Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Mamlaka ya Mungu (II) (Sehemu ya Saba)

Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu

Baada ya kusikiliza kila kitu Nilichomaliza kusema, je, fikira yenu ya hatima imebadilika? Mnaelewa vipi hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Ili kuiweka kwa urahisi, katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali isiyoshindika ya mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanavyodhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoshindika, mfumo huu wa kudhibiti na kutawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya mambo yote, zinazoruhusu binadamu kuweza kuhama hadi kwenye mwili tofauti baada ya kifo tena na tena bila uingiliaji kati, zinazofanya ulimwengu kugeuka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Mmeshuhudia hoja hizi zote na unazielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Kujua kwako vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, ni vipi unajua vyema hali halisi ya Mungu na tabia yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, uwepo wa ukuu wa Mungu na mipangilio unategemea kama binadamu wanainyenyekea? Je, hoja kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na kama binadamu watayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, mapenzi Yake. Hali hii haitabadilika kwa sababu binadamu hubadilika, na iko huru wala haitegemei mapenzi ya binadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya muda, anga, na jiografia, kwani mamlaka ya Mungu ndiyo hali yake halisi kabisa. Kama binadamu anaweza kujua na kuukubali ukuu wa Mungu, na kama binadamu anaweza kuunyenyekea, haiwezi kwa vyovyote vile kubadilisha hoja kwamba ukuu wa Mungu upo juu ya hatima ya binadamu. Hivi ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, hauwezi tu kubadilisha hoja kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, angali Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na hoja ya ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, havibadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo yako ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila muda. Kama mbingu na nchi zingepita, mamlaka Yake yasingewahi kupita, kwani Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala viumbe wote, hutosheleza viumbe wote, huunda na kupangilia viumbe wote, kama Alivyofanya siku zote. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Hii ni hoja; huu umekuwa ukweli usiobadilika tangu zama za kale!

Mtazamo na Matendo Bora ya Mtu Anayependa Kujinyenyekeza katika Mamlaka ya Mungu

Mwanadamu anatakiwa kuwa na mtazamo gani sasa katika kujua na kujali mamlaka ya Mungu, hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Hili ni tatizo la kweli linalokabili kila mmoja. Wakati wa kukabiliana na matatizo ya kweli ya maisha, unafaa kujua na kuelewa vipi mamlaka ya Mungu na ukuu Wake? Wakati hujui namna ya kuelewa, kushughulikia, na kupitia matatizo haya, ni mtazamo gani unaofaa kutumia ili kuonyesha nia yako, tamanio lako, na uhalisia wako wa kujinyenyekeza katika ukuu na mipangilio ya Mungu? Kwanza lazima ujifunze kusubiri; kisha lazima ujifunze kutafuta; kisha lazima ujifunze kujinyenyekeza. “Kusubiri” kunamaanisha kusubiria muda wa Mungu, kusubiria watu, matukio, na mambo ambayo Amekupangilia wewe, kusubiria mapenzi Yake ili yaweze kwa utaratibu kujifichua kwako. “Kutafuta” kunamaanisha kuangalia na kuelewa nia za Mungu katika fikira Zake kwako wewe kupitia watu, matukio, na mambo ambayo Amekuwekea wazi, kuelewa ukweli kupitia mambo hayo, kuelewa kile ambacho binadamu lazima watimize na njia ambazo lazima waendeleze, kuelewa kile ambacho lazima kitimizwe na njia ambazo lazima wahifadhi, waelewe ni matokeo gani ambayo Mungu analenga kutimiza kwa binadamu na ni utimilifu gani Analenga kutimiza ndani yao. “Kujinyenyekeza,” bila shaka, kunaashiria kukubali watu, matukio, na mambo ambayo Mungu amepanga, kukubali ukuu Wake na, kwa yote, kupata kujua namna ambavyo Muumba anaamuru hatima ya binadamu, namna Anavyomjaliza binadamu na maisha Yake, na namna Anavyofanya kazi ya ukweli katika binadamu. Mambo yote katika mipangilio na ukuu wa Mungu hutii sheria za kimaumbile, na kama utaamua kumwachia Mungu kupangilia na kuamuru kila kitu kwa niaba yako, unafaa kujifunza kusubiri, unafaa kujifunza kutafuta, unafaa kujifunza kujinyenyekeza. Huu ndio mtazamo ambao kila mtu anayetaka kujinyenyekeza katika mamlaka ya Mungu lazima awe nao, ubora wa kimsingi ambao kila mmoja anayetaka kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu lazima aumiliki. Ili kushikilia mtazamo kama huu, kumiliki ubora kama huu, lazima mfanye kazi kwa bidii zaidi; na ndipo mnapoweza kuingia kwenye uhalisi wa kweli.

Kumkubali Mungu kama Bwana Wenu wa Kipekee Ndiyo Hatua ya Kwanza katika Kutimiza Wokovu

Ukweli kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni ukweli ambao kila mmoja lazima atilie maanani kwa umakinifu, lazima apitie na aelewe katika moyo wake; kwani ukweli huu unao mwelekeo katika maisha ya kila mmoja, kwenye maisha ya kale, ya sasa, na ya siku za usoni ya kila mmoja, kwenye awamu muhimu ambazo kila mtu lazima apitie maishani, katika maarifa ya binadamu kuhusu ukuu wa Mungu na mtazamo ambao anafaa kuwa nao katika mamlaka ya Mungu, na kawaida, kwa kila hatima ya mwisho ya kila mmoja. Kwa hivyo inachukua nguvu za maisha yako yote kujua na kuyaelewa. Unapochukua mamlaka ya Mungu kwa umakinifu, unapoukubali ukuu wa Mungu, kwa utaratibu utaanza kutambua na kuelewa kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo. Lakini kama hutawahi kutambua mamlaka ya Mungu, hutawahi kukubali ukuu Wake, basi haijalishi ni miaka mingapi utakayoishi, hutafaidi hata chembe maarifa ya ukuu wa Mungu. Kama hutajua na kuelewa kwa kweli mamlaka ya Mungu, basi utakapofika mwisho wa barabara, hata kama utakuwa umesadiki katika Mungu kwa miongo mingi, hutakuwa na chochote cha kuonyesha katika maisha yako, maarifa yako ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu yatakuwa kwa hakika sufuri bin sufuri. Huoni kuwa jambo hili ni la huzuni mno? Kwa hivyo haijalishi umetembea kwa umbali gani maishani, haijalishi unao umri wa miaka mingapi sasa, haijalishi safari inayosalia itakuwa ya umbali gani, kwanza lazima utambue mamlaka ya Mungu na kuyamakinikia, ukubali hoja kwamba Mungu ni Bwana wako wa kipekee. Kutimiza maarifa yaliyo wazi, sahihi na kuelewa ukweli huu kuhusiana na ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni funzo la lazima kwa kila mmoja, ndio msingi wa kuyajua maisha ya binadamu na kutimiza ukweli, ndiyo maisha ya kila siku na mafunzo ya kimsingi ya kumjua Mungu ambayo kila mmoja anakabiliana nayo, na ambayo hakuna yeyote anayeweza kuyakwepa. Kama mmoja wenu angependa kuchukua njia za mkato ili kufikia shabaha hii, basi Ninakuambia, hilo haliwezekani! Kama mmoja wenu anataka kukwepa ukuu wa Mungu, basi hilo nalo ndilo haliwezekani zaidi! Mungu ndiye Bwana wa pekee wa binadamu, Mungu ndiye Bwana wa pekee wa hatima ya binadamu, na kwa hivyo haiwezekani kwa binadamu kuamuru hatima yake mwenyewe, haiwezekani kwake kuishinda. Haijalishi uwezo wa mtu ni mkubwa kiasi kipi, mtu hawezi kuathiri, sikwambii kuunda, kupangilia, kudhibiti, au kubadilisha hatima za wengine. Yule Mungu Mwenyewe wa kipekee ndiye Anayeweza kuamuru tu mambo yote kwa binadamu, kwani Yeye tu ndiye anayemiliki mamlaka ya kipekee yanayoshikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu; na kwa hivyo Muumba pekee ndiye Bwana wa kipekee wa binadamu. Mamlaka ya Mungu yanashikilia ukuu sio tu juu ya binadamu walioumbwa, lakini juu ya hata viumbe ambavyo havikuumbwa visivyoweza kuonekana na binadamu, juu ya nyota, juu ya ulimwengu mzima. Hii ni hoja isiyopingika, hoja ambayo kweli ipo, ambayo hakuna binadamu au kiumbe chochote kinaweza kubadilisha. Kama mmoja wenu angali hajatosheka na mambo kama yalivyo, akiamini kwamba una ujuzi fulani maalum au uwezo, na bado anafikiria unaweza kubahatika na kubadilisha hali zako za sasa au vinginevyo kuzitoroka; kama utajaribu kubadilisha hatima yako kupitia kwa jitihada za binadamu, na hivyo basi kujitokeza kati ya wengine na kupata umaarufu na utajiri; basi Ninakwambia, unayafanya mambo kuwa magumu kwako, unajitakia taabu tu, unajichimbia kaburi lako mwenyewe! Siku moja, hivi karibuni au baadaye, utagundua kwamba ulifanya chaguo baya, kwamba jitihada zako ziliambulia patupu. Malengo yako, tamanio lako la kupambana dhidi ya hatima, na mwenendo wako binafsi wa kupita kiasi, utakuongoza kwenye barabara isiyoweza kukurudisha kule ulikotoka, na kwa hili utaweza kujutia baadaye. Ingawaje sasa huoni ubaya wa athari hiyo, unapopitia na kushukuru zaidi na zaidi ukweli kwamba Mungu ndiye Bwana wa hatima ya maisha, utaanza kwa utaratibu kutambua kile Ninachozungumzia leo na athari zake za kweli. Haijalishi kama kwa kweli unao moyo na, haijalishi kama wewe ni mtu anayependa ukweli, inategemea tu ni mtazamo aina gani ambao utachukua kuhusiana na ukuu wa Mungu na ule ukweli. Na kwa kawaida, hili linaamua kama kweli unaweza kujua na kuelewa mamlaka ya Mungu. Kama hujawahi katika maisha yako kuhisi ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hujawahi kutambua na kukubali mamlaka ya Mungu, basi utakosa thamani kabisa, bila shaka utakuwa athari ya chukizo na zao la kukataliwa na Mungu, hayo yote ni kutokana na njia uliyochukua na chaguo ulilofanya. Lakini wale ambao, katika kazi ya Mungu, wanaweza kukubali jaribio Lake, kukubali ukuu Wake, kujinyenyekeza katika mamlaka Yake, na kufaidi kwa utaratibu hali halisi waliyopitia na matamshi Yake, watakuwa wametimiza maarifa halisi ya mamlaka ya Mungu, ufahamu halisi wa ukuu Wake, na watakuwa kwa kweli watakuwa wanatii Muumba. Watu kama hao tu ndio watakaokuwa wameokolewa kwa kweli. Kwa sababu wameujua ukuu wa Mungu, kwa sababu wameukubali, shukrani yao ya na kujinyenyekeza kwao katika hoja ya Mungu juu ya hatima ya binadamu ni ya halisi na sahihi. Wanapokabiliana na kifo wataweza, kama Ayubu, kuwa na akili isiyotishika na kifo, kujinyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Mungu katika mambo yote, bila chaguo lolote la kibinafsi, bila tamanio lolote la kibinafsi. Mtu kama huyo tu ndiye atakayeweza kurudi katika upande wa Muumba kama kiumbe cha kweli cha binadamu kilichoumbwa.

Desemba 17, 2013

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp