Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I
Mamlaka ya Mungu (I) (Sehemu ya Nne)
Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki
Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni fungu jingine lililozungumziwa na Yehova Mungu, Alisema kwa Ibrahimu, “Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.” Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani? Hadi kiwango kilichozungumziwa katika Maandiko: “kama nyota za mbinguni na mchanga ulio pwani.” Hii ni kusema kwamba Mungu alipenda kumpa Ibrahimu uzao uliokuwa mwingi kama nyota za mbinguni, na tele kama mchanga wa pwani. Mungu aliongea akitumia taswira, na kutoka kwenye taswira hii si vigumu kuona kwamba Mungu asingempa tu Ibrahimu uzao elfu moja, mbili, au hata elfu nyingi, lakini idadi isiyohesabika, iliyotosha kuwa uzao wa mataifa mengi ya dunia, kwani Mungu alimwahidi Ibrahimu kuwa atakuwa baba wa mataifa mengi. Na je, idadi hiyo iliamuliwa na binadamu au iliamuliwa na Mungu? Je, binadamu anaweza kudhibiti uzao kiasi gani atakaokuwa nao? Je, inategemea yeye? Haitegemei binadamu kujua kama atakuwa na uzao mbalimbali au la, sikwambii uzao mwingi kama “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani.” Ni nani asiyetamani uzao wake kuwa mwingi kama nyota? Kwa bahati mbaya mambo huwa hayaendi namna unavyotaka. Licha ya vile mwanadamu anaweza kuwa na mbinu au kuweza kufanya jambo fulani, haitegemei binadamu; hakuna anayeweza kusimama nje ya kile ambacho kimeamriwa na Mungu. Kiasi ambacho Atakuruhusu, hicho ndicho utakachokuwa nacho: Kama Mungu atakupa kidogo, basi hutawahi kuwa na kingi, na kama Mungu Atakupa kingi haina faida wewe kuchukia kingi hicho ulichonacho. Je, hayo si kweli? Haya yote yanategemea Mungu, si binadamu! Binadamu hutawaliwa na Mungu, na hakuna yule anayeachwa!
Wakati Mungu alisema “nitazidisha mithili,” hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hadi milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Mungu pekee ndiye anayefuzu na kuweza kufanya ahadi hii kutimia. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yataweza kutimizwa, hadi mwisho wa maelezo ya agano hili, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Viumbe vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hadi milele. Kinyume cha mambo ni, siku ambapo viumbe vyote vitatoweka ndiyo siku ile ile ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu na viumbe vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kitu kuwa kile kisichokuwepo, na Anadhibiti mabadiliko ya viumbe vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi kuliko kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kufikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kufikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni hoja ambayo Mungu tayari ameiona, na ambayo kwa kweli itaweza kutimizwa. Je, unashukuru kuyasikia haya? Je, hoja hizi zinathibitisha kwamba uzao wa Ibrahimu ulikuwa mwingi? Na ulikuwa mwingi kiasi kipi? Mwingi kiasi cha “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani” kama ilivyosemwa na Mungu? Je, uliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza hoja hii? Iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa miaka kadhaa ifikayo mamia au elfu baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na bila kusita yakaendelea kuwa hoja; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na ithibati ya mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba viumbe vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Aliruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa mamlaka ya Mungu, na Akaruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyokadirika, na zaidi, Akaruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.
Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua usukani wa kazi hii, na hoja iliyoahidiwa kwa kinywa cha Mungu kwa utaratibu huanza kugeuka na kuwa uhalisi. Miongoni mwa viumbe vyote, mabadiliko huanza kufanyika katika kila kitu kutokana na hayo, sawa na vile, kwenye mwanzo wa msimu wa mchipuko, nyasi hugeuka kuwa kijani, maua huchanua, macho ya maua yanachanua kutoka mitini, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Wakati wa msimu wa machipuko unapowadia viumbe vyote hupata nguvu, na hiki ndicho kitendo cha miujiza cha Muumba. Wakati Mungu anapokamilisha ahadi zake, viumbe vyote mbinguni na ardhini vinapata nguvu mpya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati kujitolea au kuahidi kunapotamkwa kutoka kwa Mungu, viumbe vyote vinatimiza wajibu wake, na vinashughulikiwa kwa minajili ya kutimizwa kwake, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kuhudumu kazi zao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Kunao upana wa mamlaka ya Mungu? Kuna kipimo cha muda? Je, inaweza kusemekana kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, inaweza kusemekana kuwa na ukubwa au nguvu fulani? Je, inaweza kupimwa kwa vipimo vya binadamu? Mamlaka ya Mungu hayawakiwaki yakizima, hayaji yakienda, na hakuna mtu anayeweza kupima namna ambavyo mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, wakati Mungu anabariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutaruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za maisha zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho timilifu la maneno kutoka kwenye kinywa Chake, na linaonyeshwa kwa vitu vyote, na kwa mwanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa na mamlaka Yake ni bora zaidi ya kulinganishwa, na hakina dosari kamwe. Yaweza kusemekana kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyolinganishwa, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanakoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au hata ni vipi ambavyo mageuzi makubwa yamekuwa makubwa katika harakati zao za kuishi kwenye mazingira yao—haya yote yanajulikana kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Haijalishi ni muda upi umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kama vile ndio mwanzo yametamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutambua kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutambuliwa, na, zaidi, kukamilishwa kwake na kutambuliwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba upana wa mamlaka ya Mungu na nguvu vinatosha kudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote. Mungu aliumba nuru, lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu anasimamia tu nuru, kwamba Yeye anasimamia maji tu kwa sababu Aliyaumba maji, na kwamba kila kitu kingine hakina uhusiano na Mungu. Je, hii siyo suitafahamu? Ingawaje baraka za Mungu kwa Ibrahimu zilikuwa zimefifia polepole kutoka kwenye kumbukumbu ya binadamu baada ya miaka mia kadhaa, kwake Mungu, ahadi hii ilibaki vilevile. Ilikuwa kwenye mchakato wa kukamilishwa, na haikuwahi kusitishwa. Binadamu hakuwahi kujua au kusikia namna ambavyo Mungu alisisitiza mamlaka Yake, namna ambavyo vitu vyote vilivyoundwa na kupangiliwa, na ni hadithi ngapi za ajabu zilifanyika miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu kwenye kipindi hiki cha muda, lakini kila kipande kizuri cha onyesho la mamlaka ya Mungu na ufunuo wa matendo Yake vilipitishwa na kutukuzwa miongoni mwa viumbe vyote, viumbe vyote vilijitokeza na kuongea kuhusu vitendo vya kimiujiza vya Muumba, na kila mojawapo ya hadithi iliyosimuliwa sana kuhusu ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote itaweza kutangazwa na viumbe vyote daima dawamu. Mamlaka ambayo Mungu anatawala viumbe vyote, na nguvu za Mungu, vinaonyesha viumbe vyote kwamba Mungu anapatikana kila pahali wakati wote. Wakati unashuhudia upekee wa mamlaka na nguvu za Mungu, utaona kwamba Mungu anapatikana kila mahali na nyakati zote. Mamlaka na nguvu za Mungu haviwekewi mipaka ya muda, jiografia, nafasi, au mtu yeyote, jambo au kitu. Upana wa mamlaka na nguvu za Mungu unazidi mawazo ya binadamu; haufikiriki kwa binadamu, hauwaziki kwa binadamu, na hautawahi kujulikana na binadamu.
Baadhi ya watu wanapenda kujijazia na kujifikiria, lakini, mawazo ya binadamu yanaweza kufikia wapi? Yanaweza kuzidi ulimwengu huu? Je, mwanadamu ana uwezo wa kujijazia na kufikiria uhalali na usahihi wa mamlaka ya Mungu? Je, kule kujijazia na kujifikiria kwa binadamu kunaweza kuruhusu yeye kufikia maarifa ya mamlaka ya Mungu? Vinaweza kufanya binadamu kushukuru kwa kweli na kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Mungu? Hoja zinathibitisha kwamba uingiliaji kati na kufikiria kwa binadamu ni zao tu la akili za binadamu, na hakutoi hata msaada kidogo au manufaa kidogo kwa maarifa ya binadamu kuhusu mamlaka ya Mungu. Baada ya kusoma makala ya kidhahania ya kisayansi, baadhi wanaweza kufikiria mwezi, na vile nyota zilivyo. Ilhali hii haimanishi kwamba binadamu anao ufahamu wowote wa mamlaka ya Mungu. Kufikiria kwa binadamu ni huku tu: kufikiria. Kuhusiana na hoja za mambo haya, hivi ni kusema kwamba, kwa kurejelea muunganiko wao kwa mamlaka ya Mungu, hana ung’amuzi wowote. Na je, ikiwa umeenda hadi mwezini? Je, hii inaonyesha kuwa unao ufahamu wa pande nyingi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, inaonyesha kwamba wewe unaweza kufikiria upana wa mamlaka na nguvu za Mungu? Kwa sababu huko kuingilia kati na kufikiria kwa mwanadamu hakuwezi kumruhusu kujua mamlaka ya Mungu, je, binadamu anafaa kufanya nini? Chaguo lenye hekima zaidi ni kutojijazia au kutojifikiria, ambapo ni kusema kwamba binadamu asiwahi kutegemea kufikiria na kutegemea uingiliaji kati inapohusu kujua mamlaka ya Mungu. Ni nini ambacho Ningependa kukwambia hapa? Maarifa ya mamlaka ya Mungu, nguvu za Mungu, utambulisho binafsi wa Mungu, na hali halisi ya Mungu haviwezi kutimizwa kwa kutegemea kufikiria kwako. Kwa vile huwezi kutegemea kufikiria ili kujua mamlaka ya Mungu, basi ni kwa njia gani unaweza kutimiza maarifa ya kweli ya mamlaka ya Mungu? Kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kupitia ushirika, na kupitia kwa uzoefu wa maneno ya Mungu, utaweza kuwa na hali halisi ya kujua kwa utaratibu na uthibitishaji wa mamlaka ya Mungu na hivyo basi utafaidi kuelewa kwa utaratibu na maarifa yaliyoongezeka. Hii ndiyo njia tu ya kutimiza maarifa ya mamlaka ya Mungu; hakuna njia za mkato. Kukuuliza kutofikiria si sawa na kukufanya uketi kimyakimya ukisubiri maangamizo, au kukusitisha dhidi ya kufanya kitu. Kutotumia akili zako kuwaza na kufikiria kunamaanisha kutotumia mantiki ya kujijazia, kutotumia maarifa kuchambua, kutotumia sayansi kama msingi, lakini badala yake kufurahia, kuhakikisha, na kuthibitisha kuwa Mungu unayemsadiki anayo mamlaka, kuthibitisha kwamba Yeye anashikilia ukuu juu ya hatima yako, na kwamba nguvu Zake nyakati zote zinathibitisha kuwa Yeye Mungu Mwenyewe ni wa kweli, kupitia kwa matamshi ya Mungu, kupitia ukweli, kupitia kwa kila kitu unachokabiliana nacho maishani. Hii ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote anaweza kutimiza ufahamu wa Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba wangependa kupata njia rahisi ya kutimiza nia hii, lakini unaweza kufikiria kuhusu njia kama hiyo? Nakwambia, hakuna haja ya kufikiria: Hakuna njia nyingine! Njia ya pekee ni kujua kwa uangalifu na bila kusita na kuhakikisha kile Mungu anacho na alicho kupitia kwa kila neno Analolielezea na Analolifanya. Hii ndiyo njia pekee ya kujua Mungu. Kwani kile Mungu anacho na alicho, na kila kitu cha Mungu, si cha wazi na tupu—lakini cha kweli.
Hoja ya Udhibiti wa Muumba na Utawala Juu ya Vitu Vyote na Viumbe Vilivyo Hai Inazungumzia Uwepo wa Kweli wa Mamlaka ya Muumba
Vilevile, baraka za Yehova Mungu kwa Ayubu zimerekodiwa katika Kitabu cha Ayubu. Ni nini ambacho Mungu alimpa Ayubu? “Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike” (Ayubu 42:12). Kutoka kwenye mtazamo wa binadamu, ni vitu gani alivyopewa Ayubu? Je, vilikuwa rasilimali ya binadamu? Akiwa na rasilimali hizi, je, Ayubu angeweza kuwa tajiri sana kwenye kipindi hicho? Na aliwezaje kumiliki rasilimali kama hizo? Ni nini kilisababisha utajiri wake? Bila shaka ilikuwa ni shukrani kwa baraka ya Mungu ambapo Ayubu alifanikiwa kumiliki. Namna ambavyo Ayubu alitazama rasilimali hizi, na vipi alivyochukulia baraka za Mungu, si jambo ambalo tutalizungumzia hapa. Tunapokuja katika baraka za Mungu watu wote hutamani, mchana na usiku, kubarikiwa na Mungu, ilhali binadamu hana udhibiti wowote kuhusiana na idadi ngapi ya rasilimali anaweza kufaidi katika maisha yake yote, au kama anaweza kupokea baraka kutoka kwa Mungu—na hii ni hoja isiyopingika! Mungu anayo mamlaka, na nguvu za kumpatia mwanadamu rasilimali yoyote, kumruhusu binadamu kupata tamko lolote la baraka, ilhali kuna kanuni ya baraka za Mungu. Ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki? Watu Anaowapenda, bila shaka! Ibrahimu na Ayubu walibarikiwa wote na Mungu, ilhali baraka walizopokea hazikuwa sawa. Mungu alibariki Ibrahimu kwa vizazi vingi kama mchanga na nyota. Wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Alisababisha vizazi vya mtu mmoja, taifa moja, kuwa na nguvu na ufanisi. Katika haya mamlaka ya Mungu yalitawala mwanadamu, ambaye alipumua pumzi za Mungu miongoni mwa viumbe vyote na viumbe vyenye uhai. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, huyu mwanadamu aliweza kupenyeza na kuwepo kwa kasi, na ndani ya upana, ulioamuliwa na Mungu. Haswa, uwezo wa taifa hili, kima cha upanuzi, na matarajio ya maisha vyote vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Mungu, na kanuni ya haya yote ilitokana kwa ujumla kwa ahadi ambazo Mungu alimpa Ibrahimu. Hivi ni kusema kwamba, licha ya hali zozote zile, ahadi za Mungu zingeendelea mbele bila kizuizi na kuweza kutambuliwa kulingana na uwepo wa mamlaka ya Mungu. Katika ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu, licha ya misukosuko ya ulimwengu, licha ya umri, licha ya majanga yanayovumiliwa na mwanadamu, vizazi vya Ibrahimu visingeweza kukabiliwa na hatari ya maangamizo, na taifa lao lisingefifia na kutokomea. Baraka ya Mungu kwa Ayubu, hata hivyo, ilimfanya kuwa tajiri wa kupindukia. Kile Mungu alichompa kilikuwa mseto wa viumbe hai, vinavyopumua, maelezo yake yalikuwa—idadi yao, kasi yao ya kuzaa, kima cha kuishi, kiwango cha mafuta kwenye viumbe hivyo, na kadhalika—vilidhibitiwa pia na Mungu. Ingawaje viumbe hivi hai havikumiliki uwezo wa kuongea, navyo pia vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Muumba, na kanuni za mipangilio ya Mungu zilikuwa kulingana na baraka ambayo Mungu aliahidi Ayubu. Katika baraka ambazo Mungu alimpa Ibrahimu na Ayubu, ingawaje kile kilichokuwa kimeahidiwa kilikuwa tofauti, mamlaka ambayo Muumba alitumia kutawala viumbe vyote na viumbe vilivyo na uhai yalikuwa yale yale. Kila maelezo ya mamlaka na Nguvu za Mungu yameonyeshwa kwenye ahadi Zake tofauti na baraka zake kwa Ibrahimu na Ayubu, kwa mara nyingine zaonyesha binadamu kwamba mamlaka ya Mungu ni zaidi ya kufikiria kwa binadamu. Maelezo haya yanamwambia binadamu kwa mara nyingine kwamba kama angetaka kujua mamlaka ya Mungu, basi hii itawezekana tu kupitia kwa maneno ya Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu.
Mamlaka ya Mungu ya ukuu juu ya viumbe vyote huruhusu binadamu kuweza kuona ukweli kwamba: Mamlaka ya Mungu hayapo tu katika matamshi “Mungu akasema, na Kuwepo na nuru, na kukawa na nuru, na, Kuwepo na anga, na kukawa na anga, na, Kuwepo na ardhi, na kukawa na ardhi,” lakini, vilevile namna Alivyofanya nuru ile kuendelea kuwepo, kulizuia anga dhidi ya kutoweka na Akaiweka ardhi milele ikiwa kando na maji, pamoja na maelezo ya namna Alivyotawala na kusimamia viumbe: nuru, anga, na ardhi. Nini kingine unachoona katika baraka za Mungu kwa mwanadamu? Ni wazi, kwamba baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, nyayo za Mungu hazikusita, kwani Alikuwa tu ameanza kuonyesha mamlaka Yake, na Alinuia kuhakikisha kwamba kila mojawapo ya matamshi Yake yangekuwa uhalisia, na kuhakikisha kuwa kila mojawapo ya maelezo ambayo Alizungumza yanatokea kuwa kweli, na kwa hivyo kwenye miaka iliyofuata, Aliendelea kufanya kila kitu Alichonuia. Kwa sababu Mungu anayo mamlaka, pengine inaonekana kwa binadamu kwamba Mungu huongea tu, na Hahitaji kuinua hata kidole chake ili mambo yote yaweze kutimizwa. Kufikiria hivyo, ni, lazima Niseme, mzaha! Kama utachukua mtazamo wa upande mmoja wa Mungu kuanzisha agano na binadamu kwa kutumia maneno, na ukamilishaji wa kila kitu na Mungu kwa kutumia maneno, na huwezi kuona ishara na hoja mbalimbali ambazo mamlaka ya Mungu yanatawala juu ya kila kitu, basi ufahamu wako kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni mdogo mno na wa mzaha! Kama binadamu anafikiria Mungu kuwa hivyo, basi, lazima isemwe, maarifa ya binadamu kuhusu Mungu yameendeshwa hadi kwenye shimo la mwisho, na sasa yamefika mwisho wenyewe, kwani Yule Mungu ambaye binadamu anafikiria kuhusu ni mashine tu ya kutoa amri, na si Mungu anayemiliki mamlaka. Je, umeona nini kupitia kwenye mifano ya Ibrahimu na Ayubu? Je, umeuona upande halisia wa mamlaka na nguvu za Mungu? Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Yeye kuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, pindi Mungu alipotamka maneno Yake, akiongozwa na mamlaka ya Mungu, mambo yote yalianza kukubaliana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutumika kotekote kwenye ardhi nzima, na Akaweka wazi mkondo ili kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, hakuwashawishi tu wafanyakazi Wake, lakini pia na viumbe vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivyo ni kusema kwamba upana ambao mamlaka ya Mungu yalitiliwa maanani haukujumuisha tu wajumbe, lakini, vilevile, vitu vyote, vilivyoshawishiwa ili kutii ile kazi ambayo Alinuia kukamilisha; hizi ndizo zilizokuwa tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitumiwa. Katika kufikiria kwako, baadhi ya watu wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao kuhusiana na mamlaka ya Mungu: Mungu anayo mamlaka, na Mungu anao uwezo, na hivyo basi Mungu anahitaji kubaki katika mbingu ya tatu, au Anahitajika tu kubakia mahali maalum, na hahitajiki kufanya kazi yoyote fulani, na uzima wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, ingawaje Mungu alibariki Ibrahimu, Mungu hakuhitajika kufanya kitu chochote, na ilitosha kwake Yeye kutamka tu matamshi Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka la! Ingawaje Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisia, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka ya Mungu na nguvu hufichuliwa kwa utaratibu, kuwekwa ndani ya uumbaji Wake wa vitu vyote, na udhibiti wa vitu vyote, na katika mchakato ambao Anaongoza na kusimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyovyote—vinathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo wa kihalisia wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angempa Ibrahimu na Ayubu—uamuzi ulikuwa wa Mungu. Hata ingawaje wajumbe wa Mungu waliweza kumtembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, vitendo vyao vilikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawaje binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hashuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote kwenye rekodi za Biblia, kwa hakika Yule Mmoja tu ambaye anatilia mkazo nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hali hii haivumilii shaka yoyote kutoka kwa binadamu yeyote! Ingawaje umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kifaa kilicho na, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kifaa chochote kinaweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.
Mamlaka ya Muumba Hayabadiliki na ni Yasiyokosewa
Ni nini umeona katika sehemu hizi tatu za maandiko? Je, umeona kuwa kuna kanuni ambayo Mungu hutumia mamlaka Yake? Kwa mfano, Mungu aliutumia upinde wa mvua kuanzisha agano na binadamu, ambapo Aliuweka upinde wa mvua katika mawingu ili kumwambia binadamu kuwa Yeye Hatawahi tena kutumia gharika kuangamiza ulimwengu. Je, upinde wa mvua tunaouona leo, bado ndio uleule uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu? Je, asili na maana yake vimebadilika? Bila shaka, havijabadilika. Mungu alitumia mamlaka Yake ili kutekeleza kitendo hiki, nalo agano Aliloanzisha na binadamu limeendelea hadi leo, na muda ambao agano hili litabadilishwa, bila shaka, ni uamuzi wa Mungu. Baada ya Mungu kutamka “Mimi nauweka upinde wangu wa mvua mawinguni,” siku zote Mungu alifuata agano hili, Alilifuata hadi leo. Unaona nini katika haya? Ingawaje Mungu anayamiliki mamlaka na nguvu, Anayo bidii sana na Anafuata kanuni katika vitendo Vyake, na Anashikilia maneno Yake. Bidii Yake na kanuni za vitendo Vyake, vinaonyesha namna Muumba asivyoweza kukosewa na namna ambavyo mamlaka ya Muumba yalivyo magumu kushindwa. Ingawaje Anamiliki mamlaka ya juu, na kila kitu kinatawaliwa na Yeye, na japokuwa Anazo nguvu za kutawala vitu vyote, Mungu hajawahi kuharibu mpango Wake au kutatiza mpangilio Wake mwenyewe, na kila wakati Anapotumia mamlaka Yake, ni kulingana na umakinifu unaohitajika kwenye kanuni Zake mwenyewe na hasa kwa kufuata kile kilichotamkwa kutoka kwenye kinywa Chake, na kufuata hatua na majukumu ya mpango Wake. Sina haja ya kusema kwamba kila kitu kinachotawaliwa na Mungu pia kinatii kanuni ambazo mamlaka ya Mungu yanatumika, na hakuna mwanadamu au kitu kisichojumuishwa kwenye mipangilio ya mamlaka Yake, wala hakuna anayeweza kubadilisha kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumika. Kwenye macho ya Mungu, wale wanaobarikiwa hupokea utajiri mzuri unaoletwa na mamlaka Yake, na wale wanaolaaniwa hupokea adhabu yao kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, hakuna binadamu au kitu ambacho hakijumuishwi, kwenye utumiaji wa mamlaka Yake, wala hakuna kinachoweza kubadilisha kanuni hizi ambazo mamlaka Yake yanatumiwa. Mamlaka ya Muumba hayabadilishwi kwa mabadiliko ya aina yoyote ile, na, vilevile, kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumiwa hazibadiliki kwa sababu yoyote ile. Mbingu na ardhi vyote vinaweza kupitia misukosuko mingi, lakini mamlaka ya Muumba hayatabadilika; vitu vyote vitatoweka, lakini mamlaka ya Muumba hayatawahi kutoweka. Hiki ndicho kiini cha mamlaka ya Muumba ambayo hayabadiliki na ni yasiyokosewa, na huu ndio upekee wenyewe wa Muumba!
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?