Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI | Dondoo 156

Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu, kuridhisha hamu ya mwanadamu kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Pia, katika jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadamu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu. Je, ni kufikiria tu kwa mwanadamu ama akili za mwanadamu ambazo Shetani anapotosha kwa kutumia njia hii ya sayansi? Miongoni mwa watu, matukio na mambo katika mazingira yetu ambayo tunaweza kuona na ambayo tunakutana nayo, ni yapi mengine ambayo Shetani anatumia sayansi kupotosha? (Mazingira ya kiasili.) Mko sahihi. Inaonekana kwamba mmedhuriwa sana na hili, na pia mmeathirika sana na yeye. Mbali na kutumia matokeo yote ya utafiti na mahitimisho mbalimbali ya sayansi kumdanganya mwanadamu, Shetani pia hutumia sayansi kama mbinu ya kutekeleza uangamizi na unyonyaji tele wa mazingira ya kuishi aliyopewa mwanadamu na Mungu. Anafanya hivi chini ya kisingizio kwamba iwapo mwanadamu anatekeleza utafiti wa kisayansi, mazingira ya kuishi ya mwanadamu yatakuwa bora na bora zaidi na viwango vya kuishi vya mwanadamu daima vitaboreka, na zaidi ya hayo kwamba maendeleo ya kisayansi yanafanywa ili kuhudumia mahitaji ya mwili ya mwanadamu yanayozidi kila siku na haja yao ya kuendelea kupandisha ubora wao wa maisha. Kama sio kwa sababu hizi, basi mbona sayansi iendelezwe? Huu ni msingi wa kidhahania wa maendeleo ya Shetani ya sayansi. Hata hivyo, sayansi imemletea binadamu nini? Mazingira yetu ya karibu kabisa yana nini? Si hewa ambayo binadamu hupumua imechafuliwa? Maji tunayoyanywa kweli bado ni safi? (La.) Basi, je, chakula tunachokula, kingi chake ni cha kiasili? (La.) Basi ni nini tena? Kinakuzwa kwa kutumia mbolea na kupaliliwa kwa kutumia vinasaba, na pia kuna mabadiliko yanayozalishwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za sayansi, ili kwamba hata mboga na matunda tunayoyala sio ya kiasili tena. Si rahisi sasa kwa watu kupata yai la asili kula. Na mayai hayaonji yalivyokuwa yakionja awali, baada ya kusindikwa na inayoitwa sayansi na Shetani. Kwa kuangalia taswira kubwa, anga nzima imeharibika na kuchafuliwa; milima, maziwa, misitu, mito, bahari, na kila kitu juu na chini ya ardhi vyote vimeharibiwa na inayoitwa mafanikio ya kisayansi. Kwa maneno mengine, ikolojia nzima, mazingira yote ya kuishi yaliyopewa mwanadamu na Mungu yameangamizwa na kuharibiwa na inayodaiwa kuwa sayansi. Ingawa kuna watu wengi waliopata walichotarajia katika suala la ubora wa maisha wanaotafuta, kuridhisha tamaa na miili yao, mazingira ambayo mwanadamu anaishi kimsingi yameharibiwa na kuangamizwa na “mafanikio” mbalimbali yaliyoletwa na sayansi. Hata nje ama katika nyumba zetu hatuna tena haki ya kupumua pumzi moja ya hewa safi. Hii ni huzuni ya mwanadamu? Bado kuna furaha yoyote ya kuzungumzia kwa mwanadamu kuishi katika nafasi hii ya kuishi? Mwanadamu anaishi katika nafasi hii ya kuishi na, kutoka mwanzoni, haya mazingira ya kuishi yaliumbwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Maji ambayo watu hunywa, hewa ambayo watu hupumua, chakula ambacho watu hula, mimea, miti, na bahari—haya mazingira ya kuishi yote yalipewa mwanadamu na Mungu; ni asili, na hutekeleza kulingana na amri asili iliyotolewa na Mungu. Kama hakungekuwa na sayansi, watu wangekuwa na furaha na wangefurahia kila kitu kikiwa cha asili kabisa kulingana na njia ya Mungu na kulingana na kile Mungu amewapa wafurahie. Sasa, hata hivyo, haya yote yameangamizwa na kuharibiwa na Shetani; nafasi ya kimsingi ya kuishi ya mwanadamu haipo tena katika hali yake asili zaidi. Lakini hakuna anayeweza kutambua kilichosababisha matokeo ya aina hii ama jinsi haya yalikuja kuwa, na zaidi ya hapo hata watu zaidi wanaelewa na kukaribia sayansi kwa kutumia mawazo waliyoingiziwa na Shetani Je, hii si ya kuchukiza sana na ya kusikitisha? Kwa kuwa Shetani sasa amechukua nafasi ambamo wanadamu wapo na mazingira yao ya kuishi na kuwapotosha kuwa katika hali hii, na kwa kuwa wanadamu wanaendelea kwa njia hii, kuna haja yoyote ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu hawa duniani? Kuna haja ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu? (La.) Iwapo wanadamu watazidi kuendelea kwa njia hii, watachukua mwelekeo upi? (Uharibifu.) Wanadamu wataharibiwa vipi? Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na mapigo kusambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? (Ndiyo.) Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—mnaweza kutambua hitimisho ya asili ya wanadamu itakuwa vipi? Matokeo ya mwisho asilia yatakuwa yapi? (Uharibifu.) Itakuwa uharibifu: kukaribia uharibifu hatua moja kwa wakati. Kukaribia uharibifu kwa hatua moja kwa wakati! Inaonekana sasa kama sayansi ni aina ya ushombwe ambao Shetani amemwandalia mwanadamu, ili wakati mnapojaribu kupambanua mambo mnafanya hivyo katika hali ya ukungu; haijalishi mnaangalia kwa ugumu aje, hamwezi kuona mambo kwa wazi, na haijalishi mnajaribu sana vipi, hamwezi kuyatambua. Shetani, hata hivyo, bado anatumia jina la sayansi kuzidisha hamu yako na kukuongoza kwa pua, mguu mmoja mbele ya mwingine, kuelekea shimo na kuelekea kifo.

Umetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana