Matamko ya Kristo Mwanzoni - Sura ya 5

Milima na mito inabadilika, mtiririko wa maji katika uelekeo wake, na maisha ya mwanadamu hayastahimili kama ifanyavyo nchi na anga. Mwenyezi Mungu pekee ndiye uzima wa milele na uliofufuka, ambao unaendelea, kizazi baada ya kizazi, milele! Vitu vyote na matukio yote yapo mikononi Mwake, na Shetani yupo chini ya wayo Wake.

Leo, ni kwa uteuzi wa Mungu ulioamuliwa kimbele ndiyo Anatuokoa kutoka katika mshiko wa Shetani. Yeye ni Mkombozi wetu kwa kweli. Uzima wa milele na uliofufuka wa Kristo kwa kweli umefinyangwa ndani yetu, ukituwekea hatima kuunganika na uzima wa Mungu, ili tuweze kuja ana kwa ana na Yeye kwa kweli, kumla Yeye, kumnywa Yeye, na kumfurahia Yeye. Huku ndiko kujitolea bila ubinafsi kwa damu ya moyo wa Mungu.

Misimu inakuja na kwenda; Mungu anapitia katika upepo na jalidi, na kukumbana na dhiki, mateso, na taabu nyingi za maisha, kukataliwa na kashfa nyingi za ulimwengu, mashtaka mengi ya uongo ya serikali, lakini bado imani ya Mungu wala azimio Lake halijapungua hata kidogo. Akiwa amejitolea kikamilifu kwa mapenzi ya Mungu, na ukamilishaji wa usimamizi na mpango wa Mungu, Anayaweka maisha Yake mwenyewe kando. Kwa watu Wake wote, Anafanya kila juhudi, Akiwalisha na kuwanyunyizia kwa makini. Haijalishi sisi ni wapumbavu kiasi gani, au jinsi tulivyo wagumu, tunahitaji tu kutii mbele Yake, na uzima uliofufuka wa Kristo utabadilisha asili yetu ya zamani…. Kwa ajili ya wazaliwa hawa wote wa kwanza, Anafanya kazi kwa bidii mchana na usiku, akikosa kula na kupumzika. Mchana na usiku ngapi, kupitia katika joto kali na baridi kali kiasi gani, Anatazama kwa moyo wa dhati akiwa Sayuni.

Ulimwengu, makazi, kazi na kila kitu, Ameviacha kabisa, kwa furaha, kwa hiari, na raha za ulimwengu hazimhusu Yeye…. Maneno yatokayo kinywani Mwake yanatuchoma kweli, yakifichua vitu vilivyofichika ndani ya mioyo yetu. Tunawezaje kukosa kushawishika? Kila sentensi ambayo inatoka kinywani Mwake inaweza kutimika kwetu wakati wowote. Chochote tunachokifanya, katika uwepo Wake au kilichojificha mbali na Yeye, hakuna chochote ambacho Hajui, hakuna chochote Asichoelewa. Yote yanafunuliwa mbele Yake kwa kweli, licha ya mipango na matayarisho yetu wenyewe.

Tukiwa tumeketi mbele Yake tukihisi raha ndani ya roho yetu, watulivu na tusio na wasiwasi, na bado tunahisi utupu na kuwa wadeni kwa Mungu: Hii ni ajabu isiyofikirika na isiyowezekana kufanikisha. Roho Mtakatifu anatosha kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli! Ni ushahidi usiopingika! Sisi wa kundi hili tumebarikiwa kwa njia isiyoeleweka! Isingekuwa kwa neema na rehema za Mungu, tungeweza tu kwenda kwa mateso ya milele na kumfuata Shetani. Ni Mwenyezi Mungu pekee anayeweza kutuokoa!

Ah! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo! Ni Wewe ndiwe umeyafungua macho yetu ya kiroho, ukituruhusu tutazame siri za ulimwengu wa kiroho. Matarajio ya ufalme hayana mipaka. Hebu tuwe waangalifu tunapongoja. Siku haiwezi kuwa mbali sana.

Miale ya moto ya vita inazunguka, moshi wa mzinga umejaa hewani, hali ya anga inakuwa ya joto kiasi, hali ya hewa inabadilika, tauni itaenea, na watu wanaweza tu kufariki, bila matumaini ya kuishi.

Ah! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo! Wewe ndiwe ngome yetu isiyoshindwa. Wewe ndiwe kimbilio letu. Tunakusanyika chini ya mabawa Yako, na janga haliwezi kutufikia. Huo ndio ulinzi na utunzaji Wako mtukufu.

Sote tunapaza sauti zetu katika wimbo; tunaimba kwa kusifu, na sauti za sifa zetu zinavuma kote Sayuni! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo, Ametuandalia ile hatima nzuri. Muwe waangalifu—oh, iweni wenye kulinda! Kufikia sasa, saa sio mbali sana.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp