Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 188

Miongoni mwa wanadamu, Ninawaainisha watu katika aina tatu. Aina ya kwanza ni wasioamini, wale wasio na imani za kidini. Wanaitwa wasioamini. Wengi wa wasioamini wanaamini tu katika pesa, wanatafuta tu maslahi yao wenyewe, wana tamaa ya vitu, na wanaamini katika ulimwengu yakinifu, si katika mzunguko wa uhai na mauti au katika semi za miungu na mapepo. Ninawaainisha kama wasioamini na ni wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni watu mbalimbali wenye imani tofauti na wasioamini. Miongoni mwa wanadamu, Ninawagawa hawa wenye imani katika aina kuu kadhaa: Ya kwanza ni Wayahudi, wa pili ni Wakatoliki, ya tatu ni Wakristo, ya nne ni Waislamu, na ya tano ni wafuasi wa Budha—kuna aina tano. Hizi ndizo aina mbalimbali za watu wenye imani. Aina ya tatu ni wale wanaomwamini Mungu, inayohusiana nanyi. Waumini kama hawa ni wale wanaomfuata Mungu leo. Hawa watu wamegawanyika katika aina mbili. Wateule wa Mungu na watendaji huduma. Hizi aina kuu zimebainishwa wazi. Basi sasa, akilini mwenu mnaweza kutofautisha wazi aina na madaraja ya binadamu. Ya kwanza ni wasioamini—nimesema wasioamini ni watu gani. Je, wale wanaomwamini Mtu Mzee aliye Angani wanahesabika kama wasioamini? Wengi wa wasioamini wanamwamini yule Mzee aliye Angani; wanaamini kuwa upepo, mvua na radi vyote vinadhibitiwa na huyu Mzee aliye Angani, ambaye wanategemea kwa upanzi wa mimea na uvunaji wa mazao—bali kwa kutaja imani kwa Mungu wanapoteza hamu. Je, hii yaweza kuitwa imani kwa Mungu? Watu kama hao wanahesabiwa katika wasioamini. Mnaelewa hili, siyo? Msifahamu visivyo vikundi hivi. Aina ya pili ni watu wa imani. Aina ya tatu ni wale wanaomfuata Mungu leo. Na kwa nini Nimewagawa wanadamu wote katika aina hizi? (Kwa sababu wana vituo na hatima tofautitofauti.) Hicho ni kipengele kimoja. Kwa sababu, wakati haya matabaka na aina mbalimbali za watu wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, kila mmoja atakuwa na sehemu tofauti ya kuenda, watapitia sheria ya mzunguko tofauti wa uhai na mauti na hii ndiyo sababu Nimewaainisha wanadamu katika hizi aina kuu.

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini (Vifungu teule)

Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, anathibitisha majina yao, anwani, na umri. Walichokifanya maishani mwao, Kila kitu walichokifanya maishani mwao kinanakiliwa kwenye kitabu na usahihi wake unahakikishwa. Baada ya kukaguliwa, matendo na mienendo ya mtu maishani mwake vinatumika kuamua ikiwa ataadhibiwa au ataendelea kupata mwili kama mwanadamu, ambayo ni hatua ya kwanza. Je, hii hatua ya kwanza inaogofya? Haiogopeshi sana, kwani kitu cha pekee kilichofanyika ni kwamba mtu amewasili katika mahali pa giza na pageni. Hilo halitishi sana.

Katika hatua ya pili, ikiwa mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya maishani mwake, kama ametenda vitendo vingi viovu, basi atapelekwa mahali pa adhabu ili kuadhibiwa. Hiyo ndiyo itakuwa mahali ambapo kwa hakika ni kwa ajili ya adhabu ya watu. Maelezo kuhusu jinsi watakavyoadhibiwa yanategemea dhambi walizotenda, na ni vitendo vingapi viovu walitenda kabla hawajafa—ambalo ni tukio la kwanza kutokea katika hatua ya pili. Kwa sababu ya mambo waliyoyafanya, na maovu waliyoyafanya kabla hawajafa, wapatapo mwili baada ya adhabu yao—wazaliwapo upya tena katika ulimwengu yakinifu—watu wengine wataendelea kuwa wanadamu, na wengine watakuwa wanyama. Yaani, baada ya mtu kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanaadhibiwa kwa sababu ya maovu waliyotenda; zaidi, kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya, katika kupata mwili kwao kunakofuata hawawi wanadamu, ila watakuwa mnyama. Baadhi ya wanyama watakaokuwa ni ng’ombe, farasi, nguruwe, na mbwa. Watu wengine wanaweza kuwa ndege kule angani, au bata au bata bukini.… Baada ya kupata mwili kama mnyama, wanapokufa wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, na sawa na mara ya kwanza, kutegemea mienendo yao kabla hawajafa, ulimwengu wa kiroho utaamua kama wapate mwili kama mwanadamu au la. Watu wengi hutenda maovu mengi sana, dhambi zao ni nzito sana, na kwa hivyo wapatapo mwili wanakuwa wanyama mara saba hadi mara kumi na mbili. Mara saba hadi mara kumi na mbili—hilo linaogopesha? (Linaogopesha.) Ni nini kinawaogopesha? Mtu kuwa mnyama, hilo linaogopesha. Na kwa mwanadamu, ni kipi cha uchungu zaidi kuhusu kuwa mnyama? Kutokuwa na lugha, kuwa tu na mawazo sahili, kuweza tu kufanya vitu ambavyo wanyama hufanya na kula vitu ambavyo wanyama hula, na kuwa na fikira sahili na kuwa na viziada lugha vya mnyama, kutoweza kutembea wima, kutoweza kuwasiliana na wanadamu, na mienendo yoyote na vitendo vya wanadamu kutokuwa na uhusiano na wanyama. Yaani, miongoni mwa vitu vyote, kuwa mnyama kunakufanya kuwa chini zaidi ya viumbe hai wote, na ni kuchungu zaidi kuliko kuwa mwanadamu. Hiki ni kipengele kimoja cha adhabu ya ulimwengu wa kiroho kwa wale waliofanya maovu mengi na kutenda dhambi kubwa. Ukali wa adhabu utakavyokuwa, hili hubainishwa na aina ya mnyama ambaye mtu anakuwa. Kwa mfano, kuwa nguruwe ni bora kuliko kuwa mbwa? Je, nguruwe huishi vizuri au vibaya kuliko mbwa? Vibaya zaidi, siyo? Watu wakiwa ng’ombe au farasi, je, wataishi vizuri zaidi au vibaya kuliko nguruwe? (Vizuri zaidi.) Inaonekana mkipewa fursa, mnapenda ustaarabu. Je, ingekuwa faraja zaidi kama mtu angekuwa paka? Itakuwa faraja zaidi kuliko kuwa farasi au ng’ombe. Mngeweza kuchagua kati ya wanyama, mngechagua kuwa paka, na hiyo ni faraja zaidi kwa sababu mngeweza kuupitisha muda wenu mwingi usingizini. Kuwa ng’ombe au farasi ni kazi nzito, na kwa hivyo watu wakipata mwili na kuwa ng’ombe au farasi, wanapaswa kutia bidii—ambayo inaonekana kama adhabu nzito. Kuwa mbwa ni afadhali kidogo kuliko kuwa ng’ombe au farasi, kwa kuwa mbwa ana uhusiano wa karibu na bwana wake. Aidha, siku hizi watu wengi hufuga mbwa na baada ya miaka mitatu au mitano mbwa huyu huwa amejifunza kuelewa mengi ya yale wanasema! Kwa kuwa mbwa anaweza kuelewa maneno mengi ya bwana wake, ana uelewa mzuri wa bwana wake, na nyakati zingine anaweza kutohoa tabia na mahitaji kutoka bwana wake, kwa hiyo bwana anamtunza mbwa vyema, na mbwa anakula na kunywa vyema, na akiwa na maumivu anatunzwa zaidi—je, hivi mbwa hapati maisha ya furaha? Hivyo, kuwa mbwa ni bora kuliko kuwa ng’ombe au farasi. Katika hili, ukali wa adhabu ya mtu unaamua ni mara ngapi mtu anapata mwili kuwa mnyama, na anapata mwili kuwa aina gani ya mnyama. Mnaelewa, ndio?

Kwa sababu walitenda dhambi nyingi sana walipokuwa hai, watu wengine wataadhibiwa kwa kupatiwa miili kama wanyama mara saba hadi kumi na mbili. Baada ya kuadhibiwa vya kutosha, wanaporudi katika ulimwengu wa kiroho wanapelekwa mahali pengine. Roho mbalimbali mahali hapa zimeadhibiwa tayari, na ni aina ya roho ambazo ziko tayari kupata mwili kama wanadamu. Mahali hapa panaziainisha roho katika makundi kulingana na aina ya familia watakamozaliwa, ni aina gani ya nafasi watashikilia baada ya kupata mwili, na kadhalika. Kwa mfano, watu wengine watakuwa waimbaji wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa waimbaji; wengine watakuwa wafanyabiashara wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa wafanyabiashara; na ikiwa mtu atakuwa mtafiti wa kisayansi akiwa mwanadamu, basi anawekwa miongoni mwa watafiti wa kisayansi. Baada ya kuwekwa katika makundi, kila mmoja anatumwa kulingana na wakati tofauti na tarehe iliyowekwa, sawa tu na jinsi watu hutuma barua pepe siku hizi. Katika hili kutakuwa kumekamilika mzunguko mmoja wa uhai na mauti. Tangu siku mtu anawasili katika ulimwengu wa kiroho hadi wakati adhabu yao inakamilika, wanaweza kupata mwili kama wanyama mara nyingi, halafu wajitayarishe kupata mwili kama wanadamu; huu ni mchakato mzima.

Na wale waliokamilisha adhabu yao, na hawajapata mwili kuwa wanyama, je, watapelekwa kwa haraka katika ulimwengu yakinifu kuwa wanadamu? Au watachukua muda gani ndipo waje miongoni mwa wanadamu? Ni kwa haraka gani hawa watu watakuwa wanadamu? Kwa hili kuna mipaka ya kiwakati. Kila kitu kinachofanyika katika ulimwengu huu wa kiroho kinapitia mipaka ifaayo kiwakati na sheria—ambayo, Nikiieleza kutumia tarakimu, mtaelewa. Kwa wapatao mwili baada ya muda mfupi, wakati wanapokufa kuzaliwa kwao upya kama wanadamu kutatayarishwa. Wakati mfupi zaidi ni siku tatu. Kwa watu wengine, ni miezi mitatu, kwa wengine ni miaka mitatu, kwa wengine ni miaka thelathini, kwa wengine ni miaka mia tatu, kwa wengine hata ni miaka elfu tatu, na kadhalika. Hivyo basi ni nini kinaweza kusemwa kuhusu hizi sheria za kiwakati, na vipimo vyake ni vipi? Kuwasili kwa roho katika ulimwengu yakinifu, ulimwengu wa mwanadamu, kunategemea uhitaji: inalingana na nafasi itakayochukuliwa na hii roho duniani. Watu wakipata mwili kama wanadamu wa kawaida, wengi wao wanapewa mwili haraka sana, kwa sababu dunia ya wanadamu ina uhitaji mkubwa wa watu wa kawaida kama hao, na kwa hiyo siku tatu baadaye wanatumwa tena katika familia ambayo ni tofauti kabisa na ile waliyokuwa kabla hawajafa. Lakini wapo ambao wana nafasi maalum katika ulimwengu huu. “Maalum” inamaanisha kuwa hakuna uhitaji mkubwa wa hawa watu katika ulimwengu wa wanadamu; si watu wengi wanaohitajika kuishikilia nafasi hiyo, kwa hiyo basi inaweza kuwa miaka mia tatu kabla hawajapata mwili. Ambako ni kusema, hii roho itakuja mara moja tu katika kila miaka mia tatu, au hata mara moja kila baada ya miaka elfu tatu. Na ni kwa nini hivi? Ni kwa sababu kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu, nafasi hiyo haihitajiki katika dunia ya mwanadamu, na kwa hiyo wanatunzwa mahali fulani katika ulimwengu wa kiroho. Tazama Confucius, kwa mfano. Alikuwa na athari kubwa katika utamaduni wa jadi wa Uchina. Kuwasili kwake kulikuwa na athari kubwa kwenye utamaduni, elimu, desturi, na kufikiri kwa watu wa wakati ule. Lakini mtu kama huyu hahitajiki katika kila enzi, na kwa hiyo alilazimika kubaki katika ulimwengu wa kiroho, akisubiri huko kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu kabla ya kupata mwili. Kwa kuwa ulimwengu wa mwanadamu haukuhitaji mtu kama huyu, alilazimika kusubiri bila kufanya chochote, kwa kuwa kulikuwa na nafasi chache sana kama yake, kulikuwa na machache ya yeye kufanya, na hivyo basi alitunzwa sehemu fulani katika ulimwengu wa kiroho kwa muda mrefu, bila kufanya chochote, na kutumwa wakati ambapo ulimwengu wa mwanadamu ulimhitaji. Hizo ndizo sheria za kiwakati za milki ya kiroho kuhusu haraka ambayo watu wengi wanapata miili. Iwe ni mtu wa kawaida au maalum, ulimwengu wa kiroho una sheria mwafaka na desturi sahihi kwa utayarishaji wa watu kupata mwili, na hizi sheria na desturi hutoka kwa Mungu, zinatumwa kutoka kwa Mungu, na haziamuliwi au kudhibitiwa na msimamizi yeyote au kiumbe chochote katika ulimwengu wa kiroho.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp