mungu. Je, unajua ni familia ya aina gani watu waliochaguliwa na Mungu wanazaliwa ndani mara nyingi, kama inavyohusu watu wengi? Ni familia mashuhuri? Kunaweza kuwa na nyingine. Hatuwezi sema kwa uhakika hakuna yoyote, lakini kuna chache sana. Ni familia za utajiri wa kupindukia, kama yenye mabilioni ama yenye mamilioni nyingi? Mara nyingi huwa si aina hii ya familia. Kwa hivyo Mungu anapangia watu hawa familia za aina gani zaidi? (Familia za kawaida.) Kwa hivyo familia za kawaida ni zipi? Ni familia zinazofanya kazi. Wafanyakazi wanategemea mishahara yao kuishi na wanaweza kumudu mahitaji ya kimsingi. Hawatakuruhusu kwenda njaa wakati wowote, lakini huwezi kutarajia mahitaji yako yote ya mwili kutoshelezwa. Kisha kuna familia za ukulima. Wakulima wanategemea kupanda mazao kwa chakula chao, na wana nafaka za kula, na kwa vyovyote vile, hutakuwa na njaa, lakini huwezi kuwa na nguo nzuri sana. Tena kuna familia zingine ambazo zinashughulika katika biashara ama zinazoendesha biashara ndogondogo, na zingine ambazo wazazi ni wenye akili, na hizi zinaweza kuhesabika kama familia za kawaida. Kuna baadhi ya wazazi ambao ni wafanyakazi wa ofisi ama maafisa wadogo wa serikali kwa kiwango zaidi, ambazo haziwezi kuhesabika kama familia mashuhuri pia. Watu wengi zaidi wanazaliwa katika familia za kawaida, na haya yote yanapangiliwa na Mungu. Kusema kwamba, kwanza kabisa mazingira haya unayoishi si familia ya uwezo mkubwa ambayo unaweza kufikiria, lakini badala yake ni familia uliyoamuliwa na Mungu, na watu wengi wataishi katika mipaka ya aina hii ya familia; hatutazungumza mambo ya pekee hapa. Kwa hivyo je, hadhi ya kijamii? Hali ya uchumi ya wengi wa wazazi ni wastani na hawana hadhi ya juu ya kijamii—kwao ni vizuri tu kuwa na kazi. Kuna wowote walio magavana? Kuna wowote walio maraisi? (La.) Kwa zaidi ni watu kama mameneja wa biashara ndogo ama wakubwa wa muda mfupi. Hadhi zao za kijamii ni kuwa katikati, na hali zao za uchumi ni wastani. Sababu nyingine ni mazingira ya kuishi ya familia. Kwanza kabisa, hakuna wazazi ambao wanaweza kushawishi kwa wazi watoto wao kutembea njia ya uaguzi na kupiga ramli; hawa pia ni wachache. Wazazi wengi ni wa kawaida kiasi na ni wa hali moja na nyinyi. Mungu anaweka mazingira ya aina hii kwa ajili ya watu wakati sawa na kuwachagua, na ni kwa manufaa sana ya kazi Yake ya kuokoa watu. Kwa nje, inaonekana kwamba Mungu hajafanya chochote kikuu kwa mwanadamu; Anafanya kila kitu kwa siri tu, kwa unyenyekevu na kwa kimya. Lakini kwa hakika, vyote ambavyo Mungu anafanya vinafanywa kuweka msingi wa wokovu wako, kuandaa njia mbeleni na kuandaa hali zote muhimu za wokovu wako. Mara moja wakati maalum wa kila mtu, Mungu anawarudisha mbele Yake—wakati unapofika kwako kusikia sauti ya Mungu, huo ndio wakati unapokuja mbele Yake. Wakati hili linafanyika, watu wengine wamekuwa wazazi tayari wenyewe, ilhali wengine ni watoto wa mtu tu. Kwa maneno mengine, watu wengine wameoa na kupata watoto ilhali wengine bado hawajaoa, na hawajaanza bado familia zao. Lakini licha ya hali za watu, Mungu tayari ameweka nyakati utakapochaguliwa na injili na maneno Yake yatakapokufikia. Mungu ameweka hali, ameamulia mtu fulani ama muktadha fulani ambamo injili itapitishwa kwako, ili uweze kusikia maneno ya Mungu. Mungu tayari amekuandalia hali zote muhimu ili, bila kujua, unakuja mbele Yake na unarudishwa kwa familia ya Mungu. Pia, bila kujua, unafuata Mungu na kuingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua, kuingia katika njia ya Mungu ya kazi ambayo, hatua kwa hatua amekuandalia. Ni njia za aina gani ambazo Mungu hutumia wakati Anapofanya mambo kwa ajili ya mwanadamu wakati huu? Kwanza, angalau kabisa ni utunzaji na ulinzi ambao mwanadamu hufurahia. Kando na hayo, Mungu huweka watu, matukio, na vitu mbalimbali ili mwanadamu aweze kuona kuwepo Kwake na matendo Yake miongoni mwao. Kwa mfano, kuna watu wengine wanaomwamini Mungu kwa sababu mtu katika familia yao ni mgonjwa, na wanasema "Mmoja wa familia yangu ni mgonjwa, nitafanya nini?" Watu wengine kisha wanasema "Mwamini Bwana Yesu!" Kwa hivyo wanaanza kumwamini Mungu, na imani hii kwa Mungu imekuja kwa sababu ya hali hii. Kwa hivyo ni nani aliyepangilia hali hii? (Mungu.) Kwa njia ya maradhi haya, kuna familia zingine ambamo wote ni waumini, vijana na wazee, ilhali kuna familia zingine ambamo imani ni ya kibinafsi. Inavyoonekana, unamwamini Mungu kwa sababu ya maradhi, lakini kwa hakika ni hali uliyopewa ili uje mbele ya Mungu—huu ni wema wa Mungu. Kwa sababu maisha ya familia ya watu wengine ni magumu na hawawezi kupata amani yoyote, fursa ya bahati inakuja ambapo mtu anapitisha injili na kusema, "Familia yako ina magumu. Mwamini Bwana Yesu. Mwamini Bwana Yesu na utakuwa na amani." Bila fahamu, mtu huyu basi anakuja kumwamini Mungu katika hali asili, kwa hivyo hii si aina ya hali? (Ndiyo.) Na je, familia yake kuwa na amani si neema aliyopewa na Mungu? (Ndiyo.) Kisha kuna wengine wanaokuja kumwamini Mungu kwa sababu zingine. Kuna sababu tofauti na njia tofauti za imani, lakini licha ya sababu inakuleta kumwamini Yeye, yote hakika yamepangwa na kuongozwa na Mungu. Kwanza, Mungu hutumia njia kadhaa ili kukuchagua na kukuleta katika familia Yake. Hii ndiyo neema Mungu anayompa kila mwanadamu.

Sasa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, Hampi tena mwanadamu neema na baraka tu kama Alivyofanya mwanzoni, wala halazimishi watu kwenda mbele. Wakati wa hatua hii ya kazi, ni nini mwanadamu ameona kutoka kwa vipengele hivi vyote vya kazi ya Mungu ambavyo wamepitia? Wameona upendo wa Mungu, na hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kwa wakati huu, Mungu zaidi ya hayo, anamtegemeza, tia nuru, na kumwongoza mwanadamu, ili aje kujua nia Zake polepole, kujua maneno Anayozungumza na ukweli Anaompa mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati amevunjika roho, wakati hana popote pa kugeukia, Mungu atatumia maneno Yake kufariji, kushauri na kuwatia moyo, ili mwanadamu wa kimo kidogo aweze kupata nguvu polepole, kuinuka kwa wema na kuwa radhi kushirikiana na Mungu. Lakini wakati wanadamu hawamtii Mungu ama wanampinga Yeye, ama wanapofichua upotovu wao, Mungu hataonyesha huruma kuwarudi na kuwafundisha nidhamu. Kwa ujinga, kutojua, unyonge, na uchanga wa mwanadamu, hata hivyo, Mungu ataonyesha uvumilivu na ustahimilivu. Kwa njia hii, kupitia kazi yote Mungu anamfanyia mwanadamu, mwanadamu anapevuka, anakua na anakuja kujua nia za Mungu polepole, kujua baadhi ya ukweli, kujua ni nini mambo mema na ni nini mambo hasi, kujua uovu ni nini na kujua giza ni nini. Mungu hamrudi na kumfundisha nidhamu mwanadamu siku zote wala Haonyeshi uvumilivu na ustahimilivu siku zote. Badala yake anampa kila mtu kwa njia tofauti, katika hatua zao tofauti na kulingana na kimo na ubora wa tabia yao tofauti. Anamfanyia mwanadamu mambo mengi na kwa gharama kubwa; mwanadamu hafahamu lolote la gharama hii ama mambo haya Mungu anafanya, ilhali yote ambayo anafanya kwa kweli inafanywa kwa kila mtu. Upendo wa Mungu ni wa kweli: Kupitia neema ya Mungu mwanadamu anaepuka janga moja baada ya jingine, ilhali kwa unyonge wa mwanadamu, Mungu anaonyesha ustahimili wake muda baada ya muda. Hukumu na kuadibu kwa Mungu yanaruhusu watu kuja kujua polepole upotovu wa wanadamu na kiini chao cha kishetani. Kile ambacho Mungu anapeana, kutia nuru Kwake kwa mwanadamu na uongozi Wake yote yanawaruhusu wanadamu kujua zaidi na zaidi kiini cha ukweli, na kujua zaidi kile ambacho watu wanahitaji, njia wanayopaswa kuchukua, kile wanachoishia, thamani na maana ya maisha yao, na jinsi ya kutembea njia iliyo mbele. Haya mambo yote ambayo Mungu anafanya hayatengwi na lengo Lake la awali. Ni nini, basi lengo hili? Je, mnajua? Mbona Mungu anatumia njia hizi kufanya kazi Yake kwa mwanadamu? Anataka kutimiza matokeo gani? Kwa maneno mengine, ni nini ambacho anataka kuona kwa mwanadamu na kupata kutoka kwake? Kile ambacho Mungu anataka kuona ni kwamba moyo wa mwanadamu unaweza kufufuliwa. Njia hizi ambazo anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu ni za kuamsha bila kikomo moyo wa mwanadamu, kuamsha roho ya mwanadamu, kumwacha mtu kujua alipotoka, ni nani anayemwongoza, kumsaidia, kumkimu, na ni nani ambaye amemruhusu mwanadamu kuishi hadi sasa; ni ya kuwacha mwanadamu kujua ni nani Muumbaji, ni nani wanapaswa kuabudu, ni njia gani wanapaswa kutembelea, na mwanadamu anapaswa kuja mbele ya Mungu kwa njia gani; yanatumika kufufua moyo wa mwanadamu polepole, ili mwanadamu ajue moyo wa Mungu, aelewe moyo wa Mungu, na aelewe utunzaji mkuu na wazo nyuma ya kazi Yake kumwokoa mwanadamu. Wakati moyo wa mwanadamu umefufuliwa, hataki tena kuishi maisha ya uasherati, tabia potovu, lakini badala yake kutaka kufuatilia ukweli kwa kuridhishwa kwa Mungu. Wakati moyo wa mwanadamu umeamshwa, anaweza basi kujinusuru kutoka kwa Shetani, kutoathiriwa tena na Shetani, kutodhibitiwa na kudanganywa na yeye. Badala yake, mwanadamu anaweza kushiriki katika kazi ya Mungu na katika maneno Yake kwa njia njema kuridhisha moyo wa Mungu, na hivyo kupata uchaji wa Mungu na uepukaji wa uovu. Hili ndilo lengo la awali la kazi ya Mungu.

Kuzungumza kuhusu uovu wa Shetani hivi sasa kulimfanya kila mtu kuhisi kana kwamba watu huishi kwa huzuni sana na kwamba maisha ya mwanadamu yamejaa bahati mbaya. Lakini mnahisi vipi sasa kwani Nimezungumza kuhusu utakatifu wa Mungu na kazi ambayo anafanya kwa mwanadamu? (Furaha sana.) Tunaweza kuona sasa kwamba kila kitu Mungu anafanya, kila kitu ambacho anapanga kwa uangalifu kwa mwanadamu ni safi kabisa. Kila kitu anachofanya Mungu ni bila kasoro, kumaanisha ni bila dosari, hakihitaji yeyote kukosoa, kutoa mawaidha ama kufanya mabadiliko yoyote. Kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa kila mtu hakina shaka; Anaongoza kila mtu kwa mkono, Anakuchunga kwa kila muda na Hajawahi kuondoka upande wako. Watu wanapokua katika mazingira haya na kukua na usuli wa aina hii, tunaweza kusema kwamba watu kwa kweli wanakua katika kiganja cha mkono wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo sasa bado mnahisi hisia za hasara? (La.) Je, kuna yeyote anayehisi kuvunjika moyo bado? (La.) Kwa hivyo kuna yeyote anayehisi kwamba Mungu amewaacha wanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nini hasa Mungu amefanya? (Anawahifadhi wanadamu.) Wazo na utunzaji mkuu nyuma ya kila anachofanya Mungu hayapingwi. Hata zaidi, wakati Mungu anapofanya kazi Yake, hajawahi kuweka sharti ama mahitaji yoyote kwa yeyote kati yenu kujua gharama anayokulipia, kwa hivyo uhisi shukrani kwake kwa kina. Je, Mungu amewahi kufanya chochote kama hiki kabla? (La.) Katika miaka yenu mirefu yote, kimsingi kila mtu amekutana na hali nyingi hatari na kupitia majaribu mengi. Hii ni kwa sababu Shetani yupo kando yako, macho yake yakikutazama kila wakati. Anapenda janga linapokupata, wakati maafa yanakupata, wakati hakuna chochote kinaenda sawa kwako, na anapendelea unaponaswa na wavu wa Shetani. Kuhusu Mungu, anakulinda kila wakati, kukuweka mbali na bahati moja mbaya baada ya nyingine na kutokana na janga moja baada ya jingine. Hii ndiyo maana Nasema kwamba kila kitu ambacho mwanadamu anacho—amani na furaha, baraka na usalama wa kibinafsi—yote hakika yanadhibitiwa na Mungu, na Anaongoza na kuamua maisha na hatima ya kila mtu. Lakini, je, Mungu ana dhana iliyovimbishwa ya cheo chake, kama wanavyosema watu wengine? Kukuambia "Mimi ni mkuu kabisa wa wote, ni Mimi ninayechukua watamu wenu, lazima nyote mniombe huruma na kutotii kutaadhibiwa na kifo." Je, Mungu amewahi kutishia wanadamu kwa njia hii? (La.) Ashawahi kusema "Wanadamu ni wapotovu kwa hivyo haijalishi Ninavyowashughulikia, utendeaji wowote holela utatosha; Sihitaji kupanga mambo vizuri sana kwa sababu yao." Je, Mungu anafikiria kwa njia hii? (La.) Kwa hivyo Mungu ametenda kwa njia hii? (La.) Kinyume na haya, utendeaji wa Mungu wa kila mtu ni wenye ari na ambao umewajibika, umewajibika zaidi hata kuliko vile ulivyo kwa wewe mwenyewe. Sivyo hivi? Mungu haongei bure, wala hasimami juu akijifanya kuwa muhimu wala hadanganyi watu. Badala yake, Anafanya vitu ambavyo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya kwa uaminifu na kwa ukimya. Mambo haya yanaleta baraka, amani na furaha kwa mwanadamu, yanamleta mwanadamu kwa amani na kwa furaha mbele ya macho ya Mungu na ndani ya familia Yake na yanamletea mwanadamu akili sahihi, kufikiria sahihi, maoni sahihi na akili timamu wanapaswa kuwa nayo kuja mbele ya Mungu na kupokea wokovu wa Mungu. Kwa hivyo Mungu amewahi kuwa mdanganyifu kwa mwanadamu katika kazi Yake? (La.) Ashawahi kuonyesha maonyesho ya uongo ya ukarimu, Akimtuliza mwanadamu na mazungumzo ya kufurahisha, kisha kumpuuza mwanadamu? (La.) Je, Mungu ashawahi kusema kitu kimoja na kisha kufanya kingine? (La.) Je, Mungu ashawahi kupeana ahadi tupu na kujigamba, Akikuambia kwamba Anaweza kukufanyia hili ama kukusaidia kufanya lile, na kisha kutoweka? (La.) Hakuna udanganyifu ndani ya Mungu, hakuna uongo. Mungu ni mwaminifu na kila kitu Anachofanya ni halisi. Yeye ndiye wa pekee ambaye watu wanaweza kutegemea na wa pekee ambaye watu wanaweza kuaminia maisha yao na yote wanayo Kwake. Kwa vile hakuna udanganyifu ndani ya Mungu, tunaweza kusema kwamba Mungu ndiye wa kweli zaidi? (Ndiyo.) Bila shaka tunaweza, siyo? Ingawa, kuzungumza kuhusu maneno haya sasa, likitumika kwa Mungu ni dhaifu sana, cha ubinadamu sana, hakuna lolote tunaloweza kufanya kulihusu kwa vile hii ni mipaka ya lugha ya binadamu. Si sahihi sana hapa kumwita Mungu wa kweli, lakini tutatumia neno hili kwa sasa. Mungu ni mwaminifu. Kwa hivyo tunamaanisha nini kwa kuongea kuhusu vipengele hivi? Je, tunamaanisha tofauti kati ya Mungu na mwanadamu na tofauti kati ya Mungu na Shetani? Tunaweza kusema hivi. Hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kuona chembe cha tabia potovu ya Shetani kwa Mungu. Je, Niko sahihi kusema hivi? Ninaweza kupata Amina kwa sababu ya hili? (Amina!) Hatuoni uovu wowote wa Shetani ukifichuliwa kwa Mungu. Yote ambayo Mungu hufanya na kufichua ni muhimu sana na ya msaada sana kwa mwanadamu, yanafanywa kumkimu mwanadamu kabisa, yamejaa uhai na yanampa mwanadamu njia ya kufuata na mwelekeo wa kuchukua. Mungu hajapotoka, na zaidi ya hayo, kuangalia sasa kila kitu Mungu hufanya, tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu? (Ndiyo.) Kwa sababu Mungu hana upotovu wowote wa mwanadamu na hana chochote sawa na, au kinachofanana na tabia potovu ya mwanadamu ama kiini cha Shetani, kutoka mtazamo huu tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu. Mungu hafichui upotovu wowote, na ufunuo wa kiini Chake katika kazi Yake yote ni thibitisho tunalohitaji kwamba Mungu Mwenyewe ni mtakatifu. Je, mnaona hili? Sasa, kujua asili takatifu ya Mungu, kwa sasa wacha tuangalie hivi vipengele viwili: 1) Hakuna tabia potovu ndani ya Mungu; 2) kiini cha kazi ya Mungu kwa mwanadamu kinamruhusu mwanadamu kuona kiini cha Mungu mwenyewe na kiini hiki ni kizuri kabisa. Kwa kuwa vitu ambavyo kila namna ya kazi ya Mungu inamletea mwanadamu ni vitu vizuri. Kwanza, Mungu anamhitaji mwanadamu kuwa mwaminifu—hili si zuri? Mungu anampa mwanadamu maarifa—hili si zuri? Mungu anamfanya mwanadamu aweze kutambua kati ya mema na maovu—hili si zuri? Anamruhusu mwanadamu kuelewa maana na thamani ya maisha ya binadamu—hili si zuri? Anamruhusu mwanadamu kuona ndani ya kiini cha watu, matukio na mambo kulingana na ukweli—hili si zuri? (Ndiyo ni zuri.) Na matokeo ya haya yote ni kwamba mwanadamu hadanganywi tena na Shetani, haendelei kudhuriwa na Shetani ama kudhibitiwa na yeye. Kwa maneno mengine, yanawaruhusu watu kujinusurisha kabisa kutoka upotovu wa Shetani, na hivyo kutembea polepole njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Mmetembea umbali gani katika njia hii sasa? Ni vigumu kusema, sivyo? Lakini angalau sasa mna uelewa wa mwanzo wa jinsi Shetani anampotosha mwanadamu, vitu vipi ni ovu na vitu vipi ni hasi? (Ndiyo.) Kwa uelewa huu wa mwanzo, angalau mnatembea sasa njia sahihi. Je, tunaweza kusema hivyo? (Ndiyo.)

Tutamaliza sasa kuzungumzia kuhusu utakatifu wa Mungu, kwa hivyo nani miongoni mwenu, kutoka yote ambayo mmesikia na kupokea, anaweza kusema utakatifu wa Mungu ni nini? Utakatifu wa Mungu ninaozungumzia unarejelea nini? Lifikirie kidogo. Je, ukweli wa Mungu ni utakatifu Wake? Je, uaminifu wa Mungu ni utakatifu Wake? Je, kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu ni utakatifu Wake? Je, unyenyekevu wa Mungu ni utakatifu Wake? Je, upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni utakatifu Wake? Mungu humpa mwanadamu ukweli na uhai bure—huu ni utakatifu Wake? (Ndiyo.) Utakatifu wote ambao Mungu anafichua ni wa kipekee; hayapo katika binadamu potovu, wala hayawezi kuonekana hapo. Hakuna hata chembe ya hayo yanaweza kuonekana katika mchakato wa upotovu wa Shetani wa mwanadamu, wala katika tabia potovu ya Shetani wala katika kiini ama asili ya Shetani. Chote ambacho Mungu Anacho na Alicho ni ya kipekee na Mungu tu Mwenyewe anacho kiini cha aina hii, ni Mungu Mwenyewe tu anamiliki kiini cha aina hii. Baada ya kuzungumza hili hadi sasa, kuna yeyote kati yenu ambaye ameona yeyote mtakatifu hivi miongoni mwa wanadamu? (La.) Kwa hivyo, kuna yeyote mtakatifu hivi miongoni mwa watu maarufu, watu wakuu na mashuhuri mnaoabudu katika ubinadamu? (La.) Kwa hivyo sasa tunasema kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee, je anadhihirisha hili katika jina na vile vile katika ukweli? (Ndiyo.) Anadhihirisha. Zaidi ya hayo, kuna pia sehemu yake ya utendaji. Je, kuna tofauti zozote kati ya utakatifu ninaozungumzia sasa na utakatifu ambao mlifikiria, kuelewa na kudhania awali? (Ndiyo.) Kwa hivyo tofauti hii ni kubwa kiasi gani? (Kubwa sana!) Kubwa ni kubwa kiasi gani? Tumia maneno yenu, kuieleza. Watu humaanisha nini sanasana wanapoongea kuhusu utakatifu huu? (Baadhi ya tabia ya nje.) Tabia, ama kama njia ya kuelezea kitu, wanasema kwamba ni kitakatifu. Kwa hivyo maelezo haya ya "utakatifu" ni dhahania? Ni kitu tu kinachoonekana kuwa safi na kizuri, kitu kinachoonekana ama kusikika kuwa kizuri kwa watu, si chochote cha asili yoyote halisi ya utakatifu. Hii ni dhahania. Kando ya hili, kipengele cha utendaji cha "utakatifu" ambacho watu wanafikiria kinarejelea nini hasa? Je hasa ni kile wanachokifikiria ama kudhania kuwa? Kwa mfano, Wanabudhaa wengine hufariki wakati wanatia vitendoni, wanaaga wakiwa wamekaa pale wakilala. Watu wengine husema kwamba wamekuwa watakatifu na kuruka mbinguni. Hii pia ni aina ya ubunifu. Pia kuna wengine ambao wanafikiria kwamba kichimbakazi anayeelea chini kutoka mbinguni ni mtakatifu. Kwa kweli, wazo la watu la neno "takatifu" limekuwa tu kama fikira tupu na dhahania ambayo kimsingi haina kiini, na zaidi ya hayo haina chochote kuhusu kiini cha utakatifu. Kiini cha utakatifu ni upendo wa kweli, lakini hata zaidi ya hili ni kiini cha ukweli, cha haki na mwanga. Neno "takatifu" linafaa tu linapotumika kwa Mungu; hakuna chochote katika uumbaji kinachostahiki kuitwa takatifu. Mwanadamu lazima aelewe hilo. Kuanzia sasa kuendelea, tunatumia neno "takatifu" kwa Mungu pekee. Hii ni ya kufaa? (Ndiyo, inafaa.)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp