Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Utakatifu wa Mungu (II) (Sehemu ya Nne)

5. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu

Mienendo ya kijamii ilianza lini? Je, ni kitu kipya? (La.) Hivyo mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.) Katika akili zenu, ni kipengele kipi cha mienendo hii kinaweza kumpotosha mwanadamu? Ni mienendo ipi inawavutia sana? Watu wengine husema: “Sisi sote tumefikia umri fulani, tuko katika miaka ya arobaini, hamsini, sitini, sabini ama themanini ambapo hatuwezi kufaa katika mienendo hii na haituvutii tena.” Je, hii ni sahihi? Wengine husema: “Hatufuati watu mashuhuri, hicho ni kitu ambacho vijana walio katika umri wa ujana na ishirini wanafanya; pia hatuvai nguo za mitindo ya kisasa, hicho ni kitu ambacho watu wanaojali sura wanafanya.” Kwa hivyo ni ipi kati ya hii inaweza kuwapotosha? (Misemo maarufu.) Je, hii misemo maarufu inaweza kuwapotosha watu? Huu ni msemo mmoja, na mnaweza kuona iwapo unawapotosha watu au la, “Pesa inaifanya dunia izunguke”; huu ni mwenendo? Si hiki ni kitu kibaya zaidi kulinganishwa na mienendo ya mavazi na chakula mliyotaja? (Ndiyo.) “Pesa inaifanya dunia izunguke” ni filosofia ya Shetani na inaenea miongoni mwa wanadamu wote, katika kila jamii ya binadamu. Mnaweza kusema kwamba ni mwenendo kwa sababu umepatiwa kila mtu na sanasana uko katika mioyo yao. Watu walienda kutoka kutoukubali msemo huu hadi kuuzoea ili wanapokutana na maisha halisi, polepole waliukubali kwa kimya, kukiri uwepo wake na hatimaye, waliupa muhuri wao wa idhini. Je, hii si njia ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Pengine watu hawaelewi msemo huu kwa kiwango sawa, lakini kila mtu ana viwango tofauti vya tafsiri na kukiri kwa msemo huu kutokana na mambo ambayo yamefanyika karibu nao na uzoefu wao binafsi, siyo? Licha ya kiwango cha uzoefu mtu anao na msemo huu, ni nini athari mbaya unaweza kuwa nao katika moyo wa mtu? (Watu wangeheshimu pesa.) Kitu fulani kinafichuliwa kupitia tabia ya binadamu ya watu katika dunia hii, ikiwemo kila mmoja wenu. Hiki kinafasiriwa vipi? Ni ibada ya pesa. Ni vigumu kutoa hili kwa moyo wa mtu? Ni vigumu sana! Inaonekana kwamba upotovu wa Shetani kwa mwanadamu ni kamili kabisa! Hivyo baada ya Shetani kutumia mwenendo huu kuwapotosha watu, unaonyeshwa vipi kwao? Hamhisi kwamba hamtaishi katika dunia hii bila pesa yoyote, kwamba hata siku moja haiwezekani? (Ndiyo.) Hadhi ya watu inatokana na kiasi cha pesa wako nayo na pia heshima yao. Migongo ya maskini imekunjwa kwa aibu, ilhali matajiri wanafurahia hadhi zao za juu. Wanatenda kwa njia ya kujigamba na wana majivuno, wakiongea kwa sauti kubwa na kuishi kwa kiburi. Msemo na mwenendo huu unaleta nini kwa watu? Si watu wengi wanaona kupata pesa kunastahili gharama yoyote? Si watu wengi hutoa Heshima na uadilifu wao wakitafuta pesa zaidi? Si watu wengi hupoteza fursa ya kufanya wajibu wao na kumfuata Mungu kwa sababu ya pesa? Si hii ni hasara kwa watu? (Ndiyo.) Si Shetani ni mbaya kutumia mbinu hii na msemo huu kumpotosha mwanadamu kwa kiwango kama hicho? Si hii ni hila yenye kijicho? Unaposonga kutoka kuukataa huu msemo maarufu hadi mwishowe kuukubali kama ukweli, moyo wako unaanguka kabisa chini ya mshiko wa Shetani, na hivyo unakuja kuishi naye bila kusudi. Msemo huu umekuathiri kwa kiwango kipi? Unaweza kujua njia ya ukweli, unaweza kujua ukweli, lakini huna nguvu ya kuufuatilia. Unaweza kujua kwa hakika neno la Mungu, lakini huko radhi kulipa gharama, huko radhi kuteseka kulipa gharama. Badala yake, kwako, ni afadhali utoe siku zako za baadaye na kudura yako kwenda kinyume na Mungu hadi mwisho kabisa. Licha ya kile Mungu anasema, licha ya kile Mungu anafanya, licha ya kiasi unagundua kwamba upendo wa Mungu kwako ni wa kina na mkubwa, bado ungeendelea kwa njia hiyo kwa ukaidi na kulipa gharama ya msemo huu. Hiyo ni kusema huu msemo tayari unadhibiti tabia na fikira zako, na unaona afadhali hatima yako idhibitiwe na msemo huu kuliko kuyatoa yote. Watu wanafanya hivi, wanadhibitiwa na msemo huu na kutawaliwa nao. Hii si athari ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Hii si filosofia na tabia potovu ya Shetani ikikita mizizi kwa moyo wako? Ukifanya hivyo, si Shetani amefikia lengo lake? (Ndiyo.) Unaona jinsi Shetani amempotosha mwanadamu kwa njia hii? (La.) Hukumwona. Unaweza kumhisi? (La.) Hukuihisi. Je, unaona uovu wa Shetani hapa? (Ndiyo.) Shetani humpotosha mwanadamu wakati wote na pahali pote. Shetani anaifanya isiwezekane kwa mwanadamu kujilinda dhidi ya upotovu huu na anamfanya mwanadamu awe mnyonge kwake. Shetani anakufanya ukubali fikira zake, mitazamo yake na mambo maovu yanayotoka kwake katika hali ambapo huna kusudi na huna utambuzi wa kile kinachokufanyikia. Watu wanakubali kikamilifu vitu hivi na hawavibagui. Wanapenda sana vitu hivi na kuvishikilia kama hazina, wanaviacha vitu hivi viwatawale na kuwachezea, na hivi ndivyo upotovu wa Shetani kwa mwanadamu unakuwa wa kina na kina zaidi.

Shetani hutumia mbinu hizi nyingi kumpotosha mwanadamu. Mwanadamu ana maarifa na baadhi ya nadharia za kisayansi, mwanadamu anaishi na ushawishi wa desturi ya kitamaduni, na kila mtu anarithi desturi ya kitamaduni. Mwanadamu ataendeleza desturi ya kitamaduni aliyopewa kutoka kwa Shetani na pia kutenda pamoja na mienendo ya kijamii ambayo Shetani anawapa wanadamu. Binadamu hawezi kutengana na Shetani, kushiriki na kile ambacho Shetani anafanya wakati wote, kukubali udanganyifu, kiburi, kijicho, na uovu wake. Mwanadamu alipomiliki tabia hizi za Shetani, amekuwa na furaha ama huzuni kuishi miongoni mwa wanadamu hawa na katika dunia hii? (Huzuni.) Mbona unasema hivyo? (Amefungwa na vitu hivi na maisha yake ni mapambano machungu.) Hmm. Mtu fulani ambaye ana miwani na anaonekana wa hekima; pengine kamwe hapigi kelele, awe daima na lugha ya kushawishi, wa busara, na zaidi ya hayo, kwa sababu ya umri wake mkubwa, pengine amepitia vitu vingi na kuwa na uzoefu mkubwa; pengine anaweza kuzungumza kwa undani kuhusu masuala makubwa na madogo na kuwa na msingi dhabiti wa kile anachosema; pengine pia ana seti ya nadharia ya kutathmini uhalisi na sababu ya vitu; na watu pengine wanaweza kuangalia tabia yake, sura yake, na kuona jinsi anavyotenda na kuona uadilifu wake na hulka yake na kutopata dosari kwake. Watu kama hawa hasa wanashughulika na mienendo ya kijamii ya sasa na hawachukuliwi kuwa wa mtindo wa kizamani Ingawa mtu huyu anaweza kuwa mzee, kamwe hayuko nyuma ya nyakati na kamwe si mzee sana kufunzwa. Juujuu, hakuna anayeweza kupata dosari kwake, lakini ndani amepotoshwa na Shetani kabisa na kikamilifu. Juujuu hakuna chochote kibaya, yeye ni mpole, ni muungwana, anayo maarifa na maadili fulani; ana uadilifu na vitu anavyojua vinalingana na vile wanavyojua vijana. Hata hivyo, kuhusu asili na kiini chake, mtu huyu ni mfano kamili na unaoishi wa Shetani, ana usawa kabisa na Shetani. Hili ni “tunda” la upotovu wa Shetani kwa mwanadamu. Kile Nilichosema kinaweza kuwaumiza, lakini chote ni ukweli. Maarifa ambayo mwanadamu anasoma, sayansi anayoelewa, na mbinu anazochagua kuingiliana na mienendo ya jamii, bila ubaguzi, ni vyombo vya upotovu wa Shetani. Huu ni ukweli kabisa. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi miongoni mwa tabia ambayo imepotoshwa kabisa na Shetani na mwanadamu hana njia ya kujua utakatifu wa Mungu ni nini na kiini cha Mungu ni nini. Hii ni kwa sababu juujuu mtu hawezi kupata dosari kwa njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu; hakuna anayeweza kuamua kutoka kwa tabia ya mtu kwamba kuna chochote kibaya. Kila mtu anaendelea na kazi yake kwa kawaida na kuishi maisha ya kawaida; wanasoma vitabu na magazeti kwa kawaida, wanasoma na kuzungumza kwa kawaida; watu wengine hata wamejifunza kuwa na sura ya kinafiki ya maadili ili waweze kusema salamu zao, kuwa na heshima, kuwa na adabu, kuwaelewa wengine, kuwa na urafiki, kuwasaidia wengine, kuwa wenye hisani, na wataepuka kulalamika kwa wengine na kuepuka kutumia watu kwa manufaa yao. Hata hivyo, tabia yao iliyopotoka ya kishetani imekita mizizi ndani yao; kiini hiki hakiwezi kubadilishwa kwa kutegemea juhudi za nje. Mwanadamu hana uwezo wa kujua utakatifu wa Mungu kwa sababu ya kiini hiki, na licha ya kiini cha utakatifu wa Mungu kuwekwa wazi kwa mwanadamu, mwanadamu hakichukulii kwa umakini. Hii ni kwa sababu Shetani tayari amemiliki kabisa hisia, fikira, mitazamo, na mawazo ya mwanadamu kupitia njia mbalimbali. Huu umiliki na upotovu si wa muda mfupi ama wa mara kwa mara; upo kila mahali na kila wakati. Kwa hivyo, watu wengi ambao wamemwamini Mungu kwa miaka mitatu au minne—hata miaka sita na saba—bado wanashikilia mawazo na mitazamo ambayo Shetani amewaekea kana kwamba wanashikilia hazina. Kwa sababu mwanadamu ameukubali uovu, kiburi, na mambo kutoka kwa asili ya kijicho ya Shetani, bila kuepukika kwa mahusiano ya ana kwa ana ya mwanadamu mara nyingi kuna migogoro, mara nyingi kuna magombano na kutokuwa na uwiano, mambo ambayo yameumbwa kwa sababu ya asili ya kiburi ya Shetani. Iwapo Shetani angempa mwanadamu vitu vyema—kwa mfano, iwapo Uconfucius na Utao wa desturi ya kitamaduni ambayo mwanadamu alikubali ilichukuliwa kuwa vitu vizuri—watu wa aina sawa wanapaswa kuweza kupatana na wengine baada ya kukubali vitu hivyo, siyo? Hivyo mbona kuna mgawanyiko mkubwa kati ya watu waliokubali vitu sawa? Mbona hivyo? Ni kwa sababu viti hivi vimetoka kwa Shetani na Shetani husababisha mgawanyiko miongoni mwa watu. Vitu ambavyo Shetani anapatiana, bila kujali jinsi vinavyoonekana kuwa vya heshima na vikubwa juujuu, vinamletea mwanadamu na vinaleta katika maisha ya mwanadamu kiburi pekee, na si chochote ila udanganyifu wa asili ovu ya Shetani. Sivyo? Mtu ambaye angeweza kujificha, kumiliki maarifa mengi, ama kuwa na malezi mazuri angekuwa na wakati mgumu kusitiri tabia yao potovu ya kishetani. Hiyo ni kusema, haijalishi mtu huyu atajificha kwa njia ngapi, kama ulimfikiri kuwa mtakatifu, ama kama ulifikiri ni mkamilifu, ama kama ulifikiri ni malaika, haijalishi ulifikiri ni mtu safi vipi, maisha yake yangekuwaje nyuma ya pazia? Utaona asili ipi katika ufunuo wa tabia yake? Bila shaka ungeona asili ovu ya Shetani. Mtu anaweza kusema hivyo? (Ndiyo.) Kwa mfano, tuseme mnamjua mtu wa karibu nanyi ambaye mlifikiri kuwa mtu mzuri, ama ulimfikiri kuwa mtu mzuri, pengine mtu uliyemwabudu kama Mungu. Kwa kimo chako cha sasa, unawafikiri vipi? Kwanza, unaangalia iwapo mtu wa aina hii ana ama hana ubinadamu, iwapo ni mwaminifu, iwapo ana upendo wa kweli kwa watu, iwapo maneno na vitendo vyao vinafaidi na kusaidia wengine. (La.) Yaitwayo wema, upendo na uzuri unaofichuliwa hapa, ni nini kweli? Yote ni uongo, yote ni sura ya kinafiki. Hii sura ya kinafiki ya nyuma ya pazia ina madhumuni maovu ya chinichini: Ni ya kumfanya mtu huyo apendwe na kuabudiwa kama Mungu. Je, mnaona jambo hili kwa dhahiri? (Ndiyo.)

Mbinu ambazo Shetani anatumia kuwapotosha watu zinaletea nini binadamu? Kuna chochote chema kuzihusu? (La.) Kwanza, mwanadamu anaweza kutofautisha kati ya mema na mabaya? Unaona, katika dunia hii, awe ni mtu fulani mkubwa ama jarida fulani, yote yatasema kwamba hiki ama kile ni chema ama kibaya, si hayo ni barabara? Si hayo ni sahihi? (La.) Tathmini zao za matukio na watu ni za haki? Kuna ukweli ndani ya tathmini hizi? (La.) Je, dunia hii ama binadamu huu unatathmini vitu vyema na hasi kulingana na kiwango cha ukweli? (La.) Mbona watu hawana uwezo huo? Watu wamesoma maarifa mengi na wanajua mengi kuhusu sayansi, uwezo wao si mkubwa kutosha? Mbona hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi? Mbona hivi? (Kwa sababu watu hawana ukweli; sayansi na maarifa si ukweli.) Kila kitu Shetani anauletea binadamu ni uovu na upotovu na hakina ukweli, uhai, na njia. Na uovu na upotovu ambao Shetani anamletea mwanadamu, unaweza kusema kwamba Shetani ana upendo? Unaweza kusema kwamba mwanadamu ana upendo? Watu wengine wanaweza kusema: “Huko sahihi, kuna watu wengi duniani kote wanaosaidia maskini na watu wasio na makazi. Si hao ni watu wazuri? Pia kuna mashirika ya hisani ambayo yanafanya kazi nzuri, si kazi yote wanayofanya ni ya uzuri?” Kwa hivyo tunasema nini kuhusu hayo? Shetani anatumia mbinu na nadharia mbalimbali kumpotosha mwanadamu; huu upotovu wa mwanadamu ni dhana isiyo dhahiri? La, siyo dhahiri. Shetani pia anafanya vitu vingine vya utendaji, na pia anakuza mtazamo au nadharia katika dunia hii na katika jamii. Katika kila nasaba na katika kila kipindi cha historia anakuza nadharia na kuingiza baadhi ya fikira ndani ya wanadamu. Fikira na nadharia hizi polepole zinakita mizizi katika mioyo ya watu, na kisha watu wanaanza kuishi kwa nadharia na fikira hizi; si wanakuwa Shetani bila kusudi? Si watu wako kitu kimoja na Shetani? Wakati watu wamekuwa kitu kimoja na Shetani, ni nini mtazamo wao kwa Mungu mwishowe? Si ni mtazamo sawa ambao Shetani anao kwa Mungu? Hakuna anayethubutu kukubali haya, siyo? Ni ya kutisha sana! Mbona Nasema kwamba asili ya Shetani ni ovu? Hii inaamuliwa na kuchambuliwa kulingana na kile Shetani amefanya na vitu ambavyo Shetani amefichua; si bila ustahili kusema kwamba Shetani ni mwovu. Iwapo Ningesema tu kwamba Shetani ni mwovu, mngefikiri nini? Mngefikiri, “Bila shaka Shetani ni mwovu.” Hivyo nitakuuliza: “Ni kipengele kipi cha Shetani ni ovu?” Ukisema: “Shetani kumpinga Mungu ni uovu,” bado hutakuwa ukizungumza kwa uwazi. Sasa tumesema mambo maalum kwa njia hii; je, mna uelewa kuhusu maudhui maalum ya kiini cha uovu wa Shetani? (Ndiyo.) Sasa kwa kuwa mmekuwa na huu uelewa wa asili ovu ya Shetani, ni kiasi gani mnaelewa kuhusu nyinyi wenyewe? Je, mambo haya yanahusiana? (Ndiyo.) Je, uhusiano huu unawaumiza? (La.) Ni wenye msaada kwenu? (Ndiyo.) Ninaposhiriki kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, ni muhimu Niwe na ushirika kuhusu kiini ovu cha shetani, ni nini maoni yako? (Ndiyo, ni muhimu.) Mbona? (Uovu wa Shetani unauweka utakatifu wa Mungu katika heshima ya juu.) Je, ndivyo ilivyo? Hii ni sahihi kidogo kwa sababu bila uovu wa Shetani, watu hawatajua kuhusu utakatifu wa Mungu; hii ni sahihi. Hata hivyo, ukisema kwamba utakatifu wa Mungu upo tu kwa sababu ya tofauti yake na uovu wa Shetani, hii ni sahihi? Hii hoja si sahihi. Utakatifu wa Mungu ni kiini kiasilia cha Mungu; hata ingawa Mungu anaufichua kupitia matendo Yake, hili bado ni onyesho asili la kiini cha Mungu na ni kiini kiasilia cha Mungu; daima kimekuwepo na ni cha Mungu Mwenyewe lakini mwanadamu hawezi kukiona. Hii ni kwa sababu mwanadamu anaishi katikati ya tabia potovu ya Shetani na chini ya ushawishi wa Shetani, na hawajui kuhusu utakatifu, sembuse maudhui maalum ya utakatifu wa Mungu. Hivyo, ni muhimu kweli kwamba tushiriki kwanza kuhusu kiini ovu cha Shetani? (Ndiyo, ni muhimu.) Unaona, tumeshiriki kuhusu vipengele vingi vya upekee wa Mungu na hatukutaja kiini cha Shetani, siyo? Watu wengine wanaweza kuonyesha baadhi ya shaka kama, “Unashiriki kuhusu Mungu Mwenyewe, mbona Unazungumza daima kuhusu jinsi Shetani anawapotosha watu na jinsi asili ya Shetani ni ovu?” Umeyaweka mapumzikoni mashaka haya? (Ndiyo.) Uliyawekaje mapumzikoni? (Kupitia ushirika wa Mungu, tulitofautisha kile ambacho ni ovu.) Wakati watu wana utambuzi wa uovu na wakati wana ufafanuzi sahihi wa uovu, wakati watu wanaweza kuona wazi maudhui maalum na udhihirisho wa uovu, chanzo na kiini cha uovu—wakati utakatifu wa Mungu unajadiliwa sasa—watu basi watatambua wazi, ama kuufahamu wazi kama utakatifu wa Mungu, kama utakatifu wa kweli. Nisipojadili uovu wa Shetani, watu wengine wataamini kimakosa kwamba kitu fulani ambacho watu wanafanya katika jamii ama miongoni mwa watu—ama kitu fulani katika dunia hii—kinaweza kuhusiana na utakatifu. Si mtazamo huu ni wa makosa? (Ndiyo.)

Hivi, Nimeshiriki kuhusu kiini cha Shetani. Mmefikia uelewa upi wa utakatifu wa Mungu kupitia uzoefu wenu wa miaka ya hivi karibuni, kutokana na nyinyi kuona neno la Mungu na kutokana na kupitia kazi Yake? Endelea, na uuzungumzie. Si lazima utumie maneno yanayofurahisha sikio, zungumza tu kutoka kwa uzoefu wako mwenyewe, utakatifu wa Mungu ni upendo Wake tu? Ni upendo wa Mungu tu tunaoelezea kama utakatifu? Huo utakuwa wa upande mmoja sana, siyo? Si huo utakuwa wa upande mmoja? (Ndiyo.) Mbali na upendo wa Mungu, kuna vipengele vingine vya kiini cha Mungu ambavyo mmeona? (Ndiyo.) Mmeona nini? (Mungu anachukia tamasha na likizo, mila, na ushirikina; huu ni utakatifu wa Mungu.) Ulisema tu kwamba Mungu anachukia mambo fulani; Mungu ni mtakatifu kwa hivyo Anachukia vitu, inamaanisha hivyo? (Ndiyo.) Katika mizizi ya hayo, ni nini utakatifu wa Mungu? Utakatifu wa Mungu hauna maudhui makubwa, ni kwamba tu Anachukia vitu? Katika akili zenu mnafikiria, “Kwa sababu Mungu anachukia vitu hivi ovu, hivyo mtu anaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu”? Si huu ni uvumi hapa? Si hii ni aina ya dhana na hukumu? Ni nini mwiko mkubwa zaidi inapokuja kwa kuelewa kiini cha Mungu? (Kuacha ukweli nyuma.) Ni wakati tunaacha ukweli nyuma kuzungumza kuhusu mafundisho ya kidini, huu ni mwiko mkubwa sana kufanya. Kitu kingine? (Uvumi na ubunifu.) Uvumi na ubunifu, huu pia ni mwiko wa nguvu sana. Mbona uvumi na ubunifu si wa manufaa? Vitu unavyobashiri kuhusu na kufikiria vitu ambavyo kweli unaweza kuona? (La.) Ni kiini cha kweli cha Mungu? (La.) Nini tena ni mwiko? Ni mwiko kuhesabu tu kifungu cha maneno yanayosikika kuwa mazuri kueleza kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Si huku ni kujigamba na upuuzi? Hukumu na uvumi ni upuuzi, kama tu kuchukua maneno yanayosikika kuwa mazuri. Sifa tupu pia ni upuuzi, siyo? (Ndiyo.) Je, Mungu anafurahia kusikiza watu wakisema upuuzi wa aina hii? (La, hafurahii.) Ni nini kisawe cha “kutofurahia” kitu? (Kuhisi kutostareheka.) Anahisi kutostareheka kusikia huu upuuzi! Mungu anaongoza na kuokoa kundi la watu, na baada ya kundi hili la watu kusikia maneno Yake hawaelewi Anachomaanisha. Mtu anaweza kuuliza: “Mungu ni mwema?” na wangejibu, “Mwema!” “Mwema vipi?” “Mwema sana sana!” “Mungu anampenda mwanadamu?” “Ndiyo!” “Kiasi gani?” “Sana, sana zaidi!” “Unaweza kuelezea upendo wa Mungu?” “Ni wa kina zaidi kuliko bahari, wa juu zaidi kuliko anga!” Si huu ni upuuzi? Si huu upuuzi ni sawa na kile mlichotoka kusema kuhusu, “Mungu anachukia tabia potovu ya Shetani, hivyo Mungu ni mtakatifu”? (Ndiyo.) Si kile mlichotoka kusema ni upuuzi? Mengi ya haya mambo ya upuuzi yanayosemwa yanatoka wapi? (Shetani.) Yanatoka kwa Shetani. Mambo ya upuuzi yanayosemwa kimsingi yanatoka kwa kutowajibika kwa watu na kutomheshimu Mungu. Tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Hukuwa na uelewa wowote lakini bado uliongea upuuzi, si huku ni kutowajibika? Si ni kutomheshimu Mungu? Umesoma kiasi kidogo cha maarifa, umeelewa kiasi kidogo cha kufikiria, na kiasi kidogo cha mantiki, ambayo umetumia hapa na, zaidi, umefanya hivyo ukimjua Mungu. Unafikiri Mungu anahisi kutostareheka kuyasikia hayo? Mnawezaje kumjua Mungu mkitumia mbinu hizi? Je, si hayo yanasikika kuwa ya kufedhehesha? Kwa hivyo, inapokuja kwa maarifa ya Mungu, mtu lazima awe makini sana; mahali unapojua Mungu, zungumza tu kuhusu hayo. Zungumza kwa uaminifu na kivitendo na usipambe maneno yako na pongezi za kawaida na usitumie sifa isiyostahilika; Mungu haihitaji na kitu kama hiki kinatoka kwa Shetani. Tabia ya Shetani ni ya kiburi na Shetani anapenda kupewa sifa isiyostahilika na kusikia maneno mazuri. Shetani ataridhishwa na kufurahia iwapo watu watataja maneno yote mazuri ambayo wamejifunza na kutumia maneno haya kwa Shetani. Lakini Mungu hahitaji hii; Mungu hahitaji kuvishwa kilemba cha ukoka ama sifa isiyostahilika na Hahitaji kwamba watu wazungumze upuuzi na kumsifu kwa upofu. Mungu anachukizwa sana na hata Hatasikiza sifa ambayo haiko sambamba na ukweli. Hivyo, wakati watu wengine wanamsifu Mungu kwa upofu na kile wanachosema hakilingani na kile kiko katika mioyo yao na wanapofanya viapo kwa upofu na kumwomba ovyo ovyo, Mungu hasikizi hata kidogo. Lazima uwajibike kwa kile unachosema. Ikiwa hujui jambo, sema tu; ikiwa unajua jambo, onyesha hivyo kwa njia ya kitendo. Sasa, kwa maudhui halisi ya utakatifu wa Mungu, mna uelewa maalum kuuhusu? (Nilipofichua uasi, nilipokuwa na makosa, nilipokea hukumu na kuadibu kwa Mungu, na hapo niliona utakatifu wa Mungu. Na nilipokabiliana na mazingira ambayo hayakukubaliana na matarajio yangu, niliomba kuhusu mambo haya na kutafuta nia za Mungu na Mungu aliponipa nuru na kuniongoza na maneno Yake, niliona utakatifu wa Mungu.) Haya yametoka kwa uzoefu wako mwenyewe, siyo? (Nimeona kwa kile Mungu amezungumzia kwamba mwanadamu amepotoshwa na kudhuriwa na Shetani hivi. Hata hivyo, Mungu ametoa yote kutuokoa na kutokana na haya naona utakatifu wa Mungu.) Hii ni njia ya kweli ya kuzungumza na ni maarifa ya kweli. Kuna maoni mengine tofauti na haya? (Sijui iwapo uelewa wangu ni sahihi au la. Naona uovu wa Shetani kutoka kwa maneno alisema ili kumlaghai Hawa kutenda dhambi na ushawishi wake wa Bwana Yesu. Kutoka kwa maneno ambayo kwayo Mungu aliwaambia Adamu na Hawa kile walichoweza na wasichoweza kula, naona kwamba maneno ya Mungu ni wazi na safi na kwamba ni ya kuaminiwa; kutoka kwa haya naona utakatifu wa Mungu.) Kwa kile mmesikia watu hawa wakisema, mnasema Amina zaidi kwa maneno ya nani? Matamshi ya nani, ushirika wa nani ulikuwa karibu zaidi na ushirika wa mada yetu leo, ya nani ilikuwa ya kweli zaidi? Ushirika wa dada wa mwisho ulikuwa vipi? (Mzuri.) Unasema Amina kwa kile alichosema, ni nini alichosema kilichokuwa sahihi kwa lengo? Unaweza kuwa wazi, sema unachotaka kusema na usijali kuhusu kutokuwa sahihi. (Katika maneno ambayo ndugu alizungumza hivi karibuni, nilisikia kwamba neno la Mungu linaeleweka kwa urahisi na ni wazi sana, si kama maneno ya Shetani yasiyo ya moja kwa moja. Niliona utakatifu wa Mungu kwa haya.) Hii ni sehemu ya hayo. Je, nyote mlisikia kilichosemwa hivi karibuni? (Ndiyo.) Kilikuwa sahihi? (Ndiyo.) Hebu tumpigie dada makofi. Vizuri sana. Naona kwamba mmepata kitu katika shirika hizi mbili za hivi karibuni, lakini lazima nyinyi mwendelee kufanya kazi kwa bidii. Ni lazima mfanye kazi kwa sababu kuelewa kiini cha Mungu ni somo kubwa sana; si kitu ambacho mtu anaweza kuelewa mara moja ama anaweza kuzungumza wazi kwa maneno machache tu.

Kila kipengele cha tabia potovu ya Kishetani ya watu, maarifa, filosofia, fikira na mitazamo ya watu, na vipengele binafsi vinawazuia pakubwa kujua kiini cha Mungu; hivyo mnapozisikia mada hizi, mada zingine zinaweza kuwa mbali kwenu kufikia, mada zingine pengine hamtaelewa, ilhali mada zingine pengine kimsingi hamtalingana nazo na hali halisi. Licha ya hayo, Nimesikia kuhusu uelewa wenu wa utakatifu wa Mungu na Najua kwamba katika mioyo yenu mmeanza kukubali kile Nilichosema na kushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu. Najua kwamba katika mioyo yenu hamu yenu ya kuelewa kiini cha utakatifu wa Mungu imeanza kuchipuka. Lakini ni nini kinachonifanya kuwa na furaha zaidi? Ni kwamba wengine wenu tayari wanaweza kutumia maneno rahisi sana kuelezea maarifa yenu ya utakatifu wa Mungu. Ingawa hiki ni kitu rahisi kusema na Nimekisema awali, katika mioyo ya wengi wenu hii bado haijakubaliwa ama kuweka alama. Hata hivyo, wengine wenu wameweka maneno haya moyoni na ni vizuri kabisa na huu ni mwanzo mzuri sana. Natumai kwamba kwa mada ambazo mnafikiri kuwa za maana sana—ama kwa mada ambazo ziko mbali kwenu kufikia—mtaendelea kutafakari, na kufanya ushirika zaidi na zaidi. Kwa yale masuala ambayo yako mbali kwenu kufikia kutakuwa na mtu wa kuwapa mwongozo zaidi. Mkishiriki katika ushirika zaidi kuhusu maeneo ambayo mnaweza kufikia sasa, Roho Mtakatifu atafanya kazi Yake na mtakuwa na uelewa mkubwa zaidi. Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa. Iwapo mwanadamu anamwamini Mungu lakini hamjui Mungu, na iwapo mwanadamu anaishi miongoni mwa baadhi ya barua na mafundisho ya kidini, hutawahi kufikia wokovu hata kama utatenda na kuishi kulingana na maana ya juujuu ya ukweli. Hiyo ni kusema, iwapo imani yako kwa Mungu haitokani na kumjua, basi imani yako haimaanishi chochote. Unaelewa, sivyo? (Ndiyo, tunaelewa.) Ushirika wetu utaishia hapa kwa leo. (Mshukuru Mungu!)

Januari 4, 2014

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?