Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 148

Kazi ya Roho Mtakatifu siku zote inafanywa kwa hiari; wakati wowote Anapopanga kazi Yake, Roho Mtakatifu ataitekeleza. Kwa nini sikuzote Nasema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni ya uhalisi? Kwamba siku zote ni mpya na haijawahi kuwa zee, na siku zote inakuwa na uhai zaidi? Kazi ya Mungu ilikuwa bado haijawahi kupangwa wakati ulimwengu ulipoumbwa; hivi sivyo kamwe ilivyofanyika! Kila hatua ya kazi hufikia athari yake bora kwa wakati wake mwafaka, nazo haziingiliani kati. Kunao wakati mwingi ambapo mipango katika akili zako hazilingani kamwe na kazi ya hivi punde ya Roho Mtakatifu. Kazi Yake si rahisi kama wanavyofikiria watu, wala si ngumu kama watu wengi wanavyofikiria; inajumuisha kuwaruzuku watu wakati wowote na mahali popote kulingana na mahitaji yao ya sasa. Hakuna aliye wazi zaidi kuhusu kiini halisi cha watu kama Yeye, na ni kwa sababu hii mahususi ndiposa hakuna kinachoweza kufaa mahitaji ya kihalisi ya watu kama vile ambavyo kazi Yake inavyofanya. Hivyo basi, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kazi Yake ilipangiwa milenia kadha mbele. Anavyofanya kazi miongoni mwenu sasa, kulingana na hali yenu, Yeye pia Anafanya kazi na kuongea wakati wowote na mahali popote. Wakati watu wako katika hali fulani, Yeye huongea maneno hayo ambayo hasa ndiyo wanayohitaji ndani yao. Ni kama hatua ya kwanza ya kazi Yake ya nyakati za kuadibu. Baada ya nyakati za kuadibu, watu walionyesha tabia fulani, walikuwa na mienendo ya kuasi katika njia fulani, hali fulani nzuri ziliibuka, hali fulani mbaya pia ziliibuka, na mipaka ya juu ya hali hii ya ubaya ikafikia kiwango fulani. Mungu alifanya kazi Yake kutokana na mambo haya yote, na hivyo basi Alichukua haya yote ili kuweza kutimiza athari bora zaidi kwa ajili ya kazi Yake. Anatekeleza tu kazi Yake ya kuruzuku miongoni mwa watu kulingana na hali zao za sasa. Yeye Hutekeleza kila hatua ya kazi Yake kulingana na hali halisi za watu. Uumbaji wote umo mikononi Mwake; Angekosa kuujua? Kwa mujibu wa hali za watu, Mungu hutekeleza hatua inayofuata ya kazi inayofaa kufanywa, wakati na mahali popote. Kazi hii haikupangwa maelfu ya miaka kabla; hii ni dhana ya kibinadamu tu! Yeye hufanya kazi kwa kadri Anavyoangalia athari ya kazi Yake, na kazi Yake inaendelea kuwa ya kina na kukuzwa; kwa kadri Anavyoendelea kuangalia matokeo ya kazi Yake, ndipo Anapotekeleza hatua inayofuata ya kazi Yake. Yeye hutumia mambo mengi ili kuingia kwenye mpito hatua kwa hatua na kufanya kazi Yake mpya kuonekana na watu baada ya muda. Aina hii ya kazi inaweza kuruzuku mahitaji ya watu, kwani Mungu anawajua watu vizuri mno. Hivi ndivyo Anavyotekeleza kazi Yake kutoka mbinguni. Vilevile, Mungu mwenye mwili anafanya kazi Yake kwa njia iyo hiyo, Akipangilia kulingana na uhalisia na utendakazi miongoni mwa binadamu. Hakuna yoyote kati ya kazi Zake iliyopangwa kabla ya ulimwengu kuumbwa, wala kupangwa kwa umakinifu kabla ya wakati. Miaka 2,000 baada ya ulimwengu kuumbwa, Yehova aliona binadamu walikuwa wamepotoka sana kiasi cha kwamba Alikitumia kinywa cha nabii Isaya kutabiri kwamba baada ya Enzi ya Sheria kukamilika, Angetekeleza kazi Yake ya kukomboa binadamu katika Enzi ya Neema. Huu ulikuwa mpango wa Yehova, bila shaka, lakini mpango huu uliweza pia kufanywa kulingana na hali ambazo Aliangalia wakati huo; bila shaka Yeye hakuufikiria mara moja baada ya kumwumba Mwanadamu. Isaya alitabiri tu, lakini Yehova hakuandaa matayarisho mara moja wakati wa Enzi ya Sheria; badala yake, Alianza kazi hii katika mwanzo wa Enzi ya Neema, wakati mjumbe alipojitokeza katika ndoto ya Yusufu na kumpa yeye nuru, wakimwambia kwamba Mungu angekuwa mwili, na hivyo kazi Yake ya kupata mwili ikaanza. Kama watu wanavyofikiria Mungu hakujitayarishia kazi Yake ya kuwa mwili baada ya kuumba ulimwengu; jambo hili liliamuliwa tu kulingana na kiwango cha maendeleo ya binadamu na hadhi ya vita Vyake na Shetani.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp