Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Mamlaka ya Mungu (I) (Uendelezo wa Sehemu ya Pili)

Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine

Bila kuchoka, kazi ya Muumba ya kuumba viumbe vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa viumbe vyote. Siku hii ilikuwa mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine isiyo ya kawaida. Nini, basi, kilikuwa mpango wa Muumba mkesha wa siku hii mpya? Ni viumbe vipi vipya ambavyo Angezalisha, je, Angeviumba? Sikiliza, hii ndiyo sauti ya Muumba….

“Naye Mungu aksema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri” (Mwa 1:24-25). Viumbe hai gani ndivyo vinavyojumuishwa hapa? Maandiko yanasema: ng’ombe, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye siku hii hakukuweko tu na aina zote za viumbe hai kwenye nchi, lakini pia vyote vilikuwa vimeainishwa kulingana na aina, na, vilevile, “Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.”

Kama tu kwenye siku zile tano za awali, na kwa sauti sawa, kwenye siku ya sita Muumba akashurutisha kuzaliwa kwa viumbe hai Alivyotamani, na vikajitokeza kwenye nchi, kila kimoja kulingana na aina yake. Wakati Muumba anapotekeleza mamlaka Yake, hakuna matamshi Yake yanayotamkwa bure bilashi, na kwa hivyo, kwenye siku ya sita, kila kiumbe hai ambacho Alikuwa amenuia kuumba kikajitokeza wakati ule Aliochagua. Muumba aliposema “Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake,” nchi ilijawa mara moja na maisha, na juu ya ardhi kukaibuka pumzi za aina zote za viumbe hai…. Kwenye jangwa lenye nyasi za kijani, ng’ombe wanene, wakichezesha mikia yao huku na kule, walijitokeza mmoja baada ya mwengine, kondoo waliokuwa wakitoa milio walikusanyika kwa makundi, na farasi waliotoa milio wakaanza kurukaruka…. Mara moja, nchi pana tambarare yenye utulivu ikajaa uhai…. Kujitokeza kwa mifugo hii mbalimbali kulikuwa mandhari ya kupendeza kwenye nchi ile tambarare iliyotulia, na kujitokeza huko kukaleta nguvu zisizo na mipaka…. Wangekuwa wenza wa nchi ile tambarare, na wenyeji wakuu wa nchi ile tambarare, kila mmoja akitegemea mwengine; na vilevile ndivyo pia wangekuwa walezi na walinzi wa ardhi hizi, ambazo zingekuwa makao yao ya kudumu, na ambazo zingewapa kila kitu walichohitaji, chanzo cha ukuzwaji wa milele kwa minajili ya kuwepo kwao …

Kwenye siku iyo hiyo ambayo mifugo hii mbalimbali ilijitokeza, kwa tamko la Muumba, wadudu wengi pia walijitokeza, mmoja baada ya mwengine. Hata ingawaje ndio waliokuwa viumbe hai wadogo zaidi miongoni mwa viumbe vyote, nguvu zao za uhai zilikuwa bado uumbaji wa kimiujiza wa Muumba, na hawakuwasili wakiwa wamechelewa sana…. Baadhi yao walipigapiga mabawa yao madogo, huku wengine wakitambaa polepole; baadhi waliruka juu kwa juu, wengine wakapepesuka; wengine walichimba wakienda mbele, huku wengine wakirudi nyuma kwa haraka; wengine walienda upandeupande, wengine wakaruka juu na chini…. Wote walishughulika kwa kujaribu kujitafutia makao: Baadhi walisukumana na kujipata kwenye nyasi, baadhi walianza kuyachimba mashimo ardhini, baadhi wakapaa hadi kwenye miti, wakiwa wamejificha kwenye msitu…. Ingawaje walikuwa wadogo kwa ukubwa, hawakuwa radhi kuvumilia mateso ya njaa, na baada ya kupata makao yao binafsi, walikimbia kutafuta chakula ili kuweza kujilisha. Baadhi yao walipanda juu ya nyasi ili wale ncha zake laini, baadhi yao walikamata uchafu kwenye vinywa vyao na kuanza kulisha matumbo yao, wakila kwa bidii na kwa furaha (kwao, hata uchafu ulikuwa mlo wenye ladha); wengine walikuwa wamejificha misituni, lakini hawakusita kupumzika, kwani majimaji ndani ya majani yale ya kijani kolevu cha kumetameta yaliwapa mlo wenye utomvu mwingi…. Baada ya wao kushiba, bado wadudu hawakusita kufanya shughuli zao; ingawa walikuwa wadogo kwa kimo, walimilikiwa na nishati ya ajabu pamoja na uchangamfu usio na mipaka, na kwa viumbe vyote wao ndio walikuwa amilifu zaidi na wenye bidii zaidi. Hawakuwahi kuwa wazembe, na hawakuhusika katika mapumziko yoyote. Baada ya kushiba, bado walifanya kazi na wakafanyiza miili yao bidii kwa minajili ya siku zao za usoni, wakiwa wamejishughulisha na kukimbia hapa na pale kwa minajili ya kesho yao ili waweze kuishi…. Kwa utaratibu waliweza kuimba nyimbo zenye midundo tofauti ili kuhimizana na kusihi kila mmoja wao aendelee na kazi. Waliweza pia kuongeza furaha kwenye nyasi, miti, na kila inchi ya udongo, huku wakifanya kila siku, na kila mwaka kuwa wa kipekee…. Wakiwa na lugha zao binafsi na kwa njia zao wenyewe, walipitisha taarifa kwa viumbe vyote vilivyokuwa ardhini. Na wakitumia mkondo wao binafsi maalum wa maisha, waliweka alama katika viumbe vyote, na baadaye wakaacha alama…. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana na mchanga, nyasi, na misitu, na walipatia mchanga nguvu na uthabiti, vivyo hivyo kwenye nyasi, na misitu na wakaweza kuleta ushawishi na salamu za Muumba kwa viumbe hai vyote …

Mtazamo wa Muumba ulienea kotekote kwenye viumbe vyote ambavyo Alikuwa ameumba na wakati huu kwa muda huo macho Yake yalitulizia misitu na milima, akili Yake ikigeuka. Huku matamshi Yake yakitamkwa wazi kwenye misitu mingi, na juu ya milima, kulionekana aina ya viumbe fulani vilivyokuwa tofauti na vyovyote vile vilivyokuwa vimekuja hapo awali: Walikuwa wanyama wa mwitu waliotamkwa kwa kinywa cha Mungu. Walikuwa wamepitiliza muda mrefu ajabu, walitikisa vichwa vyao na kupigapiga mikia yao, huku kila mmoja wao akiwa na uso wake pekee. Baadhi yao walikuwa na manyoya mengi, baadhi yao walikuwa wamejikinga, baadhi yao walikuwa na meno ya sumu, baadhi yao walikuwa wanakenua, baadhi yao walikuwa na shingo-ndefu, baadhi yao walikuwa na mkia—mfupi, baadhi walikuwa na macho—mapana, baadhi walikuwa na mtazamo wa woga, baadhi walikuwa wamejiinamia ili wale nyasi, baadhi walikuwa na damu midomoni mwao, baadhi walikuwa wakidundadunda kwa miguu miwili, baadhi walikuwa wakirukaruka kwa kwato nne, baadhi walikuwa wakiangalia mbele juu ya mti, baadhi walikuwa wamejilalia tu wakisubiria misituni, baadhi walikuwa wakitafuta vyumba vya chini kwa chini ili kupumzika, baadhi walikuwa wakikimbiakimbia na kuonyesha furaha ya kipekee kwenye nchi tambarare, baadhi walikuwa wakinyatianyatia kwenye misitu…; baadhi walikuwa wakinguruma, baadhi walikuwa wakitoa milio mikali, baadhi walikuwa wakibweka, baadhi walikuwa wakilia…; baadhi walikuwa na sauti nyororo, baadhi walikuwa na sauti ya kati, baadhi walikuwa na sauti nzito, baadhi walikuwa na sauti safi na yenye mdundo wa kimuziki…; baadhi walikuwa wa kuogofya, na baadhi walikuwa warembo, na baadhi walikuwa wakitisha, baadhi walikuwa wa kuvutia, baadhi walikuwa wa kutishia, baadhi walikuwa wasio na hatia ila wachangamfu…. Mmoja baada ya mwengine, wote walikuja. Tazama namna walivyotembea, kwenye uhuru, wasijue chochote kuhusu wenzao waliokuwa kando yao, wasitake hata kuchukua muda kutazamana…. Kila mmoja akiwa na maisha fulani waliyopewa na Muumba, na umwitu wao binafsi, na ukatili, walionekana kwenye misitu na pia juu ya milima. Viumbe vya kudharauliwa kati ya vyote, na vyenye kuamrisha kabisa—ni nani aliyewafanya kuwa mabingwa wa kweli wa milimani na misituni? Kutoka muda ambao Kuonekna kwao kuliamriwa na Muumba, waliweza “kuweka madai” hayo katika misitu, na “kuweka madai” kwenye milima, kwani Muumba alikuwa tayari amepangilia mipaka yao na Akaamua upana wa uwepo wao. Hawa ndio waliokuwa mabwana wa kweli wa milimani na misitu, na ndiyo maana walikuwa na umwitu mwingi na kwa hivyo wenye dharau. Waliitwa “wanyama wa mwituni” kimsingi kwa sababu, kati ya viumbe vyote, ndio waliokuwa wasiowezekana, wenye unyama, na wasiofugwa. Wasingeweza kufugwa, hivyo basi wasingeweza kulelewa na wasingeishi kwa amani na mapatano na mwanadamu au kufanya kazi kwa niaba ya mwanadamu. Ni kwa Sababu hawakuweza kufugwa, hawakuweza kumfanyia kazi mwanadamu, ndiyo maana iliwalazimu kuishi kwa umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kusongelewa na mwanadamu. Na ilikuwa kwa sababu waliishi umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kukaribiwa na mwanadamu ndiposa waliweza kutimiza wajibu wao waliopewa na Muumba: kuilinda milima na misitu. Ule umwitu wao uliilinda milima na kulinda misitu, na ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi na wenye hakikisho la uwepo wao na utekelezaji wao. Wakati uo huo, umwitu wao uliendeleza na kuhakikisha usawazisho miongoni mwa viumbe vyote. Kuwasili kwao kulileta msaada na ukitaji mizizi kwenye milima na misitu; kuingia kwao kuliweza kuingiza nguvu na uthabiti zaidi kwenye milima ile mitupu na misitu mitupu. Kuanzia hapa kwenda mbele, milima na misitu ikawa ni makao yao ya kudumu, na wasingewahi kupoteza maskani yao, kwa sababu milima na misitu ilionekana na ikawepo kwa ajili yao, na wanyama wa mwituni wangetimiza wajibu wao na kufanya kila kitu ambacho wangeweza ili kuilinda. Kwa hivyo, pia, wanyama wa mwituni wangeweza kutii kwa umakinifu kule kusihiwa na Muumba ili waweze kushikilia eneo lao, na kuendelea kutumia asili yao ya kinyama ili kuendeleza usawazisho wa viumbe vyote vilivyoanzishwa na Muumba, na kuonyesha waziwazi mamlaka na nguvu za Muumba!

Katika Mamlaka ya Muumba, Viumbe Vyote ni Timilifu

Viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile vilivyoweza kusonga na vile visingeweza kusonga, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu na wanyama wa mwituni, wote walioumbwa kwenye siku ya sita—wote walikuwa wazuri mbele ya Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, viumbe hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha utimilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza. Hatua kwa hatua, Muumba alifanya kazi Aliyonuia kufanya kulingana na mpango Wake. Kimoja baada ya kingine, vitu hivi Alivyonuia kuumba vilijitokeza, na kujitokeza kwa kila kiumbe kulikuwa onyesho la Mamlaka ya Muumba, na uthibitishaji wa mamlaka Yake, na kwa sababu ya uthibitishaji huu, viumbe vyote visingeweza kufanya chochote kingine ila kushukuru kwa neema ya Muumba na riziki ya Muumba. Huku vitendo hivi vya kimiujiza vya Mungu vikijionyesha, ulimwengu huu ulijaa, vipande kwa vipande, ukiwa na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, na ukabadilika kutoka kwa fujo na giza hadi kwa wazi na uangavu, kutoka kwenye utulivu wa kutisha hadi kwa uchangamfu na nguvu zisizokuwa na mipaka. Miongoni mwa viumbe vyote vya uumbaji, kutoka kwa wale wakubwa hata wadogo, toka kwa wadogo hata kwa wale wadogo zaidi, hakuna hata kiumbe kimoja ambacho hakikuumbwa kupitia kwa Mamlaka na nguvu za Muumba, na kukawa na upekee na haja ya ndani kwa ndani na thamani ya uwepo wa kila kiumbe. Licha ya tofauti zao katika maumbo na muundo, lazima viumbe hivi vingeumbwa na Muumba ili viwepo chini ya mamlaka ya Muumba. Wakati mwingine watu wataona mdudu, yule aliye na sura mbaya kabisa na watasema, “Mdudu yule ni sura mbaya kweli, hakuna vile ambavyo kiumbe chenye sura mbaya kama hicho kinaweza kuwa kiliumbwa na Mungu—hakuna njia ambayo Angeumba kitu chenye sura mbaya hivyo.” Mtazamo wa kijinga ulioje! Kile wanachofaa kusema ni, “ingawaje mdudu huyu ana sura mbaya sana, aliumbwa na Mungu, na kwa hivyo, lazima awe na kusudio lake la kipekee.” Kwenye fikira za Mungu, Alinuia kupatia kila mojawapo ya sura, na kazi na matumizi aina zote, katika viumbe mbalimbali vilivyo na uhai Alivyoumba, na hivyo basi hamna kati ya viumbe hivyo ambavyo Mungu aliumba vilivyoumbwa vikiwa vimefanana. Kuanzia sura yao ya nje hadi mkusanyiko wao wa ndani, kuanzia katika mazoea yao ya kuishi hadi mahali pa kuishi—kila kiumbe ni tofauti. Ng’ombe wana sura ya ng’ombe, punda wana sura ya punda, paa ana sura ya paa, na ndovu wana sura ya ndovu. Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi kinachovutia zaidi na ni kipi kinachotisha zaidi kwa sura? Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi chenye manufaa zaidi na uwepo wa kile ambacho hakihitajiki sana? Baadhi ya watu wanapenda namna ambavyo ndovu hufanana, lakini hakuna anayetumia ndovu kutayarisha mashamba ya kupanda: baadhi ya watu wanapenda namna simba na chui mkubwa mwenye milia walivyo, kwani sura inavutia zaidi miongoni mwa viumbe vyote, lakini je, unaweza kuwafuga nyumbani? Kwa ufupi, kuhusiana na viumbe vyote, binadamu anafaa kurejelea mamlaka ya Muumba, hivi ni kusema kwamba, rejelea mpangilio uliochaguliwa na Muumba katika viumbe vyote; huu ndio mtazamo wenye hekima zaidi. Mtazamo tu wa kutafutiza, na wa kuwa mtiifu, kwa nia ama makusudio ya mwanzo ya Muumba ndio ukubalifu wa kweli na hakika wa mamlaka ya Muumba. Ni vyema kwa Muumba, kwa hivyo ni sababu gani ambayo binadamu atakuwa nayo ya kusema kwamba si vyema?

Hivyo basi, viumbe vyote vilivyo katika mamlaka ya Muumba vitaweza kuchezesha mdundo mpya wa ukuu wa Muumba, vitaanza utangulizi mwema kwa minajili ya kazi Yake kwenye siku mpya, na kwa muda huu Muumba ataufungua ukurasa mpya katika kazi ya usimamizi Wake! Kulingana na sheria ya mimea ya machipuko, kukomaa kwa kiangazi, mavuno ya mapukutiko, na hifadhi ya kipupwe iliyochaguliwa na Muumba, viumbe hivi vyote vitaweza kutilia mkazo mpango wa usimamizi wa Muumba na vitakaribisha siku yao mpya, mwanzo mpya, na mkondo mpya wa maisha, na hivi karibuni vitu vitaweza kuzaana katika mfululizo usioisha ili kuweza kukaribisha kila siku katika ukuu wa mamlaka ya Muumba …

Hakuna Kiumbe Chochote Kati ya Vile Vilivyoumbwa na Vile Ambavyo Havikuumbwa Kinaweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba

Tangu Alipoanza uumbaji wa viumbe vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni njia gani Alitumia, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, viumbe vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwenye muda kabla ya mwanadamu kuumbwa ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba viumbe vyote kwa minajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwenye viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, nuru, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, zikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila mojawapo kilipewa maisha kwa matamshi ya Muumba, na kila kiumbe mojawapo kilizaana kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimojawapo kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawaje hawakupokea pumzi za Muumba, bado walionyesha maisha na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa mifumo na miundo yao mbalimbali; ingawaje hawakupokea uwezo wa kuongea aliopewa mwanadamu na Muumba, kila kimojawapo kilipokea njia ya kuelezea maisha yao ambayo walipewa na Muumba, na ambayo ilitofautiana na ile lugha ya Mwanadamu. Mamlaka ya Muumba hayatoi tu nguvu za maisha kwenye vifaa vinavyoonekana kuwa tuli, ili visiwahi kutoweka, lakini, vilevile, hupatia silika ya kuzaana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, vitaweza kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatilia mkazo mamlaka Yake haikubaliani kwa lazima na mtazamo wa mambo makubwamakubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka ya umbo lolote; Anaweza kuamuru utendaji mambo katika ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya maisha na kifo cha viumbe vyote, na, vilevile, Anaweza kushughulikia viumbe vyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala viumbe vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya pekee ya Muumba miongoni mwa viumbe vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu ya maisha tunayoishi, na hayatawahi kusita, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kubadilisha utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote-ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki ile hali halisi ya Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, ingawaje vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kuwakilisha Mungu. Ingawaje wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba viumbe vyote, na kuamuru viumbe vyote, na kushikilia kuwa na ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haviwezi kusawazishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Kwenye Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba viumbe vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kutuma mmojawapo wa wajumbe Wake au malaika kuumba viumbe vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote, viumbe vyote visivyoumbwa viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni sharifu au kina yahe, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kubadilisha utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!

Kupitia ushirika uliotajwa hapo juu, je, tunaweza kusema yafuatayo: Muumba na Kiongozi wa viumbe vyote tu, Yule anayemiliki mamlaka ya kipekee na nguvu za kipekee, ndiye Anayeweza kuitwa Mungu Mwenyewe wa kipekee? Wakati huu, unaweza kuhisi kwamba swali kama hilo ni la kina sana. Wewe, kwa muda huu, huwezi kulielewa, na huwezi kung’amua kiini cha ndani na kwa hivyo kwa muda huu unahisi kwamba ni swali gumu kujibu. Kwa hivyo, Nitaendelea na ushirika Wangu. Kinachofuata, Nitakuruhusu kutazama vitendo halisi vya dhana nyingi za mamlaka na nguvu zinazomilikiwa na Mungu pekee, na hivyo basi Nitakuruhusu kuelewa kwa kweli, kushukuru, na kujua upekee wa Mungu, na maana ya mamlaka ya kipekee ya Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp