Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Uyahudi. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyotoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Wanaisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Wanaisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Uyahudi, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kwa kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi pekee, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Wanaisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaowakomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Wanaisraeli pekee, na si Mungu wa Wayahudi pekee; ni Mungu wa viumbe vyote. Hatua mbili za awali za kazi Yake zilifanyika Israeli, na kwa njia hii, dhana zingine zimepata umbo ndani ya watu. Watu wanafikiri kuwa Yehova alikuwa anafanya kazi Israeli na Yesu Mwenyewe alifanya kazi Yake Yudea—zaidi ya hayo, ilikuwa kupitia kupata mwili ndiyo Alifanya kazi Yudea—na hata hivyo, kazi hii haikuenea zaidi ya Israeli. Hakuwa kazini na Wamisri; Hakuwa kazini na Wahindi; Alikuwa tu kazini na Wanaisraeli. Watu basi wanaunda dhana mbalimbali; zaidi ya hayo, wanapanga kazi ya Mungu ndani ya mawanda fulani. Wanasema kwamba wakati Mungu yuko kazini, ni lazima ifanywe miongoni mwa wateule na ndani ya Israeli; mbali na Israeli, Mungu hana mpokeaji mwingine wa kazi Yake, wala Hana mawanda mengine ya kazi Yake; wana madhubuti hasa ya “kumwadhibu” Mungu mwenye mwili, kutomruhusu kuenda zaidi ya eneo la Israeli. Hizi zote ni dhana za mwanadamu? Mungu aliunda mbingu na dunia yote na vitu vyote, na kuumba viumbe vyote; Anawezaje kuzuia kazi Yake kwa Israeli peke yake? Katika hali hiyo, kungekuwa na haja gani ya kufanya uumbaji Wake wote? Aliiumba dunia nzima; Ametekeleza mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita sio tu ndani ya Israeli lakini pia na kila mtu ulimwenguni. Bila kujali kama wanaishi Uchina, Amerika, Uingereza ama Urusi, kila mtu ni uzao wa Adamu; wote wameumbwa na Mungu. Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuondoka katika mawanda ya uumbaji wa Mungu, na hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuepuka utambulisho wa “ukoo wa Adamu.” Wote ni viumbe vya Mungu, na wote ni wa ukoo wa Adamu; pia ni wazawa wapotovu wa Adamu na Hawa. Sio tu Wanaisraeli ndio viumbe vya Mungu, lakini ni watu wote; hata hivyo, wengine miongoni mwa viumbe wamelaaniwa, na wengine wamebarikiwa. Kuna mambo mengi ya kupendeza kuwahusu Wanaisraeli; Mungu awali alikuwa kazini nao kwa sababu walikuwa watu wenye upotovu wa kiasi kidogo zaidi. Wachina ni wa chini wakilinganishwa nao, na hawawezi hata kutumaini kulingana nao; hivyo, Mungu awali alifanya kazi miongoni mwa watu wa Israeli, na hatua ya pili ya kazi Yake ilifanywa tu Uyahudi. Kwa sababu hii, watu huunda dhana nyingi na kanuni nyingi. Kwa kweli, iwapo Angetenda kulingana na dhana za binadamu, Mungu angekuwa tu Mungu wa Waisraeli; kwa njia hii Asingeweza kupanua kazi Yake katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, kwa sababu Angekuwa tu Mungu wa Wanaisraeli badala ya Mungu wa viumbe vyote. Unabii ulisema kuwa jina la Yehova lingekuwa kubwa kwa mataifa yasiyo ya kiyahudi na kuwa jina la Yehova lingeenezwa kwa mataifa yasiyo ya kiyahudi—mbona walisema hivi? Iwapo Mungu angekuwa Mungu wa Wanaisraeli tu, basi Angefanya kazi tu Israeli. Zaidi ya hayo, Asingepanua kazi hii, na Asingefanya huu unabii. Kwa sababu Alifanya huu unabii, Angehitaji kuipanua kazi Yake katika mataifa yasiyo ya kiyahudi na katika kila taifa na mahali. Kwa sababu Alisema hivi, basi Atafanya hivyo. Huu ndio mpango Wake, kwani Yeye ndiye Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote, na Mungu wa viumbe vyote. Bila kujali iwapo yuko kazini na Waisraeli ama Uyahudi nzima, kazi Anayoifanya ni kazi ya ulimwengu mzima na kazi ya binadamu wote. Kazi Anayoifanya leo katika taifa la joka kubwa jekundu—katika taifa lisilo Israeli—bado ni kazi ya binadamu wote. Israeli inaweza kuwa kituo cha kazi Yake duniani; vivyo hivyo, Uchina pia inaweza kuwa kituo cha kazi Yake duniani miongoni mwa mataifa yasiyo ya kiyahudi. Sasa Hajatimiza unabii kwamba “jina la Yehova litakuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya kiyahudi”? Hatua ya kwanza ya kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya kiyahudi inahusu kazi hii Anayoifanya katika taifa la joka kuu jekundu. Kwa Mungu mwenye mwili kufanya kazi katika nchi hii na kuwa miongoni mwa hawa watu waliolaaniwa inaenda hasa kinyume na mawazo ya mwanadamu; hawa watu ni wadogo zaidi na wasio na thamani yoyote. Hawa wote ni watu ambao Yehova alikuwa amewaacha mbeleni. Watu wanaweza kuachwa na watu wengine, lakini wakiachwa na Mungu, hawa watu hawatakuwa na hadhi, na watakuwa na thamani ya kiwango cha chini kabisa. Kama sehemu ya viumbe, kukaliwa na Shetani ama kuachwa na watu wengine yote mawili ni mambo machungu, lakini sehemu ya viumbe ikiachwa na Mungu wa uumbaji, hii inaashiria kwamba hadhi yake iko katika kiwango cha chini kabisa. Uzao wa Moabu ulilaaniwa, na ulizaliwa ndani ya nchi hii isiyo na maendeleo makubwa; bila shaka, uzao wa Moabu ni watu walio na hadhi ya chini kabisa chini ya ushawishi wa giza. Kwa sababu hawa watu walimiliki hadhi ya chini kabisa zamani, kazi inayofanywa miongoni mwao inaweza kabisa kuzivunja dhana za mwanadamu, na pia ni kazi yenye faida kubwa zaidi kwa mpango Wake mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita. Ili Afanye kazi miongoni mwa watu hawa ni kitendo kinachoweza zaidi kuzivunja dhana za mwanadamu; Akiwa na hili Anazindua enzi; na jili Anavunja dhana za mwanadamu; Akiwa na hili Anatamatisha kazi ya Enzi ya Neema. Kazi Yake ya awali ilifanywa Uyahudi, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uziduzi wa enzi. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndiyo ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu “anakuwa” Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, chombo cha kuabudiwa na kila kiumbe chenye uhai.

Kwa sasa bado kuna watu wengine wasioelewa ni aina gani ya kazi mpya ambayo Mungu amezindua. Mungu amefanya mwanzo mpya kwa mataifa yasiyo ya kiyahudi na kuanza enzi nyingine na kuzindua kazi nyingine, na Yuko kazini miongoni mwa ukoo wa Moabu. Je, hii si kazi Yake mpya kabisa? Hakuna yeyote katika enzi zote aliyeipitia kazi hii, wala hakuna aliyeisikia, wala hata kuithamini. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, kutoeleweka kwa Mungu, ukubwa wa Mungu, utakatifu wa Mungu vinategemea hatua hii ya kazi katika siku za mwisho, kuibuka wazi. Hii siyo kazi mpya inayovunja dhana za mwanadamu? Kuna wale bado wanaofikiria hivi: “Kwa sababu Mungu alimlaani Moabu na kusema kuwa Angeuacha ukoo wa Moabu, Angewaokoaje sasa?” Hao ni wale watu kutoka katika mataifa yasiyo ya kiyahudi waliolaaniwa na kulazimishwa nje ya Israeli; Waisraeli waliwaita “mbwa wasio wa kiyaudi.” Kwa mtazamo wa kila mtu, wao sio mbwa wasio wa kiyahudi tu, lakini mbaya zaidi, wana wa uharibifu; kwa maneno mengine, wao si wateule wa Mungu. Ingawa walikuwa wamezaliwa awali ndani ya eneo la Israeli, hao sio sehemu ya watu wa Israeli; wao pia walifukuzwa kwenda kwa mataifa yasiyo ya kiyahudi. Wao ndio watu wa chini zaidi. Ni kwa sababu hasa ni watu wa chini zaidi miongoni mwa binadamu ndiyo maana Mungu anatekeleza kazi Yake ya kuzindua enzi mpya miongoni mwao. Kwa sababu wao ni wawakilishi wa binadamu wapotovu na kazi ya Mungu haikosi uchaguzi ama madhumuni, kazi Anayoifanya miongoni mwa watu hawa leo pia ni kazi inayofanywa miongoni mwa viumbe. Nuhu alikuwa miongoni mwa viumbe, kama ulivyo ukoo wake. Yeyote duniani aliye na mwili na damu ni sehemu ya viumbe. Kazi ya Mungu imeelekezwa kwa viumbe vyote; haitekelezwi kulingana na kama mtu amelaaniwa baada ya kuumbwa. Kazi Yake ya usimamizi imeelekezwa kwa viumbe vyote, sio wale wateule wasiolaaniwa. Kwa sababu Mungu anataka kutekeleza kazi Yake miongoni mwa viumbe Vyake, kwa hakika Ataifanya hadi kukamilika kwa mafanikio; Atafanya kazi miongoni mwa hao watu walio na manufaa kwa kazi Yake. Kwa hivyo, Anavunja mikataba yote ya kufanya kazi miongoni mwa watu; Kwake, maneno “kulaaniwa,” “kuadibu” na “kubarikiwa” hayana maana! Wayahudi ni wazuri hasa, na wateule wa Israeli sio wabaya pia; ni watu wenye ubora mzuri wa tabia na ubinadamu mzuri. Awali Yehova alizindua kazi Yake miongoni mwao na Akafanya kazi Yake ya awali, lakini ingekuwa bila maana kama Angewatumia kama wapokeaji wa kazi Yake ya ushindi sasa. Ingawa wao pia ni sehemu ya viumbe na wana vipengele vingi vyema, ingekuwa bila maana kutekeleza hatua hii ya kazi miongoni mwao. Asingeweza kumshinda yeyote, wala Asingeweza kushawishi viumbe vyote. Huu ndio umuhimu wa uhamisho wa kazi Yake kwa watu hawa wa taifa la joka kubwa jekundu. Maana ya ndani zaidi hapa ni ya uzinduzi Wake wa enzi, ya kuvunja Kwake kwa kanuni zote na dhana zote za mwanadamu na pia kwa kumaliza Kwake kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kama kazi Yake ya sasa ingefanywa miongoni mwa Wanaisraeli, ikifika wakati ambao mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilika, kila mtu angeamini kuwa Mungu ni Mungu tu wa Wanaisraeli, kuwa Wanaisraeli tu ndio wateule wa Mungu, kuwa Wanaisraeli tu ndio wanaostahili kurithi baraka na ahadi za Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili katika taifa lisilo la kiyahudi la joka kubwa jekundu; Ametimiza kazi ya Mungu kama Mungu wa viumbe vyote; Amekamilisha kazi Yake yote ya usimamizi, na Atamaliza sehemu kuu ya kazi Yake kwa taifa la joka kubwa jekundu. Kiini cha hatua hizi tatu za kazi ni wokovu wa mwanadamu—ambao ni, kufanya viumbe vyote vimwabudu Bwana wa viumbe. Hivyo basi, kila hatua ya kazi hii ni muhimu sana; Mungu hatafanya chochote kisicho na maana ama thamani. Kwa upande mmoja, hatua hii ya kazi inajumuisha kuzindua enzi na kukamilisha enzi mbili za awali; kwa upande mwingine inajumuisha kuvunja dhana zote za mwanadamu na njia ya zamani ya imani ya mwanadamu na maarifa. Kazi ya enzi mbili za awali ilifanywa kulingana na dhana tofauti za binadamu; hatua hii, hata hivyo, inafuta kabisa dhana za binadamu, na hivyo kuwashinda binadamu kikamilifu. Kwa kutumia ushindi wa ukoo wa Moabu na kutumia kazi iliyotekelezwa miongoni mwa ukoo wa Moabu, Mungu atawashinda binadamu wote katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa kina zaidi wa hatua hii ya kazi Yake, na ndicho kipengele cha thamani ya hatua hii ya kazi Yake. Hata kama sasa unajua kuwa hadhi yako ni ya chini na kuwa una thamani ya chini, bado utahisi kwamba umekutana na jambo linalofurahisha sana: Umerithi baraka kubwa, ukapata ahadi kubwa, na unaweza kamilisha hii kazi kubwa ya Mungu, na unaweza kuuona uso wa kweli wa Mungu, kujua tabia Yake ya asili, na kufanya mapenzi ya Mungu. Hatua mbili za awali za kazi ya Mungu zilifanywa Israeli. Iwapo hatua hii ya kazi Yake katika siku za mwisho bado ingefanywa miongoni mwa Wanaisraeli, viumbe vyote havingeamini kwamba Wanaisraeli tu ndio waliokuwa wateule, lakini pia mpango wa usimamizi wa Mungu wote haungefikia athari iliyotaka. Wakati ambapo hatua hizi mbili za kazi Yake zilifanywa Israeli, hakuna kazi yoyote mpya iliyokuwa imefanywa na hakuna kazi yoyote ya Mungu ya kuzindua enzi ilikuwa imewahi kufanywa katika mataifa yasiyo ya kiyahudi. Hatua hii ya kazi ya kuzindua enzi inafanywa kwanza katika mataifa yasiyo ya kiyahudi, na zaidi ya hayo, inafanywa kwanza miongoni mwa ukoo wa Moabu; hii imezindua enzi mpya. Mungu amevunja maarifa yoyote yaliyo ndani ya dhana za binadamu na hajaruhusu yoyote yaendelee kuwa hai. Katika kazi Yake ya kushinda Amevunja dhana za binadamu, hiyo njia ya zamani, ya maarifa ya binadamu, Anaruhusu watu waone kuwa kwa Mungu hakuna kanuni, kwamba hakuna kitu kizee kumhusu Mungu, kwamba kazi Anayoifanya ni ya uhuru kabisa, ni huru kabisa, kwamba Yeye yuko sahihi katika chochote Anachofanya. Ni lazima utii kikamilifu kazi yoyote Anayoifanya miongoni mwa viumbe. Kazi yoyote Anayoifanya ni ya maana na inafanywa kulingana na mtazamo Wake na maarifa Yake na sio kulingana na chaguo za watu na dhana za watu. Anafanya yale mambo yaliyo na manufaa kwa kazi Yake; kama kitu hakina manufaa kwa kazi Yake, Hatakifanya, hata kiwe kizuri vipi! Anafanya kazi na kuchagua mpokeaji na eneo la kazi Yake kulingana na maana na madhumuni ya kazi Yake. Hafuati kanuni za zamani, wala Hafuati fomula nzee; badala yake, Anapanga kazi Yake kulingana na umuhimu wa kazi; mwishowe, Anataka kufikia matokeo yake ya kweli na madhumuni yanayotarajiwa. Iwapo huelewi mambo haya sasa, kazi hii haitatimiza matokeo yoyote kwako.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp