Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Utakatifu wa Mungu (II) (Sehemu ya Tatu)

Kuhusu utakatifu wa Mungu, hata kama inaweza kuwa mada inayojulikana, katika majadiliano inaweza kuwa dhahania kiasi kwa watu wengine, na maudhui yake yanaweza kuwa ya kina sana. Hii ni kwa sababu zamani, watu hawakushughulika sana na kipengele cha utendaji wa mada hii. Lakini msijali, tutaishughulikia polepole na Nitawasaidia kuelewa maana ya utakatifu wa Mungu. Wacha tuseme hili kwanza: Iwapo unataka kujua mtu, angalia tu kile anachofanya na matokeo ya vitendo vyake, na utaweza kuona kiini cha mtu huyo—hebu tushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu kutoka kwa mtazamo huu kwanza. Kwa maneno mengine kiini cha Shetani ni ovu, na kwa hivyo vitendo vya Shetani kwa mwanadamu vimekuwa kumpotosha bila kikomo. Shetani ni mwovu, kwa hivyo watu ambao amepotosha hakika ni waovu, siyo? Kuna yeyote anayeweza kusema, “Shetani ni mwovu, pengine mtu aliyepotosha ni mtakatifu”? Ni mzaha, siyo? Je, hata inawezekana? (La.) Kwa hivyo usimfikirie hivyo, wacha tumzungumzie kutoka kwa kipengele hiki. Shetani ni mwovu, kuna upande muhimu na wa matendo kwa jambo hili na haya si mazungumzo matupu tu. Hatujaribu kusema uwongo juu ya Shetani; tunashiriki tu kuhusu ukweli na uhalisi. Hii inaweza kuumiza watu wengine ama sehemu fulani ya watu, lakini hakuna nia mbaya hapa; pengine mtasikia haya leo na kuhisi kutostareheka kiasi, lakini siku fulani hivi punde, wakati mnaweza kumtambua, mtajichukia, na mtahisi kwamba kile tulichozungumzia leo ni cha manufaa kwenu na chenye thamani. Kiini cha Shetani ni ovu, kwa hivyo matokeo ya vitendo vya Shetani bila shaka ni ovu, ama kwa kiwango cha chini kabisa, yanahusiana na uovu wake, tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Kwa hivyo, je Shetani anampotosha mwanadamu vipi? Kwanza lazima tuangalie hasa—uovu uliofanywa na Shetani duniani na miongoni mwa binadamu ambao unaonekana, ambao watu wanahisi; mmewahi kuyafikiria haya awali? Pengine hamkuyafikiria sana, kwa hivyo wacha Nitaje pointi kadhaa muhimu. Kila mtu anajua kuhusu nadharia ya mageuko ambayo Shetani anapendekeza, siyo? Je, si hii ni sehemu ya maarifa yanayosomwa na mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani kwanza anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu, na huwafunza maarifa na mbinu yake mwenyewe. Kisha anatumia sayansi kuwapotosha wanadamu, akiamsha mvuto wao kwa maarifa, sayansi, na vitu vya ajabu, ama kwa vitu ambavyo watu wanataka kuchunguza. Vitu vifuatavyo vinavyotumiwa na Shetani kumpotosha mwanadamu ni desturi ya kitamaduni na ushirikina, na baada ya vitu hivyo, anatumia mienendo ya kijamii. Hivi vyote ni vitu ambavyo watu wanapatana navyo katika maisha yao ya kila siku na hivi vyote vinahusiana na vitu vilivyo karibu na watu, vitu wanavyoona, wanavyosikia, wanavyogusa na wanavyopitia. Mtu anaweza kusema kwamba vinazunguka kila mtu, haviwezi kutorokwa na kuepukika. Wanadamu hawana njia ya kuepuka kuathiriwa, kuambukizwa, kudhibitiwa, na kufungwa na vitu hivi; hawana nguvu za kuvisukuma mbali.

1. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu

Kwanza tutazungumza kuhusu maarifa. Si kila mtu angechukulia maarifa kuwa kitu chema? Ama kwa kiwango cha chini kabisa, watu wanafikiri kwamba kidokezo cha neno “maarifa” ni chema badala ya hasi. Kwa hivyo mbona tunataja hapa kwamba Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu? Si nadharia ya mageuko ni kipengele cha maarifa? Si sheria za kisayansi za Newton ni sehemu ya maarifa? Si mvuto wa dunia ni sehemu ya maarifa, siyo? (Ndiyo.) Hivyo mbona maarifa yametajwa miongoni mwa maudhui anayoyatumia Shetani kumpotosha mwanadamu? Maoni yenu hapa ni yapi? Je, maarifa yana hata chembe cha ukweli ndani yake? (La.) Kwa hivyo ni nini kiini cha maarifa? (Yanaenda kinyume na ukweli.) Maarifa ambayo mwanadamu anatafiti yanafunzwa kwa msingi upi? Yanalingana na nadharia ya mageuko? Si maarifa ambayo mwanadamu amechunguza, ujumla wake, unatokana na ukanaji Mungu? (Ndiyo.) Kuna sehemu yoyote ya maarifa haya ambayo ina uhusiano na Mungu? Je, yanahusiana na kumwabudu Mungu? Yanahusiana na ukweli? (La.) Hivyo Shetani anatumiaje maarifa kumpotosha mwanadamu? Nimetoka tu kusema kwamba hakuna sehemu yoyote ya maarifa haya inahusiana na kumwabudu Mungu ama na ukweli. Watu wengine wanayafikiria hivi: “Yanaweza kutokuwa na chochote kuhusiana na ukweli, lakini hayawapotoshi watu.” Mnafikiri nini kuhusu haya? Ulifundishwa na maarifa kwamba furaha ya watu ilitegemea kile walichokiumba na mikono yao? Je, maarifa yaliwahi kukufunza kwamba hatima ya mwanadamu ilikuwa mikononi mwake? (Ndiyo.) Haya ni mazungumzo ya aina gani? (Ni upuuzi.) Sahihi! Ni upuuzi! Maarifa yanatatiza kujadili. Unaweza kuiweka kwa urahisi kwamba eneo la maarifa ni maarifa tu. Hili ni eneo la maarifa linalofunzwa kwa msingi wa kutomwabudu Mungu na kutokuwa na uelewa kwamba Mungu aliumba mambo yote. Watu wanaposoma aina hii ya maarifa, hawaoni Mungu anatawala mambo yote, hawaoni Mungu anaongoza ama anasimamia mambo yote. Badala yake, wanayofanya tu ni kutafiti na kuchunguza, bila kikomo kwa sehemu hiyo ya maarifa, na kutafuta majibu kwa msingi wa maarifa. Hata hivyo, iwapo watu hawamwamini Mungu na badala yake wanatafiti tu, kamwe hawatapata majibu ya kweli, siyo? Maarifa yanakupa tu riziki, yanakupa tu kazi, yanakupa tu mapato ili usiwe na njaa, lakini kamwe hayawezi kukufanya kumwabudu Mungu, na hayatakuweka mbali na maovu. Kadiri unavyosoma maarifa, ndivyo utatamani zaidi kuasi dhidi ya Mungu, kumtafiti Mungu, kumjaribu Mungu, na kwenda kinyume na Mungu. Hivyo sasa, tunaona yapi ambayo maarifa yanawafunza watu? Yote ni filosofia ya Shetani. Je, filosofia za Shetani na kanuni za kuishi zinazopatikana kwa wanadamu potovu zina uhusiano wowote na ukweli? (La.) Hazina uhusiano wowote na ukweli na, kwa kweli, ni kinyume cha ukweli. Watu mara nyingi husema, “Maisha ni mwendo”; haya ni mazungumzo ya aina gani? (Upuuzi.) Watu pia wanasema, “Mwanadamu ni chuma, mchele ni chuma, mwanadamu huhisi anataabika kwa njaa asipokula mlo”; hii ni nini? Hata ni uwongo mbaya zaidi na inachukiza kuisikia. Hivyo, maarifa ni kitu ambacho pengine kila mtu anakijua. Kwa yanayoitwa maarifa ya mwanadamu, Shetani amejaza kidogo filosofia yake ya maisha na kufikiria kwake. Na wakati Shetani anafanya haya, Shetani anamruhusu mwanadamu kutumia kufikiria kwake, filosofia, na mtazamo wake ili mwanadamu aweze kukana uwepo wa Mungu, kukana utawala wa Mungu juu ya mambo yote na utawala juu ya hatima ya mwanadamu. Kwa hivyo, masomo ya mwanadamu yanapoendelea, anahisi uwepo wa Mungu kuwa usio yakini anapopata maarifa zaidi, na mwanadamu anaweza hata kuhisi kwamba Mungu hayupo. Kwa vile Shetani ameongeza mitazamo, mawazo, na fikira kwa akili ya mwanadamu, je, si binadamu amepotoshwa na jambo hili Shetani anapoweka fikira hizi ndani ya akili yake? (Ndiyo.) Ni nini msingi wa maisha ya mwanadamu sasa? Kweli anategemea maarifa haya? La; msingi wa maisha ya mwanadamu ni fikira, mitazamo na filosofia za Shetani ambazo zimefichwa kwa maarifa haya. Hapa ndipo kiini cha upotovu wa Shetani wa mwanadamu unafanyika, hili ndilo lengo la Shetani na mbinu yake ya kumpotosha mwanadamu.

Kwanza tutazungumzia kipengele cha juujuu zaidi cha mada hii. Je, sarufi na maneno katika masomo ya lugha yaliweza kuwapotosha watu? Maneno yanaweza kupotosha watu? (La.) Maneno hayapotoshi watu; ni chombo kinachowaruhusu watu kuongea na chombo ambacho watu wanatumia kuwasiliana na Mungu. Zaidi, lugha na maneno ni jinsi ambavyo Mungu anawasiliana na watu sasa, ni vyombo, ni vya umuhimu. Moja ongeza moja ni mbili, haya ni maarifa, siyo? Mbili zidisha kwa mbili ni nne, haya ni maarifa, siyo? Lakini yanaweza kukupotosha? Hii ni akili ya wote na kanuni kwa hivyo haiwezi kupotosha watu. Kwa hivyo ni maarifa gani yanayopotosha watu? Ni maarifa ambayo yamechanganywa mitazamo na fikira za Shetani, Shetani anataka kujaza mitazamo na fikira hizi ndani ya binadamu kupitia maarifa. Kwa mfano, katika insha, kuna chochote kibaya na maneno yaliyoandikwa? (La.) Shida inaweza kuwa wapi? Mitazamo na nia ya mwandishi alipoandika insha hiyo na pia maudhui ya fikira zake—haya ni mambo ya kiroho—yanaweza kuwapotosha watu. Kwa mfano, iwapo ungekuwa ukitazama kipindi kwenye runinga, ni mambo yapi ndani yake yangeweza kubadili mtazamo wako? Je, yale yaliyosemwa na wasanii, maneno yenyewe, yangeweza kuwapotosha watu? (La.) Ni mambo yapi ambayo yangeweza kuwapotosha watu? Ingekuwa fikira na maudhui ya kiini ya kipindi, ambayo yangewakilisha mitazamo ya mwelekezi, na taarifa iliyo kwa mitazamo hii ingeshawishi mioyo na akili za watu. Siyo? (Ndiyo.) Je, mnajua Narejelea nini katika mjadala Wangu wa Shetani kutumia maarifa kuwapotosha watu? (Ndiyo, tunajua.) Hutafahamu vibaya, siyo? Hivyo unaposoma riwaya ama insha tena, unaweza kutathmini iwapo fikira zilizoelezwa katika insha hiyo zinapotosha ama hazipotoshi mwanadamu ama kuchangia kwa binadamu? (Tunaweza kufanya hivyo kidogo.) Hiki ni kitu ambacho lazima kisomwe na kupitiwa polepole, si kitu kinachoeleweka kwa urahisi mara moja. Kwa mfano, unapotafiti ama kusoma sehemu ya maarifa, baadhi ya vipengele vyema vya maarifa hayo vinaweza kukusaidia kuelewa baadhi ya akili ya wote kuhusu eneo hilo, na kile ambacho watu wanapaswa kuepukana nacho. Chukua mfano wa “umeme,” hili ni eneo la maarifa, siyo? Ungekuwa mjinga kama hungejua kwamba umeme unaweza kuwatetemesha watu, siyo? Lakini utakapoelewa sehemu hii ya maarifa, hutakuwa na uzembe kuhusu kugusa kitu cha umeme na utajua jinsi ya kutumia umeme. Haya yote ni mambo mema. Unaelewa kile tunachojadili kuhusu jinsi maarifa yanawapotosha watu? (Ndiyo, tunaelewa.) Iwapo unaelewa hatutaendelea kukizungumzia zaidi kwa sababu kuna aina nyingi za maarifa ambazo zinasomwa duniani na lazima mchukue wakati wenu kuzitofautisha wenyewe.

2. Jinsi ambavyo Shetani Hutumia Sayansi Kumpotosha Mwanadamu

Sayansi ni nini? Si sayansi imewekwa kwa hadhi ya juu na kuchukuliwa kuwa muhimu katika akili za karibu kila mtu? (Ndiyo, imewekwa kwa hadhi ya juu.) Sayansi inapotajwa, si watu wanahisi, “Hiki ni kitu ambacho watu wa kawaida hawawezi kuelewa, hii ni mada ambayo tu watafiti wa kisayansi ama wataalam wanaweza kugusia. Haina uhusiano wowote na sisi watu wa kawaida”? Je, ina uhusiano lakini? (Ndiyo.) Shetani anatumiaje sayansi kuwapotosha watu? Hatutazungumza kuhusu mambo mengine isipokuwa mambo ambayo watu mara nyingi wanapatana nayo katika maisha yao binafsi. Je, umesikia kuhusu jeni? Nyote mnalijua neno hili, siyo? Je, jeni ziligunduliwa kupitia sayansi? (Ndiyo.) Jeni zinamaanisha nini hasa kwa watu? Hazifanyi watu kuhisi kwamba mwili ni kitu cha ajabu? Wakati watu wanajulishwa kwa mada hii, si kutakuwa na watu—hasa wenye kutaka kujua—ambao watataka kujua zaidi ama kutaka maelezo zaidi? Hawa watu wanaotaka kujua wataweka nguvu zao zote kwenye mada hii na wakati hawana shughuli watatafuta maelezo kwenye vitabu na Intaneti kujifunza maelezo zaidi kuihusu. Sayansi ni nini? Kuongea waziwazi, sayansi ni fikira na nadharia ya vitu ambavyo mwanadamu anataka kujua, vitu visivyojulikana, na ambavyo hawajaambiwa na Mungu; sayansi ni fikira na nadharia za siri ambazo mwanadamu anataka kuchunguza. Wigo wa sayansi ni upi? Unaweza kusema kwamba unajumuisha mambo yote, lakini mwanadamu anafanya vipi kazi ya sayansi? Je, ni kupitia utafiti? Inahusiana na kutafiti maelezo na sheria za vitu hivi na kuweka mbele nadharia zisizoaminika ambazo watu wote wanafikiria, “Wanasayansi hawa ni wakubwa mno! Wanajua mengi na wana maarifa mengi kuelewa mambo haya!” Wanapendezwa sana na watu hao, siyo? Watu wanaotafiti sayansi, wana mitazamo ya aina gani? Hawataki kutafiti ulimwengu, kutafiti mambo ya ajabu ya maeneo ya maslahi yao? (Ndiyo.) Matokeo ya mwisho ya haya ni nini? Baadhi ya sayansi ina watu wanaofikia mahitimisho yao kwa kubahatisha, nyingine ina watu wanaotegemea uzoefu wa binadamu kwa mahitimisho yao na hata eneo lingine la sayansi litakuwa na watu wanaofikia mahitimisho yao kutokana na uzoefu ama uchunguzi wa kihistoria na usuli. Sivyo? (Ndiyo.) Hivyo, sayansi inawafanyia nini watu? Kile sayansi inafanya ni kwamba inawaruhusu tu watu kuona vyombo katika ulimwengu wa maumbile na tu kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu; haimruhusu mwanadamu kuona sheria ambazo Mungu anatumia kutawala mambo yote. Mwanadamu anaonekana kupata majibu kutoka kwa sayansi, lakini majibu hayo yanachanganya na yanaleta tu uradhi wa muda mfupi, uradhi ambao unawekea moyo wa mwanadamu mipaka kwa ulimwengu wa maumbile. Mwanadamu anahisi kwamba tayari amepata majibu kutoka kwa sayansi kwa hivyo licha ya suala litakaloibuka, wanajaribu kuthibitisha au kukubali hili kwa msingi wa mitazamo yao ya kisayansi. Moyo wa mwanadamu unamilikiwa na sayansi na kushawishiwa nayo hadi pahali ambapo mwanadamu tena hana akili ya kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kuamini kwamba mambo yote yanatoka kwa Mungu na mwanadamu anapaswa kumwangalia kupata majibu. Hii si ukweli? Kadiri ambavyo mtu anaamini sayansi, anakuwa mjinga zaidi, akiamini kwamba kila kitu kina suluhisho la sayansi, kwamba utafiti unaweza kutatua chochote. Hamtafuti Mungu na haamini kwamba Yupo; hata watu wengine ambao wamemfuata Mungu kwa miaka mingi wataenda na kutafiti vimelea kwa msukumo ama kutafuta baadhi ya maelezo ili kupata jibu la suala. Mtu kama huyo haangalii masuala kwa mtazamo wa ukweli na wakati mwingi anataka kutegemea mitazamo na maarifa ya kisayansi ama majibu ya kisayansi kutatua shida; lakini hamtegemei Mungu na hamtafuti Mungu. Je, watu kama hao wana Mungu katika mioyo yao? (La.) Hata kuna watu wengine wanaotaka kutafiti Mungu kwa njia sawa na vile wanasoma sayansi. Kwa mfano, kuna wataalam wengi wa kidini walioenda mahali safina ilisimama baada ya mafuriko makubwa. Wameiona safina, lakini katika kuonekana kwa safina hawaoni uwepo wa Mungu. Wanaamini tu hadithi na historia na haya ni matokeo ya utafiti wao wa kisayansi na utafiti wa dunia ya maumbile. Ukitafiti vitu yakinifu, viwe maikrobaiolojia, falaki, ama jiografia, hutawahi kupata matokeo yanayosema kwamba Mungu yupo ama kwamba anatawala mambo yote, Sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo sayansi inamfanyia nini mwanadamu? Si inamweka mbali na Mungu? Si hii inawaruhusu watu kumtafiti Mungu? Si hii inawafanya watu kuwa na shaka zaidi kuhusu uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anataka kutumia vipi sayansi kumpotosha mwanadamu, na atumie mahitimisho ya kisayansi kuwadanganya na kuwanyima watu hisia? Shetani anatumia majibu yenye maana nyingi kushikilia mioyo ya watu ili wasitafute ama kuamini uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Hivyo, hii ndiyo sababu tunasema ni njia moja Shetani anawapotosha watu.

3. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu

Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Kutoka mwanzo, familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha, ama mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwenye fikira za watu. Watu wanafikiria nini kuhusu mambo haya? Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na uhai wa kutii, na hata kamwe hawataki kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu. Kuna vipengele vingine vya desturi ya kitamaduni, kama kile kilichopitishwa na Confucius ama Mencius, ama mambo waliyofunzwa watu na Utao ama Uconfucius ambayo yamekuwa sehemu ya kila mtu hadi ndani kwa mifupa yao. Sivyo? (Ndiyo.) Desturi ya kitamaduni inajumuisha nini? Inajumuisha likizo ambazo watu wanasherehekea? Kwa mfano, Tamasha la Majira ya machipuko, Tamasha la Taa, Siku ya Kufagia Kaburi, Tamasha la Mashua ya Joka, pamoja na Tamasha ya Zimwi na Tamasha ya Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani. Baadhi za familia hata husherehekea wakati wazee wanahitimu umri fulani, ama wakati watoto wanahitimu umri wa mwezi 1 na wakati wako na umri wa siku 100. Hizi zote ni likizo za desturi. Je, si usuli wa likizo hizi unajumuisha desturi ya kitamaduni? Ni nini kiini cha desturi ya kitamaduni? Kina chochote cha kufanya na kumwabudu Mungu? Kina chochote cha kufanya na kuwaambia watu kuweka katika vitendo ukweli? (La.) Kuna likizo zozote za watu kutoa sadaka kwa Mungu, kwenda kwa madhabahu ya Mungu na kupokea mafunzo Yake? Kuna likizo kama hizi? (La.) Watu hufanya nini katika likizo hizi zote? (Kumwabudu Shetani. Kula, kunywa na shughuli za burudani.) Katika nyakati za sasa zinaonekana kuwa hafla za kula, kunywa, na kujiburudisha. Ni nini chanzo cha desturi ya kitamaduni? Desturi ya kitamaduni imetoka kwa nani? (Shetani.) Imetoka kwa Shetani. Katika usuli wa hizi likizo za desturi, Shetani anaingiza mambo ndani ya mwanadamu, haya ni mambo gani? Kuhakikisha kwamba watu wanakumbuka mababu zao, hili ni mojawapo ya mambo haya? Kwa mfano, wakati wa Tamasha la Kufagia Kaburi watu husafisha makaburi na kutoa sadaka kwa mababu zao hivyo watu hawatasahau mababu zao. Pia, Shetani anahakikisha kwamba watu wanakumbuka kuwa wazalendo, kama katika Tamasha la Mashua ya Joka. Je, Tamasha la Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani? (Kupatana kwa familia.) Ni nini usuli wa kupatana kwa familia? Sababu zake ni nini? (Hisia.) Kuwasiliana na kuunganika kihisia. Bila shaka, iwapo ni kusherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya wa Mwezi ama Tamasha la Taa, kuna njia nyingi za kuelezea sababu za usuli. Haijalishi mtu anaelezea sababu iliyo nyuma yazo, kila moja ni njia ya Shetani ya kuingiza filosofia yake na kufikiria kwake kwa watu, ili waweze kupotea kutoka kwa Mungu na wasijue kwamba kuna Mungu, na kwamba watoe sadaka ama kwa mababu zao au Shetani, ama kwamba ni udhuru wa kula, kunywa na kujifurahisha kwa ajili ya matamanio ya mwili. Kila ya likizo hizi inaposherehekewa, fikira na mitazamo ya Shetani yanapandwa kwa kina ndani ya akili za watu na hata hawajui. Wakati watu wanafika umri wa kati ama zaidi, fikira na mitazamo hii ya Shetani tayari yamekita mizizi ndani sana ya mioyo yao. Zaidi, watu wanafanya juhudi zao kabisa kueneza fikira hizi, ziwe sahihi ama si sahihi, kwa kizazi kifuatacho bila wasiwasi pasipo kuchagua. Sivyo? (Ndiyo.) Ni jinsi gani desturi hii ya kitamaduni na likizo hizi zinapotosha vipi watu? Unajua? (Watu wanawekewa mipaka na kufungwa na kanuni za hizi desturi kana kwamba hawana muda ama nguvu kumtafuta Mungu.) Hiki ni kipengele kimoja. Kwa mfano, kila mtu anasherehekea wakati wa Mwaka Mpya wa Mwezi, usingesherehekea, hungehisi huzuni? Je, kuna miiko yoyote ambayo unapaswa kushikilia? Hungehisi, “Wai, sikusherehekea Mwaka Mpya. Siku hii ya Mwaka Mpya wa Mwezi ilikuwa mbaya sana; mwaka huu wote utakuwa mbaya”? Si ungehisi kutokuwa na utulivu na kuogopa kiasi? Kuna hata watu wengine ambao hawajatoa sadaka kwa mababu zao kwa miaka mingi na ghafla wamekuwa na ndoto ambapo mtu aliyekufa anawaomba pesa, watahisi nini ndani yao? “Inahuzunisha kwamba huyu mtu aliyekufa anahitaji pesa ya kutumia! Nitawachomea baadhi ya pesa ya karatasi, nisipo hiyo hakika haitakuwa sawa. Sisi tunaoishi tunaweza kupatana na shida kidogo nisipochoma baadhi ya pesa ya karatasi, ni nani anayeweza kusema wakati janga litatokea?” Daima watakuwa na wingu hili dogo la hofu na wasiwasi katika mioyo yao. Ni nani anayewapa wasiwasi? (Shetani.) Shetani huleta wasiwasi. Si hii ndiyo njia moja ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? Anatumia mbinu na udhuru mbalimbali ili kukudhibiti, kukutishia, kukufunga, hadi kiasi kwamba unachanganyikiwa na kumkubali na kumnyenyekea; hivi ndivyo Shetani anampotosha mwanadamu. Nyakati nyingi ambapo watu ni wanyonge ama hawaelewi vyema hali ilivyo, wanaweza bila kutaka, kufanya kitu kwa njia iliyochanganyikiwa, yaani, wanaanguka chini ya mshiko wa Shetani bila kusudi na wanaweza kufanya kitu bila kusudi na wasijue wanafanya nini. Hii ni njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu. Hata kuna watu wachache sasa ambao wanasita kuachana na desturi za kitamaduni ambazo zimekita mizizi na hawawezi tu kuziacha. Ni hasa wakati ni wanyonge na wasipoonyesha hisia ndipo wanataka kusherehekea likizo za aina hizi na wanataka kukutana na Shetani na kumridhisha Shetani tena, ambako kupitia huko wanaweza pia kujifariji ndani yao. Ni nini usuli wa hizi desturi za kitamaduni? Mkono mweusi wa Shetani unavuta nyuzi nyuma ya pazia? Asili ovu ya Shetani inatawala na kudhibiti vitu? Shetani anadhibiti hivi vitu vyote? (Ndiyo.) Wakati watu wanaishi katika desturi ya kitamaduni na kusherehekea likizo za desturi za aina hizi, tunaweza kusema kwamba haya ni mazingira ambapo wanadanganywa na kupotoshwa na Shetani, na zaidi ya hayo wana furaha kupotoshwa na Shetani? (Ndiyo.) Hiki ni kitu ambacho nyinyi nyote mnakiri, ambacho nyote mnakijua.

4. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu

Mnalijua neno “ushirikina,” siyo? Kuna usawa unaopatana kati ya ushirikina na desturi ya kitamaduni, lakini hatutazungumza kuhusu huo leo, badala yake Nitajadili unaokabiliwa mara nyingi: uganga, uaguzi, kuchoma ubani, na kuabudu Buddha. Watu wengine wanafanya uganga, wengine wanaabudu Buddha na kuchoma ubani, ilhali wengine wanabashiriwa ama wanaambiwa bahati zao kwa kumruhusu mtu kusoma vipengele vya nyuso zao. Wangapi kati yenu wameambiwa bahati zao ama wamesomwa uso? Hiki ni kitu ambacho watu wengi wanataka, siyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? Watu wanapata faida ya aina gani kutoka kwa uaguzi na uganga? Wanapata uradhi wa aina gani kutoka kwa hayo? (Udadisi.) Ni udadisi tu? Haiwezi kuwa udadisi. Ni nini lengo la ubashiri? Mbona ufanyiwe? Si kwa ajili ya kuona siku za baadaye? Watu wengine wanasomwa nyuso zao ili kutabiri siku za baadaye, wengine wanafanya hivyo ili kuona iwapo watakuwa na bahati nzuri au la. Wengine wanafanya hivyo ili kuona vipi ndoa zao zitakuwa, na bado wengine wanafanya hivyo kuona bahati itakayoletwa na mwaka ulio mbele. Watu wengine wanasomwa nyuso zao kuona matarajio yao na yale ya wana na binti zao yatakuwa vipi na kuona vipengele vyote vya vitu hivi, na wanabiashara wengine wanafanya hivyo kuona watatengeneza pesa ngapi ili waweze kupata mwongozo kwa kile wanachopaswa kufanya. Je, ni kuridhisha udadisi tu? (La.) Wakati watu wanasomwa nyuso zao ama kufanya vitu vya aina hii, ni kwa faida ya siku zao za baadaye binafsi na wanaamini kwamba haya yote yanahusiana kwa karibu na hatima zao. Je, kuna yoyote katika mambo haya yaliyo ya manufaa? (La.) Mbona si ya manufaa? Si kitu kizuri kujua kidogo kuhusu mambo hayo? Hii inakusaidia kujua wakati shida inaweza kutokea, ili uweze kuiepuka kama ulikuwa unajua kuihusu awali, siyo? Kupigiwa ramli kunaweza kukuruhusu kuongozwa kuhusiana nako, ili mwaka ulio mbele uweze kuwa mzuri na unaweza kuwa tajiri ukifanya biashara. Si hii ni ya manufaa? (La.) Iwapo ina manufaa haituhusu, hatutaishiriki leo; mjadala wetu hauhusishi maudhui na mada hii. Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Kile ambacho watu wanajua kuhusu vitu kama ubashiri, kusoma uso, na uaguzi ni ili waweza kujua bahati zao zitakuwa vipi katika siku za baadaye na vile njia iliyo mbele inakaa, lakini mwishowe, ni mikono ya nani inadhibiti vitu hivi? (Mikono ya Mungu.) Viko katika mikono ya Mungu. Kwa kutumia mbinu hizi, Shetani anataka watu wajue nini? Shetani anataka kutumia kusoma uso na uaguzi ili kuwaambia watu kwamba anajua bahati zao mbeleni, na Shetani anataka kuwaambia watu kwamba anajua vitu hivi na anavidhibiti. Shetani anataka kutumia fursa hii na kutumia mbinu hizi kudhibiti watu, ili kwamba watu wanamwekea imani isiyoweza kutambua na kutii kila neno lake. Kwa mfano, ukisomwa uso, mwaguzi akifunga macho yake na kukwambia kila kitu ambacho kimekufanyikia katika miongo michache iliyopita kwa uwazi kamili, ungehisi vipi ndani yako? Ghafla ungehisi, “Nimependezwa sana na huyu mwaguzi, yuko sahihi sana! Sijawahi kumwambia yeyote maisha yangu ya nyuma, alijuaje kuyahusu?” Haitakuwa vigumu sana kwa Shetani kujua maisha yako ya nyuma, siyo? Mungu amekuongoza hadi leo, na Shetani pia amewapotosha watu wakati huo wote na amekufuata. Kupita kwa miongo kwako si chochote kwa Shetani na si vigumu kwake kujua vitu hivi. Wakati unajua kwamba alichosema Shetani ni sahihi, si unampa moyo wako? Siku zako za baadaye na bahati yako, si unategemea udhibiti wake? Papo hapo, moyo wako utahisi heshima ama ustahi kwake, na kwa watu wengine, nafsi zao pengine tayari zimenyakuliwa naye. Na utamwuliza mwaguzi mara moja: “Napaswa kufanya nini baada ya hapa? Napaswa kuepukana na nini mwaka ujao? Ni vitu gani ambavyo sipaswi kufanya?” Na kisha atasema hupaswi kwenda pale, hupaswi kufanya hili, usivae nguo za rangi fulani, hupaswi kwenda pahali kama hapo na hapo unapaswa kufanya mambo fulani zaidi…. Si utatia vyote anavyosema moyoni mara moja? Ungevikariri haraka kuliko neno la Mungu. Mbona ungevikariri haraka hivyo? Kwa sababu ungetaka kumtegemea Shetani kwa sababu ya bahati njema. Si hapa ndipo anaunyakua moyo wako? Unapofanya kile anachosema na maneno yake sasa yanakuwa ukweli kama alivyotabiri, hungetaka kurudi nyuma kwake na kujua ni bahati gani mwaka unaokuja utaleta? (Ndiyo.) Utafanya chochote Shetani anakwambia ufanye na utaepukana na vitu anakwambia uepukane navyo, si unatii vyote anasema? Utaletwa chini ya bawa lake haraka sana, kupotoshwa, na kuwekwa chini ya udhibiti wake. Hii inafanyika kwa sababu unaamini anachosema ni ukweli na kwa sababu unaamini kwamba anajua kuhusu maisha yako ya nyuma, maisha yako ya sasa, na vitu ambavyo siku za badaye zitaleta. Hii ni mbinu Shetani anatumia kudhibiti watu. Lakini kwa kweli, ni nani aliye katika udhibiti? Ni Mungu Mwenyewe, si Shetani. Shetani anatumia tu hila zake hapa kudanganya watu wajinga, kuwadanganya watu wanaoona tu ulimwengu wa maumbile kumwamini na kumtegemea. Kisha, wataanguka katika mshiko wa Shetani na kutii kila neno lake. Lakini Shetani wakati wowote hupunguza jitihada watu wanapotaka kumwamini na kumfuata Mungu? Shetani hapunguzi jitihada. Katika hali hii, watu kweli wanaanguka katika mshiko wa Shetani? (Ndiyo.) Tunaweza kusema kwamba tabia ya Shetani hapa haina haya hata kidogo? (Ndiyo.) Mbona tungesema hivyo? (Shetani anatumia hila.) Hila za Shetani ni za ulaghai na zinadanganya. Shetani hana haya na anawadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti kila kitu chao na kuwadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti hatima zao. Hii inawafanya watu wajinga kuja kumtii kabisa na anawadanganya na sentensi moja ama mbili tu na katika kuchanganyikiwa kwao, watu wanasujudu mbele yake. Hivyo, Shetani anatumia mbinu za aina gani, anasema nini kukufanya umwamini? Kwa mfano, pengine hujamwambia Shetani idadi ya watu katika familia yako, lakini anaweza kusema kwamba kuna watatu katika familia yako, akiwemo binti ambaye ana miaka 7, na pia umri wa wazazi wako. Iwapo ulikuwa na tuhuma na shaka zako mwanzoni, hutahisi kwamba anaaminika zaidi kidogo baada ya kusikia hayo? Na kisha Shetani anaweza kusema, “Kazi imekuwa ngumu kwako leo, wakubwa wako hawakupi utambuzi unaostahili na daima wanafanya kazi dhidi yako.” Baada ya kuyasikia hayo, ungefikiri, “Hiyo ni sahihi kabisa! Mambo hayajakuwa yakienda vizuri kazini.” Hivyo ungemwamini Shetani zaidi kidogo. Kisha angesema kitu kingine kukudanganya, kukufanya umwamini hata zaidi. Kidogo kidogo, utajipata huwezi kupinga ama kuwa na tuhuma kwake tena. Shetani anatumia tu hila chache zisizo na maana, hata ndogo zisizojalisha, kukufadhaisha. Unapofadhaishwa, hutaweza kupata njia zako, hutajua kile cha kufanya, na utaanza kufuata kile Shetani anasema. Hii ni mbinu ya “ah nzuri sana” anayotumia Shetani kumpotosha mwanadamu pahali unapoingia katika mtego wake bila kusudi na unashawishiwa naye. Shetani anakwambia mambo machache ambayo watu wanafikiria kuwa mambo mazuri, na kisha anakwambia kile cha kufanya na kile cha kuepuka na hivyo ndivyo unaanza kufuata njia hiyo bila kusudi. Punde unapoanza kufuata njia hiyo, haitakuwa chochote ila shida kwako; daima utakuwa ukifikiria kile alichosema Shetani na kile alichokwambia ufanye, na bila kujua utamilikiwa naye. Mbona hivi? Ni kwa sababu wanadamu hawana ukweli na hivyo hawawezi kusimama dhidi ya majaribu na ushawishi wa Shetani. Wanapokabiliwa na uovu, udanganyifu, usaliti, na kijicho cha Shetani, wanadamu ni wajinga sana, ni wachanga na wanyonge, siyo? Si hii ni mojawapo ya njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? (Ndiyo.) Mwanadamu anadanganywa na kulaghaiwa bila kusudi, kidogo kidogo, kupitia mbinu mbalimbali za Shetani, kwa sababu hawana uwezo wa kutofautisha kati ya mema na hasi. Hawana kimo hiki, na uwezo wa kumshinda Shetani.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp